Nashukuru nilizaliwa kwenye familia yenye dini nayoabudu na wewe pia ndugu nakushauri ushukuru kama nami navyoshukuru

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,140
2,012
Akili ya mwanadamu inamuwezesha kungamua uwepo wa muumba wa viumbe vyote hapa duniani, uelewa juu ya muumba unaletwa na dini mbalimbali hapa duniani. Lengo la kuandika waraka huu ni kutaka kuonyesha kwamba hakuna haja ya kubishana dini ipi ni bora kwa sababu zote zinabeba ujumbe mmoja.

Dini na wazazi, asilimia kubwa ya waumini wa dini husika wamekuwa waumini wa dini hiyo kutokana na kulewa na walezi waliokuwa wakiabudu dini hiyo, na hao walezi wamejifunza dini hiyo kutoka kwa wazazi wao na kuendelea. Kutokana na ukweli huo hamna haja ya kuona dini yako ni bora kuliko ya mwenzio kwasababu hukuchagua dini yako ulipo kuwa mchanga, na endapo ungezaliwa kwenye familia yenye dini tofauti na yako sasa nayo pia ungeiona bora kuliko ambayo unaabudu sasa.

Dini na geography, dini pia zina asili ya mahala ilipoenea, ukienda mashariki ya kati kuna uislam ukienda europe kuna ukristo ukienda asia kuna Buddhism. Haya maeneo watu huabudu dini husika ni kawaida.

Nadhani nimeeleweka pointi zangu na wote mliopata bahati ya kusoma ujumbe huu ni matumaini yangu hamtaingia tena kwenye ubishani usio na mashiko kwamba dini ipi ni bora. Nachoweza kuwashauri endapo ukakumbana na mtu anayeikwezwa dini yake akiilinganisha na yako mjibu “NASHUKURU NILIZALIWA KWENYE FAMILIA YENYE DINI NAYOABUDU NA WEWE PIA NDUGU NAKUSHAURI USHUKURU KAMA NAMI NAVYOSHUKURU”.

Tunashukuru kwasababu tumebahatika kujua uwepo wa muumba kupitia dini zetu kuna nafsi nyingine hazijapata nafasi hii.
 
Back
Top Bottom