Ndoa naiona chungu na sijui la kufanya.
Mke wangu ananichukulia kama mtoto, aninaamrisha, ananitumikisha na pia huwa ananipiga.
Nimejaribu kupambana naye lakini nimejikuta nikiambulia maumivu na majeraha.
Sina pa kwenda kwani naishi naye kwenye tuliyoijenga wote.
Amekuwa na tabia ya kunikataza kuongea na baadhi ya marafiki zangu, na pia simu yangu amekuwa akinipora na kuangalia watu ninaowasiliana nao.
Nimezaa naye watoto wawili.
Mkubwa ana umri wa miaka tisa na mdogo wake ana umri wa miaka mitano.
Kibaya zaidi mtoto wetu mkubwa amekuwa akiwasilimulia wenzake jinsi ninavyokula kipondo.
Majirani wote wanajua taabu ninayoipata kutoka kwa mwanamke huyu wa kinyiha.
Unyumba ni hadi atake mwenyewe na nikimaliza kabla yake napigwa sana halafu naambiwa tuendelee na tendo la ndoa ambalo kwangu naona adhabu.
Nifanyeje kujinusuru na mateso haya?
mwanamke kumpiga mwanaume ni kitu cha kawaida. mimi mwezi uliopita, kusema ukweli, nilimuuzi sana waifu, akanitandika kibao cha uhakika hadi madogo sebuleni walikisikia....lakini nilicheka sana na kunyamaza kwasababu niliona nimekosea na nilideserve kumwomba msamaha kwasababu nilijua alifanya hivyo kwa provocation tu/hasira tu hakuwa yeye.
nasema hakuwa yeye kwasababu kabla hatujamjua Mungu, mimi nilikuwa na black belt ya shotokan karate, yaani sensei, ninao uwezo wa kutandika wanaume wasio professional hata watano peke yangu....na zamani, nilikuwa nampa kipondo waifu, kipondo cha mcheza karate kila siku...hahaha, lakini nilipookoka, nikabadilika...hivyo aliponitandika kibao nilijua tu kuwa sio kwamba anaona kuwa yeye ana nguvu kuliko mimi, bali amepitiwa tu, shetani amempitia kufanya vile ili mimi nirudie matapishi yangu ya zamani ya kumite...hahaha.
kawaida, si rahisi mwanaume kupigwa na mwanamke, kwa kabila la mashemeji zangu, ikitokea hivyo, basi ujue mwanaume uyo atakuvizia usiku akucharaze mapanga, akupige nondo au akishindwa kabisa atachukua kamba na utamkuta ananing'inia kwa hasira.
bro, huyo mkeo anakupiga akijua kuwa hautamfanya lolote, yaani utamhurumia kwani yeye ndo mama watoto wako. anajua wewe unampenda huwezi kumharibia reception/uso kwa mangumi ya mwanaume. NAKUSHAURI USIMPIGE hata kama unazijua ngumi, kwasababu si yeye, ni shetani aliyeko ndani yake. unaweza kumpiga ukashangaa ndo amendondoka moja kwa moja kwa ngumi moja tu, na unaenda kuishia jela na watoto atalea nani...watu wengine wana mshipa umebaki mmoja tu, na hao ndo huwa wabishi sana kwasababu wanajua utaogopa kuwamalizia...mwombe Mungu aondoe iyo roho chafu kwa huyo mama, ajue ya kuwa mume ni kichwa cha nyuma na mwanamke analazimika kumheshimu na kumtii mmewe. akizidi sana, chukua taxi mlete nilipo mimi nitamfundisha adabu nione kama ataendelea kujifanya anapigana na wanaume....