Naseeb Abdul (Diamond Platinumz), akaliwa kooni na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Sipingi wala kuzuia serikali kufanya kazi yake ila kuna mambo yanachefua na kuudhi kama sio kufedhehesha unapochota maji kisimani kwenda kumwaga mtoni kwa kigezo kwamba maji ya mto yanafaidisha wengi kwa kuwa yanatiririka ila ya kisima yanamfaidisha mmiliki tu!

Diamond anastahili kupewa ruzuku kabisa, tujiulize ni utitiri wa watu wangapi anaowalipa mshahara,ambao serikali imeshindwa kuwaajiri, ana contribute kiasi gani kwenye uchumi wa nchi kupitia sanaa yake?

Serikali kupitia vyombo vyake vya usimamizi na ukusanyaji wa mapato ni kwa namna gani wameweza kukusanya mapato kupitia kampuni na taasisi zinazozalisha kwa kiwango kikubwa na ni vipi wametumia mapato husika?

Kaanza lini Music? Na Tra wameanza lini ......👎
 
Wivu tu, dogo katoka mbali mpaka kapata mafanikio Kuna watu w anabakia kulalama tu
Diamond kuanzia kuuza mi rumba hadi kuwa star ni hatua kubwa sana tena mtoto wa t Andale. ....hard work pays always

Swali
Dmond hatakiwi kulipa kodi?
 
Think...think...a bit further...ur half way to the truth...!!!

👉👉 Tax, ni lazima kwa kila kipato mtu akiingiza...No doubt, no qns about tht...🆒🆗

👉👉 What triggered all these, aanze kudaiwa leo, tokea 2010 to 2015 hajaulizwa...!? What is behind the door...!? Hapa ndio ujiulize...!!! Kuna kitu kikubwa...!!!


My very accurate assumptions kwnn wameanza mfuatialia...!

1: Labda kakataa kuimbia CCM ktk uchaguzi ujao...!!

2: Au kaingia mkataba na Lowassa ili amwimbie ktk kampeni zake za kutaka URAIS ndani ya CCM...meaning huenda kasha sign na contract nae...


Hizo sbb mbili hapo are possible causes tht triggered all these kwa sasa...!!!



Nimesikitishwa sana na baadhi ya watu mnaowashangaa TRA kwa maamuzi hayo badala kuwapongeza.
Mimi binafsi naona wamechelewa, walitaliwa wafanye hili suala zamani sana.
Kimantiki, mtanzania yeyote anayepata kipato ni lazima alipe kodi.
Yaani mwl anaelipwa laki nne analipa kodi halafu mnashangaa TRA kufuatilia kodi za Diamond?
Tuwekeni mapenzi na itikadi pembeni, kodi ni lazima ilipwe.
Hapa sitaki kuzungumzia hzo kodi wanazosamehewa wakezaji, cziungi mkono hata kwa dawa, ila hazina uhusiano na ulipaji kodi wa Diamond
 
[h=2]Lucky Dube – Taxman Lyrics[/h] I pay my gardener to clean up my garden
I pay my doctor to check out da other ting
I pay my lawyer to fight for my rights
And I pay my bodyguard to guard my body
There's only one man I pay
But I don't know what I'm paying for
I'm talking about the taxman
I'm talking about the taxman
I'm talking about the taxman

What have you done for me lately
Mr Taxman
What have you done for me lately
Mr Taxman
What have you done for me lately
Mr Taxman
What have you done for me lately
Mr Taxman

You take from the rich, take from the poor
You even take from me, can't understand it now
I pay for the police to, err...I don't know why
'Cause if my dollar was good enough
There wouldn't be so much crime in the streets
They tell me you're a fat man
And you always take and never give

What have you done for me lately
Mr Taxman

Soma dhima na Malengo ya kuwa na TRA na mamlaka zinazohusu mapato.
 
Tatizo la vijana wetu ni hii mijivuno ya Instagram ambayo mtu anataka kujipenadisha hata wakati hana uwezo huo. Huyu dogo katoka baada ya wimbo wa Mbagala hasa mwaka 2011 kuelekea 12 wala sio kabla. na kibaya zaidi show zake zote mapromoter ndio huchukua mchongo zaidi yake maana yeye husema kiwango tu cha ku perfom.

Sidhani kama kuna shida kubwa kuorodhesha fedha zote za mapato ikiwa sio yeye anayepanga na kugharamia show zake, na wala sio yeye anayepanga bei za cd kuuzwa isipokuwa hukatiwa chake mapema. na katika mabillioni yaloingizwa yeye alikatiwa sii zaidi ya asilimia 20 tu, hivyo Naseeb hana Utajiri huo kama inavyodaiwa. Majivuno ya mitandaoni imemponza..

Tunachoweza kumuasa ni kwamba kazi kama hizi anatakiwa kuwa na Mhasibu, kama anavyotakiwa kuwa na manager na wakili. hawa ni watu muhimu sana katika biashara yoyote ambayo unatakiwa kulipa kodi na maswala ya kisheria. Diamond hana utajiri huo, kwa bahati sana nafahamiana sana na mama yake toka enzi za Club na hakika wame struggle sana kufikia hapa walipo. Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi ktk janga hili..

- Lakini ndio maisha, misifa mingi mwisho wake huombewa kaburi!
 
Sipingi diamond kulipa kodi napinga double standard kwanini msanii mmoja tu, wakati wapo wengi hii ndo maana watu kulipa kodi tunachukulia kama uonezi fulani hivi, tra mjaribu kuondoa double standard hizo!!!!!!!
 
The sign of corrupt state,hivi Mwigulu JOKA LA MAKENGEZA YA PESA aka VISETI ameshalipa kodi ya pesa za IPTL na MERAMETA.Eti serikali inafulahia pesa za chenji za rada wahusika wanazidi kutupiga tu.Joka ebu tupige tena kabla ya kumaliza mwaka.WAJINGA NDIO WALIWAO
 
Soma dhima na Malengo ya kuwa na TRA na mamlaka zinazohusu mapato.

Nilikuwa najaribu kuonyesha hata wanamziki wakubwa walivoonekana kukerwa na mambo ya kodi!! Huyo dube aliwahi kuulizwa kuwa anapinga watu wasilipe kodi? akajibu.....nataka kujua tu pesa yangu inaenda wapi na inafanya kweli lichokusudiwa! (au ndio zinakusanywa apewe Chenge?)
 
Tuweke siasa pembeni, KWANINI asilipe kodi?? Who's Diamond by the way?? Kodi ni lazima ilipwe kwa kila kipato cha mtu yoyote na haiwezekani eti kusema kwa vile wachimba madini wamekwepa kodi basi na huyo diamond asilipe Naaaaah .....Kodi ni malipo kwa serikali msilete siasa kwenye sheria na pesa...sasa ndo atajua kuchunga matumizi nikiangalia na soon ataanza "Child support" huko uganda ..ni balaa.

Nafikiri issue sio Kwanini Diamond asilipe kodi, kila mwananchi anaepata Income ni lazima alipe kodi. Issue kwann Diamond, kwann tasnia ya muziki ambayo ndio inaanza kukua kwa kasi. Kwanini TRA isingeanza na watu wenye utajiri ambao hauwiani na kodi walizolipa TRA, kwanini haikuanza na wanasiasa na watu wa fani zingine?? Kwann haikuanza na wafanyakazi wa TRA wenye utajiri wa kupindukia?? Nafikiri kuna Siasa zaidi ya kodi. Revenue leakage nyingi sana kuliko kumrudisha nyuma huyu dogo. Wangetoa elimu kwanza kwa hawa wasanii kwani wengi wao hawaijui sheria ya kodi ya mapato sababu wengi wao darasa la saba.
 
Sipingi diamond kulipa kodi napinga double standard kwanini msanii mmoja tu, wakati wapo wengi hii ndo maana watu kulipa kodi tunachukulia kama uonezi fulani hivi, tra mjaribu kuondoa double standard hizo!!!!!!!

Kamanda umenena vema.....tuone wasanii woote wakiandikiwa barua kama ile hata kama wanadaiwa kiasi kidogo mnoo!!
 
Tunashindwa kuelewa tu kutokana na umaarufu wa dlamond ndio uliofanya jambo ili kujulikana lakini ukwel ni kwamba kulipa kodi ni jukumu la kila raia katika nchi yoyote kinyume chake usipolipa kodi utatoa faini au kifungo jela!!! Tusiingize siasa kwenye mambo ya msingi
 
Mi nahisi anayetakiwa kulipa kodi ni huyo meneja wa daimond Baada ya dai kuchukua chake halafu kwani Tz kuna msanii mmoja tu mbona hatuskii kina barnaba wakidaiwa??
 
Kwa sasa Daimond ana mashabiki wengi kushinda hata CCM asa kama ni fitna wajue kuwa Dai akishawishi tu nusu ya mashabiki wake wawapigie Ukawa basi ndo mwisho wa ccm ...
 
Naam hawa TRA walikuwa wapi miaka yote hii pamoja na umaarufu wa Diamond nchini na nchi za nje hawakujua kama ana mapato? Kwanini hawakuanza kumfuatilia 2010/2011 wasubiri mpaka 2015? Je wana data ulipaji kodi kama kodi ililipwa za wacheza sinema, wacheza mpira wote nchini ambao huingia mikataba ya mamilioni tangu mwaka huo wa 2010 mpaka 2014? Je wafanyakazi wa TRA ambao wanapokea rushwa wanalipa kodi inayostahiki? Yule mama kamishna wa TRA aliyekataa kuhojiwa na Tume ya Maadili kuhusu rushwa aliyopokea toka kwa Ruge ya shilingi milioni 80 kalipa kodi kiasi gani? Kwanini bado yuko kazini pamoja na kuthibitika kwamba ni mwizi na mpokea rushwa?

2010 mpaka 2014. kabla ya hapo je? Data mnazo? na kwanini msubirie mpaka miaka minne ipite? au mlijua anavuma kama upepo kisha anatoweka?
 
Maskini kijana wa watu Diamond kachumia juani sasa wanataka kumtoa mbuzi wa kafara.
 
tatizo lilianza pale alipotoa single ya kumfagilia lowassa... bila ya jujijua wanazidi kuipa umaarufu maradufu kile kibao...
 
Vijana wamebuni njia ya kipato TRA mnaibuka from nowhere mnajidai kukusanya kodi.
Ni kipi serikali ilichowekeza katika industry ya music ili uhalali wa kuchukua kodi uwepo?

Broo fikiria vizuri, bila mapato barabara zote za lami usingeziona! je wasanii hawazitumii? viwanja vya ndege vinavyojengwa ni mapato yetu navyo huvioni? wasanii wanaenda kupiga show ambapo miundo mbinu iko vizuri. unadhani miundo mbinu bora inashuka toka mbinguni? unaonekana hulipi kodi ww ndo maana hujui matumizi ya kodi!
 
Back
Top Bottom