Naomba nikwambie ukweli tu kua hutopata sponsor kwa njia hii hata siku moja, sanasana utapata matapeli, na kama ungekua mdada wangejitokeza wanaojifanya kukusponsor kumbe kuna kitu wanakitaka kutoka kwako.
Jiulize, kwa nini mtu yeyote yule aku~sponsor wewe? Ni mtu mzima, tayari umesoma kitu kingine, una nini special cha kumfanya mtu akulipie wewe hela, naomba jibu lako lisiwe tu "mi maskini" hakuna tajiri ambaye yeye kazi yake ni kugawa tu pesa na hapo umesema 7Million, aitoe kwa mtu ambaye hata hamjui wala hana faida yoyote ile kwake. Kama ingekua ni wewe upo kwenye level zao sidhani kama ungetoa, matajiri wengi wanaombwa pesa na watu mbalimbali kila siku.
Sababu chache zinazoweza mpa mtu sponsorship, na hii nisiite sponsorship bali scholarship, na sio ya short courses, ni full scholarship ya kitu kama degree,
1. Mtu ambaye ni very smart, anafaulu masomo yake yote, track record nzuri na kaonyesha kua anafuture nzuri huko mbele, naongelea hapa A tupu sio kupata BBB alafu ukadhani ni smart hayo ni matokeo ya kawaida sana.
2. Mtu ambaye yupo kwenye group la special needs, naongelea kama wanawake kwenye sector flani, au ana matatizo ya mwili, na hawa wanapewa scholarship mara nyingi na institutions ambazo zinapewa funding kutoka sehemu mbalimbali.
Usipoteze muda wako kutafuta email za watu wenye pesa na kuwatumia ujumbe wakusponsor, unless una kitu very compelling to offer labda umegundua dawa ya ukimwi au kurefusha maisha then utakua unapoteza muda wako. Na hizi short courses ni ngumu sana kupata sponsorship kwa kua wengi hawaoni umuhimu wa hizi courses. Kama ni mfanyakazi wa umma labda ungeweza bahatika maana serikali nayo kuna courses chache hua inatoa scholarship, jaribu kuzifuatilia ujue.