Lakini baba yako alikuwa dhaifu sana.Mungu ni mwema Asante
Umesema baba yako alikua muislamu vp ulibadili dini wewe na mama yako??Labda ila mimi kwa upande wangu Sina kisasi ndani yangu maana mama yangu aliponichukua ilikuwa ni kunifariji na kanisani kwa sana ni vile tu tunasamehe ila hatusahau
Umesema baba yako alikua muislamu vp ulibadili dini wewe na mama yako??
How mkuu unaweza ukashusha uzi...Ni mbaya sana, asilimia 90 ya matatizo ya afya ya akili (anxiety & depression) source yake ni Childhood Traumatic experiences..
Bahati nzuri ni kwamba you can be healed na ukawa free kabisa.
Naweza kumsaidia yeyote ku release traumatic experiences za utotoni.
mamamzungu Mara nyingi mtesi wa Mwanamke ni Mwanamke, bado najiuliza Why KE hawapendani?Inaendelea
Mzee aliporudi kutoka safarini akanichukua tukarudi wote nyumbani akawa ananiuliza kwanini nimetoroka nyumbni nikamueleza mama alitaka kunipiga hivyo nikaogopa na kuondoka Mzee alinibembeleza na maneno ya kitoto.. safari hii kidogo mzee alikaa nyumbni hakuwa na safari safari zaidii ya kwenda kazini
Nyumba tuliyokuwa tunakaa ni kota nimesahau jina ilivyokuwa ikiitwa ila kwa wale wa TMA wanafahamu hatukuwa tunakaa maghorofani wala mabatini ni zile nyumba za peke ake peke ake.. Yule mama alijulikana mpk kambini kuwa ana roho mbaya nakumbuka kuna siku alinipiga sana mpk akajichapa mwenyewe na bomba la maji maana nilikwepa aliumia mkono akakasirika akanifukuza nyumbani akiniambia nikamfuate mama yangu.. Baba alikuwa yupo kazini, alinitupia nguo nnje ambazo zilikuwa kwenye shangazi kaja na kufunga mlango, ilibidi niondokee nyumbani nikaelekea kazini kwa Mzee maana sikujua pa kumpata mama
Yaani kwa nilivyokuwa nilikuwa kama mtoto wa mtaani.. Nilifika kazini kwa Mzee pale getini walinioji maana nilikuwa mtoto hawakuweza kunifanya chochote nikawatajia jina la Mzee maana Mzee alikuwa anajulikana walinipeleka moja kwa moja.. Mzee wangu baada ya kuniona alinipeleka sehemu nikamsubiria baadae tukaondoka wote hatukuenda nyumbani moja kwa moja tulipitia Bar
Mzee alikuwa mnywaji ila sio mlevi ila siku ile nilishuhudia akilewa, alikuwa na rafiki yake pale bar.. Mimi walinitafutia sehemu yangu ya kukaa huku wenyewe wakibaki wakipiga story mimi nilikuwa nawaona ila siwasikii wanachoongea
Kwa mara ya kwanza nilimuona Mzee wangu analia huku mwenzie akimpigapiga mabega kwa wakati huo sikujuaa analilia nini maana sikuwa nasikia wanachoongea… Tulikaa na Mzee pale mpk usiku tukarudi nyumbani.. tukiwa njiani Mzee alikuwa akiniambia ananipenda sana nivumilie tu ananitafutia shule ya bweni nisikae nyumbani… Tulifika nyumbani nakumbuka nilikuwa nimesinzia akanibeba na kunilaza kitandani alivyotoka tu Mimi nikashuka kulala chini maana yule mama alinikataza kulala kitandani akisema naozesha godoro lake kwa kujikojolea…. Kumbe Mzee alirudi kuniangalia akakuta nimelala chini a kaniuliza kwanini nimeshuka kitandani nikamwambia mama ananikaza kulala kitandani nitakojoa Mzee alikunjaa suraa akaniambia Hakuna kulala chini nilale hapo hapo yeye akaenda chumbani nikawa nasikia wanagombana
Maisha yaliendelea nikiwa nasubirii kupelekwa shule ya bweni bado nilikuwa nateswa mno yule mama alikuwa ananifinya usoni akisema kuwa nina ringa na rangi kwa vile mama yangu ni mzuri basi ataniharibu sura hiyo na Hakuna wa kunipenda [emoji24][emoji24] Yule mama alikuwa ananifinya usoni anatoa mpk ngozi kiasi kwamba ilinifanya nisijiamini katika ukuaji wangu nashukuru kwa sasa zinaonekana japo kwa mbali sana…
Yule mama alikuwa hana aibu alikuwa anatembea na rafiki za baba pale Kota ilikuwa ni aibu… Walikuwa wakigombana na Mzee mpk majirani wanajua alikuwa anatembea na madereva wa Mzee… Mzee kila siku anabdadilisha madereva
Muda ambao Mzee anakuwa safarini kikazi yule mama alikuwa anaingiza wanaume ndani na Mimi nilikuwa nawaona ananiambia nikisema ataniua na Mimi kwa kuogopa sikuwai kusema chochote
Siku moja usiku nilisikia Mzee wangu wanagombana na mama wa kambo kuhusu mimi kuwa siwezi kwenda hiyo shule na watoto wake wabaki hapo nitafute shule nyinginee yaani kwa maana huyo mama alitaka niende shule anayotaka yeye…
Muda ulienda dada angu ilirudi likizo.. ukweli nampenda mno dada angu sijui nisemeje kwa sababu ni mtetezi wangu siku zote… alipokuwa yupo nyumbani basi niliishi kwa raha.. sikuwa nafanyishwa makazi maana nilikuwa naambiwa nifue nguo za wadogo zangu na huyo dada angu kila siku nawafulia na kuzinyoosha hata Kama nimesahau kuzifua ninaamshwa usiku kwenda kuzifua Yule mama alininyanyasa sana
Kwaiyo dada yangu alipokuwepo ilikuwa ndio pona yangu.. Dada yangu ni mpole na sio muongeaji ila likifika suala kuhusu mimi anacharuka alikuwa ananiambia chochote wakikwambia Hakuna kufanya kuna dada wa kazi analipwa mshahara na huyo ndugu yangu mwinginee ni mkubwa anaweza kujifulia mwenyewe
Nakumbuka usiku wa siku dada aliyorudi kutoka shule tukiwa tumelala.. dada yangu ambae kanizidi mwaka 1 akanituma niende nnje nikamuanulie soksi zake hapo ilikuwa saa 4 dada yangu a kamwambia aende mwenyewe mimi sio mfanyakazi wake basi ikazuka vurugu akaanza kumtukana dada… kumbuka dada ndio first born hivyo ametuzidi sana akawa anamdharau ikabidi dada angu ampige kofi la uso akaanza kupiga kelele kumwita mama yake huku akimtukana dada…. Mama yake alivyokuja wakaanza kupigana na dada kwamba kwanini ampige mwanae ikawa ugomvi mkubwa na Hakuna wa kuamua maana tuliobaki wote watoto na Mzee alikuwa safarini
Mungu si athumani siku ile kumbe Mzee alikuwa ndio anarudi safari ameingia amechoka halafu kakuta kuna ugomvi na yule mama kashika kisu anataka kumchoma sister… ikabidi Mzee amnyang’anye kile kisu
Yule mama kuona hivyo akaenda kuchukua chupa ya bia ili kunipiga nayo alivyoirusha mimi niliiona nikaikwepa bahatii mbaya ikampata mtoto wake wa kiume ambae ni mdogo wangu… likaanza balaa lingine kwamba sister kasababisha mtoto wake akifa atamuua akawa anamwambia baba amuondoe dada pale nyumbani kwanini anamtetea sana dada au ni hawara yake aliongeaa maneno machafu
Ilibidi Mzee amtoe sister akaenda lipa guest akalala huku… Yule Mama akasema hataki kumuona kabisa dada pale nyumbani atafute pa kukaa ikabidi baba yangu amuombee sister kwa rafiki yake ambae ni kabila moja hivyo tunamwita shangazi ndio kulala na kukaa kwake
Maisha ya manyanyaso yaliendelea kuna siku tena alinipiga sana akatishia kunichoma pasi nikakimbia kwa majirani jioni yake watoto wakawa wanazunguka nyumba wanaimba nyimbo ya kumwambia aache roho mbaya… nafikiri walitumwa na wazazi wao… kuna siku Mzee wangu alinipeleka kwenye shule inaitwa Joseph Primary school Arusha nikafanya interview na nilipitaa maana niliambiwa nijiandaee kwenda shule nimefaulu… nikashangaa nimepelekwa kwa mtu mwingine kumbe alikuwa mwalimu mkuu wa shule ninayoenda… Ajabu si kwenda kule Joseph primary nilipelekwa shule nyingine ipo kijijini huko inaitwa Engaruka Juu primary… ile shule ilikuwa mbaya kwa kipindi kile sijui kwa sasa hivi
Ila nashukuru nilipumzika kwa muda kwa kukaa mbali na home hata likizo sikuwa naenda nyumbani nilikuwa nikikaa kwa mwalimu mkuu… Nashukuru Mungu yule mwalimu alinipenda pamoja na mke wake kwani nilikuwa nawasaidia kipindi cha likizo kuwalelea mtoto wao… Japo napo nilinusurika kubakwa na mwanaume aliekuwa akikaa pale sikumbuki alikuwa nani yao…
Sikumbuki jina vizuri alikuwa anaitwa mwalimu Olais au Alois ila alikuwa na binti yake wa kwanza akiitwa Angel sikumbuki walipo ila mara ya mwisho nakumbuka walikuwa wakiishi Ng’aramtoni Mungu akubariki sana kama utasoma hapa nakuomba unitafute japo nikushukuru kwa mdomo maana ulinilea kama mtoto wako
Muda ulienda mpk pale nilipoambiwa kwamba nirudi nyumbani nikiwa shule hapo nikawa nashangaa kuna nini maana sio muda wa likizo halafu kwanini sirudi na wanafunzi wenzangu ila sikuwa na namnaa yule mwalimu ndio kama mzazi wangu sasa alinipeleka nyumbani kwake nikaa kama siku mbili nikaja kupata taarifa za msiba mwa mzee wangu
Mzee wangu alifariki tarehe 4/9 mimi napata taarifaa baada ya mazishi yaani wiki imeishaa kumbe yule mama hakutaka sisi tujue kila akiulizwa nilipo hasemii maana Hakuna mtu alikuwa akifahamu ninaposoma zaidi yake na Mzee hivyo taarifa ya msiba alifika kwa kuchelewa.. na mama yangu aliambiwa na mshemeji zake… sikumzika baba yangu wala kuhuzuria msiba…
Kurudi nyumbani nikakuta waombolezaji tu wapo yule mama na watoto wake hawapo.. taarifa iliyokuwepo ni kuwa alienda kijijini walivyozika tu akageuza siku ile ile akawaambia bibi na babu yangu mzaa baba hawezi kukaa na manyani anarudi mjini hilo neno MPa Leo ukienda. Kijijini ndugu wa baba lazima waliogee wanamchukia sana huyo mama wa kambo…
Kumbe nia yake ya kurudi mjini ilikuwa aje kukusanya vitu vyote na kuondoka navyo… Yule mama ana roho mbaya alibeba kila kitu cha thamani pale nyumbani akapeleka anapopajua yeye aliuza gari pikipiki baiskel na hakutoa hata senti alifanya ukatili sana mpk nguo za marehemu alienda kugawa kwao ndugu wa marehemu hakupata chochote
Mambo yalienda cha kushukuru Mzee aliacha wosia na watoto wake wote tulikuwemo msimamizi wa mirathi mkuu aliandikwa dada yangu… yule mama hakuwa na aibu alitusumbua kwenye mirathi kiasi kwamba ilichukua miaka 7 mpk kugawana mirathi… alikuwa anataka tugawane kila kitu yeye apate zaidi alijengewa nyumba ila alitaka na nyumba nyingine ambayo ni yetu tuiuzee tugawane kwa kuwa mama ni muungwana tukainunua sisi ile nyumba kwa hela za mirathii
Mpk sasa Hakuna undugu uliopo kati yetu na watoto wake… watoto hawawwjui ndugu za baba yao sisi ndio tunaojulikana huko kwa Baba na wanatupenda
Hayo ni machache kati ya mengi alionifanyia hakutaka nifanikiwe Mungu ni mwema katika watoto wake Hakuna alienifikia nilipo kielimu na kimaisha… watoto wake wananipigia simu kuniambia tusahau yaliyopita mimi nawajibu nishawasehe ila kila nikikumbuka mama yao alivyoninyanyasa roho inaniuma sana… nawaza kama Mzee asingefariki uenda ningeanza mimi kufa maana yule mama angeweza kuniua
Ushaurii wanaume mnaozaa watoto kwa mama tofauti kuweni makini raha zenu zisifanye watoto wenu wateseke… mtoto hawezi kushitak kokote haswa kama anatishiwa
Jitahidi watoto wenu wawe wa mama mmoja angalau kuna msingi mzuri
Mimi niliteswa sana kama ingekuwa ni video ungeona ninayofanyiwa sidhani kama umgestahimili
Mwishoo
Pole sanaInaendelea

Jipange ukalipe kisasi, mimi ningelipa tuNimelelewa katika mazingira kama yako tofauti jinsia tu.
Mama yangu alifariki miezi mitatu baada ya kumzaa mdogo wangu wa kike, wakati huo nikiwa na miaka kama 2-3, baada ya mama kufariki baba alioa mwanamke mwingine!
Hapa sasa nikaanza kulelewa na mama wakambo!! hapo dunia ilikuwa CHUNGU kwa mateso niliyopitia (sisi wengine tunasubiri kwenda mbinguni, jehanam tumeshatoka[emoji28])
nilikuwa natoroka lakini kutoroka kwenyewe ni kwenda kwa jirani, kesho yake ikifahamika nilipo mzee ananifuata; nae ananishushia kipigo mpaka nyumbani (sikuwa nasema sababu rasmi za kutoroka nyumbani kwa kuogopa mateso zaidi maana hata hivyo muda mwingi nilikuwa nakaa na huyo adui yangu "mama wa kambo")
Shule:
nilianza darasa la kwanza mpaka 7 nikiwa pale nyumbani, sikuwahi kufeli japo nilikuwa naenda shule mara 2/3 kwa wiki, yaani nilikuwa nafaulu kimiujiza fulani hivi [emoji28]
pale shule ya msingi ni mm nilieonekana kama kituko flani hivi: uchafu, nimo! utoro, nimo! uchelewaji shuleni nimo! so shuleni ni kichapo, nyumbani kichapo! hata sasa hivi nikitaja jina la hiyo shule kuna watu nahisi watanijua!
Kazi mgumu ngumu zote za nyumbani zilikuwa zangu, makosa yote madogo madogo yanayojitokeza pale nyumbani nawajibishwa mimi (adhabu kama ya mwizi)
kwangu ilikuwa ni bora kwenda shule nikaadhibiwe hata na waalimu wote kuliko kushinda nyumbani.
Kwenda shule ilikuwa a big chance kwangu na mara nyingine nilikuwa naenda shule kwa kutoroka (hapa ni ile siku nimepewa taarifa kwamba "kesho hakuna kwenda shule")
nikitoka shule chakula sikuti na nikikikuta ujue kuna pilipili ya kutosha!
*kumwagiwa maji ya moto na moto wenyewe
*kulishwa ugali mabichi na kulala njaa
kufinywa mashavu na vibao bila kosa
*zikipikwa nyama zinawekewa mchuzi kwa ajili ya mtu fulani [emoji19][emoji19]
Nilipumua pumua baada ya kumaliza std 7 (nilipangishiwa chumba karibu na shule ya sekondari)......... ........
pamoja na hayo: pia Nashukuru Mungu sijawahi/sikuwahi kuanguka kimasomo, nakubalika na maisha yanaendelea..
hata hivyo malezi hayo nahisi yaliniathiri kisaikolojia, pia yaliniimarisha pakubwa.
AYA YA MWISHO KATIKA POST YA MLETA MADA ISIPUUZWE
Sioni umuhimu wa kufanya hivyo, wala simshauri yeyote kulipa kisasiJipange ukalipe kisasi, mimi ningelipa tu