Napendekeza - kilimo na ufugaji forum

Mgombezi

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
610
178
JF Support Team

Naomba kutoa pendekezo la kuwepo kwa KILIMO NA UFUGAJI FORUM ndani ya JF kama zilivyotengwa forum za Business & Economic, Jukwaa la Siasa n.k. Kwa sasa naona mada nyingi zinazohusu Kilimo na Ufugaji zimekuwa zikiwekwa katika Business & Economic Forum, ambapo bado ni jambo jema bali pendekezo langu linalenga katika kupata mada husika kwa urahisi.

Hivyo basi taarifa zote zinazohusu Kilimo na Ufugaji zinaweza kukusanya na kuwekwa katika forum hiyo, kuna nyakati kumekuwa na mada ambazo zimekuwa zikirudiwa kujadiliwa.

Wadau mnaonaje hili, ni mapendekezo tu.

Nawakilisha!
 
Mkuu Mgombezi
ni wazo zuri kama itatekelezwa.. naamini itawavuta watu wengi kuangalia sekta hii kwa marefu na mapana kwani bado ni mbichi kabisa.
nigependekezwa iitwe KILIMO KWANZA Forum kuakisi kampeni ya kitaifa ya Kilimo Kwanza.:coffee:
 
Itasaidia kuongeza michango ya mawazo kwenye mada za kilimo na ufugaji. Pia itakuwa rahisi kutafuta mada husika zilizokwishajadiliwa zamani.
 
Mkuu hili wazo ni zuri,sana.na ombi hili lilishawahi kutumwa apo awali.MODs tunaomba uweke forum ya kilimo na Ufugaji.mimi najitolea muda kufuatilia hili.
ktk Chai Day nilifanyia kazi jambo kama hili kwa kutengeneza forum ya Jamii farm-kilimo na ufugaji.Busara yangu ikaona bora nisiwe wa kwanza kulitamka. Incase JF MoDs wakikataa itabidi tufanye hivyo. You can view it Jamii Farm
 
Naungamkono Mkuu unayosema ni sahihi tunaomba wahusika walishughulikie
 
JF Support Team

Naomba kutoa pendekezo la kuwepo kwa KILIMO NA UFUGAJI FORUM ndani ya JF kama zilivyotengwa forum za Business & Economic, Jukwaa la Siasa n.k. Kwa sasa naona mada nyingi zinazohusu Kilimo na Ufugaji zimekuwa zikiwekwa katika Business & Economic Forum, ambapo bado ni jambo jema bali pendekezo langu linalenga katika kupata mada husika kwa urahisi.

Hivyo basi taarifa zote zinazohusu Kilimo na Ufugaji zinaweza kukusanya na kuwekwa katika forum hiyo, kuna nyakati kumekuwa na mada ambazo zimekuwa zikirudiwa kujadiliwa.

Wadau mnaonaje hili, ni mapendekezo tu.

Nawakilisha!

Hata mimi mwezi jana nimewasiliana na invisible akasema wataangalia, kumbe lilisha wahi kushughulikiwa! wazo zuri
 
Back
Top Bottom