Nashindwa kusahau kabisa hili jambo linaniumiza

Inaendelea

Mzee aliporudi kutoka safarini akanichukua tukarudi wote nyumbani akawa ananiuliza kwanini nimetoroka nyumbni nikamueleza mama alitaka kunipiga hivyo nikaogopa na kuondoka Mzee alinibembeleza na maneno ya kitoto.. safari hii kidogo mzee alikaa nyumbni hakuwa na safari safari zaidii ya kwenda kazini

Nyumba tuliyokuwa tunakaa ni kota nimesahau jina ilivyokuwa ikiitwa ila kwa wale wa TMA wanafahamu hatukuwa tunakaa maghorofani wala mabatini ni zile nyumba za peke ake peke ake.. Yule mama alijulikana mpk kambini kuwa ana roho mbaya nakumbuka kuna siku alinipiga sana mpk akajichapa mwenyewe na bomba la maji maana nilikwepa aliumia mkono akakasirika akanifukuza nyumbani akiniambia nikamfuate mama yangu.. Baba alikuwa yupo kazini, alinitupia nguo nnje ambazo zilikuwa kwenye shangazi kaja na kufunga mlango, ilibidi niondokee nyumbani nikaelekea kazini kwa Mzee maana sikujua pa kumpata mama

Yaani kwa nilivyokuwa nilikuwa kama mtoto wa mtaani.. Nilifika kazini kwa Mzee pale getini walinioji maana nilikuwa mtoto hawakuweza kunifanya chochote nikawatajia jina la Mzee maana Mzee alikuwa anajulikana walinipeleka moja kwa moja.. Mzee wangu baada ya kuniona alinipeleka sehemu nikamsubiria baadae tukaondoka wote hatukuenda nyumbani moja kwa moja tulipitia Bar

Mzee alikuwa mnywaji ila sio mlevi ila siku ile nilishuhudia akilewa, alikuwa na rafiki yake pale bar.. Mimi walinitafutia sehemu yangu ya kukaa huku wenyewe wakibaki wakipiga story mimi nilikuwa nawaona ila siwasikii wanachoongea

Kwa mara ya kwanza nilimuona Mzee wangu analia huku mwenzie akimpigapiga mabega kwa wakati huo sikujuaa analilia nini maana sikuwa nasikia wanachoongea… Tulikaa na Mzee pale mpk usiku tukarudi nyumbani.. tukiwa njiani Mzee alikuwa akiniambia ananipenda sana nivumilie tu ananitafutia shule ya bweni nisikae nyumbani… Tulifika nyumbani nakumbuka nilikuwa nimesinzia akanibeba na kunilaza kitandani alivyotoka tu Mimi nikashuka kulala chini maana yule mama alinikataza kulala kitandani akisema naozesha godoro lake kwa kujikojolea…. Kumbe Mzee alirudi kuniangalia akakuta nimelala chini a kaniuliza kwanini nimeshuka kitandani nikamwambia mama ananikaza kulala kitandani nitakojoa Mzee alikunjaa suraa akaniambia Hakuna kulala chini nilale hapo hapo yeye akaenda chumbani nikawa nasikia wanagombana

Maisha yaliendelea nikiwa nasubirii kupelekwa shule ya bweni bado nilikuwa nateswa mno yule mama alikuwa ananifinya usoni akisema kuwa nina ringa na rangi kwa vile mama yangu ni mzuri basi ataniharibu sura hiyo na Hakuna wa kunipenda [emoji24][emoji24] Yule mama alikuwa ananifinya usoni anatoa mpk ngozi kiasi kwamba ilinifanya nisijiamini katika ukuaji wangu nashukuru kwa sasa zinaonekana japo kwa mbali sana…

Yule mama alikuwa hana aibu alikuwa anatembea na rafiki za baba pale Kota ilikuwa ni aibu… Walikuwa wakigombana na Mzee mpk majirani wanajua alikuwa anatembea na madereva wa Mzee… Mzee kila siku anabdadilisha madereva
Muda ambao Mzee anakuwa safarini kikazi yule mama alikuwa anaingiza wanaume ndani na Mimi nilikuwa nawaona ananiambia nikisema ataniua na Mimi kwa kuogopa sikuwai kusema chochote

Siku moja usiku nilisikia Mzee wangu wanagombana na mama wa kambo kuhusu mimi kuwa siwezi kwenda hiyo shule na watoto wake wabaki hapo nitafute shule nyinginee yaani kwa maana huyo mama alitaka niende shule anayotaka yeye…

Muda ulienda dada angu ilirudi likizo.. ukweli nampenda mno dada angu sijui nisemeje kwa sababu ni mtetezi wangu siku zote… alipokuwa yupo nyumbani basi niliishi kwa raha.. sikuwa nafanyishwa makazi maana nilikuwa naambiwa nifue nguo za wadogo zangu na huyo dada angu kila siku nawafulia na kuzinyoosha hata Kama nimesahau kuzifua ninaamshwa usiku kwenda kuzifua Yule mama alininyanyasa sana

Kwaiyo dada yangu alipokuwepo ilikuwa ndio pona yangu.. Dada yangu ni mpole na sio muongeaji ila likifika suala kuhusu mimi anacharuka alikuwa ananiambia chochote wakikwambia Hakuna kufanya kuna dada wa kazi analipwa mshahara na huyo ndugu yangu mwinginee ni mkubwa anaweza kujifulia mwenyewe

Nakumbuka usiku wa siku dada aliyorudi kutoka shule tukiwa tumelala.. dada yangu ambae kanizidi mwaka 1 akanituma niende nnje nikamuanulie soksi zake hapo ilikuwa saa 4 dada yangu a kamwambia aende mwenyewe mimi sio mfanyakazi wake basi ikazuka vurugu akaanza kumtukana dada… kumbuka dada ndio first born hivyo ametuzidi sana akawa anamdharau ikabidi dada angu ampige kofi la uso akaanza kupiga kelele kumwita mama yake huku akimtukana dada…. Mama yake alivyokuja wakaanza kupigana na dada kwamba kwanini ampige mwanae ikawa ugomvi mkubwa na Hakuna wa kuamua maana tuliobaki wote watoto na Mzee alikuwa safarini

Mungu si athumani siku ile kumbe Mzee alikuwa ndio anarudi safari ameingia amechoka halafu kakuta kuna ugomvi na yule mama kashika kisu anataka kumchoma sister… ikabidi Mzee amnyang’anye kile kisu
Yule mama kuona hivyo akaenda kuchukua chupa ya bia ili kunipiga nayo alivyoirusha mimi niliiona nikaikwepa bahatii mbaya ikampata mtoto wake wa kiume ambae ni mdogo wangu… likaanza balaa lingine kwamba sister kasababisha mtoto wake akifa atamuua akawa anamwambia baba amuondoe dada pale nyumbani kwanini anamtetea sana dada au ni hawara yake aliongeaa maneno machafu

Ilibidi Mzee amtoe sister akaenda lipa guest akalala huku… Yule Mama akasema hataki kumuona kabisa dada pale nyumbani atafute pa kukaa ikabidi baba yangu amuombee sister kwa rafiki yake ambae ni kabila moja hivyo tunamwita shangazi ndio kulala na kukaa kwake

Maisha ya manyanyaso yaliendelea kuna siku tena alinipiga sana akatishia kunichoma pasi nikakimbia kwa majirani jioni yake watoto wakawa wanazunguka nyumba wanaimba nyimbo ya kumwambia aache roho mbaya… nafikiri walitumwa na wazazi wao… kuna siku Mzee wangu alinipeleka kwenye shule inaitwa Joseph Primary school Arusha nikafanya interview na nilipitaa maana niliambiwa nijiandaee kwenda shule nimefaulu… nikashangaa nimepelekwa kwa mtu mwingine kumbe alikuwa mwalimu mkuu wa shule ninayoenda… Ajabu si kwenda kule Joseph primary nilipelekwa shule nyingine ipo kijijini huko inaitwa Engaruka Juu primary… ile shule ilikuwa mbaya kwa kipindi kile sijui kwa sasa hivi

Ila nashukuru nilipumzika kwa muda kwa kukaa mbali na home hata likizo sikuwa naenda nyumbani nilikuwa nikikaa kwa mwalimu mkuu… Nashukuru Mungu yule mwalimu alinipenda pamoja na mke wake kwani nilikuwa nawasaidia kipindi cha likizo kuwalelea mtoto wao… Japo napo nilinusurika kubakwa na mwanaume aliekuwa akikaa pale sikumbuki alikuwa nani yao…

Sikumbuki jina vizuri alikuwa anaitwa mwalimu Olais au Alois ila alikuwa na binti yake wa kwanza akiitwa Angel sikumbuki walipo ila mara ya mwisho nakumbuka walikuwa wakiishi Ng’aramtoni Mungu akubariki sana kama utasoma hapa nakuomba unitafute japo nikushukuru kwa mdomo maana ulinilea kama mtoto wako

Muda ulienda mpk pale nilipoambiwa kwamba nirudi nyumbani nikiwa shule hapo nikawa nashangaa kuna nini maana sio muda wa likizo halafu kwanini sirudi na wanafunzi wenzangu ila sikuwa na namnaa yule mwalimu ndio kama mzazi wangu sasa alinipeleka nyumbani kwake nikaa kama siku mbili nikaja kupata taarifa za msiba mwa mzee wangu

Mzee wangu alifariki tarehe 4/9 mimi napata taarifaa baada ya mazishi yaani wiki imeishaa kumbe yule mama hakutaka sisi tujue kila akiulizwa nilipo hasemii maana Hakuna mtu alikuwa akifahamu ninaposoma zaidi yake na Mzee hivyo taarifa ya msiba alifika kwa kuchelewa.. na mama yangu aliambiwa na mshemeji zake… sikumzika baba yangu wala kuhuzuria msiba…

Kurudi nyumbani nikakuta waombolezaji tu wapo yule mama na watoto wake hawapo.. taarifa iliyokuwepo ni kuwa alienda kijijini walivyozika tu akageuza siku ile ile akawaambia bibi na babu yangu mzaa baba hawezi kukaa na manyani anarudi mjini hilo neno MPa Leo ukienda. Kijijini ndugu wa baba lazima waliogee wanamchukia sana huyo mama wa kambo…

Kumbe nia yake ya kurudi mjini ilikuwa aje kukusanya vitu vyote na kuondoka navyo… Yule mama ana roho mbaya alibeba kila kitu cha thamani pale nyumbani akapeleka anapopajua yeye aliuza gari pikipiki baiskel na hakutoa hata senti alifanya ukatili sana mpk nguo za marehemu alienda kugawa kwao ndugu wa marehemu hakupata chochote

Mambo yalienda cha kushukuru Mzee aliacha wosia na watoto wake wote tulikuwemo msimamizi wa mirathi mkuu aliandikwa dada yangu… yule mama hakuwa na aibu alitusumbua kwenye mirathi kiasi kwamba ilichukua miaka 7 mpk kugawana mirathi… alikuwa anataka tugawane kila kitu yeye apate zaidi alijengewa nyumba ila alitaka na nyumba nyingine ambayo ni yetu tuiuzee tugawane kwa kuwa mama ni muungwana tukainunua sisi ile nyumba kwa hela za mirathii

Mpk sasa Hakuna undugu uliopo kati yetu na watoto wake… watoto hawawwjui ndugu za baba yao sisi ndio tunaojulikana huko kwa Baba na wanatupenda

Hayo ni machache kati ya mengi alionifanyia hakutaka nifanikiwe Mungu ni mwema katika watoto wake Hakuna alienifikia nilipo kielimu na kimaisha… watoto wake wananipigia simu kuniambia tusahau yaliyopita mimi nawajibu nishawasehe ila kila nikikumbuka mama yao alivyoninyanyasa roho inaniuma sana… nawaza kama Mzee asingefariki uenda ningeanza mimi kufa maana yule mama angeweza kuniua

Ushaurii wanaume mnaozaa watoto kwa mama tofauti kuweni makini raha zenu zisifanye watoto wenu wateseke… mtoto hawezi kushitak kokote haswa kama anatishiwa
Jitahidi watoto wenu wawe wa mama mmoja angalau kuna msingi mzuri

Mimi niliteswa sana kama ingekuwa ni video ungeona ninayofanyiwa sidhani kama umgestahimili

Mwishoo
Daaaah pole sana kwa mapito hayo. Siku zote huwa nasema ukifanya mabaya unajifanyia mwenyewe na ukifanya mema unajifanyia mwenyewe. Huwa nashangaaa mtu umeingia kwenye ndoa ambayo umemkuta mwenzako na watoto huo ujasiri wa kutesa watoto wa wenzio unaupata wapi. Khaaaa jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu
 
Nililelewa na mama wa kambo watatu tofauti. Sikuweka rohoni baya lolote nililotendewa. Kuna wengine niliwadeliti na kuna mmoja hata akiniambia anaumwa jinonitawasha gari kumpeleka hospitali. Wote hao wameshaachana na mzee.

Wa mwisho nilimpenda sana na alinipenda pia. Siku ameachana na Mzee nilikosa raha karibu mwezi mzima.

Namshukuru Mungu maisha yanaendelea vizuri sana upande wangu nadhani ni kutokana na mikono niliyopitia pia.

Uzuri mama wakambo wengi uwa hawadili sana na watoto wa kiume
 
Ubaya ni kuwa watu hao ni wachache sana kukuta mtu kalelewa na wazazi wote wawili

Ila naamini ndoa haina mtaalamu ukienda vizuri na Mungu utaishi na yatima vzr mpk hiyo dhana uaisahau
Angalau kupunguza maumivu aliyelelewa na wazazi wake wawili wenye ndoa yupo kwenye chain muunganiko wa kiMungu tofaut na asiye wanakuwa na shida ya saikolojiko balance
 
Nililelewa na mama wa kambo watatu tofauti. Sikuweka rohoni baya lolote nililotendewa. Kuna wengine niliwadeliti na kuna mmoja hata akiniambia anaumwa jinonitawasha gari kumpeleka hospitali. Wote hao wameshaachana na mzee.

Wa mwisho nilimpenda sana na alinipenda pia. Siku ameachana na Mzee nilikosa raha karibu mwezi mzima.

Namshukuru Mungu maisha yanaendelea vizuri sana upande wangu nadhani ni kutokana na mikono niliyopitia pia.

Uzuri mama wakambo wengi uwa hawadili sana na watoto wa kiume

Hapo mwisho ndio umemaliza angalau mama wa kambo wa sasa ni wa kidigitarii yaani usasa mwinginee hata akikuchukia hawezi kukuonyesha ila mama wa kambo wa kuanzia 2010 kushuka chini ni balaa yaani ni moto
 
Angalau kupunguza maumivu aliyelelewa na wazazi wake wawili wenye ndoa yupo kwenye chain muunganiko wa kiMungu tofaut na asiye wanakuwa na shida ya saikolojiko balance

Labda ila mimi kwa upande wangu Sina kisasi ndani yangu maana mama yangu aliponichukua ilikuwa ni kunifariji na kanisani kwa sana ni vile tu tunasamehe ila hatusahau
 
Hii ni historia ya maisha yangu na mambo yaliyonisibu

Mimi ni mtoto wa mwisho kuzaliwa kwenye tumbo la mama yangu kati ya watoto wa5, baba yangu alifariki mwaka 2007 nikiwa darasa.. Mama yangu ni mke wa kwanza kwani baba yangu alikuwa muislam alioa wake watatu… hivyo walitengana na mama na sisi tulibaki kulelewa na mama yetu

Nakumbuka ilikuwa mwaka 2005 Mama yangu mzazi aliuguliwa na mama yake yaani bibi yetu ikamlazimu kusafiri kwenda kwao kwaajili ya kumuuguza bibi hivyo alituchukua na kutupeleka kwa baba mkoa X wakati huo baba alikuwa akiishi na mke wake wa mwisho ambae aliezaa nae watoto 3 wawili wadogo kwangu mmoja ni mkubwa kwangu tulipishana mwaka 1

Safari mpk kwa Mzee mkoa X tulifika na kupokelewa tukiwa mama, dada yangu na kaka yangu… mama akaeleza kilichomsibu na kuwa hawezi kwenda na sisi wote huko kijijini inabidi atuache hapo kwa Mzee atatupitia akirudii..

Ile siku ninaikumbuka sana yule mama yetu wa kambo alimwambia Mzee hawezi kubaki na mtoto wa mtu tena haswa alimkata Kaka yangu kwa madai kuwa kaka yangu ndio kila kitu kwa Mzee yaani anapendwa sana ukizingatia wakiume kwetu ni wawili tu na yeye ndio mkubwa akaapa kuwa Kama mama atamuacha kaka pale nyumbani angemuua kwa kumuwekea sumu kiukweli mama yangu mzazi alilia sana ukizingatia hakuwa na uwezo alimtegemea mzee nikikumbuka hilo tukio huwa linaniumiza sana

Yule mama wa kambo alisema ni bora nibaki mimi maana mimi ni mdogo ananimudu… baba sijui Kama alikuwa na akili zake timamu Mungu amrehemu alisema tu dada yangu atapelekwa shule ya bweni.. mimi ningebaki kusubiri kuanza shule na bro wangu ataondoka na mama…. Basi mama hakuwa na namna aliondoka na kaka angu akaniacha na sister

Dada nae alikaa kwa muda mwisho akapelekwa shule ya bweni nikabaki mimi… Aisee ukweli nikikumbuka Yale maisha ni afadhari Mzee alifariki ili mimi nipone na hayo mazingira

Maisha yakaanza mimi na ndugu zangu na huyo mama wa kambo.. Yule mama hakuwa kunipenda hata mara moja alikuwa ananinyima chakula, mavazi na hata shule alikuwa akinikataza kwenda

Hapo Mzee wangu hakuwepo maana Mzee wangu alikuwa kwenye system pale TMA so alikuwa anasafiri mara kwa mara anaweza akaenda akaa hata miezi6 ndio anarudi home

Nilikuwa nalia jikoni wenzangu wanalia sebuleni alikuwa akinipimia chakula sishibi na kuninyima maji ya kunywa usiku nisinywe sababu nilikuwa najikojolea[emoji45][emoji45] ukweli nilikuwa nakojoa lakini ni kwasababu ya uoga maana wakati nakaa na mama niliacha kukojoa nikiwa na mwaka 2 tu hata kitandani sikojoi.. hii tabia ilianzia kwa huyo mama wa kambo..

Katika maisha ambayo nikiyakumbuka huwa naumia sana ni hayo yule mama alinitesa sana alinipiga Kama ng’ombe akitumia mpira ule wa kukingia maji kunichapia hakuwai kutumia fimbo..alikuwa ananitukana na kuniita majina mabaya wakanitungia majina yeye na watoto wake wananiita SIMBILISI huwezi amini hadi dada wa kazi alikuwa ananiita hilo jina.. wakati mwingine walikuwa wakiniambia nina macho makubwa kama rungu nilinyanyaswa sana…ilifikia kipindi shule sionekani walimu wanatuma barua anasoma anachana nakumbuka nilikuwa darasa la kwanza alichoma nguo zangu za shule viatu madaftari nikabaki sina chochote cha shule nikawa siendi shule wenzangu wanaenda mimi nipo nyumbani na tunasoma shule moja..

Nakumbuka hiyo siku nilitoroka kwenda shule kufika walimu wananiuliza kwanini nimekuja bila unform nikawaeleza mama kazichoma ikabidi wamwite ndugu yangu kumuuliza akasema ni kweli mama kachoma ikabidi mwalimu aongozane na Mimi mpk home yule mama alimfukuza mwalimu kama mbwa na Mimi kilichofatia niliambiwa ni kupigwa,, kuona hivyo ikabidi nitoroke nikaenda kwa rafiki za baba nilikaa huko karibu miezi3 hakuwai kunitafuta mpk baba alivyorudi ndio alinifuata kumbuka mambo yote yanatokea yeye hayupo yupo nnje ya nchi kipindi hicho nakumbuka alikuwa Ethiopia ila alipokuwa akirudi alikuwa anaambiwa na majirani ila sikuona anachokifanya

Mzee alipokuwa akirudi angalau nilipata raha kidogo alituletea Zawadi kila mtu mimi na mwenzangu wa kike tuliletewa vitu vya kufanana kama ni nguo au viatu tofauti ni rangi tu.. ukweli tulikuwa na maisha mazuri ikizingatia Mzee walikuwa na wadhifa kazini nakumbuka enzi za kikwete alikujaga TMA tukaenda kupata nae chakula enzi hizo

Inaendelea
TMA ya mamlaka ya hali ya hewa?
 
Inaendelea

Mzee aliporudi kutoka safarini akanichukua tukarudi wote nyumbani akawa ananiuliza kwanini nimetoroka nyumbni nikamueleza mama alitaka kunipiga hivyo nikaogopa na kuondoka Mzee alinibembeleza na maneno ya kitoto.. safari hii kidogo mzee alikaa nyumbni hakuwa na safari safari zaidii ya kwenda kazini

Nyumba tuliyokuwa tunakaa ni kota nimesahau jina ilivyokuwa ikiitwa ila kwa wale wa TMA wanafahamu hatukuwa tunakaa maghorofani wala mabatini ni zile nyumba za peke ake peke ake.. Yule mama alijulikana mpk kambini kuwa ana roho mbaya nakumbuka kuna siku alinipiga sana mpk akajichapa mwenyewe na bomba la maji maana nilikwepa aliumia mkono akakasirika akanifukuza nyumbani akiniambia nikamfuate mama yangu.. Baba alikuwa yupo kazini, alinitupia nguo nnje ambazo zilikuwa kwenye shangazi kaja na kufunga mlango, ilibidi niondokee nyumbani nikaelekea kazini kwa Mzee maana sikujua pa kumpata mama

Yaani kwa nilivyokuwa nilikuwa kama mtoto wa mtaani.. Nilifika kazini kwa Mzee pale getini walinioji maana nilikuwa mtoto hawakuweza kunifanya chochote nikawatajia jina la Mzee maana Mzee alikuwa anajulikana walinipeleka moja kwa moja.. Mzee wangu baada ya kuniona alinipeleka sehemu nikamsubiria baadae tukaondoka wote hatukuenda nyumbani moja kwa moja tulipitia Bar

Mzee alikuwa mnywaji ila sio mlevi ila siku ile nilishuhudia akilewa, alikuwa na rafiki yake pale bar.. Mimi walinitafutia sehemu yangu ya kukaa huku wenyewe wakibaki wakipiga story mimi nilikuwa nawaona ila siwasikii wanachoongea

Kwa mara ya kwanza nilimuona Mzee wangu analia huku mwenzie akimpigapiga mabega kwa wakati huo sikujuaa analilia nini maana sikuwa nasikia wanachoongea… Tulikaa na Mzee pale mpk usiku tukarudi nyumbani.. tukiwa njiani Mzee alikuwa akiniambia ananipenda sana nivumilie tu ananitafutia shule ya bweni nisikae nyumbani… Tulifika nyumbani nakumbuka nilikuwa nimesinzia akanibeba na kunilaza kitandani alivyotoka tu Mimi nikashuka kulala chini maana yule mama alinikataza kulala kitandani akisema naozesha godoro lake kwa kujikojolea…. Kumbe Mzee alirudi kuniangalia akakuta nimelala chini a kaniuliza kwanini nimeshuka kitandani nikamwambia mama ananikaza kulala kitandani nitakojoa Mzee alikunjaa suraa akaniambia Hakuna kulala chini nilale hapo hapo yeye akaenda chumbani nikawa nasikia wanagombana

Maisha yaliendelea nikiwa nasubirii kupelekwa shule ya bweni bado nilikuwa nateswa mno yule mama alikuwa ananifinya usoni akisema kuwa nina ringa na rangi kwa vile mama yangu ni mzuri basi ataniharibu sura hiyo na Hakuna wa kunipenda [emoji24][emoji24] Yule mama alikuwa ananifinya usoni anatoa mpk ngozi kiasi kwamba ilinifanya nisijiamini katika ukuaji wangu nashukuru kwa sasa zinaonekana japo kwa mbali sana…

Yule mama alikuwa hana aibu alikuwa anatembea na rafiki za baba pale Kota ilikuwa ni aibu… Walikuwa wakigombana na Mzee mpk majirani wanajua alikuwa anatembea na madereva wa Mzee… Mzee kila siku anabdadilisha madereva
Muda ambao Mzee anakuwa safarini kikazi yule mama alikuwa anaingiza wanaume ndani na Mimi nilikuwa nawaona ananiambia nikisema ataniua na Mimi kwa kuogopa sikuwai kusema chochote

Siku moja usiku nilisikia Mzee wangu wanagombana na mama wa kambo kuhusu mimi kuwa siwezi kwenda hiyo shule na watoto wake wabaki hapo nitafute shule nyinginee yaani kwa maana huyo mama alitaka niende shule anayotaka yeye…

Muda ulienda dada angu ilirudi likizo.. ukweli nampenda mno dada angu sijui nisemeje kwa sababu ni mtetezi wangu siku zote… alipokuwa yupo nyumbani basi niliishi kwa raha.. sikuwa nafanyishwa makazi maana nilikuwa naambiwa nifue nguo za wadogo zangu na huyo dada angu kila siku nawafulia na kuzinyoosha hata Kama nimesahau kuzifua ninaamshwa usiku kwenda kuzifua Yule mama alininyanyasa sana

Kwaiyo dada yangu alipokuwepo ilikuwa ndio pona yangu.. Dada yangu ni mpole na sio muongeaji ila likifika suala kuhusu mimi anacharuka alikuwa ananiambia chochote wakikwambia Hakuna kufanya kuna dada wa kazi analipwa mshahara na huyo ndugu yangu mwinginee ni mkubwa anaweza kujifulia mwenyewe

Nakumbuka usiku wa siku dada aliyorudi kutoka shule tukiwa tumelala.. dada yangu ambae kanizidi mwaka 1 akanituma niende nnje nikamuanulie soksi zake hapo ilikuwa saa 4 dada yangu a kamwambia aende mwenyewe mimi sio mfanyakazi wake basi ikazuka vurugu akaanza kumtukana dada… kumbuka dada ndio first born hivyo ametuzidi sana akawa anamdharau ikabidi dada angu ampige kofi la uso akaanza kupiga kelele kumwita mama yake huku akimtukana dada…. Mama yake alivyokuja wakaanza kupigana na dada kwamba kwanini ampige mwanae ikawa ugomvi mkubwa na Hakuna wa kuamua maana tuliobaki wote watoto na Mzee alikuwa safarini

Mungu si athumani siku ile kumbe Mzee alikuwa ndio anarudi safari ameingia amechoka halafu kakuta kuna ugomvi na yule mama kashika kisu anataka kumchoma sister… ikabidi Mzee amnyang’anye kile kisu
Yule mama kuona hivyo akaenda kuchukua chupa ya bia ili kunipiga nayo alivyoirusha mimi niliiona nikaikwepa bahatii mbaya ikampata mtoto wake wa kiume ambae ni mdogo wangu… likaanza balaa lingine kwamba sister kasababisha mtoto wake akifa atamuua akawa anamwambia baba amuondoe dada pale nyumbani kwanini anamtetea sana dada au ni hawara yake aliongeaa maneno machafu

Ilibidi Mzee amtoe sister akaenda lipa guest akalala huku… Yule Mama akasema hataki kumuona kabisa dada pale nyumbani atafute pa kukaa ikabidi baba yangu amuombee sister kwa rafiki yake ambae ni kabila moja hivyo tunamwita shangazi ndio kulala na kukaa kwake

Maisha ya manyanyaso yaliendelea kuna siku tena alinipiga sana akatishia kunichoma pasi nikakimbia kwa majirani jioni yake watoto wakawa wanazunguka nyumba wanaimba nyimbo ya kumwambia aache roho mbaya… nafikiri walitumwa na wazazi wao… kuna siku Mzee wangu alinipeleka kwenye shule inaitwa Joseph Primary school Arusha nikafanya interview na nilipitaa maana niliambiwa nijiandaee kwenda shule nimefaulu… nikashangaa nimepelekwa kwa mtu mwingine kumbe alikuwa mwalimu mkuu wa shule ninayoenda… Ajabu si kwenda kule Joseph primary nilipelekwa shule nyingine ipo kijijini huko inaitwa Engaruka Juu primary… ile shule ilikuwa mbaya kwa kipindi kile sijui kwa sasa hivi

Ila nashukuru nilipumzika kwa muda kwa kukaa mbali na home hata likizo sikuwa naenda nyumbani nilikuwa nikikaa kwa mwalimu mkuu… Nashukuru Mungu yule mwalimu alinipenda pamoja na mke wake kwani nilikuwa nawasaidia kipindi cha likizo kuwalelea mtoto wao… Japo napo nilinusurika kubakwa na mwanaume aliekuwa akikaa pale sikumbuki alikuwa nani yao…

Sikumbuki jina vizuri alikuwa anaitwa mwalimu Olais au Alois ila alikuwa na binti yake wa kwanza akiitwa Angel sikumbuki walipo ila mara ya mwisho nakumbuka walikuwa wakiishi Ng’aramtoni Mungu akubariki sana kama utasoma hapa nakuomba unitafute japo nikushukuru kwa mdomo maana ulinilea kama mtoto wako

Muda ulienda mpk pale nilipoambiwa kwamba nirudi nyumbani nikiwa shule hapo nikawa nashangaa kuna nini maana sio muda wa likizo halafu kwanini sirudi na wanafunzi wenzangu ila sikuwa na namnaa yule mwalimu ndio kama mzazi wangu sasa alinipeleka nyumbani kwake nikaa kama siku mbili nikaja kupata taarifa za msiba mwa mzee wangu

Mzee wangu alifariki tarehe 4/9 mimi napata taarifaa baada ya mazishi yaani wiki imeishaa kumbe yule mama hakutaka sisi tujue kila akiulizwa nilipo hasemii maana Hakuna mtu alikuwa akifahamu ninaposoma zaidi yake na Mzee hivyo taarifa ya msiba alifika kwa kuchelewa.. na mama yangu aliambiwa na mshemeji zake… sikumzika baba yangu wala kuhuzuria msiba…

Kurudi nyumbani nikakuta waombolezaji tu wapo yule mama na watoto wake hawapo.. taarifa iliyokuwepo ni kuwa alienda kijijini walivyozika tu akageuza siku ile ile akawaambia bibi na babu yangu mzaa baba hawezi kukaa na manyani anarudi mjini hilo neno MPa Leo ukienda. Kijijini ndugu wa baba lazima waliogee wanamchukia sana huyo mama wa kambo…

Kumbe nia yake ya kurudi mjini ilikuwa aje kukusanya vitu vyote na kuondoka navyo… Yule mama ana roho mbaya alibeba kila kitu cha thamani pale nyumbani akapeleka anapopajua yeye aliuza gari pikipiki baiskel na hakutoa hata senti alifanya ukatili sana mpk nguo za marehemu alienda kugawa kwao ndugu wa marehemu hakupata chochote

Mambo yalienda cha kushukuru Mzee aliacha wosia na watoto wake wote tulikuwemo msimamizi wa mirathi mkuu aliandikwa dada yangu… yule mama hakuwa na aibu alitusumbua kwenye mirathi kiasi kwamba ilichukua miaka 7 mpk kugawana mirathi… alikuwa anataka tugawane kila kitu yeye apate zaidi alijengewa nyumba ila alitaka na nyumba nyingine ambayo ni yetu tuiuzee tugawane kwa kuwa mama ni muungwana tukainunua sisi ile nyumba kwa hela za mirathii

Mpk sasa Hakuna undugu uliopo kati yetu na watoto wake… watoto hawawwjui ndugu za baba yao sisi ndio tunaojulikana huko kwa Baba na wanatupenda

Hayo ni machache kati ya mengi alionifanyia hakutaka nifanikiwe Mungu ni mwema katika watoto wake Hakuna alienifikia nilipo kielimu na kimaisha… watoto wake wananipigia simu kuniambia tusahau yaliyopita mimi nawajibu nishawasehe ila kila nikikumbuka mama yao alivyoninyanyasa roho inaniuma sana… nawaza kama Mzee asingefariki uenda ningeanza mimi kufa maana yule mama angeweza kuniua

Ushaurii wanaume mnaozaa watoto kwa mama tofauti kuweni makini raha zenu zisifanye watoto wenu wateseke… mtoto hawezi kushitak kokote haswa kama anatishiwa
Jitahidi watoto wenu wawe wa mama mmoja angalau kuna msingi mzuri

Mimi niliteswa sana kama ingekuwa ni video ungeona ninayofanyiwa sidhani kama umgestahimili

Mwishoo
Mdogo wangu pole sana, lakini ulivyoyasema hapa, moyoni utapata nafuu, naamini hata hapo ulipo kuna mzigo uliokuwa unakusumbua, umeshautua tayari.
 
Childhood traumas huwa zinamuandama mtu maisha yake yote hadi kaburini. Zile vitu zisikie tu.
Ni mbaya sana, asilimia 90 ya matatizo ya afya ya akili (anxiety & depression) source yake ni Childhood Traumatic experiences..

Bahati nzuri ni kwamba you can be healed na ukawa free kabisa.
Naweza kumsaidia yeyote ku release traumatic experiences za utotoni.
 
Mama wa kambo alinipenda sana kama mtoto wake wa kumzaa.
Ilifika wakati alinichukua tukaenda kukaa kwa mama yake mzazi zaidi ya siku 14. Nawapenda sana wadogo zangu ambao ni watoto wa yule mama. Yule bibi (mama yake mama wa kambo) alinipenda kama mjukuu wake wa kibaolojia. Nilikuwa nikitaka kitu nipate kwa haraka toka kwa baba namuomba mama amueleze baba. Kuna watu wana roho nzuri dunia hii.
Nasikitika nilishindwa kuhudhuria mazishi yake alipofariki nikiwa shule ya bweni mkoa wa mbali na taarifa nilichelewa kuzipata.
May her soul rest in peace.
 
Sijataka hata kimaliza baba yako alowekewa dawa mpaka asiweze kumfukuza huyo mke. Hadi nimeskia hasira.
 
Back
Top Bottom