Battor
JF-Expert Member
- Mar 21, 2019
- 2,206
- 3,981
Kwasababu oxygen ni gas na tabia ya gas ni kusambaa kalingana na shape ya container yake. Sasa sehemu ambako oxygen ni nyingi zaidi itasambaa kwenda hadi sehemu ambako kuna oxygen kidogo.Kwa mujibu wa sayansi, hewa au oxygen inatokana na mimea, lakini kiuhalisia tunaona hewa au upepo mwingi unakuja kutokea baharini na baharini hakuna mimea.
Pia maeneo ya majangwani hakuna mimea ila kuna upepo mkali, je hewa huzalishwa kwa njia gani katika maeneo hayo?
Naomba mnieleweshe kwa wale wanao fahamu sayansi ya mazingira....
Miti inazalisha oxygen lakini ni kwa asilimia ndogo sana ukilinganisha na oxygen inayozalishwa baharini, na inasambaa hadi kwenye sehemu zenye mgandmizo mdogo wa hewa kama jangwani.
Umeshawahi kujiuliza je, usiku huwa oxygen inatoka wapi ukizingatia miti pia haitoi oxygen? Ni sababu distribution ya oxygen ni ya global hivyo huku ikiwa usiku kuna mahali ni mchana hivyo oxygen inayozalishwa huko itasambaa hadi kukufikia wewe huko ulipo usiku.
Ubora wa hewa utategemea kiwango cha uzalishaji na kiwango cha matumizi mfano sehemu ya jangwa kukiwa na idadi kubwa ya watu hewa itakuwa mbaya maana matumizi yatakuwa ni makubwa na hakuna miti itayoweza angalau kuchuja hewa safi na kuchukua co2.
Inasemekana hata leo ikitokea bahari na mimea ikaacha kutoa oxygen, itachukua miaka 500 hadi oxygen kuisha kabisa.