Pole aisee, wengi tumepitia hali ulio nayo saivi lakini kuvumilia ndio iliotuwezesaha kuvuka salama, waliopaniki waliendelea kupata maumivu na vilio wakati wote. lakini ukichukulia kama ni jambo la kukupeleka htua nyingine siku ipo utakuja kucheka toka moyoni.kuna punda mmoja aliangukia shimoni,na kushindwa kupanda akaanza kulia na kupiga makelele,majirani waliposikia kelele hizo walitoka kuona ninini. Walipogundua ni punda yule na kwasababu walikuwa hawampendi au mwenye nae hwampendi waliazimia kumfukia hukohuko chini, mwenye mawe alitupia vifusi vya udongo walimwagia shimoni ili afie huko,lakini yule mnyama alijua huu ndio mzaada kwaio kila wakijaza ye anajikunguta anapanda juu maudongo na mawe yanakuwa chini japo mara nyingine aliumia lakini aliendelea kufanya hivyo mwishowe katokea juu ya shimo nawale watu ilibidi wakimbie! Kwaiyo dada uwapo katika hali hio jikungute iwe ni ngazi yako ya kupandia juu siku ipo utakua unafuraha ya moyo, lakini usiikaribie dhambi tubu sali toa sadaka jali , ubaikiwe.