Mjadala wa Kitaifa: Mapinduzi ya Tasnia ya Filamu Nchini Tanzania

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
918
1,994
mdundiko.jpeg


Zamaradi Mketema ameandika sehemu..


Natamani sana siku moja atokee mtu kwenye hii sekta atutambulishe hata kama sio kimataifa basi africa tu. R.I.P KANUMBA alianza kuonesha mwangaza na juhudi binafsi zilionekana na kila mtu aliona huenda angefika mbali.. lakini baada ya hapo sioni tena!!!!

Mbona hapa nyumbani ni wakubwa tu..? Nini kinawakwamisha..? Kwanini wasanii wetu wa filamu ukubwa wao unaishia nyumbani tu....!!? Tatizo ni nini!!!????? kiukweli ni kama inakatisha tamaa na inaonekana kabisa watu wamerelax na ustar wa bongo wakati wana nafasi ya kufanya vizuri zaidi... wana bongo movie tukifika kwa wenzetu unaona kabisa tunapwaya kiasi gani.. Ujanja wetu ni nyumbani tu!!?? why!!!?? tukianza utanzania wa kufichaficha tutasifiana uongo lakini tukiwa wakweli na nafsi zetu tutaliona hilo na kuchukulia kama challenge..!!! ukweli ni kwamba hii tasnia inasikitisha!!! tena sana nahisi sasahivi tunafanya filamu kwa ajili ya nyumbani tu na tukiingia kwenye mabendi tukisharushwa tumeridhika!! kweli!! hapa ndio mnapotaka mfike!!? ukifika sehemu ukiwa juu nchini kwako tunachotegemea ni wewe kupasua mawimbi uende mbali zaidi nje ya mipaka!! lakini ukiamua kurelax hapo ulipo inamana unasubiri kushuka sababu kiukweli huwezi kukaa juu milele!!! kwanini mmeridhika hivi!!! kaka JB tatizo ni nini!!!??

Mi nakuangalia wewe kama mfano wa msanii mkubwa sana kwenye tasnia kwa sasa... mbona umerelax!!!??? umeridhika na ustar wa tanzania!!!? una kila kitu cha kukufikisha mbali... kinachohitajika ni juhudi binafsi tu ili kesho na sisi tufike mahala pazuri!! hebu tuongee wapenzi.. Mnahisi huku kwenye bongo movie TATIZO LIKO WAPI!???

JB akajibu;

"Kwako Zamaradi na wengine wote..

Kwanza napenda niwashukuru wote kwa jinsi mnavyotuwazia mema. Naomba nichukue nafasi hii kuwapongeza waigizaji wote wa Tz na waandaaji wa filamuU kwa kuthubutu kutengeneza filamu hizi katiks mazingira magumu. Najua watanzania wengi wangependa kuona tukipeperusha bendera nje,lakini naomba muwape wasanii muda.

Tasnia hii ni changa na ina changamoto ambazo zinakatisha tamaa. Hebu tujiulize kwa nini wasomi wengi waliosomea filamuu UDSM na BAGAMOYO hawafanyi filamu hizi? Wasambazaji wengi wakubwa mamu,wananchi na hata hans pop walijaribu wakakimbia, kuna producer mkubwa hapa nchini JOHN RIBER ambaye ametengeneza filamuu kama NERIA na YELLOW CARD lakini naye ukimwambia njoo kwenye hizi filamu atakupa jibu.

Nakubali tuna makosa mengi kama ubora wa filamu zetu na stori lakini nataka niwaambie mazingira ya kufanya filamu bongo yanakatisha tamaa wizi wa kazi zetu umezidi na wasambazaji wengi wamekimbia. Binafsi najipanga kuwa mtayarishaji zaidi kuliko mwigizaji kwa sasa kupitia JERUSALEM FILMS na ndio maana filamu nyingi natoa nafasi kwa vijana ambao kama mabadiliko ya sera ya filamu yatafanywa watatuwakilisha nje.

Kiswahili kisichukuliwe poa kwani kina nafasi kibwa sana. Tukumbuke SHARUK KHAN ni actor tajiri 2 dunian lakini filamu zake ni za kihindi. Hebu sote tusaidiane kupambana na changamoto hizi na tuanze na EAST AFRICA kwanza huku tukiboresha, wasomi wa filamu msikimbie njooni tuanze wote na tuwape moyo wasanii wetu waliojaribu kusimamisha tasnia hii kwa vimtaji toka mifukoni mwao na vipaji walivyopewa na mungu bila msaada kutoka popote. Asanteni kwa kutuunga mkono kwemye filamu zetu."
------------

Tulitazame sasa hili suala kwa pamoja..

Tasnia yetu pendwa nchini, Tasnia ya sanaa ya maigizio, hasa kwenye upande wa Filamu, Sina shaka hata kidogo kwamba baada ya Muziki, Sanaa ya Filamu na Maigizo ndiye inafuatia kupendwa zaidi hapa nchini, Idadi ya watazamaji na wafuatiliaji inathibitisha hilo!

Bahati mbaya Tasnia hii inaelekea kufa kibudu. Narudia, Tasnia ya Filamu nchini inaelekea kufa KIBUDU. Hali ni mbaya sana kwenye upande huu wa sanaa nchini licha ya kuwa ndiyo FANI inayoongoza kwa kutoa Ajira kwa vijana wengi zaidi nchini. Tukubaliane hapo kwanza!

Makosa yapo Mengi. Mbaya zaidi yote si makosa yanayohitaji kuonwa mpaka na Mtaalamu pekee. Hata Asiye na utaalamu wa Sound engineering atajua kwamba sauti kwenye Bongo movies ni tatizo, asiyefahamu mambo ya script akitazama tu atajua, Asiyejua umuhimu wa continuity naye hali kadhalika, achilia mbali yule asiyejua kiingereza kwa ufasaha, inamuhitaji elimu ya kujua tafsiri ya toilet tu kung'amua kwamba kiingereza cha kwenye subtitles ni majanga. Mtiririko wa hadithi na uhalisia ni tatizo sugu. Inasikitisha sana.

Sitagusia hata moja katika hayo!

Leo Nagusa upande wa Mapinduzi ya Ujumla. Kwanini tasnia hii inaporomoka badala ya kukua zaidi? Kwanini hakuna mabadiliko chanya? Kwanini filamu nchini zimebaki kuwa na mabaka mabaka ya ulalahoi? Kwanini hatuvuki mipaka? Kwanini hatufanyi kweli? Kwanini muziki unatoboa zaidi kuliko filamu? Nini tatizo?

MAONI YANGU

1. Wasanii waanze kutengeneza 'image' nzuri

Maana kwa sasa imeshachafuka. Nasema ukweli, Tasnia hii ina taswira ya uhuni kupitiliza. Na hii ni kutokana na wasanii wakubwa (vioo) kukumbwa na kashfa chafu. Kucha kutwa magazetini kuandikwa upuuzi, pengine wapo wanaolipwa kwa kuuza gazeti, lakini sidhani kama wanacholipwa kina thamani kubwa kupita kazi ya sanaa wanayoifanya.

2. Ianzishwe mikakati madhubuti

Ni wakati sasa kwa wasanii kutengeneza Mipango Madhubuti na mikakati (Action plans) itakayowaongoza kufanya kazi kwa usiriaz. Inawezekana, najua mlishajaribu huko nyuma, lakini bado inawezekana.

3. Upekee na Usasa

Hapa namaanisha kufanya movie kisasa na kwa upekee kabisa. Itazamwe mifano ya filamu kama ya CHUMO (by Sharo Milionea & Jokate), Siri ya Mtungi nk(wataalamu sio kikwazo panapo fedha).

4. Kushirikisha Wadau

Watanzania na wapenzi wa filamu za kibongo ni wengi sana. Hakuna tu utaratibu wa kufanya research ili kuwa na data kamili, lakini kwa observation tu ni dhahiri kwamba Bongo Movie haijatupwa kivile. Ni basi tu wana-tasnia wenyewe mnachosha. Sijui lengo lenu ni nini haswa! Ni ajabu mtu kuua ajira yako kwa mikono yako mwenyewe!

Supporters wapo wengi sana. Wapo watazamaji wa hizi movies ni watu wenye uwezo mkubwa pengine hata wa kuwekeza. Achana na Mapedjee wanaohonga kwa lengo la kufurahisha nafsi zao, kuonekana, au malengo yao binafsi yasiyo na tija (japo wakitumiwa vizuri inaweza kusaidia sehemu). Hapa nazungumzia matajiri, wafanyabiashara wakubwa, wanasiasa, hata mawakala wa biashara, wakitumika vizuri, watafanya kitu.

Kinachohitajika ni ushawishi tu! Yaani wasanii wenyewe wahakikishe wawe na mipango na uwezo wa kumshawishi mtu/shirika/kampuni kuwekeza (kama si kufadhili) kazi zao. Serikali Pengine imeshindwa hili!

Na ushawishi huja pale penye tija. Mtu aone umuhimu wa kufanya hivyo, sio kuchoma pesa zake bure. Mbona michezo mingi inadhaminiwa? Mpira wa miguu, Ndondi, Riadha n.k. Kwanini isiwe Bongo Movie? Ni kujiongeza tu.

5. Kuomba fedha na access kubwa zaidi

Kilio cha wasanii wengi kushindwa kufanya movie zenye ubora ni Mitaji. Wanalalamika hawana fedha za kutosha kuweza kucheza baadhi ya story. Ni kweli kabisa. Na hii pengine ndiyo sababu kubwa hata thamani ya kazi zao kwa wasambazaji inashuka siku hadi siku. Hii ni kutokana na bidhaa kuwa ni low quality.

Sasa basi, katika mikakati yao, ni vyema wakazingatia ni vipi watapata mitaji ya kucheza story zinazohusika. Kisha watafute Soko zuri la kuuza bidhaa yao kwa bei itakayowanufaisha, sio watakayopangiwa na 'muhindi'.

Hatua za kupata mitaji zaweza kuwa;

*Kuomba udhamini kutoka kwa makampuni rafiki - Hapa namaanisha yale makampuni yanayohusiana na kazi zao. Kwa mfano Makampuni ya bidhaa za Camera, Deki, Simu, na kadhalika. Kwa ufupi, yale makampuni yanayoshabihiana na kazi za filamu yatakuwa rahisi zaidi kuitika!

*Kuomba mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha - Kwa kuwa filamu ni biashara kama zilivyo biashara nyingine kubwa, kampuni za utengenezaji wa hizi filamu (RJ, Jerusalem, 5effects, Timamu African Media n.k) zikiandaliwa mazingira mazuri zinaweza kukopesheka.

*Kutoa fursa kwa wahisani na wawekezaji - Kampuni za utayarishaji wa filamu zinaweza kutoa nafasi kwa wawekezaji kuwekeza kwenye kiwanda cha filamu nchini. Hapa kutawawezesha wawekezaji kuweza kuikuza zaidi tasnia hii kwa kuweka mitaji yao mikubwa na kuisimamia ili ipatikane faida. Inawezekana!

Pia, wasanii waombe access kubwa kutoka serikalini ili waweze kutambulika Rasmi na kuaminiwa. Haya yote yatawezekana endapo shirikisho la filamu nchini (TAFF) litakuwa na makali na sauti ya nguvu.

6. Wasanii watumie wataalamu kwenye kazi zao

Hapa namaanisha ni wakati sasa waandaaji wa filamu pamoja na wasanii kwa ujumla waanze kushirikisha wataalamu kwenye kazi zao. Kwa maana wafanye tafiti ndogo ndogo kuhusiana filamu husika (mfano kwenda maktaba kutafuta vitabu vinavyoelezea let's say masuala ya historia, kama hadithi ya movie inagusia huko) na kupata majibu ya kitaalamu kutoka kwa wataalamu hao. Hii ni faida kwani 'uhalisia' wa movie utakuwa maradufu!

Ushirikishwaji uanzie kwenye masuala ya story, production mpaka kwenye masuala mazima ya masoko. Uwanja huu ni mpana sana, nadhani mwanga umeanza kuonekana hapo!
-------------

Kwa kipekee kabisa, niwapongeze Timamu Effects / Timamu African Media kwa kuonyesha njia. Nathubutu kusema hawa ndio role models kwenye filamu za Kitanzania. Ni wenzetu, walianzia chini, lakini wamejitahidi kukua kifani, kimaudhui na kimapinduzi hususan kwenye ubora wa story na quality ya uandaaji wa filamu zao zote.

Nashauri waigwe na kuwa dira ya tasnia ya filamu nchini, waendelee kufanya mambo makubwa zaidi ili hatimaye na Tanzania tufikie levo angalau za Nigeria na Ghana. Nimefurahi kuona wamepata tuzo kadhaa za kimataifa na kubwa zaidi ni za hivi karibuni huko Marekani katika Future Africa Awards.

Hongera Timoth Conrady na Timu yako!

10704045_791446940918170_5283163046252936479_n.jpg


Naomba niishie hapa ili kutoa nafasi kwa wengine kuchangia mawazo yao. Kwa pamoja tuweke mitazamo chanya na yenye taswira ya kimapinduzi kweli ili hatimaye tuwe tumeshiriki kwenye kuboresha tasnia ya filamu nchini.

Nawasilisha..
 

Attachments

  • Bado-Natafuta.jpg
    Bado-Natafuta.jpg
    57.7 KB · Views: 463
  • ofside.jpg
    ofside.jpg
    8 KB · Views: 376
  • follish.jpeg
    follish.jpeg
    13.9 KB · Views: 377
umeongea ukweli sana ila bongo movie wana tatizo moja kubwa wana inferiority compex waanzie hapo

Bongo movie ni waoga na wavivu kupindukia tena wakiongozwa na JB ndio maana kajitetea kwa hoja hizo!

JB ana sahau hata kipindi cha Uhai wa Kanumba hayo matatizo yalikuwepo lakini juhudi binafsi tuliziona na kweli kanumba aliipeleka Bongo movie level ya kimataifa na kwakuwa alikuwa haogopi kusemwa au kusengenywa na alikuwa anapenda kujifunza!

Hawa wakina JB tuliwategemea sana lakini wamewekeza kwenye migogoro wenyewe kwa wenyewe na hawana ushirikiano kabisa yani ushirikiano wao ulizikwa kwenye msiba wa Kanumba!

Bongo movie kumejaa watu wenye vipaji vya hali ya juu nikimchukua Monalisa +JB sina lakusema lakini wote hao ni wavivu wakupindukia na hawapendi kujifunza na wanasahau Kanumba alipitia kwenye mazingira hayo hayo!

Bongo movie imekufa na itafika mahala watu wataacha kununua kazi zao kabisa mfano Mimi nilikuwa mteja wa Kanumba na JB lakini baada ya kifo cha Kanumba niliacha kununua kabisa kazi zao kwanza nilikuja kugundua kuwa Kanumba alikuwa anawapa changamoto na sasa wamebweteka wana subiri watu waje kuwekeza....huu ni ukichaa kabisa!

Kanumba alikufa na tasnia hii haina miaka kumi mbele itakuwa ni historia kama mtu niliyemtegemea kama JB anashindwa kupambana na changamoto ambazo wenzao walizikabili anabaki kulalamika!

Kwa Bongo movie hawa hata mtu akiwekeza hakuna mabadiliko maana wamejaa wavivu na waendekeza migogoro na wawekezaji wa kwenye birthday tuuu!

Kanumba alikufa na Bongo movie!

R.I.P Kanumba!
 
Jitihada pekee ndio zinaweza kutupeleka mbali,nilishawahi kuwatafuta hawa wasanii wakubwa niwape proposal kuhusu namna gani tunaweza kuweka effects nzuri ambazo hata hollywood wanazitumia kwenye muvie,tena nilijitolea bure,lakini cha ajabu hamna hata mmoja alikua interested,ndio hapo nikaamini kweli either wanalogana wenyewe au elimu unahusika hapo.Personally naona kuna opportunity nzuri sana kwenye hi tasnia,na uwezi tunao mkubwa.I will play my part
 
Sanaaa ikua kwa watu wa sampuli ya wema,wolper,kajala ,ant ezekiel.....haiwezekani....

These are just whoooreeesss.

Wako kwenye biashara ya ukahaba.....Never never never

JB ,Monalisa wako vizuri but ni wavivu.

Kinachokosekana ni hard work tu ...basiii....Vikwazo vipo...the only succesful man is the one who can overcome the obstacles
 
Sanaaa ikua kwa watu wa sampuli ya wema,wolper,kajala ,ant ezekiel.....haiwezekani....

These are just whoooreeesss.

Wako kwenye biashara ya ukahaba.....Never never never

JB ,Monalisa wako vizuri but ni wavivu.

Kinachokosekana ni hard work tu ...basiii....Vikwazo vipo...the only succesful man is the one who can overcome the obstacles

Bado naamini wanaweza kufanya kitu.. Wajipe ushindani tu wa kikazi na wasanii wa muziki..
Maisha binafsi yabaki kuwa binafsi, yasichanganywe na kazi..
 
Back
Top Bottom