Napenda sana mavazi ya wanawake wa kiislamu hasa mambo safi

View attachment 354866
View attachment 354867
Habari wadau..

Kiukweli mimi ni mkristo..

Ila napenda sana wadada wa kiislamu wanavyovaa mavazi yao na ushungii

Yaani yana staha sana na yanafanya uone mumewe anaenjoy sana..

Unamkuta mdada kashuka kwenye range lake na hijab yake...

na hata akivaa suti au formal dress la ofisini.. akipiga na ushungi wake anapendeza sana..

yaani unaona tofauti kubwa sana kati ya mke wa mtu wa kiislam na wa kikristo..

Mtu baba ana oil com, lake oil, home shopping na mabiashara mengine makubwa makubwa lakini ana staha.. hana dharau.. dress code ya heshima tele hadi unatamani awe wako..

Ila ukute mambo safi wa dini yetu..

Hicho kiminii.. kikuku na nyodo ofisini..

Hayo mavazi ni kama anashiriki umiss

Waislamu japo mna mapungufu yenu ila kwenye dress code ya wanawake mpo juu sana..

Kuna tofauti kubwa ya mavazi ya mwanamke aliyeolewa wa kiislam na kikristo..

Hata kumtongoza kipuuzi puuzi mtu unaogopa mavazi yake tu yalivyo mpa heshima kubwa...
Mi mwenyewe yananikosha sana. Ila cha kushangaza kuna siku moja nimlimsikia mdada mmoja wa ki islam akitamani wavaavyo wadada wasio wa islam kwa namna wanavyo onesha miguu yao yenye mivuto. Nao pia wanapenda opozitly
 
Huyo ame astray
 
Ule ni utamaduni wa kiarabu. Uislamu ndo umekopi utamaduni wa kiarabu na kuuendeleza.

So sifia waarabu walioanzisha na sio waislamu.
Jifunze kwanza ndipo useme.
Jiulize aya za hijabu zimekuja lini? Na kabla ya hapo wanawake wa kiarabu walikuwa wanavaa vipi?

Kukusaidia yapo masharti 8 ya vazi la mwanamke wa kiislamu. Na yameletwa na Mtume Muhammad,kabla ya hapo hayakuwepo
 
Kasome Quran kuhusu sitara ya mwanamke utaelewa vizuri mkuu. Kanzu ndio utamaduni wa kiarabu lakini hijabu au mtandio ni utamaduni wa kiislamu na sio utamaduni wa mwarabu.
Muongo, hijabu ni utamaduni wa kiislamu? Toka enzi za middle Persians huko, wanawake walivaa hivyo na hawakuwa waislamu tena watumia nguvu za giza hadi basi.

Waisraeli enzi na enzi walivaa hivyo pia au ulikuwa unauzungumzia ule uislamu wa kufikirika ambao nguzo zake uliousimamisha si hizi za leo za kwenda kuhiji Makha, kufunga Ramadhan nk?
 
Ule ni utamaduni wa kiarabu. Uislamu ndo umekopi utamaduni wa kiarabu na kuuendeleza.

So sifia waarabu walioanzisha na sio waislamu.
Nuns habit and Hijab are one and same thing. Hongera watawa/nuns kwa kuendeleza tamaduni ya waarabu.
 
Muongo, hijabu ni utamaduni wa kiislamu? Toka enzi za middle Persians huko, wanawake walivaa hivyo na hawakuwa waislamu tena watumia nguvu za giza hadi basi.

Waisraeli enzi na enzi walivaa hivyo pia au ulikuwa unauzungumzia ule uislamu wa kufikirika ambao nguzo zake uliousimamisha si hizi za leo za kwenda kuhiji Makha, kufunga Ramadhan nk?
Mkuu unaweza kupinga kwa lugha nzuri ili kuelimisha kuliko kutukana
 
Ukristu si dini ya kimwili ni ya kiroho, "spiritual" inasemekana Mungu ni roho na uabudiwa ktk roho. Aliwaumba wakiwa uchi na waliishi hivyo. Umeambiwa usipofikia viwango vya kufanana na mtoto hutofika Mbinguni kamwe. TAFAKARI!

So, dhambi si kutenda tu ni hata kutamani. Hapo nini maana yake, ukiuvaa Ukristu hutotapika najisi, hivyo si lazima zitumike nguvu za ziada za kimwili kama mavazi kuushika Ukristu, fanana na mtoto, hata wote wakiwa uchi hawazioni tofauti zao kamwe.

Hata hivyo, kwa mila zetu mpya za kiafrika si vyema kujiweka uchi. Halafu wengi wetu hatuujui Ukristu, tunauchanganya na tamaduni za kimagharibi. Mwanamke ni marufuku kusali pasi kufunika kichwa chake, mwanaume haruhusiwi kufunika kichwa chake, fundisho la kikristu hilo. Wapo wanalitii sana, hata pale Riverside father Nkwera, anaishi hivyo na kanisa lake.
 
Ule ni utamaduni wa kiarabu. Uislamu ndo umekopi utamaduni wa kiarabu na kuuendeleza.

So sifia waarabu walioanzisha na sio waislamu.

Ule sio utamaduni wa kiarabu ! Ule ni utamaduni wa Kiislam, nchi za waarabu ni nyingi, je wanavaa kama hivo? Nenda Bahrain sehemu ambazo watu wake baadhi ni waarabu lakini hawavai hivo!

Huo ni Uislam na Uarabu SIO uislam kamwe !

Na haya hayakuanza kwenye Uislam tunaona masanamu yanayoshabihishwa na Bikira Maria (Mwenye ez Mungu amjaalie Salaam) yamevaa kama huyo Dada hapo juu! na tunaona Masister wa Roma wa Kikatoliki kule Italia wakibaa kama hivo! ukiangalia Sinema za Mitume ilopita Nabii Mussa (Moses) (Salaam ziwe juu yake) NAbii Yusuf (Joseph) (Salaam ziwe juu yake) Ndio maana tunasisitiza Mtume Muhammad Ni Mrithi wa Mitume yote ilotangulia na ndio chimbuko la Uislam.

Nakupa vipande vya Quraan kukuonesha kuwa hilo si vazi la waarabu. Sura ya Nuru kuanzia aya ya 30 mpaka 31

Hapa wanaambiwa wanaume

30. Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za wanayo yafanya.

Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.

Haya ni MAneno ya kweli kutoka kwa Mwenye ez Mungu.
 
Jifunze kwanza ndipo useme.
Jiulize aya za hijabu zimekuja lini? Na kabla ya hapo wanawake wa kiarabu walikuwa wanavaa vipi?

Kukusaidia yapo masharti 8 ya vazi la mwanamke wa kiislamu. Na yameletwa na Mtume Muhammad,kabla ya hapo hayakuwepo

Umesahau kama Mtume S.A.W alikuwa Mwarabu
 
Mie napenda vya ndani tu mavazi yao huwa wakati mwingie siyaonagi ndiyo maana naendelea kuwamix tu
 
Mkuu unaweza kupinga kwa lugha nzuri ili kuelimisha kuliko kutukana
Kuna mahali nimetukana hapo Mkuu? Wapi? Mbona ni lugha nyeupe pee kabisa au mi siyajua matusi? Nioneshe Mkuu, kuna kuangamia kwa kukosa maarifa. Yataje tu hayo matusi ili kama nina jema nililolikusudia nilioneshe au kama nimekosea niombe radhi. Kwangu matusi ni mwiko Mkuu haswa ktk kujifunza.
 
Mkuu unaweza kupinga kwa lugha nzuri ili kuelimisha kuliko kutukana
Hapa kidogo naweza kukuelewa, ingawa bado kuna kitu labda hujanielewa. Kuna maneno mawili ilinilazimu niyatafakari nilipoambiwa nimetumia matusi. "Muongo" na "kufikirika" labda.

Nianze na la uongo, labda ni kali ilitakiwa niseme "hukusema ukweli" au "wewe hujui" lingepunguza huo munkari, samahani kwa waliokwazika na aksante kwa kunifunza jambo. Unajua humu tuko wa jamii na tamaduni tofauti, ndo chanzo sorry.

Kufikirika, hapa kwangu sipata mbadala hili neno. Labda kulingana na imani au udadafuzi mwingi nilioufanya. Mi imani kwamba uislamu haukuanzishwa na Mtume Muhammad, hainiingii akilini, ndo maana nikatumia neno "kufikirika" haupo, ni dhahania tu, chini ya hapo nimekuwekea kwanini ni kufikirika, uislamu una nguzo zake, Nabii Sulemani lazima angeenda kuhiji tu. Yesu, Musa, na wengine.

Kwahiyo kwangu, middle Persians hawakuwa waislamu, kwanza si tu uislamu hawakuwa hata Ibrahimists. Ila walivaa hijabu kama zivaliwavyo leo, labda tofauti ni nakshi kule zilizidi, tena si hijabu hii rahisi no ile total hadi uso.
 
Ule sio utamaduni wa kiarabu ! Ule ni utamaduni wa Kiislam, nchi za waarabu ni nyingi, je wanavaa kama hivo? Nenda Bahrain sehemu ambazo watu wake baadhi ni waarabu lakini hawavai hivo!

Huo ni Uislam na Uarabu SIO uislam kamwe !

Na haya hayakuanza kwenye Uislam tunaona masanamu yanayoshabihishwa na Bikira Maria (Mwenye ez Mungu amjaalie Salaam) yamevaa kama huyo Dada hapo juu! na tunaona Masister wa Roma wa Kikatoliki kule Italia wakibaa kama hivo! ukiangalia Sinema za Mitume ilopita Nabii Mussa (Moses) (Salaam ziwe juu yake) NAbii Yusuf (Joseph) (Salaam ziwe juu yake) Ndio maana tunasisitiza Mtume Muhammad Ni Mrithi wa Mitume yote ilotangulia na ndio chimbuko la Uislam.

Nakupa vipande vya Quraan kukuonesha kuwa hilo si vazi la waarabu. Sura ya Nuru kuanzia aya ya 30 mpaka 31

Hapa wanaambiwa wanaume

30. Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za wanayo yafanya.

Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.

Haya ni MAneno ya kweli kutoka kwa Mwenye ez Mungu.
Iko poa kabisa.
 
Hapa kidogo naweza kukuelewa, ingawa bado kuna kitu labda hujanielewa. Kuna maneno mawili ilinilazimu niyatafakari nilipoambiwa nimetumia matusi. "Muongo" na "kufikirika" labda.

Nianze na la uongo, labda ni kali ilitakiwa niseme "hukusema ukweli" au "wewe hujui" lingepunguza huo munkari, samahani kwa waliokwazika na aksante kwa kunifunza jambo. Unajua humu tuko wa jamii na tamaduni tofauti, ndo chanzo sorry.

Kufikirika, hapa kwangu sipata mbadala hili neno. Labda kulingana na imani au udadafuzi mwingi nilioufanya. Mi imani kwamba uislamu haukuanzishwa na Mtume Muhammad, hainiingii akilini, ndo maana nikatumia neno "kufikirika" haupo, ni dhahania tu, chini ya hapo nimekuwekea kwanini ni kufikirika, uislamu una nguzo zake, Nabii Sulemani lazima angeenda kuhiji tu. Yesu, Musa, na wengine.

Kwahiyo kwangu, middle Persians hawakuwa waislamu, kwanza si tu uislamu hawakuwa hata Ibrahimists. Ila walivaa hijabu kama zivaliwavyo leo, labda tofauti ni nakshi kule zilizidi, tena si hijabu hii rahisi no ile total hadi uso.
Nashukuru kwakuniekewa.
Kuhusu uislamu ulianzia wapi,nakushauri jifunze hasa nini uislamu na ni lipi lengo lake.

Uislamu maana yake ni kujinyenyekeza kwa muumba,kwa kutii mafundisho na maagizo yake na kujiweka mbali kwa kujiepusha na aliyoyakataza.
Utayajua hayo kupitia manabii na mitume aliowaleta. Akawapa vitabu uwe muongozo wao.

Lengo kuu likiwa ni kumuabudu yeye pekee bila kumshirikisha na chochote.
Hili ndio lengo kuu la mafundisho ya mitume wote waliotumwa.

Pamoja na kutofautiana zama,lakini lengo kuu limebaki hilo. Wote wanaungana kwenye lengo kuu. Wanatofautiana jinsi na njia ya kulifikia lengo hilo kutokana na kutofautiana zama na mazingira.

Mfano amri kumi kuu alizokuja nazo Mussa, yakwanza ni kukataza ushirikina. Uwepo wa miungu tofauti na Mungu muumba.
Ukija kwa Yesu anasema " na uzima wa milele ni huu,wakujue wewe Mungu wa pekee na wakweli na Yesu kristo uliemtuma".

Ukija kwa Muhammad nae alifundisha shahada mbili kama msingi wa kuwa muislamu au kinyume chake.
1. Kukiri na kuamini kwamba Mungu ni mmoja asie na mshirika.
2. Kukiri na kuamini kuwa Muhammad katumwa na Mungu huyo mmoja.

Ukitazama mafundisho hayo,utakubaliana nami kwamba,wote walifundisha uwepo wa Mungu mmoja asie na mshirika. Na pia iliwapasa wafuasi wao wakiri utume wa hao wajumbe.

Huu ndio msingi wa kuwa uislamu haukuanzishwa na Muhammad. Kwani mitume wote mafundisho yao ya msingi yalifanana ila tuu walitofautiana njia ya kuyaendea.

Ama kuhusu nguzo tano alizofundisha Muhammad,hiyo ni njia aliyokuja nayo kwa ajili ya kufikia lengo kuu ambalo ndio nguzo ya kwanza(amri)
 
Back
Top Bottom