habari zenu wa mmu. Leo nimefanya maamuzi mazito kabisa. Ni hivi mimi nina mpenzi wangu ambae tuna muda wa miezi 6 tangu tumekua pamoja japo muda 80 percent ya mapenzi yetu yalikua kwa njia ya mawasiliano, as kwanza tulikua mikoa tofauti na nilivyokuja dar yeye yupo dar hii lakini ni geti kali na anasoma chuo cha MAGOGONi. Tatizo ni kuwa yeye ananipenda sana na kila siku anaongelea swala la kuoana, wakati me sijamfikiria kumuoa. Kikubwa zaidi yeye ni bikra na uzuri hatujawahi kusex bt tulipanga siku za karibuni. Nimeamua kumwambia ukweli kuwa sitaweza kumuoa kwa vile yeye na mimi tuko dini tofauti, amelia sana but me nimeona ni bora kuliko ningemwambia baada ya kusex nae. Wadau nimefanya uamuzi sahihi au nimekosea?