Ninachohisi ni kwamba umeanza kuwa insecure kwa sababu ya distance kati yenu. As a result umeanza kumuwazia mabaya binti kuwa inawezekana anachepuka.
Ndoto inaweza kuwa ni maono kutoka kwa Mungu anajaribu kuongea na wewe kuhusu kitu fulani, na wakati mwingine tunaota aina fulani za ndoto kwa sababu ya shughuli nyingi/fikra/mawazo yetu. So inawezekana pia umeota hivyo kwa sababu ya aina ya mawazo unayomuwazia huyo binti. Kama unaamini kiasi hicho, basi muombe Mungu kwa uaminifu kabisa, kama ilikuwa ni yeye anasema nawe kwa ndoto, basi atasema na wewe tena juu ya huyo binti. That will be the only solution ili wote muwe na amani, usiwe na doubt moyoni mwako.
Kwa sababu (IMO), umbali unakufanya uamini binti anachepuka, unatamani umuache ila nafsi yako inakusuta coz huna proof ya hiyo sababu ya kumuachia. So hapa you are simply looking for justification ya kumuacha, ndo maana unaassume tu mambo mengii. Kuna mtu kakupa tricks za kumuingia mdogo ako aseme kweli, kama utaliweza hilo fanya pia to clear your doubts
Hapo kwa mama panakutisha zaidi kwa sababu ya hofu uliyomuwekea mpenzi wako. Yes kuna tabia zinakuwa common kwa kila kabila kwa baadhi ya watu, ila haziwezi kuwa common kwa kila mtu.
Wewe binafsi ni shahidi kuwa huyo sio malaya na umempa sifa nzuri ambazo sio rahisi kuzipata kwa kila mwanamke. Kama angekuwa malaya kama kabila lake, hakika ungeshamgundua kuanzia zamani huko, tabia ya asili ya mtu ni ngumu mno kuificha. Mchawi wenu hapo ni distance, kill the distance by marrying her. Finding a good woman isn't that much easy, ni neema kwa kweli
Na ombi tu kwa wanaume wote, muwaulizage tu mama zenu mapemaa ni makabila yapi hawatoki muoe. Sio mnakaa na mabinti za watu, wanahangaika na nyie katika yote, afu mwishoni uje umwambie mama hataki kabila lako. Msijitafutiage laana za machozi ya watu pasipo msingi