Nashindwa nini niamue katika situation hii

Ana story za ajabu huelewi kama ni za kweli au za kitunga. Muda mrefu sasa nimeacha kumfatilia
Uwiii, utafanya nami nianze kumfuatilia jamani.
Ila humu kuna hekaheka jamanišŸ˜…

Japo wapo wenye ishu za kweli, ila tatizo sasa jinsi ya kuiwasilisha hio habari, utafurahišŸ˜…
 
Kwanza Inaonekana mlienda Canada kwa "status ya Ukimbizi"

unachotakiwa kukifanya ni rahisi tu, kama mke wako anasumbua ni kumpeleka mzee wako kwenye "shelter" aende akapewe nyumba na serikali aishi huko.

Huyo kupata nyumba ni sahau, kwa kipindi hiki beba tu huo msalaba hadi apate nyumba

Wacongo wakifika Canada wakaanza kupewa pesa za watoto(wenfi wana watoto 5+) ko kama $3500 kila mwezi hata kazi hawafanyi tena au wanafanya kwa kupenda wao
 
Sijausoma huo uzi. Ni zaidi ya mwaka nampita tušŸ˜…šŸ˜…šŸ˜…. Nimeshindwa hata kwa kujilazimisha
Hatari sana,
Mie kwa sasa nashinda jukwaa la Siasa hivo haya majukwaa mengine napita juu juu tu
 
Mwaka 2017, mimi na familia yangu tulihamia Canada kwa matumaini ya maisha bora na ya utulivu. Hata hivyo, baada ya kufika, tulikumbana na changamoto kubwa kutoka kwa baadhi ya Wakongo wenzetu tuliowakuta hapa. Walitusambaratisha kupitia fitna na chuki walizozusha baada ya kuona familia yetu ni kubwa, yenye watoto wengi wa kiume. Walihisi tukiwa na mshikamano, tungeweza kufanikiwa haraka kuliko wao.

Kwa bahati mbaya, walifanikiwa kuchonganisha wazazi wetu hadi baba akaondoka, akatuacha tukiwa bado wageni katika mazingira tusiyoyafahamu. Serikali ilisitisha misaada yote ya kijamii kwa sababu ya hali hiyo ya kifamilia. Wakati huo, mimi nikiwa na umri wa miaka 17 na bado shuleni, nililazimika kuacha masomo ili nianze kufanya kazi na kusaidia mama pamoja na wadogo zangu.

Kwa neema ya Mungu, mama mmoja Mzungu ambaye mtoto wake alikuwa rafiki wa dada yangu, alikuja kutuonyesha upendo na msaada mkubwa. Hapo ndipo tulianza kujisimamia tena taratibu.

Leo, baada ya miaka mingi, baba amerudi akiwa hana makazi, hana kazi, na hana msaada. Alienda kuishi na mwanamke mwingine ambaye baadaye alimfukuza. Mama naye tayari ana maisha mapya na mume mwingine. Mdogo wangu alimkataa kabisa alipomwendea.

Kwa huruma, nimempa hifadhi nyumbani kwangu, ila mke wangu hajaridhika kabisa na hali hiyo.

Nimejipata nikiwa katika wakati mgumu sana—kati ya huruma kwa baba yangu na wajibu wangu wa kulinda amani na heshima ya ndoa yangu. Sipendi kumwona baba akiendelea kuteseka, lakini pia sitaki kuvunja msingi wa familia niliyojenga kwa taabu.

Nimefanya uchunguzi wangu ana madeni kibao hawezi kupata nyumba kwasababu ya credit yake mbaya ya kutolipa madeni nashindwa kumsaidia na kwa Canada mtu hawezi kukodi nyumba mbili kwa wakati mmoja yaani situation yake ni ngumu mno kutatua
Duuh wazazi nao wakati mwingine kipengere!, Msaidie kadri uwezavyo,akipotea hamna mmbadala wa baba, mbali na Mungu pekee!
 
Baba ni baba mkuu. Fanya uwezavyo umtunze pengine bila yeye usingefika hapo.
 
Back
Top Bottom