Napitia kipindi kigumu sana wana JF. Nahitaji msaada wenu

Napitia kipindi kigumu sana wana JF. Nahitaji msaada wenu

Status
Not open for further replies.
Siyo dunia haina huruma.

Nchi haina mazingira rafiki ya uwekezaji. Watu wana hela zao, wakiangalia mazingira ya uwekezaji bongo wanaona bora wawekeze masoko ya kimataifa tu.

Mkuu kama mimi binafsi naamua najinyima kununua the latest BMW X7 na mambo mengine ya anasa, nakusanya sh milioni 400- 500, niamue kuwekeza kwenye kilimo hapo TZ, kitu ambacho naweza kufanya ndani ya mwaka, bila mkopo, unafikiri kuna ajira ngapi nitatengeneza hapo?

Sasa tukikusanyana watu kama mimi kumi, tukakusanya shilingi bilioni tano, mtaji wetu utaongeza ajira vipi hapo nyumbani?

Na unafikiri kwa figisu za sasa za ardhi, uraia pacha na ujinga mwingi wa serikali, mtu mwenye akili zake timamu ambaye ana paspoti ya nje lakini ni mzawa wa Tanzania anaweza kuwekeza hivyo?
Mkuu Kiranga na kuelewa sana na upo sahihi kwa angle uliyoiweka na tatizo la ajira serikali ndio chanzo.

Nilichomaanisha mimi ni kuwa dunia hii haina huruma wakati wewe unalia hauna kipato(kazi) unatafuta hata mtaji wa laki tano ukiamini utakutoa kimasomaso,upende wa pili wa shilingi hiyo pesa watu wanaimaliza kwa starehe zao(sio kosa).

Mkuu nikuache maana na mimi nina stress na changamoto hizo hizo za ajira.
 
Pole sana mimi mwizukulu mgikuru ninaahidi kukulipia chuo kikuu walau mwaka mmoja...lakini pia unaweza kumuona saalah hapo mabibo anaweza kukusaidia njoo pm nikupe maelezo zaidi.....humu jf kumejaa wachawi na watu wenye majungu utarogwa mdogo wangu
Mkuu na mimi naomba msaada wako.....inabidi tuombe kwa njia maana nyuzi hazisomwi na sometimes moderator wanazifuta.
 
Pole sana jitahidi ukipata kazi uwe muaminifu.
Kuna kijana alikuwa anatafuta kazi hapa jamiiforum, kazi za jamii ya media, graphics na printing. Nikamchukua kumbe ni mdokozi/mwizi.
Hawa ndio wanatuharibia ..,.....

Mkuu mimi natafuta sana kazi lakini pia nina michoro mitatu tofauti ya biashara inahitaji mtaji tu.
 
Amka asubuhi jaribu kupita site wanapojenga omba kibarua beba tofauti hapo kijana
 
Mdogo wangu komaaa.....mambo sio mepesi hasa ukitokea familia za kimaskini binafsi napita changamoto kama zako na inawezekana nimekuzid so usikate tamaa. Hafu una miaka 22 tu wengine tunaitafuta 28 na bado tunavumilia.
 
Sio rahisi kama inavyoandika ndugu.
Mie nimefanya hivyo mara kibao mkuu mpaka kuja kupata connection Kwa jamaaa akawa ananibeba kwenda site kama kibarua wake Sema siku hizi Hana kazi zimekata na mie nifanya Mishe zingine tu mkuu so kweli sio rahisi ila inawezekana
 
Mkuu Kiranga na kuelewa sana na upo sahihi kwa angle uliyoiweka na tatizo la ajira serikali ndio chanzo.

Nilichomaanisha mimi ni kuwa dunia hii haina huruma wakati wewe unalia hauna kipato(kazi) unatafuta hata mtaji wa laki tano ukiamini utakutoa kimasomaso,upende wa pili wa shilingi hiyo pesa watu wanaimaliza kwa starehe zao(sio kosa).

Mkuu nikuache maana na mimi nina stress na changamoto hizo hizo za ajira.
I Once Cried cause I had no shoes, Until I saw Someone with no Feet....

Unaweza ukakuta hao wanaomaliza kwa Starehe zao wana shida kuliko wewe..., Wakicheza Kidogo tu huenda Mikopo ikasumbua na nyumba kupigwa mnada....

All in all ni kama Confucius alivyosema...

In a country well governed, poverty is something to be ashamed of. In a country badly governed, wealth is something to be ashamed of.

Kwa nchi yenye resources kama Tanzania watu kukosa their three basic needs (na sio kwa uvivu bali kwa kukosa ujira) ni aibu kubwa sana.....,
 
Pole sana kwa kipindi kigumu

Komaa utaona mungu akikutendea miujiza
 
I Once Cried cause I had no shoes, Until I saw Someone with no Feet....

Unaweza ukakuta hao wanaomaliza kwa Starehe zao wana shida kuliko wewe..., Wakicheza Kidogo tu huenda Mikopo ikasumbua na nyumba kupigwa mnada....

All in all ni kama Confucius alivyosema...

In a country well governed, poverty is something to be ashamed of. In a country badly governed, wealth is something to be ashamed of.

Kwa nchi yenye resources kama Tanzania watu kukosa their three basic needs (na sio kwa uvivu bali kwa kukosa ujira) ni aibu kubwa sana.....,
Mkuu usicheze na Njaa mbaya sana......

Natamani sana watu wangekijua jinsi gani nilikuwa potential na smart kama mtu akiniamini na kuniheshimisha kunitoa kwenye hili laana just imagine sijala tangu jana na mfukoni ni tsh 1300....hii ni haki.
 
Kijana una miaka 22 unalia maisha magumu. Kuna vijeba wana miaka 35+ na hawana muelekeo wowote!

Pambana dogo umri bado mdogo kukata tamaa...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom