Nashauri mchakato wa Katiba Mpya uanze Januari 2026, lakini Tume ya Katiba Mpya iundwe Januari 2022

z12f

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
638
467
Nashauri mchakato wa katiba mpya uanze January 2026 (umalizike October 2028), lakini tume ya katiba mpya iundwe January 2022.

Tume huru ya uchaguzi ipatikane October 2023 (miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa October 2025).

Vyama vya siasa viruhusiwe kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa from January 2022.

Mada kuu ya katiba mpya iwe:

Katiba mpya iwe na a Bill of rights, itakayoheshimu basic human rights.

Muhimili wa Mahakama uwe huru.

Muhimili wa Bunge uwe huru.

Rais wa JMT asiwe na uwezo wa kulivunja Bunge la JMT.

Ikitokea kuna mvutano wowote ule usiotatulika baina ya Rais na Bunge, a national referendum ita amua nani kati yao aachie madaraka, na hakutakuwa na uchaguzi mpaka kipindi kijacho cha uchaguzi mkuu. Kama Bunge litashindwa referendum, nchi itakuwa haina Bunge mpaka uchaguzi mkuu ujao. Kama Rais atashindwa referendum, Bunge litamchagua kaimu Rais atakae kaa mpaka uchaguzi mkuu ujao. Kaimu Rais huyo anaweza awe au asiwe Makamu wa Rais wa huyo Rais ambae ameshindwa referendum.

Principle hiyo hiyo ita apply kwa Rais wa SMZ na Baraza la wawakilishi.

Wananchi wa pande zote za Muungano watapiga referendum kama upande wao unataka Muungano au la. Na kama wanautaka Muungano, wanataka Muungano wa serikali ngapi, moja, mbili au tatu.

Wananchi wa upande husika wa Muungano, watapiga referendum kama wanataka serikali centralised (kama sasa) au serikali za mikoa (zinazoiga zile za counties za Kenya, ila kwa Tanzania zitakuwa kwa level ya mikoa na sio kwa level ya counties/districts) au serikali za majimbo kama kule Nigeria. Mimi nadhani, kwa Tanzania serikali itakayo faa ni serikali za mikoa, zinazoiga zile za counties za Kenya. Serikali za majimbo kama za Nigeria hazitafaa.

Je, Bunge la JMT litakuwa na two houses (house of representatives na Senate) au litakuwa na house moja (kama sasa hivi)?

Since uhuru wa Bunge utaongezeka, basi qualifications za wagombea ubunge zifanane kabisa na qualifications za wagombea urais. Isipokuwa tu, umri wa mgombea ubunge uwe miaka 21 au zaidi.

Since muhimili wa mahakama utakuwa huru, basi qualifications za mahakimu na majaji ziwe zina fanana kabisa na qualifications za wagombea urais isipokuwa tu, umri wa mahakimu na majaji uwe miaka 21 na kuendelea, na wawe na degree ya sheria (au degree ya somo lenye uhusiano na mambo ya sheria).

Tume hiyo mpya ya katiba inaweza ichukue au isichukue mapendekezo ya rasimu ya katiba ya tume ya Warioba.

Mwenyekiti wa tume mpya ya katiba anaweza kuwa Jaji Mary Longway.
 
Hamna kitu hapo yaleyale tu yasiyo na maana..mahakama kuwa huru maanake Nini?itasaidia vipi kuwapa wasomi ajira ili elimu zao zibuni mambo yenye tija kwenye uchumi?

Rais kutolivunja bunge Ina msaada gani je itasaidia kuzuia miradi ya maji kuibiwa?
 
Mchakato wa katiba mpya huanza na sheria ya mchakato huo. Sheria ya mchakato huo iliyopita ilikuwa nzuri ila ilichakachuliwa katikati.
Kipengele cha kwanza kilichobadilishwa ni kile kilichohusu kama wananchi wataikataa katiba pendekezwa kwenye kura ya maoni nini kifuate. Mwanzo ilikuwa wananchi wakikataa katiba pendekezwa, ilikuwa unarudi kwenye tume ya Warioba ambayo ingeendesha mchakato wa kujua kwa nini wananchi wameikataa na kuja na mapendekezo mapya. Ilipochakachuliwa ikawa kwamba ikiwa wananchi watakataa, basi itatumika katiba ya zamani.Hii ndiyo sababu iliyofanya katiba ya Warioba inavurugwa kwani watawala walitaka katiba ya zamani iendelee.

Upatikanaji wa wajumbe wa bunge la katiba ulikuwa wa hovyo kabisa; eti wdc ndiyo inachagua wajumbe toka kwenye kata. Wajumbe wa wdc ni wanasiasa na hapo lazima waingize usiasa wao, na hayo yaliendelea hadi kwenye bunge

Bunge halipaswi kujigeuza kuwa la katiba kwani nkwa vyovyote vile utatokea mgongano wa maslahi. Linapaswa kuundwa bunge la katiba tofauti na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wajumbe wa bunge hilo wapewe masharti yatakayohakikisha mgongano wa maslahi hautokei au unapunguzwa kwa kiasi kikubwa, Kwa mfano, Mjumbe wa bunge la Katiba asiruhusiwe kugombea cheo chochote cha kisiasa katika kipindi cha miaka 10 tangu katiba mpya kuanza kutumika. Hii iwahusu na ndugu zake wa karibu yaani mmewe au mkewe, mwanae, babayake au mama yake, dada au kaka yake nk. Hii inapunguza uwezekano wa kutengeneza katika kwa matarajio ya kushika madaraka na kunufaika nayo, Mtakumbuka wazi wazi kwa mfano baadhi ya wawakilishi wa wafanyakazi walivyoonyesha nia za kuwa wagombea baada ya mchakato, wakaacha kutetea maslahi ya wafanyakazi katika katiba mpya wakatetea maslahi ya vyama vya siasa walivyotegemea wawe wagombea

Mengine mengi yaliyo kwenye katiba tuliyopendekeza sisi wananchi (Katiba ya Warioba) yalikuwa ni mazuri tu
Kwa ujumla mchakato usiongozwe na nia ovu na wahusika wote waamini kuwa kinachkwenda kuundwa ni kwa manufaa ya vizazi na vizazi vijavyo.
Naamini rais atakayesimamia mchakato huo vizuri atakumbukwa kwa muda mrefu kama siyo milele - si unaona bado tunamkumbuka Warioba
 
Umetoa some good background info ya jinsi mambo yalivyokuwa wakati ule, mwanzoni mwa mchakato wa katiba mpya.
 
Back
Top Bottom