Nashukuru Wana JF kwa ushauri... Hatimaye nimefanikiwa!!!

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
Ndugu zangu Wana JF,
Mwishoni mwa mwaka uliopita nilileta post hapa nikiomba ushauri ili kulinda kibarua na kuwa jirani na familia. Wengi kama sio wote waliochangia walinipa na ushauri mzuri iloi hatimaye mambo yaweze kwenda vizuri.
Napenda kutumia fursa hii kuwajulisha kuwa hatimaye wiki iliyopita nimepokea barua inayoniruhusu kuhamia jirani na familia. Hivi ninavyoandika hapa nipo njiani kwenda kuanza kazi kwenye kituo changu kipya cha kazi fursa ambayo itanifanya sasa niungane na familia yangu.


Nawashukuruni wote mkiongozwa na Typical Tz kwa ushauri wenu.
 
Hongera sana, nakutakia kila la kheri kwenye kazi yako mkuu ndani ya kituo kipya.
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Angalia vizuri Boss wako asiwe yule walimzungumzia kina Juma nature,solo na Ferouz!!!
Mwenzio huko kwenye Ubongo wa Fleva niko mweupe kabisa.... napendelea zilizopendwa, kama Twist, Katitu, Kanda Bongoma, Bozi Boziana, Pamela Nkuta, Girlie Mafura na Ntombi. Hebu ni brief kidogo wanamsemaje huyo Boss hao jamaa?
 
All the best aisee! Lakini vipi, shukran mikono mitupu bila hata bia?
Weekend tukutane pale Royal Mushi Inn Mikocheni au Dar Live Mbagala au vipi? Hiyo ni baada ya kuangalia mechi ya Zamalek vs Jangwani pale Tai Vaaa!
 
Ok, Uongeze na familia pia.
Teh, teh, JF bwana haikosi vituko. Ngoja niangalie kwanza hii trend ya mfumuko wa bei kwanza kwani mpaka sasa ni 19%, isiposhuka hii hii familia inatosha
 
ulikuwa mtumishi wa umma??? Toa mchakato na sie wengine tuchukue hatua
 
Back
Top Bottom