Nashukuru Mungu sikusoma na kuwa mwalimu

Nashukuru Mungu sikusoma na kuwa mwalimu

Njia pekee ya kumiliki hayo yote ambayo mwalimu hawezi kuyamili kwa kutegemea mshahara ni kuwa mwanasiasa ili uibe Serikalini kama tunavyowaona wanasiasa walio wengi wanavyomiliki rasilimali muda mfupi tu waingiapo siasani

Sent using Jamii Forums mobile app
hilo nalipigia tizi " lazima nilifanyie kazi aisee... nimechoka kuwa mpenzi mtazamaji..dhidi ya walaji keki ya taifa
 
Katika kazi niliyokuwa naipenda kweli kweli basi ni uwalimu, hta pale nilipokuwa nasoma ndoto zangu zilikuwa siku moja nije kuwa mwalimu.

Nilipomaliza tu elimu yangu direct nikaaply education nikachaguliwa.

Kitu ambacho kilinishtua ni kwamba muda ambao nasubiri kwenda chuo nilikuwa kwa brother na bro alivyoniuliza nilimueleza nia yangu ya kusomea uwalimu.

Alinicheki kwa dharau alafu akanizaba kibao kimoja matata na kuniuliza umeshawahi kumuona mwalimu mwenye VX, au ata land cruiser aliyonunua akiwa kazini?

Nikamjibu hapana ?

Akaniuliza tena umeshawahi kumuona mwalimu alieyejenga nyumba ya kueleweka akiwa kazini?

Nikasema hapana.

Akasema basi achana na hilo wazo lako mfu jioni huyo kanipakiza kwenye mgari wake nasema mgari kwa sababu ni gari siyo ki vitz akanipeleka chuo na kuchukua moja kati ya kozi ya afya mukide kabisa.

Japo mpaka leo ajira hazijatoka ila napiga zangu temporary tu kwa wana leo napiga hapa kesho pale siku zinaenda ningesomea uwalimu sijui hiyo temporary ningepigia wapi na wakati sasa hivi elimu bure.
Zero IQ revealed.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida iko hapa kwa nini wamekimbia ualimu na kuiendea siasa mpaka kuwa maraisi jibu ni kwamba kule kugumu kuliko ugumu wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Siyo wanasiasa wote walitokea ualimu! Kuna wahandisi,madaktari nk waliacha fani zao,wakaingia siasa. Usipotoshe ukweli. Labda nikuulize, ni maafisa kilimo wangapi vijijini
wana Voxy na nyumba za kifahari?
 
Hapo kuna pharmacy,Nersing,MD ,Radiologist , Lab technologist,Dental specialist,na kozi nyingine nyingi zote zinaitwa Kozi za Afya.

We umekalili hizo 3 tu mkuu?
Kozi ya afya ni kama vile unesi au lab technologist? Inavyoonekana hata doto ya kufikia MD huna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hao walikuwa walimu wa zamani " "wasikuhizi wanazeeka mapema mnoo ndugu jaribu kukutana nao ujionee..wakuta kijana Mdogo uso umeshaanza kutoa makunyazi kama six pack..strees mwanzo mwisho aisee.....""
Haaaa haaa au kwasababu siwafuatilii ati, maana mie nikifika hutafuta walimu wangu, wasikuhizi sijui kitu gani kina wasibu[emoji4] [emoji4] [emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haaaa haaa au kwasababu siwafuatilii ati, maana mie nikifika hutafuta walimu wangu, wasikuhizi sijui kitu gani kina wasibu[emoji4] [emoji4] [emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
ndio hzio stress za maisha mamaa..mshahara wa chini " majukumu kimo cha ngamia...basiii muda wote unahemea juu juu kama upo " intensive care unit
 
Wengi watabisha ila huu ndo ukweli, maisha ya mwalimu, ni uakika wa kula, ila kumiliki vitu vikubwa ni ndoto.

Walimu wengi akijitahidi akajenga na kiduka kidogo, na kivits ingawa kwa mbinde, basssi, haya yote walikuwa enzi za kikwete.

Hawezi kuwa mwalimu ukawaza mambo makubwa watu wanakubana usitoke stress tupu, maendeleo utayawaza lini?

BTW, nilikuwaga mwalimu, ila kwa kulazimisha sikuwahi kupenda Yale maisha hata mazingira kha, headmaster yeye ndo kama raisi ruhusa hanipi, niende kufatilia vyuo mjini, hataki niende kusoma, form zangu za kwenda masomoni hazisain, nguo anaoenda nivae madela, siku nikisema wacha Leo, nivaepe nguo fupi hata kama ni ya heshima, ananiandikia barua ya warning, nilipataga nyumba mbali, nikichelewa hata dakika moja, nakuta kashaweka mstari wakati anajua walimu wote wanaishi shuleni except Mimi.
Nilichokaga hayo maisha, siku moja niliamua nikaacha kazi, nikasepa Chuo coz nyingine, sijawahi kujuta kuacha ualimu kha!
Unawashaurije walimu walioko makazini?
 
Katika nchi yoyote walimu ni watu muhimu sana, katika sector muhimu za nchi ualimu ni moja wapo , ila sijui kwanini kwingine walimu wanakuwa kama omba omba tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika kazi niliyokuwa naipenda kweli kweli basi ni uwalimu, hta pale nilipokuwa nasoma ndoto zangu zilikuwa siku moja nije kuwa mwalimu.

Nilipomaliza tu elimu yangu direct nikaaply education nikachaguliwa.

Kitu ambacho kilinishtua ni kwamba muda ambao nasubiri kwenda chuo nilikuwa kwa brother na bro alivyoniuliza nilimueleza nia yangu ya kusomea uwalimu.

Alinicheki kwa dharau alafu akanizaba kibao kimoja matata na kuniuliza umeshawahi kumuona mwalimu mwenye VX, au ata land cruiser aliyonunua akiwa kazini?

Nikamjibu hapana ?

Akaniuliza tena umeshawahi kumuona mwalimu alieyejenga nyumba ya kueleweka akiwa kazini?

Nikasema hapana.

Akasema basi achana na hilo wazo lako mfu jioni huyo kanipakiza kwenye mgari wake nasema mgari kwa sababu ni gari siyo ki vitz akanipeleka chuo na kuchukua moja kati ya kozi ya afya mukide kabisa.

Japo mpaka leo ajira hazijatoka ila napiga zangu temporary tu kwa wana leo napiga hapa kesho pale siku zinaenda ningesomea uwalimu sijui hiyo temporary ningepigia wapi na wakati sasa hivi elimu bure.
Mzee Kazi Ya Ualimu Ni Nzuri Sana Basi Tu Tz Wanasiasa Wanachukulia Poa!Me Ni Mwalimu Tena Kijana!Sijutii Kusomea Ualimu Mbona!Izo VX na Nyumba Kali Mbona Hata Mtu Wa Kawaida ambaye hajasoma Anaweza Pata!Ni Kukomaa Tu Na Mitikasi ya Mjini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani yeye alifundishwa na nani?? Huenda hakupitia shule kwani hata hilo gari vx analotaja hajui bei yake. Sema tu waalimu waongezewe maslahi na wale sio kuwapuuza kiasi hicho. Watu wote wenye hekima duniani wamepitia kwa waalimu. Nakubali mshahara mdogo ila tupige debe ili serikali iwafikirie. Waalimu nawapa TANO ya nguvu
 
Wengi watabisha ila huu ndo ukweli, maisha ya mwalimu, ni uakika wa kula, ila kumiliki vitu vikubwa ni ndoto.

Walimu wengi akijitahidi akajenga na kiduka kidogo, na kivits ingawa kwa mbinde, basssi, haya yote walikuwa enzi za kikwete.

Hawezi kuwa mwalimu ukawaza mambo makubwa watu wanakubana usitoke stress tupu, maendeleo utayawaza lini?

BTW, nilikuwaga mwalimu, ila kwa kulazimisha sikuwahi kupenda Yale maisha hata mazingira kha, headmaster yeye ndo kama raisi ruhusa hanipi, niende kufatilia vyuo mjini, hataki niende kusoma, form zangu za kwenda masomoni hazisain, nguo anaoenda nivae madela, siku nikisema wacha Leo, nivaepe nguo fupi hata kama ni ya heshima, ananiandikia barua ya warning, nilipataga nyumba mbali, nikichelewa hata dakika moja, nakuta kashaweka mstari wakati anajua walimu wote wanaishi shuleni except Mimi.
Nilichokaga hayo maisha, siku moja niliamua nikaacha kazi, nikasepa Chuo coz nyingine, sijawahi kujuta kuacha ualimu kha!
tatizo ulikua unajifanya mgumu ndio maana nilikua nakufanyia figisu
 
Ualimu ni kazi moja bora kabisa, ambayo inajenga kila fani.

Hata uwe engineer au mwanasheria ila bado mwalimu anabaki kuwa mwalimu maana pasipo yeye usingekuwa na professional yako.

Nasikitika kutokusoma ualimu, Mwalimu ujivunie ualimu wako.
 
Unaweza kuwa sahihi kwa upande mmoja ila pia upande wa pili ukawa sio sahihi

Kwanza akili yako umeifunga kwenye kuajiriwa that's the problem ndugu, nikupe mfano mdogo tu

Mtoto wa Dada yangu anasoma degree ya education mwaka wa mwisho ila masomo ya science ila akiwa second year nikamlink na organizations cause ndio alikua anapenda and of course ndio shughuli zangu so alipenda shughuli za mjomba ake...so the kid is bright akaanzisha CBO akiwa chuo akakutana na watu mbali mbali now yupo kwenye mradi mkubwa unaomlipa pesa nzuri tu while still anamalizia chuo simply ni facilitator...
So you see?? Not all students waliosoma education lazima washike chaki, depends with your mental laziness

Hata usome fani gani if your mind is crude then hata hilo v8 utaishia kuweka kishoka kwa lift tu...

Your mind ndio mchawi wa kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada amesema kweli tupu ualimu kwa MTU anaewaza afanikiwe kwenye maisha ni ujinga hasa kipindi hiki cha hili jiwe mbaya zaidi ni waoga mno na kazi yenyewe ni chaka tosha
 
Nilipokuwaga sijakaw mjini nipo kijijini uko hizi story walimu wanq shida sijui nini nilizisikiaga sana na nikamini sasa nilipo toka uko vijijini kuja mjini, nikawa nashangaa naona walimu wana magari, nyumba nk nikawa najiuliza inakuwaje hawa mbona niliambiwa wana shida sana

Jamaa yangu mmoja akanipeleka duka moja hivi akaniambia hili duka la mwalimu lakini pia anafanya biashara ya kukopesha pesa nikamuuliza anakopesha walimu wenzake janaa akacheka akasema siyo walimu tu hapa wanakopa madocta, nurse watumishi mbali mbali nikamwambia mbona walimu nasikia njaa sana

Jamaa akajibu tatizo walimu wapo wengi sana na wapo karibu na jamii hivyo ni vyepesi mtu kujua matatizo yao lakini shida hizi kila idara zipo sema hao wengine ni wachache hivyo kujua matatizo yao ni vigumu

Jamaa akaendelea akasema hivi unajua hao unaona madocta, wana sheria sijui bankers nk hivi unajua asilimia 90 ni watoto wa walimu yani wazazi wao ni walimu walisomesha kwa pesa ya mshahara wa mwalimu nikawaza nikaona kweli

Jamaa akaendea akasema walimu wanadharaulika sababu ya kusimamia logic na vitu vya msingi ndio maana utasikia walimu wajinga unamkopesha anakulipa na riba juu si kwamba mjinga anaheshimu ustarabu wanajua ile ni haki yako mtu bora akupe

Basi nikasema ooh kumbe walimu usipowajua unaweza wadharau sana.
 
Hapo kuna pharmacy,Nersing,MD ,Radiologist , Lab technologist,Dental specialist,na kozi nyingine nyingi zote zinaitwa Kozi za Afya.

We umekalili hizo 3 tu mkuu?

itoshe kukuona wewe mjinga na huna elimu yeyote kichwani isipo kuwa una ajenda yako kuhusu walimu , maaana aliye soma na akaelimika hana mawazo ya kitoto kama yako, tambua taifa haliwezi kuwa na aina moja tu ya mahitaji , hata wewe kufika hapo umepita kwenye mikono ya walimu na hata aliye kufundisha huo u nesi wako pia ni mwalimu sasa sijui kichwani mwako una ongelea tabaka gani la ualimu

na wanao kuunga mkono nao ni wajinga wenzio na mmekutana eajinga watupu maana yeyote yule aliye msomi kapita mikononi kwa mwalimu kuanzia mwalimu wa daraja la chini hadi mwalimu wa daraja la juu sasa sijui kama wote wangetaka kusoma afya nani angekuwa mwalimu wao .. WEWE NI MJINGA NA MTOTO KIFIKRA kama sivyo huna elimu yeyote kichwani mwako au ni muhanga wa kukosa ajira ya ualimu kwa kusoma history na kiswahili hivyo una stress za maisha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom