Nashauri salamu ya "Shikamoo" ifutwe

Nashauri salamu ya "Shikamoo" ifutwe

Habari za muda huu wana JF

Wanasema ukitaka kufanikiwa ni kuiga waliofanikiwa katika nyanja ambazo unaweza ukapita...

Inakera sana uko nchi za watu mdogo kwa mkubwa wanasalimiana kutokana na nyakati na salamu zao ziko balance....

Asubuhi ni GOOD MORNING mdogo anaweza akaipokea salamu hii kutoka kwa mkubwa na ikawa safi tu, mchana na jioni ni hivyo hivyo!

Huku kwetu mie naona hatupati maendeleo sababu ya hii salamu ya SHKAMOO

Haiwezekani unampa mtu shkamoo halafu unamuadabisha kwa adhabu huko makazini, hali hii inadhoofisha utendaji wa kazi in maximum....

Mtu mzima asipo ipata shkamoo basi mambo hayaendi! Nashauri zitumike salamu ambazo zitaleta mizania sawa kwa rika yoyote ili kushea mambo kwa uwazi zaidi.

Anyway nitaendelea kuandika hoja zangu ila niishie hapo kwasasa!

Karibuni kwa huu mjadala
Usishangae mbona bado watu wanazungumzia mabeberu na ukoloni mambo ya miaka ya 1960!
 
Shikamoo maana yake ni nakushika miguu. Kushika miguu ya mtu mzima ni kutaka baraka zake. Ndio maana watu kama wahindi wakisalimia watu wazima lazima wawashike miguu na yule mtu mzima atamshika kichwa huyo anaemsalim, ishara ya kumpa baraka na kumtakia mema.

Ila sisi ni kwasababu tumeirithi tu hatuipi uzito kiasi hiko. Ila ilitakiwa unapotoa salam ya shikamoo upige goti umshike miguu huyo mtu mzima unaemsalimu na yeye akushike kichwa akupe baraka na kukutakia mema.
Tatizo utashika muguu ya watu wangapi? Maana itabidi uache shughuli kisa "shikamoo". Maana wanao hitaji shikamoo njiani, ofisini, kwenye usafiri nk. ni wengi, nakumbuka mwalimu wangu wa Historia alikua hataki hata kulisikia, tatizo asili yake haikua kwa kheri. Babu zetu walishika miguu ya Waarabu kwa namna ya kudharauliwa..
 
Shikamoo humaanisha hivi...nipo chini ya miguu yako, mimi si lolote kwako, sina thamani juu yako, nakutukuza, unachoagiza kwangu kutekeleza ni wajibu, mimi ni dhaifu kwako, ukitaka kunipiga nipige tu hata siwezi kujitetea kwako mkuu nk.
Kwa muktadha huu inabidi shikamoo ihifadhiwe maktaba ya Taifa.
Tatizo wengi hawajui ni jinsi gani ilivyo dhalilisha babu zetu mbele ya Waarabu.. Inalembwa kuwa ni utamaduni, sijui historia n.k. Lakini iliwafanya babu zetu kuwa watwana..
 
Kitu ambacho kimenifanya nionekane jeuri mtaani na hata kwa familia nikiwa mdogo nakumbuka nilikuwa darasa la tatu niliomba maana ya hilo neno sikupewa maana yenye kueleweka toka hapo nikasema silitamki kumwambia mtu yeyote labda kama nakejeli basi nikasifika mtoto jeuri asie amkia wakubwa kiukweli lina kwaza nineno baya sana NAUNGA MKONO HOJA
 
Shikamoo maana yake ni nakushika miguu. Kushika miguu ya mtu mzima ni kutaka baraka zake. Ndio maana watu kama wahindi wakisalimia watu wazima lazima wawashike miguu na yule mtu mzima atamshika kichwa huyo anaemsalim, ishara ya kumpa baraka na kumtakia mema.

Ila sisi ni kwasababu tumeirithi tu hatuipi uzito kiasi hiko. Ila ilitakiwa unapotoa salam ya shikamoo upige goti umshike miguu huyo mtu mzima unaemsalimu na yeye akushike kichwa akupe baraka na kukutakia mema.
Sikubaliani na wewe "shikamoo " nineno lime toka kwenye lugha ipi tufafanulie na neno malhaba pia unatupoteza wewe unataka tuendelee kubaki gizani
 
Nikajua una salamu mbadala, kumbe utaahira tu. Sasa good morning ndio kitu gani? Yaani unasema shikamoo ni utumwa ila good morning ndio nzuri, kichwani una akili au makamasi?

Vijana wa siku hizi, badala watumie akili kufikiri wanatumia inye ndembe ndembe.
Muone huyu nae shikamoo ndiyo nini sasa ,mfano tumelala nyumba moja tumeamka wewe unaumwa au hauja amka vizuri mimi nakwambia shikamoo naondoka zangu kwenye shughuli zangu wewe utajisikiaje iyo siyo salamu lengo la salamu ni kujua hali ya unaemsalimia
 
Kwa hiyo good morning ndio salamu? Kwani umekatazwa kumsalimia mtu shikamoo kisha ukamuuliza umeamkaje au unaendeleaje?

Basi usisalimie kabisa punga wewe.
 
Kwa hiyo good morning ndio salamu? Kwani umekatazwa kumsalimia mtu shikamoo kisha ukamuuliza umeamkaje au unaendeleaje?

Basi usisalimie kabisa punga wewe.
Vip ukianza tu na"za asubuhi" au mchana au muda hisika nini kitakosekana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom