SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,129
- 7,898
Mwaka 1979 kulitokea maajabu ya soka ambayo mpaka leo bado hayajaweza kurudiwa katika historia ya soka la Afrika.
Simba ilicheza mchezo wa Klabu Bingwa Afrika na timu ya Mufulira Wanderers ya Zambia. Mufulira ilikuwa moja ya timu bora Afrika kipindi hicho. Katika mechi ya kwanza iliyofanyika Tanzania, Simba ilikung'utwa 0-4. Katika hali ya kawaida, hapo timu inaenda mechi ya marudiano ugenini kukamilisha tu ratiba ila katika hali ya kushangaza, Simba ilipindua matokeo kwa kushinda 5-0 mbele ya Rais wa Zambia Keneth Kaunda na hivyo kuvuka hadi hatua inayofuata.
Msimu huu wa 2023-2024, Yanga ilienda kucheza na CR Belouizdad katika mzunguko wa pili wa makundi huku ikiwa imeshafungwa 0-3 katika mechi ya kwanza. Kutokana na kanuni za CAF zilivyo na msimamo wa kundi lao, Yanga ilihitaji ushindi wa goli 4-0 ili automatically iwe imefuzu. Ushindi wowote tofauti na huo ingeilazimu Yanga kwenda kutafuta kufuzu katika mechi ya mwisho dhidi ya Al Ahly. Mpira una maajabu yake, Yanga ikafanikiwa kupata huo ushindi wa 4-0 dhidi ya CRB na hivyo kufuzu hadi hatua ya robo fainali.
Kwa mtazamo wako, ipi kati ya hizi comeback mbili ni kali zaidi? Tukumbuke Simba ilipata ushindi wa 5-0 katika ardhi ya ugenini na ni rekodi ambayo bado haijafikiwa mpaka leo katika kumbukumbu za CAF.