Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,677
- 218,188
Naomba kwanza niweke wazi kabisa kwamba mimi si mwanachama wa chama cha ACT WAZALENDO na pia si mfuasi wake na wala siingilii msimamo wa viongozi wa chama hicho kama wao wenyewe walivyoamua , bali ifahamike kwamba mimi kama Mtanzania wa kuzaliwa ninayo haki ya kujadili makandokando yoyote yanayojitokeza ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kuwekewa mipaka na yeyote kwa sababu zozote zile.
Uchaguzi wa Zanzibar kama ulivyokuwa uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano ulighubikwa na uchafu wa kila aina , watu wamedhulumiwa ushindi , wametekwa , wameteswa na kuuawa, viongozi kadhaa wa ACT WAZALENDO akiwemo Maalim Seif, Ismail Jussa na Mazrui wamekamatwa na kuteswa vibaya sana, huku viongozi wengine kama Khamis Bakari wakifariki baada ya kujeruhiwa kwa risasi , nyumba kadhaa kisiwani Pemba zimeteketea kwa kupigwa mabomu huku vikongwe wakiumizwa bila hatia yoyote.
Walioyafanya haya wapo na wanafahamika na ndio hao hao wanaotaka ushirikiano kwenye serikali na ACT inakubali ? sababu ya kukubali ushirika huu ni zipi hasa? maana ukikubali ujinga huu ni kwamba umeyakubali mauaji ya wazanzibar na mateso yao kwamba yalikuwa halali , nani atakuamini tena?
Kwa vile mimi ni Mcha Mungu , Mpenda haki na mpinga uonevu , natangaza hadharani kupinga ACT kuingia kwenye SUK ili kujiepusha na dhambi ya kujitakia ya kushabikia mateso na mauaji ya kisiasa ya raia wasio na hatia yoyote , Nawatakia kila la heri na fanaka watakaoshiriki kwenye Uharamia huo
Mungu ibariki Zanzibar.
Nakala: Juma Duni Haji