Muhimbili University(MUHAS) Special Thread

syndicate

JF-Expert Member
May 5, 2016
204
315
9d55fb0080ce14aeac3caaf61cfa3294.jpg

Habarini wadau wote wa sekta ya afya, pia wanazuoni wote toka kila pande ya Tanzania!
Karibuni sana katika uzi (thread) huu unaohusu masuala mengi kuhusu Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS!
fd97654e54ba09d7098c7877601f0dea.jpg


HISTORIA FUPI (Short History);

Kilianza mwaka 1963, Wakati huo kikiwa kama shule ya Tiba (medical school), ndani ya Chuo kikuu kishiriki cha Dar es salaam(UDSM), ya Kilichokuwa Chuo kikuu cha Afrika Mashariki.
Mwaka 1991 shule ya Tiba(medical school) ndani ya chuo kikuu Dar es salaam,UDSM!
Baada ya kukidhi vigezo kadhaa vya kitaaluma, kilipitishwa na kuwa kitivo cha Tiba yaani Faculty of medicine! na mwaka huo huo kitivo icho kikapandishwa na kuwa Chuo Kikuu Kishirikishi cha Afya Muhimbili ndani ya UDSM, Muhimbili University College of Health Science, MUCHS. Kikishirikiana na Muhimbili Medical Centre,MMC wakati huo.
Mwaka 2007 kupitia sheria ya bunge inayounda vyuo vikuu Tanzania, Chuo kikuu cha Tiba na sayansi shirikishi Muhimbili, yaani Muhimbili University of Health and Allied Science, MUHAS kilizaliwa rasmi kama chuo kikuu kinachojitegemea kwa kila kitu..!
Hapa nazungumzia miundombinu, Uongozi, na Mambo mengine ya kisheria kama Taasisi.

KUHUSU MUHAS(About MUHAS);

262653d7bf3aa1d0ad39f454ffa8ab50.jpg


ADRESS; BoX 65001, website; http:/www.muhas.ac.tz
Idadi ya wanafunzi mwaka 2017/18, Undergraduates Bachelor Degree(3,861), Dip(369), Postgraduates(526), PhD Enrolled(29).

Chuo Hiki ni chuo pekee ndani ya Tanzania ambacho kiko specific,yaani kimejikita rasmi kwenye masuala ya Afya na Sayansi Shirikishi za kitafiti pekee (Strategical Educational Institute), Kikiwa kinashirikiana na Taasisi nyingine za kitafiti wa kisayansi ndani na nje ya nchi katika kuendesha shughuli na miradi ya kisayansi, hasa ile ya kitafiti mfano mzuri Kwa kipindi fulani chuo kilikuwa kinaendesha mradi fulani wa Malaria kushirikiana Chuo kikuu cha Harvard(Harvard University) cha Marekani!

Kitaaluma Chuo hiki ndani ya Tanzania japo sio kikongwe kama vyuo vingine toka kuanzishwa kwake kama taasisi ya elimu ya juu inayojitegemea, yaani independent institute! (yaani 2007) ndani ya kipindi kifupi yaani miaka 10 (yaani 2007 mpaka 2017),
Kimeweza kuwa miongoni mwa vyuo vikuu vitatu bora kabisa vinavyotoa elimu ya juu ndani ya Tanzania kwa ujumla! (Hakika hapa kuna vichwa makini, na wabobezi wanaowajibika, Hongera).
Chuo hiki kimegawanyika katika maeneo mawili ya ufundishaji yaani campuses, Kampasi kongwe ni Muhimbili yenyewe (Main Campus).
39983e017d9d26ce9e6887a0b1865698.jpg

pia kampasi mpya ya kisasa kabisa ndani ya afrika mashariki na kati, Mloganzila kampasi (Mloganzila Kampasi).
5141e83a2066217eaab0040bf71175cf.jpg

Inayopatikana Umbali wa Km.23 nje ya jiji eneo linaloitwa Kibamba karibu kabisa na ilipo manispaa ya Ubungo,23km kutoka katikati ya jiji Dar es salaam.

MUHAS ina Taasisi(Institutes) mbili, yaani Taasisi ya Tiba na Sayansi shirikishi (Institute of Allied Health Science, IAHS) na Taasisi ya Tiba Asili (Institute of Traditional Medicine,ITMed).
IAHS wanatoa stashahada(Diploma) na Stashahada ya Juu (Advanced Diploma), Pia ITMed wanatoa Shahada za uzamivu yaani master degrees pekee.

IAHS kupitia Shule ya Afya ya Jamii na Mazingira(School of Hygiene) ina campus zake Tatu(03) nje ya Jiji la Dar es salaam, yaani Dodoma (Mpwapwa) na Tanga (Ndani Shule ya Uuguzi Tanga) kwa wale wanaosoma afya yaani ngazi ya stashahada,EHS!
Pia Moshi kwa wale wanaosoma stashahada ya Utaalam wa Mifupa yaani DOT (Diploma in Orthopedic Technology).
630a9e81a4fa7754eac8e6963eb17015.jpg


IKUMBUKWE KUWA;
Wizara ya Afya inaprogramu maalum ya kufundisha wataalamu wake Muhimbili, chini ya taasisi yake IAHS lakini wanafunzi hao hawako ndani ya tawala za kitaaluma au mfumo wa chuo kikuu cha Muhimbili, Muhimbili University,MUHAS!
Wahusika hapa ni wale wanaosoma DnMD (Diploma and certificate in Midwifery), DDLT (Diploma in Dental Laboratory Technology), Advanced Diploma in Clinical Dentistry na Midwifery yaani ADCD na ADM(Advanced Diploma in Midwifery),
Hivyo academic welfare za wanafunzi hawa ziko chini ya wizara kuanzia mitihani mpaka awards zao kama vyeti na stashahada wanazopewa wakimaliza chuo!

MAHALI KILIPO(Location);
697e3f8830a3e21eb73b476c3ea5f393.jpg

Main campus iko ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndani ya jiji kubwa, la pili kiukuaji ndani ya Afrika mashariki lakini linaloongoza kwa Idadi ya watu kwa sasa (takribani watu milioni 5-6) yaani Dar es salaam, Manispaa ya Ilala, Tarafa ya Upanga, Kata ya Upanga Magharibi Umbali wa takribani mita 700-800 toka makutano ya barabara ya Morogoro na Barabara ya Umoja wa Mataifa,United Nations Road, pia inapakana (adjacent) karibu kabisa kabisa na Shule ya sekondari ya wavulana Azania.

UONGOZI (ADMINISTRATION);

b5f635ea7c3f23bc37cd44b23119b922.jpg


Idadi ya staffs; 342

Chancellor; H.E Alhaj Dr. Ali Hassan Mwinyi.

Vice-Chancellor (VC) ; Ag.Prof.Appolinary Kamuhabwa( Anakaimu nafasi akisubiriwa mteuliwa atayechukua nafasi hiyo ndani ya taasisi hii nyeti ya Tiba Tanzania , pia ni Mteuliwa rasmi Kushika nafasi ya Naibu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Tafiti na Mashauriano,DVC-ARC)
~Former VC; Prof. Ephata E. Kaaya.

Depity VC-ARC; Prof.Andrew Pembe.
~Former DVC-ARC; Prof. Eligius F. Lyamuya.

DVC-PFA; Prof A.R.Kamuhabwa/recently Ag.VC.

DVC-HR; Prof. S.Aboud

Council Chairman;Mr.D.A Ntukamazina.

DEAN OF STUDENTS; Dr. Tumaini Nyamhanga.
~Former(Dr. Deodatus CV. Kakoko)
DEANS.

S.Medicine- Prof.S.F Kaaya(F)
Associated. Prof.PS Muganyizi

S.Dentistry-Dr.EN Simon
Associated Dr.S.Onibingire

S.Pharmacy-Prof.G.Kagashe
Associated Dr.J.Sempombe

S.Nursing-E.Tarimo
Associated Dr.C Mbekenga

S.Public Health And Social Science,PHSS. Including EHS.
Prof.DP.Urassa
Associated.R.mpembeni.

DIRECTORS.
Director.CEPD(Continuing Edu)
Dr.DAS.Mloka

Director. RP(Research and Publication)
Prof.S.Aboud
Deputy.Dr.J.Masalu

Director P.S
Prof Pembe A.
Deputy.Dr.E.Balandya

Director. Planning and Investment,P,I(Muhimbili Campus)
Dr.E.Mmbaga

Director. P.I(-Mloganzila Campus)
Prof A.Kamuhabwa
Deputy Mloganzila
Dr.P.Chillo

Director UE(Undergraduates Education)
DUE,Prof Mainen J. Moshi

Director Quality and Assurance
Dr.GH.Leyna
Deputy O.Nyongole

Director ICT
Mr.F.Sukuma
Deputy Dr.F.Mashili

Director TM
Dr. E.Innocent

Director IAHS
Mr.Lalison E. Ndolele

Director Library Services
Prof. ET.Lwoga

Director H.R
Mr.A.Nnko

Director Estate
Arch.L.Kejo

Ag.Director Finance
Mr.T.Tibenda

HOSTELS:
Chuo kinamiliki hostel zake chenyewe, kwa wanafunzi wote wanasoma post na undergraduate! pia wale wa internship.

Zipo zilizopo ndani ya mazingira ya chuo yaani main campus na zingine nje kidogo ya chuo.
Ndani ya chuo nitazitaja baadhi;

95cb5d437447c23a4acbddc449c66cd9.jpg


01.Ruvu,
02.Kagera,
03.Lukuledi
(Sifa ya hosteli hizi ni kwamba kila chumba anaishi mtu mmoja mmoja kwasababu vitanda ndani ya chumba ni kimoja kimoja but fundamental rule ya kubebana ipo pale pale, Ingawa vyumba ni cubed (Portioned)! plus vidirisha ni vidogo vidogo sana!
yaani kwa 3rd years watakaokuwa accomodated hapa ni full joto wenyewe wanaelewa!),
aisee feni linahusika sana hapa, Kutokana na Uwepo wa miradi mbalimbali ya kisayansi na Ukaribu wa chuo na Bonde la Mto msimbazi mbu wamezalishwa na kuzaliana kwa wingi hovyo kuleta usumbufu mkubwa nyakati za usiku kwa wagonjwa, wafanyakazi na Wanafunzi, Ingawa effect yao kwenye malaria ni very low said to be sterilized, lakini ni nuisance! jiandae kwa neti!

04.Chole Hostels(Masaki)

Kwa wale first year mnaenda kukaa uko chole, room moja mtalala wanne hapo ni changanyikeni. Mtakutana na watu wa tabia tofauti tofauti, wezi(angalieni sana vi-laptop vyenu na bidhaa nyingine valuable, msijiachie sana), wachafu na wapiga exiles(kwa wale wenye girlfriends nafikiri wamenielewa, kuna watu wanauwezo wa kupiga exile chumba kizima(watch out, not to that extent maybe not this time, in magufuli's voice), wapiga misuli mirefu kuliko kawaida yaani mashulez, walevi(wanatapika hovyo, na kuleta bugdha wakilewa japo hairuhusiwi kuingia na kilevi eneo al hostel, wapo wabishi), wavuta sigara na sigara kubwa!, wafujo, wasichana opportunist (Gold diggers), wale wanaojifanya wanamalengo (dating from day one to date), wasichana wasiotulia n.k

KWA WALE WA DIPLOMA:

Hostel ziko mbili; zote ziko chini ya MNH(Muhimbili National Hospital);

e05238cd0f489fd697279fbcefd823ac.jpg


01. MTC Hostel, Hii hosteli kwa Muhimbili ni kama hotel ya nyota 5, japo inachangamoto kubwa ya ukarabati wa miundombinu, miundombinu ni mibovu sana na ukarabati wake unakwenda taratibu sana na kwa kusuasua! Idadi ya wanafunzi kwa kila chumba MTC ni 2, lakini kubebana kupo, mpaka 4 wanalala humo! na mambo mengine kama yale ya pay as you have been served ni harmonised!
(WATCHOUT FIRST YEARS,
MTC ROOMS AND RESIDENTS ARE MASTERED IN EXILES!).
Hostels hizi ni changanyikeni pia anybody either symbiotic or venture capitalist from anywhere in muhas institutions can win and be accomodated! (Kiufupi zinapendwa sana, Vyumba vikubwa vya kutosheleza).
Uko utawakuta mpaka masters embarked so wengi wenu mnaopiga Paramedics lazima mkasote nursing kwanza ushamba uwatoke then ndo mje uku ( so called paradise), na hapa sio Dip tu mpka Degree wa course zingine ambao either awapendi kwenda chole au wamekosa vyumba kule au kuuza!

02.Nursing Hostels.
Uku ndo uswazi ya Muhimbili,
kila aina ya species inapatikana uku, katika kila sector,
Room zake zina accomodate watu 8, zile kubwa mpaka 10, lakini mabingwa wa kubebana wanafika mpaka 16 au 14 in one room,
dah yote maisha, ili mradi shule iende, miundombinu ni tatizo la mda mrefu,
vyoo kuziba na mashida mengine yanayosababishwa na wakina dada ni kitu cha kawaida uku,
remember, uku kuna chukua wanafunzi wengi mno.
wakiwemo wasichana wengi ambao ni manesi!,
ukipangwa uku uvumilie mengi, trust nobody except oneselfs'.

STUDENTS AFFAIRS.
Wanafunzi wa Dip from institute of Allied Health Science IAHS,
na Bachelor degree wanawakilishwa na vyombo viwili tofauti vya serikali za wanafunzi, yaani MUIAHSSO
ec7c5d97eef85b59c05e538a32b210d3.jpg

na MUHASSO[
IMG]http://www.jamiiforums.com/mobile-gallery/24f58f333097a687e59b72690769fc2a.jpg[/IMG]

, Japo kuna juhudi
mbalimbali za kuziunganisha serikali hizi pamoja kuunda serikali moja yenye maslahi kwa wanafunzi wote,
lakini bado kuna changamoto kadhaa yaani conflict of interest from both sides,
kama vile Tanganyika na Zanzibar yaani ipi itakuwa nchi na ipi itakubali kuitwa mkoa,
ukizingatia zote zilikuwa nchi zenye mamlaka kamili!
(Tuwaachie wanafunzi wanaMUHAS wenyewe waamue mustakabali wa serikali yao.
dde37facce8334eeca95cdaf53c1192d.jpg


SUP-03
First years uwe EHS, PHARM, MD, RTT,MEDICALA LAB, RADIOGRAPHY AU KOZI YOYOTE MUHAS aiseee! sikutishi, ila kama unataka uendelee kuishi kwa amani ndani ya muhas na kufurahia maisha ya shule na mtaani jitahidi we bwana usikutwe na kitu inaitwa sup3 , ngoja nielezee kidogo hii kitu yaani hapa namaanisha kupata supplementary tatu za kozi(courses) tofauti ndani ya mwaka mmoja wa masomo! kwa mfano semester ya kwanza ulipata sup 01(yaani ulifail somo moja na kuapata chini ya wastani ambao ni 50%) then semister ya pili ukapata tena sup 02 kwabahati nzuri au mbaya ni OFF YOU GO! pia ukipata sup 03 ndani ya semester moja OFF YOU GO (DISCONTINUATION no CARRY), hata kama una GPA first upper class au second upper we bwana we, utakwenda na maji hasa ukiwa first year na second year, wapo wengi waliokwenda na maji! wamedisco hapa namaanisha sup03=DISCO yaani rudi nyumbani kalime maharage na kunde, watu hawakuangalii usoni unaishia uku unajiona! atleast inshu yako isiwe ya uzembe,
utafikiriwa lakini kama ni uzembe, SUEC haikufikirii mara 02, unakwenda na maji,
Ukisoma mambo sio magumu kiviike ,KUMBUKA THIS IS MUHAS! Ukikutwa na kibomu (Desa) AU simu ndani ya chumba cha mtihani ready handed OFF YOU GO!
Kikubwa zaidi any problem consult with Dean of Students office togther with Counseling an d Guidance office they are so humble! wanasikiliza! wanashauri wanasaidia!(Inshort ni Wazazi, and they deserve) Don't go there when its too late! wahi mapema kabla mambo hayajaharibika!!

577a11234906bc6f25f7af17390324d1.jpg


MABONANZA:
Chuo kina utaratibu murua wa kuandaa mabonanza na matamasha maalumu kwa wanafunzi,
f447541b7bb9dc58dc2fcc65a31966a1.jpg

kupitia serikali za wanafunzi na wizara za michezo na burudani, Hapa udhamini mbalimbali kunogesha shughuli hizi uzingatiwa!
mfano. welcome first years (kwa first year hapa mtaenjoy sana),
Usiku wa bata, Get together parties, Farewell parties, na Sports Bonanzas.

78ad9a925fd92cec4f71264feeb4921c.jpg


KARIBUNI KWA NYONGEZA NA MASAHIHISHO, LAKINI USITUKANE, TWENDE PAMOJA, CHOCHOTE KUHUSU MUHAS LETA HAPA! Mods naomba m-repost hii thread!,its very important..!! Don't burn it!!
 
Mimi mvivu wa kusoma aisee ngoja niwaachie wengine wasome.

Mimi huyoo
 
Mmmhhh gazeti lote hili

Halafu mbona siku hizi mnaibuka na mbinu mpya mpya za kutaka watu wajifunue toka kwenye anonymous

Maana hapa mtu akichangia tu ile style yake ya kuweka maujanja yake itasomwa na kufatiliwa kwa karibu na watu wa hapo chuo mwisho wa siku anakua kajianika bila kupenda
 
Very interesting.

Zingatia huu ushauri.

Pia weka picha mpya ya Jengo la MOI ya sasa hiyo ya zamani wakati wa ujenzi itoe
Nime edit hapo juu, nimeweka! nliandika night sana ! maana sikuwa na muda wa kutosha! hope kwasasa inapendeza kidogo! karibuni sana! Changia chochote ambacho unaona kitatuweka pamoja! Ninapokea ushauri mzuri kwaajili ya maboresho, Muhas are forever!!
 
Halafu mbona siku hizi mnaibuka na mbinu mpya mpya za kutaka watu wajifunue toka kwenye anonymous [/QUOTE said:
@ Numbisa, nakuhakikishia hakuna mtu wa kukufuatilia kiasi icho, Unless uwe mange kimambi( b´se she is another case in Tz) Karibu, lete experience yako ndani ya MUHAS!!
 
Je, Na hao DDLT na DNm wanajumuishwa kwenye sherehe au matamasha mfano welcome first year ya muhas au wao hawashirikishwi??
 
Je, Na hao DDLT na DNm wanajumuishwa kwenye sherehe au matamasha mfano welcome first year ya muhas au wao hawashirikishwi??
Epafras1 Eliah, Swali zuri sana, kwe ye matamasha na sherehe mbalimbali zinazofanyika ndani ya chuo au hata nje, hata kwenye orientation na Ratiba za mitihani hasa UE wanakuwepo na wanashiriki kama kawaida japo wao hawana mtihani unaoitwa UE, unaweza ukajiuliza kwanini..!? jibu ni rahisi ni kwamba wanakamilisha ratiba ili waende sawa na wenzao! kinachowatofautisha ni Ratiba za CA, lecture theatres au room za kusomea!, Jinsi wanavyoshiriki matamasha ya michezo au mabonanza, mfano mpira n.k kulingana na uchache wao hawanabudi kujiunga na madarasa mengine! la mwisho kubwa ni siku ya ku-graduate hawaingii kwenye kitabu cha graduation cha MUHAS! wala hawapewi nafasi kwenye graduation field! Graduation zao hazijulikani zinakofanyikiaga! lakini naamini wizara huwa inawawekea utaratibu fulani wa kuagana nao kama wanafunzi!! kama kuna swali karibu..!!
 
Axant xn kw upande wang umenikosh xn ume2fumbua mach kuijuw muhimbil... me ni mwnafunz wa PCB nnandoto zakuja muhimbili MD naomb ushaur wko...
 
Axant xn kw upande wang umenikosh xn ume2fumbua mach kuijuw muhimbil... me ni mwnafunz wa PCB nnandoto zakuja muhimbili MD naomb ushaur wko...
Soma sana kijana, Japo sijajua uko form V au VI, lakini concept ni kuwa usome! PCB doesn't need a genius one but somebody wise with contents!, kama hauna content utafail na kuona umepoteza muda wako wa miaka miwili bure! Unatakiwa kuwa more strategically, Be focused, kuwa mkweli washirikishe wazazi matatizo yako ya kitaaluma, usiwe mjuaji sana kama unataka kuwa na content kubwa ya kuperform vizuri, Mshirikishe Mungu shida zako uvuke salama! kama ni mtu wa wasichana try to win them academically not sexually! Bila Division One sahau kusoma MD Muhimbili, bila Division One O´level sahau kusoma Diploma yoyote MUHAS! huo ndo ukweli! Asikudanganye mtu!! Wanaposema Wanafunzi wa MUHAS wanaringa sio kwamba wanaringa bali ni kuwa kwao vizuri kichwani toka ngazi ya Diploma mpaka Postgraduate! Ndio kuna wapa watu inferiority Complexes! ni watu humble, wako vizuri!!

Sent from my HUAWEI Y330-U11 using JamiiForums mobile app
 
Soma sana kijana, Japo sijajua uko form V au VI, lakini concept ni kuwa usome! PCB doesn't need a genius one but somebody wise with contents!, kama hauna content utafail na kuona umepoteza muda wako wa miaka miwili bure! Unatakiwa kuwa more strategically, Be focused, kuwa mkweli washirikishe wazazi matatizo yako ya kitaaluma, usiwe mjuaji sana kama unataka kuwa na content kubwa ya kuperform vizuri, Mshirikishe Mungu shida zako uvuke salama! kama ni mtu wa wasichana try to win them academically not sexually! Bila Division One sahau kusoma MD Muhimbili, bila Division One O´level sahau kusoma Diploma yoyote MUHAS! huo ndo ukweli! Asikudanganye mtu!! Wanaposema Wanafunzi wa MUHAS wanaringa sio kwamba wanaringa bali ni kuwa kwao vizuri kichwani toka ngazi ya Diploma mpaka Postgraduate! Ndio kuna wapa watu inferiority Complexes! ni watu humble, wako vizuri!!

Sent from my HUAWEI Y330-U11 using JamiiForums mobile app
Dah axant xn kw ushaur mzr naamin one day ntaingiy muhimbil ila namb contact zko ikiwezkan....
 
Axant xn kw upande wang umenikosh xn ume2fumbua mach kuijuw muhimbil... me ni mwnafunz wa PCB nnandoto zakuja muhimbili MD naomb ushaur wko...
Dah axant xn kw ushaur mzr naamin one day ntaingiy muhimbil ila namb contact zko ikiwezkan....
Hivi vijana mmeingiwa na mdudu gani?
We kweli mwanafunzi wa form six unaandika hivi? Serious???
 
Back
Top Bottom