Nashindwa kuzipenda filam za bongo....

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,885
Naona mzuka kwa watu unaongezeka

kuhusu hizi filam za bongo.....kwenye media na watu..

Sasa mimi najiuliza.kwa nini nashindwa kuzipenda hizi
filam za bongo????

Yaani nashindwa hata kutazama dakika ishirini tu ya filam hizi...
 
Hazina uhalisia
kila mrembo asiye na shule ndo ajira ya kuuza nyago
story za kuiga
too much childish
 
Ukweli ni kuwa bongo hatuna watunzi wa filamu. Kiasi fulani tuna waigizaji. Hatuna stori za maana. Nafikiria baada ya mwaka mmoja na nusua nitaandaa filamu yangu. Inshallah, nitaileta hapa wadau muichambue.
 
Naona mzuka kwa watu unaongezeka

kuhusu hizi filam za bongo.....kwenye media na watu..

Sasa mimi najiuliza.kwa nini nashindwa kuzipenda hizi
filam za bongo????

Yaani nashindwa hata kutazama dakika ishirini tu ya filam hizi...
kama ulianzaga kuangalia move za holwood toka zamani kisha uje uanze kuangalia zetu za kibongo itakuchukua muda kuzipenda.
Hii yote ni kutokana na teknologia ingawa wengi wasema stori nk, kiu kweli kasoro zipo na zinazidi kupungua siku hadi siku lakini mwisho wa siku watu wanafanisha film yenye bajeti sawa na bajeti ya tanzania na filim ya ray yenye bajeti ya 10milioni
 
Sijui kama suala ni bajeti. Kuna sinema ulaya hazina bajeti kihivyo lakini muundo wa stori unakushawishi kuwa waandaaji walichemsha bongo. Hapa Tz waandishi wa stori za movie hawana ufahamu wa kutosha. Kingine ni kuwa hatuna wataalam wa kutosha wa effects za computer.
 
Nakubaliana nawewe mkuu, lakini stori nayo sio tatizo sana, ni utaalamu tu na teknologia inafanya tushindwe kuact katika kiwango fulani
 
Nilipata kuzungumza na wahindi fulani walikuwa wanlalamika kuwa movies zinakuwa nyingi sokoni na zinafanana visa hivyo inawasumbua wao kusambaza. Stori nyingi za bongo zinazungumzia visa vya mapenzi ambapo matukio ya mapenzi kwa asili hujirudia miongoni mwa wanadamu. Katika mazingira haya tunashindwa kuendeleza mapenzi hayo hayo lakini kwa visa kama vya Titanic, Avatar au Slum Dog Millionaire. Nakusudia kuandaa filamu tofauti kidogo na zilizopo bongo kwa sasa.
 
Pamoja na matatizo yanayotajwa kama budget na mengineyo lakini still hatujawa comitted enough ktk film industry..mara zote wasanii wamekua wakikurupuka tu...unakuta mtu anaongea utadhani anaimba mashairi...yani akiona hana mbele wala nyuma ndo anakimbilia usanii...WASANII INABIDI MBADILIKE..SI KILA MTU ANAWEZA KUA MSANII..ACHENI WELEDI UCHUKUE NAFASI YAKA.,HALI IKIENDELEA HIVI MTAZIDI KUDHARAULIKA...!!
 
Nakubaliana nawe kuwa si kila mtu anaweza kuwa msanii. Inasikitisha kuwa mtu akitoka kugombea "u-miss" anaingia kuigiza. Tatizo ni movies kuwa za mapenzi pekee. Kihisia binadamu huhusisha uzuri wa mwonekano na "kupendeza" kuigiza mapenzi. Sinema zingekuwa zina maudhui tofauti,, suala la urembo wa mtu lingetumika inavyostahili.
 
kaka unapozungumzia avatar au titanic hizo ni move zilizotumia bajeti kubwa kuliko move yoyote, ni move zilizo tumia teknolojia ya hali ya juu sana, most of time ni studio na softwares angalau slam dog millioneire.
Pia lazima tujue move za mapenzi ndizo rahisi kuact kwa twknolojia yake, ningumu kuact sinema ya vita, mambo ya teknolojia, maijni, angani nk, teknolojia na bajeti inatulimiti malalamiko hayo ya wahindi ni yakibiashara zaidi kuliko uhalisia
 
Wakuu ni nani na mwenye sifa zipi ndio anapaswa kuigiza move? nakubali tatizo lipo lakini hizi lawama zingine hazina ukweli wowote.
Nina mdogo wangu wa kike walikuja kuniomba fund ya kuproduce move, nikaomba kwanza nione story script kwanza, ilikuwa ya mapenzi, nikauliza kulikoni mapenzi tu, niliambiwa na wataalamu kuwa wanatamani kuacti mambo mengine lakini kamera, teknolojia, bajeti, utaalamu na mtu wa kufinance na ategemee rejesho la pesa yake ndio utata unapokuwa.
Kwa mazingira ya kamera zilizopo, wataalamu wa it, bajeti ningumu kutengeneza move za action, vita nk
 
kaka unapozungumzia avatar au titanic hizo ni move zilizotumia bajeti kubwa kuliko move yoyote, ni move zilizo tumia teknolojia ya hali ya juu sana, most of time ni studio na softwares angalau slam dog millioneire.
Pia lazima tujue move za mapenzi ndizo rahisi kuact kwa twknolojia yake, ningumu kuact sinema ya vita, mambo ya teknolojia, maijni, angani nk, teknolojia na bajeti inatulimiti malalamiko hayo ya wahindi ni yakibiashara zaidi kuliko uhalisia

Nakubaliana nawe mkuu. Nitajaribu kufanya jaribio la hatari, kuandaa sinema ya vita ama matukio makubwa kama katika Lord of the Rings na Chronicles of Narnia. Nitajaribu.
 
Mkuu labda ukodishe director kutoka mbele, akina ray na mtitu hawa wezi kudirect move kama Lord of the rings na Chronicles, wanatumia kamera mm13 hugusi bei yake, kuna wakati nilifikiria kuandaa move ya vita ya kagera, unamega sehemu ya ilivyokuwa lakini mmmmh
 
Actually katika movie yangu kitu ambacho sitafanya ni kushika camera pekee lakini kuanzia story, script, storyboard, directing, special effects (physical effects)/makeup , visual effects, editing, costume design, subtitling, cover design na production nitafanya mwenyewe.Ni kazi ngumu lakini kwa movie ya kwanza itabidi nifanye hivyo ili kuhakikisha inakuwa kwa namna ninavyofikiri, lakini pia mimi bado underground hivyo ni vigumu kuaminiwa kwa masuala ya filamu. Kwa sasa najifua ili baada ya mwaka mmoja na nusu au miwili niwe na uwezo huo.
 
binafsi mimi naona wanajitahidi.... tukiangalia tulipotoka michezo redioni, kina mzee ,majuto, mzee small.. wanajitahidi sana .. wanahitaji small adjustments .. utakuta kipande hakina maana kinawekwa muda mrefu wakiwa wamekaa kwenye sofa tu .. huku mziki ukipiga background pale ndipo ninapoona wanachemka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom