Nashauri serikali ifungie utengenezaji na usambazaji wa Filamu za Kibongo hadi watakapojitambua

Mufti kuku The Infinity

JF-Expert Member
Sep 21, 2019
5,688
8,927
Yaani ni hivyo tu jamani, hakuna kitu kinakera (hata kama huziangalii) kama hizi filamu za bongo. Nahisi kabisa kuwa wanatuaibisha hata nje ya nchi (kwa mataifa jirani wanao angalia kazi zao)

Filamu stori haieleweki wanaigiza ili mradi tu, Unaweza kusema labda bajeti ya uandaaji ni kubwa, lakini mfano mdogo fuatilia filamu za Mexico na Philippines, hamna hata matumizi makubwa ya technology lakini story imepangwa vizuri had unafurahi. Hawa wa kwetu hata hawaeleweki.

Nina mashaka sana, nahisi huwa wanaigiza filamu wiki moja, Sio kwa uozo tunao uona, Yaani mtu unaangalia anavyoigiza unaona kabisa hapa hamna kitu. Unaona kabisa anavyo iogopa kamera.

Atleast basi muigizaji awe na elimu yoyote kuhusu uigizaji kama wafanyavyo kimataifa, Niwapongeze wote wanaoweza kukaa chini na kuenjoy kabisa kuangalia channels kama sinema zetu, Hongereni sana.

Yaani movies hata google au wikipedia hazipo.

Daah
 
Kitu hukipendi unalazimishwa kuangalia mkuu, mimi michezo sio mshabiki, kuangalia movie sio mshabiki pia, hivyo sijui kinachoendelea huko!! Wewe kama unaona hawaeleweki acha kuangalia fanya vyitu vingine!

Mimi mfano nikiona tu mpira au hizo movies sijui za wapi, pamoja na bongo fleva nahisi kutapika ni upumbavu tu!! Watu wanacheza uchi na mimi na akili zangu timamamu Nikae nawangalia ni mambo ya ajabu kweli aise!
 
Kitu hukipendi unalazimishwa kuangalia mkuu, mimi michezo sio mshabiki, kuangalia movie sio mshabiki pia, hivyo sijui kinachoendelea huko!! Wewe kama unaona hawaeleweki acha kuangalia fanya vyitu vingine.

Mm mfano nikiona tu mpira au hizo movies cjui za wapi, pamoja na bongo fleva nahisi kutapika ni upumbavu tu!! Watu wanacheza uchi na mm na akili zangu timamamu Nikae nawangalia ni mambo ya ajabu kweli aise.
Sawa mkuu
 
Kwa sasa bongo wanatengeneza maigizo na sio filamu kama zile alizokuwa akitengeneza hayati Kanumba.
 
Sawa mkuu
Filamu bora ni zile kabla ya kuwekwa sokoni hujadiliwa na kurekebisha makosa, bahati mbaya hapa huwa hawataki kuzijadili. Kuna moja ya filamu nilimsikia muongozaji akimwambia mdada aliyekuwa akifua "sasa fanya kama unaingia bafuni"! Picha hiyo ilikuwa Azam Tv Sinema Zetu.
 
Hawapendi kuwa hivyo, uwezo wao ndipo unapoishia hapo.
 
Muigizaji ndio director, editing, mtunzi na mchagua wa sanii.

Wasanii wa bongo movie ni wakurupukaji kuanzia wakwongwe mpaka wa sasa
 
Filamu bora ni zile kabla ya kuwekwa sokoni hujadiliwa na kurekebisha makosa, bahati mbaya hapa huwa hawataki kuzijadili. Kuna moja ya filamu nilimsikia muongozaji akimwambia mdada aliyekuwa akifua "sasa fanya kama unaingia bafuni"! Picha hiyo ilikuwa Azam Tv Sinema Zetu.
Ukiwa makini unaweza kuona hata vifaa wanavyotumia kama vinasa sauti na kamera

Yan sijui hawazipitiagi vizuri?
 
Mkuu una moyo Sana huwa hata nikiwa nasafiri Kwenye mabasi wakiweka move za kibongo naona heri nisome gazeti au nisinzie tu .
Huwa siangaliagi move za kibongo na sina hata moja CD wala softcopy
 
Ukiwa makini unaweza kuona hata vifaa wanavyotumia kama vinasa sauti na kamera
Yan sijui hawazipitiagi vizuri?
Ukiangalia baadhi ya movie za Nigeria zenye quality ndo na zinaigizwa vijijini huwezi kufananisha na za kibongo ,jinsi contents zao zinavyoenda na kuigiza.Ukiangalia movie za kinigeria unaweza kudhani ni ukweli
 
Ukiwa makini unaweza kuona hata vifaa wanavyotumia kama vinasa sauti na kamera

Yan sijui hawazipitiagi vizuri?
Kawaida ukimaliza kuhariri filamu huandaliwa jopo ambalo huitazama filamu yote kama ambavyo ingekuwa imekamilika, kisha hilo jopo huanza kutoa mawazo ya marekebisho kama yapo baada ya hapo huandaliwa picha kamili ya kwenda sokoni, tatizo kwenye hizi za bongo waanaaji huwa hawataki kabisa filamu zao kupitiwa na jopo kwa madai ya kijinga eti wivu!
 
Mwisho wa siku kazi zinatoka hazieleweki🤔
 
Ila hata sisi watanzania wanafki sana...nikuulize labda mara ya mwisho kununua kazi ya msanii yeyote yule kwenye platform rasmi ni lini?

Je,unadhani wao kama wasanii wanapata wapi nguvu ya kutengeneza kitu kizuri wakati hatununui? Kanumba alikua anatengeneza filamu nzuri sana na bado tulikua hatununui tunategemea CD akodi mtu mmoja tutaangalia mtaa mzima....wasanii wana matatizo lakini hata sisi walaji ni watu wa hovyo na hii si kwenye sanaa pekee ni kila sehemu.
 
Back
Top Bottom