sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,486
Mimi kama mwalimu napinga kwa nguvu zote juu ya suala la chama cha walimu Tanzania, CWT kukusanya maoni ya walimu yanayotakiwa kutolewa kwa ajili ya uundaji wa bodi ya walimu. Zipo bodi mbalimbali za kitaaluma nchini, sidhani kama bodi hizo maoni ya wanataaluma hao yaliratibiwa na kukusanywa na vyama vyao vya wafanyakazi.
Msingi wa kupinga jambo hili ni mahusiano mabaya yaliyopo kati ya walimu na chama hiki ambacho kimekuwa kinafyeka 2% ya mishahara ya walimu, utapeli wa hisa wanazomiliki walimu katika benki inayodaiwa ni ya walimu pamoja na mambo mengine mengi ambayo yanajenga uadui kati ya walimu na chama hicho ambacho imefikia mahali hata viongozi wake wanaogopa kutembelea walimu mashuleni kufanya nao vikao kwa ajili ya mahusiano yao mabaya kwao.
Ni rai yangu kuwa suala la maoni ya kuundwa bodi ya walimu yafanywe na walimu wenyewe ili wawe huru kutoa na kuratibu maoni ya uundaji wa bodi itakayozingatia nidhamu ya kazi, maslahi kwa walimu, hadhi na heshima ya kazi ya ualimu, n.k