Nashindwa kumweleza ukweli

Nashindwa kumweleza ukweli

inawezekana mkeo alishapima na anajua hali mlizo nazo, ila jinsi ya kukueleza ilikuwa ni kukwambia mkapime wote (am just thnkg loudly). maana kwa ss wanawake unapokuwa preg kupima ni lazima sio hiari. kuna mawili; (1) mueleze mkeo hali halisi (2) kubaliana na ombi lake, mchukue muongozane mkapime wote. ila pia ni vizuri kupat second and thir thought, kapime tena vituo vingine kama viwili au vi3
 
wife alipokuwa mjamzito aliniomba tukapime vvu. Nilimchenga chenga kidogo lakini hatimaye niliamua kwenda nje ya mji kupima peke yangu kabla sijaambatana nae. Baada ya counseling ya docta alinielekeza chumba cha kupimia. Nilipoingia ndani nilikutana na mtu wa vipimo ambaye ni rafiki na mke wangu na alishawahi kututembelea home. Nikuwahi kujua sehemu anayofanyia kazi. Alinipokea vizuar na kuchukua damu yangu na kuniomba nisubiri nje kidogo. Nilishangaa kidogo na kupatwa na hofu kwani majibu yangu yalichukuwa zaidi ya nusu saa kuyapata (kwa kawaida huwa inachukua not more than ten mts).
Majibu hayakuwa mazuri (nilionekana nina maambukizi),
1) sijawahi kumweleza mke wangu na huu ni mwezi wa tatu tangu kupata majibu
2) yule dada aliyenitoa damu na kufanya vipimo ameongeza safari za kuja kukutembelea home (kila weekend)
3) sina hakika kama keshamweleza mke wangu status yangu (wife hajaonyesha tofauti yoyote)

naomba ushauri wenu wadau

chukua hatua za kumueleza mkeo ili mpate ushauri wa daktari kama mko affected muweze kumlinda mtoto
 
Dah! Ngumu kumeza, pole but ndo maisha yalivyo, cha msingi mchukue mkeo mwende hospital au kituo kingine mkapime wote, wakati huo wewe ukijifanya hujui lolote kuhusu hali yako. Then baada ya majibu sasa kama mkeo atakuwa hana maambukizi muhudumu wa afya atawashauri jinsi ya kuishi ili mkeo asipate maambukizi lkn kama mkeo atakutwa na maambukizi hapo pia mtashauriwa jinsi ya kuepusha maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, so wahi mapema kumuokoa mtoto aliyeko tumboni,plz!
 
Nakushauri ukapime tena sehemu nyingine na kama majibu ni hayo hayo.Inabidi umkalishe chini mkeo umueleze ukweli...IT WILL BE WORSE WHEN SHE HEARS IT FROM SOMEONE ELSE AND NOT YOU...Na inabidi na yeye apimwe lakini nadhani kawaida mjamzito yoyote lazima apimwe ukimwi...Dah hebu nikulaumu kwanza..WHAT THE HECK WERE YOU THINKIN MAN??
​

wat the heck was he thnking kwends kupima AU??
 
Back
Top Bottom