Nashindwa kusahau kabisa hili jambo linaniumiza

Nashindwa kusahau kabisa hili jambo linaniumiza

mamamzungu Asante kwa huo ushauri. Namuomba Mungu nisipate mtoto wa nje ya ndoa. Nitapambana na huyu huyu iwe mvua iwe jua.

Familia bora ndio lengo langu kuu.
 
Mama yangu sio wa kidigitali mie ni mzee kijana kama Mshana Jr. Hiyo 2010 nilishakuwa na ndoa na hata watoto wangu wote walikuwa washazaliwa.

Basi ni wachache katika wale wengi wenye roho za kipepo
 
Ushaurii wanaume mnaozaa watoto kwa mama tofauti kuweni makini raha zenu zisifanye watoto wenu wateseke… mtoto hawezi kushitak kokote haswa kama anatishiwa
Jitahidi watoto wenu wawe wa mama mmoja angalau kuna msingi mzuri
Daah..
Ushauri mzuri
 
Ushaurii wanaume mnaozaa watoto kwa mama tofauti kuweni makini raha zenu zisifanye watoto wenu wateseke… mtoto hawezi kushitak kokote haswa kama anatishiwa
Jitahidi watoto wenu wawe wa mama mmoja angalau kuna msingi mzuri

pole sana mamamzungu
 
Pole sana...ramani ya maisha yetu iko mikononi mwa Mungu,mwanadamu anaweza chelewesha tu kwa muda,lakini mpango wa Mungu lazima utimie...wakati mwingine Mungu huyaruhusu magumu yatupate ili tuwe walimu kwa wengine.
 
Inaendelea

Mzee aliporudi kutoka safarini akanichukua tukarudi wote nyumbani akawa ananiuliza kwanini nimetoroka nyumbni nikamueleza mama alitaka kunipiga hivyo nikaogopa na kuondoka Mzee alinibembeleza na maneno ya kitoto.. safari hii kidogo mzee alikaa nyumbni hakuwa na safari safari zaidii ya kwenda kazini

Nyumba tuliyokuwa tunakaa ni kota nimesahau jina ilivyokuwa ikiitwa ila kwa wale wa TMA wanafahamu hatukuwa tunakaa maghorofani wala mabatini ni zile nyumba za peke ake peke ake.. Yule mama alijulikana mpk kambini kuwa ana roho mbaya nakumbuka kuna siku alinipiga sana mpk akajichapa mwenyewe na bomba la maji maana nilikwepa aliumia mkono akakasirika akanifukuza nyumbani akiniambia nikamfuate mama yangu.. Baba alikuwa yupo kazini, alinitupia nguo nnje ambazo zilikuwa kwenye shangazi kaja na kufunga mlango, ilibidi niondokee nyumbani nikaelekea kazini kwa Mzee maana sikujua pa kumpata mama

Yaani kwa nilivyokuwa nilikuwa kama mtoto wa mtaani.. Nilifika kazini kwa Mzee pale getini walinioji maana nilikuwa mtoto hawakuweza kunifanya chochote nikawatajia jina la Mzee maana Mzee alikuwa anajulikana walinipeleka moja kwa moja.. Mzee wangu baada ya kuniona alinipeleka sehemu nikamsubiria baadae tukaondoka wote hatukuenda nyumbani moja kwa moja tulipitia Bar

Mzee alikuwa mnywaji ila sio mlevi ila siku ile nilishuhudia akilewa, alikuwa na rafiki yake pale bar.. Mimi walinitafutia sehemu yangu ya kukaa huku wenyewe wakibaki wakipiga story mimi nilikuwa nawaona ila siwasikii wanachoongea

Kwa mara ya kwanza nilimuona Mzee wangu analia huku mwenzie akimpigapiga mabega kwa wakati huo sikujuaa analilia nini maana sikuwa nasikia wanachoongea… Tulikaa na Mzee pale mpk usiku tukarudi nyumbani.. tukiwa njiani Mzee alikuwa akiniambia ananipenda sana nivumilie tu ananitafutia shule ya bweni nisikae nyumbani… Tulifika nyumbani nakumbuka nilikuwa nimesinzia akanibeba na kunilaza kitandani alivyotoka tu Mimi nikashuka kulala chini maana yule mama alinikataza kulala kitandani akisema naozesha godoro lake kwa kujikojolea…. Kumbe Mzee alirudi kuniangalia akakuta nimelala chini a kaniuliza kwanini nimeshuka kitandani nikamwambia mama ananikaza kulala kitandani nitakojoa Mzee alikunjaa suraa akaniambia Hakuna kulala chini nilale hapo hapo yeye akaenda chumbani nikawa nasikia wanagombana

Maisha yaliendelea nikiwa nasubirii kupelekwa shule ya bweni bado nilikuwa nateswa mno yule mama alikuwa ananifinya usoni akisema kuwa nina ringa na rangi kwa vile mama yangu ni mzuri basi ataniharibu sura hiyo na Hakuna wa kunipenda [emoji24][emoji24] Yule mama alikuwa ananifinya usoni anatoa mpk ngozi kiasi kwamba ilinifanya nisijiamini katika ukuaji wangu nashukuru kwa sasa zinaonekana japo kwa mbali sana…

Yule mama alikuwa hana aibu alikuwa anatembea na rafiki za baba pale Kota ilikuwa ni aibu… Walikuwa wakigombana na Mzee mpk majirani wanajua alikuwa anatembea na madereva wa Mzee… Mzee kila siku anabdadilisha madereva
Muda ambao Mzee anakuwa safarini kikazi yule mama alikuwa anaingiza wanaume ndani na Mimi nilikuwa nawaona ananiambia nikisema ataniua na Mimi kwa kuogopa sikuwai kusema chochote

Siku moja usiku nilisikia Mzee wangu wanagombana na mama wa kambo kuhusu mimi kuwa siwezi kwenda hiyo shule na watoto wake wabaki hapo nitafute shule nyinginee yaani kwa maana huyo mama alitaka niende shule anayotaka yeye…

Muda ulienda dada angu ilirudi likizo.. ukweli nampenda mno dada angu sijui nisemeje kwa sababu ni mtetezi wangu siku zote… alipokuwa yupo nyumbani basi niliishi kwa raha.. sikuwa nafanyishwa makazi maana nilikuwa naambiwa nifue nguo za wadogo zangu na huyo dada angu kila siku nawafulia na kuzinyoosha hata Kama nimesahau kuzifua ninaamshwa usiku kwenda kuzifua Yule mama alininyanyasa sana

Kwaiyo dada yangu alipokuwepo ilikuwa ndio pona yangu.. Dada yangu ni mpole na sio muongeaji ila likifika suala kuhusu mimi anacharuka alikuwa ananiambia chochote wakikwambia Hakuna kufanya kuna dada wa kazi analipwa mshahara na huyo ndugu yangu mwinginee ni mkubwa anaweza kujifulia mwenyewe

Nakumbuka usiku wa siku dada aliyorudi kutoka shule tukiwa tumelala.. dada yangu ambae kanizidi mwaka 1 akanituma niende nnje nikamuanulie soksi zake hapo ilikuwa saa 4 dada yangu a kamwambia aende mwenyewe mimi sio mfanyakazi wake basi ikazuka vurugu akaanza kumtukana dada… kumbuka dada ndio first born hivyo ametuzidi sana akawa anamdharau ikabidi dada angu ampige kofi la uso akaanza kupiga kelele kumwita mama yake huku akimtukana dada…. Mama yake alivyokuja wakaanza kupigana na dada kwamba kwanini ampige mwanae ikawa ugomvi mkubwa na Hakuna wa kuamua maana tuliobaki wote watoto na Mzee alikuwa safarini

Mungu si athumani siku ile kumbe Mzee alikuwa ndio anarudi safari ameingia amechoka halafu kakuta kuna ugomvi na yule mama kashika kisu anataka kumchoma sister… ikabidi Mzee amnyang’anye kile kisu
Yule mama kuona hivyo akaenda kuchukua chupa ya bia ili kunipiga nayo alivyoirusha mimi niliiona nikaikwepa bahatii mbaya ikampata mtoto wake wa kiume ambae ni mdogo wangu… likaanza balaa lingine kwamba sister kasababisha mtoto wake akifa atamuua akawa anamwambia baba amuondoe dada pale nyumbani kwanini anamtetea sana dada au ni hawara yake aliongeaa maneno machafu

Ilibidi Mzee amtoe sister akaenda lipa guest akalala huku… Yule Mama akasema hataki kumuona kabisa dada pale nyumbani atafute pa kukaa ikabidi baba yangu amuombee sister kwa rafiki yake ambae ni kabila moja hivyo tunamwita shangazi ndio kulala na kukaa kwake

Maisha ya manyanyaso yaliendelea kuna siku tena alinipiga sana akatishia kunichoma pasi nikakimbia kwa majirani jioni yake watoto wakawa wanazunguka nyumba wanaimba nyimbo ya kumwambia aache roho mbaya… nafikiri walitumwa na wazazi wao… kuna siku Mzee wangu alinipeleka kwenye shule inaitwa Joseph Primary school Arusha nikafanya interview na nilipitaa maana niliambiwa nijiandaee kwenda shule nimefaulu… nikashangaa nimepelekwa kwa mtu mwingine kumbe alikuwa mwalimu mkuu wa shule ninayoenda… Ajabu si kwenda kule Joseph primary nilipelekwa shule nyingine ipo kijijini huko inaitwa Engaruka Juu primary… ile shule ilikuwa mbaya kwa kipindi kile sijui kwa sasa hivi

Ila nashukuru nilipumzika kwa muda kwa kukaa mbali na home hata likizo sikuwa naenda nyumbani nilikuwa nikikaa kwa mwalimu mkuu… Nashukuru Mungu yule mwalimu alinipenda pamoja na mke wake kwani nilikuwa nawasaidia kipindi cha likizo kuwalelea mtoto wao… Japo napo nilinusurika kubakwa na mwanaume aliekuwa akikaa pale sikumbuki alikuwa nani yao…

Sikumbuki jina vizuri alikuwa anaitwa mwalimu Olais au Alois ila alikuwa na binti yake wa kwanza akiitwa Angel sikumbuki walipo ila mara ya mwisho nakumbuka walikuwa wakiishi Ng’aramtoni Mungu akubariki sana kama utasoma hapa nakuomba unitafute japo nikushukuru kwa mdomo maana ulinilea kama mtoto wako

Muda ulienda mpk pale nilipoambiwa kwamba nirudi nyumbani nikiwa shule hapo nikawa nashangaa kuna nini maana sio muda wa likizo halafu kwanini sirudi na wanafunzi wenzangu ila sikuwa na namnaa yule mwalimu ndio kama mzazi wangu sasa alinipeleka nyumbani kwake nikaa kama siku mbili nikaja kupata taarifa za msiba mwa mzee wangu

Mzee wangu alifariki tarehe 4/9 mimi napata taarifaa baada ya mazishi yaani wiki imeishaa kumbe yule mama hakutaka sisi tujue kila akiulizwa nilipo hasemii maana Hakuna mtu alikuwa akifahamu ninaposoma zaidi yake na Mzee hivyo taarifa ya msiba alifika kwa kuchelewa.. na mama yangu aliambiwa na mshemeji zake… sikumzika baba yangu wala kuhuzuria msiba…

Kurudi nyumbani nikakuta waombolezaji tu wapo yule mama na watoto wake hawapo.. taarifa iliyokuwepo ni kuwa alienda kijijini walivyozika tu akageuza siku ile ile akawaambia bibi na babu yangu mzaa baba hawezi kukaa na manyani anarudi mjini hilo neno MPa Leo ukienda. Kijijini ndugu wa baba lazima waliogee wanamchukia sana huyo mama wa kambo…

Kumbe nia yake ya kurudi mjini ilikuwa aje kukusanya vitu vyote na kuondoka navyo… Yule mama ana roho mbaya alibeba kila kitu cha thamani pale nyumbani akapeleka anapopajua yeye aliuza gari pikipiki baiskel na hakutoa hata senti alifanya ukatili sana mpk nguo za marehemu alienda kugawa kwao ndugu wa marehemu hakupata chochote

Mambo yalienda cha kushukuru Mzee aliacha wosia na watoto wake wote tulikuwemo msimamizi wa mirathi mkuu aliandikwa dada yangu… yule mama hakuwa na aibu alitusumbua kwenye mirathi kiasi kwamba ilichukua miaka 7 mpk kugawana mirathi… alikuwa anataka tugawane kila kitu yeye apate zaidi alijengewa nyumba ila alitaka na nyumba nyingine ambayo ni yetu tuiuzee tugawane kwa kuwa mama ni muungwana tukainunua sisi ile nyumba kwa hela za mirathii

Mpk sasa Hakuna undugu uliopo kati yetu na watoto wake… watoto hawawwjui ndugu za baba yao sisi ndio tunaojulikana huko kwa Baba na wanatupenda

Hayo ni machache kati ya mengi alionifanyia hakutaka nifanikiwe Mungu ni mwema katika watoto wake Hakuna alienifikia nilipo kielimu na kimaisha… watoto wake wananipigia simu kuniambia tusahau yaliyopita mimi nawajibu nishawasehe ila kila nikikumbuka mama yao alivyoninyanyasa roho inaniuma sana… nawaza kama Mzee asingefariki uenda ningeanza mimi kufa maana yule mama angeweza kuniua




Ushaurii wanaume mnaozaa watoto kwa mama tofauti kuweni makini raha zenu zisifanye watoto wenu wateseke… mtoto hawezi kushitak kokote haswa kama anatishiwa
Jitahidi watoto wenu wawe wa mama mmoja angalau kuna msingi mzuri

Mimi niliteswa sana kama ingekuwa ni video ungeona ninayofanyiwa sidhani kama umgestahimili



Mwishoo
Painful story .....ila ashukuriwe Mungu ametenda na kutengeneza njia kwa ajili yako
 
Nimelelewa katika mazingira kama yako tofauti jinsia tu.

Mama yangu alifariki miezi mitatu baada ya kumzaa mdogo wangu wa kike, wakati huo nikiwa na miaka kama 2-3, baada ya mama kufariki baba alioa mwanamke mwingine!

Hapa sasa nikaanza kulelewa na mama wakambo!! hapo dunia ilikuwa CHUNGU kwa mateso niliyopitia (sisi wengine tunasubiri kwenda mbinguni, jehanam tumeshatoka😅)

nilikuwa natoroka lakini kutoroka kwenyewe ni kwenda kwa jirani, kesho yake ikifahamika nilipo mzee ananifuata; nae ananishushia kipigo mpaka nyumbani (sikuwa nasema sababu rasmi za kutoroka nyumbani kwa kuogopa mateso zaidi maana hata hivyo muda mwingi nilikuwa nakaa na huyo adui yangu "mama wa kambo")

Shule:
nilianza darasa la kwanza mpaka 7 nikiwa pale nyumbani, sikuwahi kufeli japo nilikuwa naenda shule mara 2/3 kwa wiki, yaani nilikuwa nafaulu kimiujiza fulani hivi 😅

pale shule ya msingi ni mm nilieonekana kama kituko flani hivi: uchafu, nimo! utoro, nimo! uchelewaji shuleni nimo! so shuleni ni kichapo, nyumbani kichapo! hata sasa hivi nikitaja jina la hiyo shule kuna watu nahisi watanijua!

Kazi mgumu ngumu zote za nyumbani zilikuwa zangu, makosa yote madogo madogo yanayojitokeza pale nyumbani nawajibishwa mimi (adhabu kama ya mwizi)

kwangu ilikuwa ni bora kwenda shule nikaadhibiwe hata na waalimu wote kuliko kushinda nyumbani.
Kwenda shule ilikuwa a big chance kwangu na mara nyingine nilikuwa naenda shule kwa kutoroka (hapa ni ile siku nimepewa taarifa kwamba "kesho hakuna kwenda shule")

nikitoka shule chakula sikuti na nikikikuta ujue kuna pilipili ya kutosha!
*kumwagiwa maji ya moto na moto wenyewe
*kulishwa ugali mabichi na kulala njaa
kufinywa mashavu na vibao bila kosa
*zikipikwa nyama zinawekewa mchuzi kwa ajili ya mtu fulani 😒😒

Nilipumua pumua baada ya kumaliza std 7 (nilipangishiwa chumba karibu na shule ya sekondari)......... ........

pamoja na hayo: pia Nashukuru Mungu sijawahi/sikuwahi kuanguka kimasomo, nakubalika na maisha yanaendelea..

hata hivyo malezi hayo nahisi yaliniathiri kisaikolojia, pia yaliniimarisha pakubwa.
AYA YA MWISHO KATIKA POST YA MLETA MADA ISIPUUZWE
 
Pole sana! Ndo maisha hayo, kikubwa samehe sahau songa mbele. Maisha safari!!!
 
Hata wataalamu wa ndoa hawashauri kuingia kwenye ndoa na mtu ambae hakulelewa na wazazi wake wote wawili kipindi Cha utoto.
Hio ndoa huwa ndoano.
Duh mbona changamoto sana,mimi sijalelewa na mzazi yeyote yule. Kumbe ndio maana sina hata girlfriend mpaka umri huu kudadadek!!
 
alaf sijui kwann wanawake wenye roho mbaya vizazi vyao vinaoshiaga vibaya sana
 
Mkuu pole sana kwa uliyopitia.

Mimi nilifukuzwa kwa Mama yangu nikiwa na miaka 5 kwa kigezo cha kwamba baba yangu sio kabila lao. Hivyo mimi ni kama mwanaharamu(kama sijakosea),wao wanaita Nyamhanga. Hapo katikati yalotokea ni mengi sana,na Mama mzazi akishiriki(sijajua kwanini aliamua kufanya vile,Mungu amsamehe)

Nikapata bahati ya kukaa na mama wa kambo kwa week zisizozidi mbili ila alitaka kuniua na kunitupa kisimani. Yule mwanamke alikua anatembeza kipigo balaa,kiasi kwamba akinipiga nikakimbia zile hasira anazimalizia katika vitu kama magodoro,mito ya makochi,n.k. Ataichana chana vipande vipande kwa kisu ndipo hasira zake zitulie.

Baada ya kutoka hapo nikakaa kwa ndugu,mke wa yule ndugu yangu alininyoosha balaa,nikaamua kutoka home baada ya kumaliza standard 7,nikiwa na miaka 13 tu. Niliishi mitaani kwa kupambana sana tangu nikiwa mdogo (niliwahi kuandika hapa JF)

So mpaka kufikia umri huu sijawahi kurudi kuishi kwa mtu yeyote,kwa kifupi sina malezi yoyote yale kutoka kwa mzazi. MTAA umenilea,mtaa umenifunza mengi.

Hawa akina Mama wa kambo ni kisanga sana.
 
Daah pole aisee mamamzungu. hii stori imenikumbusha mbali sana miaka iyoo kuna mwamba mmoja akiitwa anania. Huyu alikuwa ni dogo wa kiume wa miaka kati ya 7 au 9 ivi akiishi na walezi wake wote tulipanga nao nyumba moja zile nyumba kubwa za uswazi zinakuwa km behewa ivo kuna familia kibao mnaishi humo.

Huyu Anania alitokea kwao maeneo ya manda uko na alifika apo mjini akiishi na walezi wake, sio wazazi wake. yy alikuwa analelewa tu apo mbali na wazazi wake. nakumbuka yule mama alikuwa wa kukaa nyumbani ila uyo mbaba alikuwa mjeda ila nae alikuwa sio wa kutulia nyumbani akisafiri sana.

Huyu anania alikuwa akiteswa sana sana na huyo mmama mlezi wake. Ni miaka mingi sana imepita lakn bado nakumbuka utafikiri ndo imetokea jana tu shida na mateso ya kunyimwa chakula, kunyimwa nguo za kuvaa.

nakumbuka kuna wkt ilibidi mzazi achukue nguo zangu kumpa huyu anania baada ya kuona walezi wake hawamjali kabisa kwa mambo ya mavazi, viboko vilikuwa ndo vyake alichapwa bila utaratibu hata sababu ya kueleweka, s'tyms anamwagiwa maji chini na kuambiwa ndo atalala apo kwene ayo maji, yani azabu za yule mlezi wa anania sijawahi kuziona kwingineko aicee.

nilijifunza kitu kuna wamama ni makatiri adi shetani mwenyewe akasome. Lakn sasa cha ajabu kwa miaka ile watu wengine wa familia za jirani walikuwa wanaogopa kuingilia mambo kama hayo hata pale yalipofanywa kwa uwazi kama alivyokuwa anafanyiwa mtoto yule.

kila mtu alibaki na familia yake amefunga mdomo wake anaogopa kusema chochote kwa yule mama mkatiri au kutoa utetezi kumlinda yule dogo. ila sasa hii ilikuwa ni tz ya miaka ile! saivi mambo yamebadilika sana aisee uezi kufanya upumbav km uo hlf wanazengo wakuangalie tu. anania alifanikiwa kurudi kwao uko umandani, yule mama mkatiri alishatwaliwa mawinguni kitambo kwa mapenzi ya mjawake.
 
Back
Top Bottom