Mi pia sizipendi kwa sababu
1. scenes zinachukua muda mrefu sana, zingine hazina connection na story yenyewe.
mfano wanaweza kuonesha mtu anatoka ndani ya nyumba, anamsalimia mfanya kazi, anamuuliza habari za nyumbani, anapanda gari, anafunguliwa geti, anatoka getini reverse, anabadili gia, anaeda forward,
anatembeza gari, wanaonesha sehem mbali mbali za dar, anafika aliko kua anaenda, anapiga honi, anafunguliwa geti, anamuuliza askari kama mama yupo, anapewa jibu, anapaki gari,
anapiga hodi, anafunguliwa, wanaulizana habari, anakaribishwa, anakaribishwa tena, anapewa kiti, anaulizwa atakunywa nini, anajibu, analetewa kinywaji etc...
Hii yote inaonesha wanataka kuongeza scenes ili wauze part one, part two na part three for the budget ya movie moja. Kuna rafiki yangu hua anazipiga editing, alafu ndio analeta tuangalie. movie tatu zinatosha in 120 min.
2. Story nyingi ni za kijinga. mapenzi, uchawi, roho mbaya ya watu fulani etc. hakuna entertainment yoyote!
3. wanatumia soundtrack visivyo. yaani unakuta wanapiga "my heart will go on" wakati huo hu wanaonesha mtu kawehuka anatembea hovyo barabarani... sasa vinahusiana vipi? hawawezi kupiga instrumentals? au wapige za kiafrica basi...Hovyoooo