Nasema tumechoka na mfumo DUME

Nasema tumechoka na mfumo DUME

Tuko jinsia tofauti sasa usawa unatokea wapi hapo dada zangu
 
Mwanasaikolojia wa Kike anahitimisha kuwa wanawake wote wanapenda kufanya kazi chini ya uangalizi wa mwingine, wanapenda kufanya kazi katika vyeo vya kawaida sio kama bosi...

Wanawake wote wanapenda kuhisi kuwa uwepo wao unatambulika na kuhitajika

Anaendelea kuwa anaamini mahitaji Haya mawili ya kiroho yanatokana na ukweli kuwa wanawake wanaongozwa na MIHEMKO (EMOTIONS) wakati wanaume huongozwa na AKILI....
Mara nyingi inaonekana kwamba si kwamba wanawake sio wana akili sawa na wanaume, Bali wakati Fulani huwazidi wanaume

Udhaifu wao pekee ni kuwa wana JAZBA sana . Kufikiri kwa wanaume kunatekelezeka zaidi, wanahukumu vizuri zaidi, na wanaaaelekeza wengine ( ni wakurugenzi) vizuri zaidi

Ubora wa roho (AKILI) ya mwanaume kuizidi ya mwanamke ni kitu kilichopangwa na maumbile yenyewe....
Jitihada yoyote mwanamke atayofanya kubadilisha ukweli huu itakuwa ni KUJISUMBUA BUREE....

Wanawake lazima waukubali uhalisia kuwa wako vile kwa sababu WANA MIHEMUKO SANA NA WANAHITAJI USIMAMIZI WA MWANAUME katika maisha yao.

Lengo kubwa LA maisha ya KE ni KUJIHAKIKISHIA HATIMA YAKE YA BAADAE. na akishalipata huziambia kwa heri shughuli zake nyingine
Ni mwoga kufanya mambo ya hatari.
uoga ni hisia za moyoni, ili kuzishinda KE anahitaji msaada wa ME....Kazii zozote zinazohitaji kufikiri muda wote zinamchosha...

Shy land kula tution ya buree
Kim nana pakua elimu tuipate hapa jukwaani•
 
Last edited by a moderator:
Usawa baina ya mwanaume na mwanamke hautakuwepo mpaka pale mwanaume atakoanza kuziona siku zake na mpaka siku mwili wa mwanamke utakapoweza kuzalisha mbegu za kiume na kuweza kumpa mimba mwanamke mwenzie
 
Mko poa sana wamama tunawapenda tu ila ninyi mnatumaind kwamba tunawanyonya. Basi na uwe mfumo jike maana kama sio dume ni jike. Haviwezi kuwa vyote.Ss tutavumilia muuite mfumo jike. Lakini muwe tayari kulia zaidi.
 
Kwahiyo mnataka na mimba tubebe sisi wanaume..?? Chukulia mfano wewe ndio kiongozi unapata ujauzito unawekwa bed rest nani ataongoza sasa...?? Familia mnashindwa kulea mnakimbilia fursa.. unataka upewe fursa ipi zaidi ya kuitunza familia..?? Ama hiyo siyo fursa ya kuleta maendeleo.?? Wanawake tunajua na wenyewe mnajijua mna mapungufu mengi sana... any way kila la kheri katika harakati zenu...

Ila hako kamsemo kenu ka kuwezeshwa mnaweza ni ka uwongo bora tu mkabadilishe hakana ukweli wowote wangapi waliwezeshwa wakashindwa..??

wanawake wenyewe ndo hawa wa bongo movies.,, taarab,, baikoko,, vigodoro,, ushirikina,, majungu + umbea,, wapiga picha za uchi,, madada poa... n.k n.k.... kazi mnayo kwa kweli
 
Jitambueni kwanza kwa wingi wenu hata mkiamua mwaka huu mchague raisi mwanamke mnaweza but majungu vijicho na kupenda miterezo mtamuachia nani? zamani kuna mademu shuleni unamuuliza mbona hujisomei? anakujibu kuna jamaa huko linanisomea (mume atakae kuja kumuoa )sasa kwa akili ya kushikiwa hivyo mnategemea nini?
 
Sijui nianze vipi, lakini kwa ufupi kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu sisi wanawake wa tanzania nasema kwa niaba ya wengi tumechoka na mfumo dume.

Kila mahali unaenda unakuta midume imejitutumuaaaaaa, mara miruzi fyuuuuuuuu, mara anti samahani oooooooh ~!@#@$%#@^#&$* tumechoka.Haya tuanze na majumbani mwetu, kila kitu kipaumbele anapewa mwanaume. Shule yeye, urithi yeye, nyumba yeye.

Tukija makazini hivyo hivyo, tunafanywa kama vitu, hupati kazi mpaka utangulize kitu.Jamani tumechoka.Tukija katika uchumi, tunadhalishwa sana na hatuthaminiwi juzi shangazi yangu karudi nyumani kakuta mjomba kauza mazao yote aliyolima.

Tumejaribu tumeshaweza kuwa na benki yetu, maana nyingine zimekuwa zikitunyanyapaa na hazijui mahitaji yetu. Kutokana na malaamiko yaliyomo vyuoni na sisi tunataka chuo chetu kikuuu tusinyanyaswe kijinsia na mijibaba mikware yenye kutoka udenda ionapo mwanamwali.

Bado kwenye nafasi za uongozi wa nchi hii tumesahauliwa tunadharauliwa sana. Yaani isingalikuwa wabunge wa viti maalimu, wabunge wanawake wangekuwa wa kuhesabu. Mwaka huu na sisi tunataka raisi mwamamke.

Historia ambayo imepindishwa pindishwa kuhusu uhuru wa nchi hii. Wanawake hawatajwi kabisaaaaa. Nauliza: Hivi ni wanaume peke yao ndio waliopigania uhuru wa nchi hii. Ni budi sasa iandikwe upya. Sisi tulishiriki kwa hali na mali zaidi, tena zaidi kupigania uhuru wa nchi hii, tulikuwa wahamasishaji wakubwa mikoani kuanzia Usangi mpaka Uyole. Mtwara mpaka Ngara. Kama si wanawake wa nchi hii usingepatikana. Toka uhuru tumekuwa tukipewa ahadi hewa, mnatutumia tu kushida huku mkituachia kanga, tishert , elfu kumikumi na sahani za wali miharagwe, lakini hamtekelezi madai yetu. Mwaka huu nasema hatukubali tena kutumiwa. PATACHIMBIKA


Kwa kumalizia ni haki katika nchi hii, sisi kinamama wa nchi hii mifumo ya mahakama imejaa mfumo dume tunaonewa mahakamani hatupati haki. Mahakimu wengi wanaume, wazee wamahakama wengi wanaume, majaji weeeeeeengi wanaume. Tena nauliza toka uhuru mpaka sasa mbona kumekuwa na wasomi wengi wanawake?, mbona hakuna jaji mkuu mwanamke. Ni wakati sasa na sisi wanawake tupate mahakama zetu. Mashauri yote ya yanayousisha wanawake yapelekwe kwenye mahakama zetu, natena nasema na sisi ni raia wa nchi hii.

ONYO :

  1. WANAUME ACHENI WANAWAKE TUDAI HAKI ZETU.
  2. WANAUME ACHENI BUNGE NA SEREKALI WAFANYE KAZI ZAO PINDI WATAKAPOAMUA KUTEKELEZA MADAI YETU.NASEMA ACHENI KABISA
  3. MADAI YETU NI YAMSINGI OLE WAKE ATAKAYEYAPUUZIA NA KUKEBEHI
​TUNAJUA TUNATAKA NINI KATIKA NCHI HII NA SISI NI WALIPA KODI PIA.

Tukiwezeshwa tunawezaaaaa
unajaribu kubishana na mungu.IQ ya mwanamke nu fupi kufanya maamuzi wala uongozi
 
Back
Top Bottom