Ndugu kwanza nakushukuru kwa ujasiri ulio nao. Nataka nikupe experience ndogo ya kile ulichokiona. Miaka kadhaa nyuma nikiwa chuo kikuu niliugua sana kiasi cha kushindwa kufanya shughuli ndogo ndogo kama kufua na kadhalika. Ilifikia hatua nikashindwa kutembea kabisa, miguu na mikono ilivimba sana. Mwishowe niliamua kutoka kuahirisha masomo ili angalau kama ni mauti inikute nyumbani. Kabla sijafanya hivyo, nilimtaarifu binti mmoja ambae nilikuwa nae kwenye mahusiano kwa muda mrefu. Alinishauri kutokukatisha masomo na akaamua kuja kukaa na Mimi. Alinisaidia sana, tuliomba na kusali pamoja hadi nikapata unafuu Baada ya miaka miwili ya shida na mateso. Nilipoanza mwaka wa tatu, semester ya pili, nilimuomba arudi nyumbani kwetu atulie ili nimalizie masomo kwa sababu kipindi hicho kozi zilikuwa taiti sana. Alipofika nyumbani, wiki kadhaa baadae, nilikuwa nikimuota akifanya mapenzi na rafiki yangu. Nilipokuwa nikijaribu kumuuliza, alikuwa anakataa. Nilipomaliza chuo, nilipata kazi moja kwa moja kwenye taasisi binafsi pamoja na stahiki zote. Nilirudi nyumbani nikaongea kwa upole sana na huyu mpenzi wangu maana nilimpenda sana japo alikuwa na elimu ndogo. Alinisimulia kila kitu alichokuwa akifanya na rafiki yangu.
Wakati mwingine tunaepushwa na mambo mengi yaliyo nje ya uwezo wetu kwa watu tunaofikiri ni wazuri kwetu. Acha kumuoa huyu MTU unless upo tayari kukabiliana na hayo.!!