DINHO
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 886
- 1,750
Kwenye kutafuta ajira kuna mambo mengi sana. Wasakatonge tunahangaika huku na huko kutafuta mrija wa Asali, iwe nje ya nchi au ndani ya nchi, iwe serikali au taasisi binafsi.
Sasa basi nikiwa mmoja wa wasakatonge nilibahatika kuomba hizi kazi za TRA, na mara baada ya kuomba nikafanikiwa kupata Group moja la tulioomba kazi.
Kupitia hili group bhana, juzi usiku nikaona mjadala umeanza, mmoja wa wanagroup alitoa angalizo kuwa iwapo wasailiwa watafanana kwa marks basi kuna kigezo cha mavazi kinatumika katika kuwaondoa au kuwapata best candidate.
Kwamba watu wavaze official, kwenye usaili inakuwa rahisi kupata kazi, na mjadala ukawa mkubwa sana.
Tiliozoea kufanya saili mbalimbali hasa za serikali tukakubaliana yes mavazi ni muhimu sana, na yanachangia kwa asilimia kubwa kwenye kuchaguliwa kupata kazi.
Hapa sasa akatokea member mmoja akasema kigezo cha Mavazi hakitumiki kwenye kuchagua best candidate kwa maana Mavazi ni kipimo cha utajiri wa mtu au familia. Hivyo kigezo cha Mavazi hakiwezi kuwa sifa moja wapo ya mtu kuajiriwa na kwamba mtu anaajiriwa kwa uwezo wake kichwani.
Na ikiwa umepata ajira basi taasisi husika ndio itakuwa kanuni na taratibu za mavazi ya taasisi hiyo kama mwajiriwa.
Akaenda mbali zaidi akasema kama mavazi yanaamua nani aajiriwe kwanini wasiweke sare maalumu za usaili ili watu wote waende wakiwa sawa kimavazi?
Nilitamani kuona ule mjadala unaendelea nipate kuona namna gani sisi vijana tunaweza kuchambua mambo kisomi na kwa kuzingatia Dunia inavyoenda. Bahati mbaya leo asubuhi nimeingia nimeona group sasa wenye uwezo wa kutuma kitu ni Admins tu.
Binafsi nimeona saili nyingi ma HR wakiangalia mavazi, na wengi wamekosa kazi kupitia uvaaji.
Je, wadau tujadili hapa, mavazi yana uhusiano na upatikanaji wa kazi? Na je unakubaliana na hoja ya jamaa kuwa mavazi hayapaswi kuwa kigezo cha mtu kuajiriwa bali weledi na uwezo wake wa kujua mambo?