LURIGA
JF-Expert Member
- May 26, 2013
- 2,515
- 3,928
Kwa roho zetu hizi za kiswahili mwingine ukimsalimia ukamshika miguu yeye anaweza kukushika kichwa lakini huku moyoni mwake anakulaani badala ya kukubariki. CHEZEA ROHO MBAYA YA KISWAHILI WEWE!Shikamoo maana yake ni nakushika miguu. Kushika miguu ya mtu mzima ni kutaka baraka zake. Ndio maana watu kama wahindi wakisalimia watu wazima lazima wawashike miguu na yule mtu mzima atamshika kichwa huyo anaemsalim, ishara ya kumpa baraka na kumtakia mema.
Ila sisi ni kwasababu tumeirithi tu hatuipi uzito kiasi hiko. Ila ilitakiwa unapotoa salam ya shikamoo upige goti umshike miguu huyo mtu mzima unaemsalimu na yeye akushike kichwa akupe baraka na kukutakia mema.