Nashauri salamu ya "Shikamoo" ifutwe

Nashauri salamu ya "Shikamoo" ifutwe

Shikamoo humaanisha hivi...nipo chini ya miguu yako, mimi si lolote kwako, sina thamani juu yako, nakutukuza, unachoagiza kwangu kutekeleza ni wajibu, mimi ni dhaifu kwako, ukitaka kunipiga nipige tu hata siwezi kujitetea kwako mkuu nk.
Kwa muktadha huu inabidi shikamoo ihifadhiwe maktaba ya Taifa.
Kitu kinaweza kuwa kilekile lakini kikabadilishwa maana. Shikamoo ni salamu anayopewa mtu anayekuzidi umri na haimanishi shikamoo ni utumwa. Vipi kuhusu kugonga, kugongewa, shoga, tigo? mbona hayajawekwa kwenye maana ya msingi? Na kwanini yamepewa maana ya ziada? Kasome kitabu cha Semantiki na Pragmatic utajifunza mengi kuhusu lugha ya KIswahili. Watu wengi hawajui Lugha ya Kiswahili ndiyo maana wanaona shikamoo ni utumwa.
 
Nikajua una salamu mbadala, kumbe utaahira tu. Sasa good morning ndio kitu gani? Yaani unasema shikamoo ni utumwa ila good morning ndio nzuri, kichwani una akili au makamasi?
Vijana wa siku hizi, badala watumie akili kufikiri wanatumia inye ndembe ndembe.
Naye anajiona mjanja kutamka Good Morning wakati ndiyo utumwa wenyewe. Watafute kitabu kinaitwa Semantiki na Pragmatiki wanajifunza mengi sana
 
Shikamoo humaanisha hivi...nipo chini ya miguu yako, mimi si lolote kwako, sina thamani juu yako, nakutukuza, unachoagiza kwangu kutekeleza ni wajibu, mimi ni dhaifu kwako, ukitaka kunipiga nipige tu hata siwezi kujitetea kwako mkuu nk.
Kwa muktadha huu inabidi shikamoo ihifadhiwe maktaba ya Taifa.
Duuuh !
 
"Nipo chini ya miguu yako" nido maana halisi ya (shkamoo).
Kuna maana ya msingi na maana ya ziada. Hatuko huko kwenye maana ya msingi tupo kwenye maana ya ziada ambayo ni salamu anayosalimiwa mtu anayemzidi umri. Kasome kitabu cha Semantiki na Pragmatiki utajifunza mengi sana. Vipi kuhusu kugonga, Tigo, shoga, umeme ? Mtu akisema huyo jamaa ana umeme unaelewa ana umeme wa TANESCO? Shikamoo inaleta mipaka na heshima kati ya mtu anayekuzidi umri. Utakuta mtu anaona shikamoo ni utumwa halafu anaanza kusalimia Good morning. Huyo anayesalimia Good morning inabidi akapimwe mkojo
Katafute kitabu cha SEMANTIKI NA PRAGMATIKI
 
Shikamoo humaanisha hivi...nipo chini ya miguu yako, mimi si lolote kwako, sina thamani juu yako, nakutukuza, unachoagiza kwangu kutekeleza ni wajibu, mimi ni dhaifu kwako, ukitaka kunipiga nipige tu hata siwezi kujitetea kwako mkuu nk.
Kwa muktadha huu inabidi shikamoo ihifadhiwe maktaba ya Taifa.
Atoto hebu toa neno hapa kabla hujapata hiyo shikamoo😀
 
Niliwahi kutaka kuleta hii hoja.

Niliwahi kumsikia Godbless Lema alipokutana na Rais Magufuli msibani akamuamkia shikamoo. Nadhani hadi goti alipiga.
 
Minaona isifutwe, lakini ifanyiwe maboresho kidogo na iongezwe herufi "B" pale katikati ya "M" na "OO"
 
sijakulia kwenye shikamoo salamu hii imeshamiri sana huku bara sijui Nini shida
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom