Nape waombe radhi serikali ya mapinduzi Zanzibar, adai Seif alikubali muafaka sababu ya njaa zake!

ANGALIA MAUNO YA MTU HUYU , UNADHANI ANAWEZA KUFIKIRI MAMBO KWA UBONGO AMA KWA KIUNO HIKOHIKO.
Alianza ndani ccm matusi , wakamchekea anakuja hadi kwa viongozi wa Ngazi ya Makamu Ya Makamu wa ZNZ, Akimaliza atamcha Kikwete , nani anabisha ..................
263787_230841496937271_100000342668655_811926_2580271_n.jpg

 
hii ni CCJ inaji re establish .... hapa kuna very coordinated underground movements za kutafuta support ya hili genge la Nape na Sita ..... there is a dirty game played inside CCM ..... and i am sure CCM will be in a rat trap soon...... usije ukashangaa CCJ ikarudi ki vingine
 
Kama kuna mtu aliye karibu na Nape, basi amshauri aombe msahama kwa Maalim Seif personally na kwa CUF- Zanzibar. Kuna tofuati kubwa sana kati ya CUF-Zanzibar na CUF- Tanzania Bara na naweza kusema hivi ni vyama viwili tofauti. Kwa kiasi kikubwa baada ya serikali ya umoja wa kitaifa (SUK) CCM -Zanziar are on thier way out, hoja nyingi za CUF zinakubalika na wana-ccm lakini walikosa ujasiri wa kuongea hadharani kabla ya SUK. Kwa sasa hivi mchawi ni Tanzania Bara na blunder ya Nape inazidi inazidisha munkari wa CUF ku-dismantle CCM. It is a bit technical lakini kama ccm wanataka kuwa na matawi hata mawili basi Nape aombe msamaha yaishe. Itakula kwa ccm hii kitu, tena vibaya mno. dont understimate Maalim Seif.
 
ANGALIA MAUNO YA MTU HUYU , UNADHANI ANAWEZA KUFIKIRI MAMBO KWA UBONGO AMA KWA KIUNO HIKOHIKO.Alianza ndani ccm matusi , wakamchekea anakuja hadi kwa viongozi wa Ngazi ya Makamu Ya Makamu wa ZNZ, Akimaliza atamcha Kikwete , nani anabisha ..................
263787_230841496937271_100000342668655_811926_2580271_n.jpg
Sure.as Tanzanians we have to be very carefully with this group-ccj founder atherwise itakula kwetu
 
kwa wanaoelewa siasa ya Tanzania hivi ni sahihi kweli kwa kijana mdogo kama nape kumusema maalim seif mbele ya umma kuwa alikuwa ananjaa ndio mana aliidai madai yake serikali asiyoitambua.Kwa maoni yangu kamkosea heshima itabidi amuombe radhi.

Hizi ni siasa mpya! Nape yupo sahihi kwa wakati wake.
 
Hii Nimeikuta katika gazeti la Tanzania Daima.
Kama ni kweli haya yamesemwa na CCM ni hatari sana kwa mwafaka wa ZNZ.
Tunaelekea wapi ?

_______________________________________________________________________________________________________________

Matusi haya kwa Maalim Seif hayavumiliki



Josephat Isango

Tanzania Daima 24/07/2011


JULAI 17, mwaka huu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Nape Nnauye, amembeza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, kuwa njaa yake ndiyo iliyomfanya aitambue Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na hatimaye kukubali kuingia kwenye serikali ya mseto.

Haya ni madai mazito sana dhidi ya kiongozi wa chama cha siasa aliyepewa dhamana ya kuwaongoza wanachama kote Tanzania Bara na visiwani. Tena mtoa kauli, yaani Nape Nnauye naye hakusema kwa bahati mbaya, alisema alichojua, alikisema kilivyo, na kinapaswa kupokewa kilivyokusudiwa. Ujumbe umetumwa na umepokewa.

Nnauye aliyasema hayo wiki hii wakati akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wenye lengo la kuelezea maana ya CCM kujivua gamba uliofanyika jijini Mbeya.

Alisema baada ya Hamad kubanwa na njaa kali aliamua kurudi kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kudai alipwe mafao yake kama kiongozi wa serikali hiyo, wakati akiwa haitambui.

Siamini sana kama kweli Maalim Seif, alifikia kiasi cha kuwa ombaomba wa chakula. Siamini kabisa kama kweli Maalim Seif akiwa Katibu Mkuu wa Chama cha wananchi (CUF) alikuwa halipwi mshahara unaomwezesha kujikimu. Kupata chakula, kuvaa, kupata matibabu, na kuweka mafuta katika gari na kuhudhuria mikutano.

sijui Maalim Seif amemkosea nini Nape na chama chake mpaka anamvua nguo hadharani mbele ya Watanzania? Nape hivi kweli juhudi zote za CCM kusaka muafaka kumbe ilikuwa ni danganya toto?

Mbona Nape unawatukana Wazanzibari na Wapemba? Mbona unawakosea kina Karume waliojipatia heshima kwa jambo la muafaka? Haya si maneno ya kutamkwa na kiongozi mwenye busara. “Tulimuuliza anataka alipwe mafao yake na serikali ipi, maana wakati huo yeye (Sharif Hamad) na chama chake walikuwa hawaitambui serikali, ndipo alipokubali kuitambua serikali ya Karume (Rais Mstaafu wa Zanzibar),” alisema Nape.

Ni vema Nape akatuambia serikali ya chama chake ilimuuliza Maalim Seif kuhusu mafao anayoyataka mbali na yale yaliyopo kwa mujibu wa sheria na Katiba ya Zanzibar ambayo inaweka bayana ni viongozi wa aina gani wanapaswa kulipwa mafao.

Kama nilivyowahi kusema, CCM wana fedha, wanaweza kununua vitu vingi sana, ila wameshindwa kununua mtu mmoja tu angalau mwenye nafuu ya kufikiri, atakayewashauri hiki waseme na kile wasiseme. Hiki waseme wapi na hiki wasiseme wapi. Si kila ukweli unasemwa kila mahali.

Ingawa katika hili ambalo ni la kipuuzi, Nape alisema ukweli kuwa kilichokusudiwa na CCM kwa inavyoonekana nia ya CCM haikuwa muafaka, wala maridhiano ya kisiasa ila kukiangamiza kabisa Chama cha Wananchi (CUF) na kumuondolea heshima kwa wanachama wake Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad.

Rais Kikwete alisema suala la mpasuko wa kisiasa linamkosesha raha, alitamani muafaka upatikane. Jambo hilo alilisema mwaka 2005 alipokuwa akifungua Bunge. Kwa wajuvi wa mambo, kauli ile ilikuwa ikimaanisha alivyokuwa akikerwa na wana ndugu wa Zanzibar. Kutengana, kuuana, kuharibiana mali na vitendo vingine vilivyokuwa vikiharibu sifa nzuri ya nchi hiyo.

Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, alifanya jitihada za makusudi za kufuta historia mbaya ya visiwa hivyo kwa kushirikiana na CUF kufanya maridhiano ya kugawana madaraka ambayo pia waliwashirikisha wananchi wa visiwa hivyo.

Nape ameamua kuwatukana Karume na Maalim Seif, wazee hawa walijitutumua kupiga kampeni za serikali ya mseto, kumbe katika CCM wengine walikuwa na malengo tofauti. Wanawaona wenzao wa CUF wana njaa, hawaangalii kuwa jambo hilo lilifanyika kwa manufaa ya taifa.

Karume alikuwa akisema: “Lugha ya hapana inastahili kusikika katika sula la kataa malaria, kataa dawa za kulevya, kataa bangi lakini huwezi kukataa amani na utulivu ndiyo maana nitawashangaa wote watakao kataa suala la serikali ya umoja wa kitaifa.”

Mbona hapa suala la njaa halitajwi? Nape alikuwa wapi siku hizo? Kwanini Nape anawakosea adabu wazee hawa? Mbona anapayuka ovyo? Hakuna mshauri huko CCM? Mbona anawatukana Wazanzibari waliopiga kura kutaka serikali ya mseto kuondoa migongano isiyo ya maana?

Upuuzi gani huu? Mwanasiasa gani huyu? Hizi ndizo propaganda na itikadi za chama chake kutukana waliotangulia na kuasisi mambo mazuri?

Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, aliwahi kuwasisitiza wananchi wa Zanzibar kupiga kura ya ndio ilikayofanyika Julai 31, 2010 iliyoamua kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi wa mwaka jana.

Alisema angewashangaa sana Wazanzibari ambao wangepiga kura ya hapana kwa vile maridhiano yaliyofikiwa yamesaidia kujenga amani na mshikamano kwa wananchi wake, hivyo kuna haja ya kuendelezwa ili kudumisha amani ambayo vizazi vijavyo vitakuja kurithi mazuri na hali ya amani inayoendelezwa hivi sasa.

Maneno kama haya yalipaswa kuja kubezwa na kijana mdogo kama Nape? CCM inatupeleka shimoni. Inatuchagulia viongozi wapuuzi wanajisemea ovyo, wanasema kila kitu wanachofikiri bila kufikiri athari yake.

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, ni miongoni mwa walioshadidia kauli hiyo ya serikali ya mseto akasema: “Ndugu wananchi tujiandae vizuri katika kura ya maoni kwa sababu amani haiuzwi dukani, zipo nchi hazina amani kama vile Somalia, hawana serikali, ni matatizo makubwa katika nchi hiyo, sasa sisi tuwe wamoja, tujenge nchi yetu na nchi hujengwa pale penye umoja na mshikamano.”

Hivi hawa wazee wote walikuwa na ajenda ya njaa ya Katibu Mkuu wa CUF? Kweli wazee hawa walikosa busara kiasi hicho? Hapana, Nape amezidi kuropoka. Katika hili, anapaswa kuomba radhi hadharani. Kuwaomba radhi wanachama wa CUF kwa kumdhalilisha kiongozi wao, kuwaomba radhi Wazanzibari waliopiga kura ya maoni kukubali maridhiano.

Kauli ya Nape ambayo mpaka sasa hakuna kiongozi mkuu mwingine wa CCM aliyejitokeza kuisahihisha au kuilaani kunathibitisha Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi ametumwa kuharibu maridhiano, na huyo aliyekutuma haijulikani kama ana nia nzuri au mbaya.

Nape hana wakubwa? alitumwa na nani kusema udhalilishaji kule Mbeya? Ulitumwa na nani useme kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, alisukumwa na njaa kutaka serikali ya umoja wa kitaifa?

Hivi Nape anatambua kuwa chama chake ndicho kilichoridhia serikali ya mseto hata kama kwa shingo upande, sasa kwanini amdhalilishe Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar? Kiongozi huyo anatoa matamshi hayo kwa matakwa ya chama chake au ana kundi lake lenye ajenda iliyojificha?

Inawezekana kiongozi huyo ametoa kauli ile kwa manufaa ya kundi hilo? Binafsi nashindwa kuelewa kwanini mpaka sasa CUF wamekaa kimya, ukimya wa CUF unathibitisha kuwa viongozi wao walioko madarakani ni waganga njaa, na kuwa hawakuwa wapinzani ila walitaka kutambuliwa.

CUF jiepusheni na aibu ya kuwepo madarakani halafu mnadharauliwa na kubezwa hadharani. Mbona maneno haya Nape hakuyasema Zanzibar? Mbeya walikuwa wamemuuliza Nape? Nini hatima ya kauli za kipuuzi na kupuuzwa kama hii?

Kama hiyo haikutosha, Katibu wa Fedha na Uchumi, naye akajidai kumtolea uvivu, kwa kumtukana mzee wa watu, akasema kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ni mfano wa wanasisa wapinzani wanaofikiria masilahi.

Nchemba Mwigulu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM) alisema kuwa baada ya kupata uongozi ngazi ya serikali mzee huyu sasa ameanza kunyoa ndevu, jamani matusi gani haya kwa Makamu wa Kwanza wa Rais aliyekubali kuingia kwenye maridhiano ili kuleta umoja wa kitaifa Zanzibar?

Mwigulu naye anapaswa kumwomba radhi mzee huyu na kuwaomba radhi Wazanzibari.

Sikutegemea kauli kama hizi kutoka CCM, eti “Mnakumbuka kule Zanzibar walikufa watu 27 lakini leo Maalim Seif yuko Ikulu na ndevu zake ananyoa, ananawiri tu, je, waliokufa wamefaidika na nini?”

Tuwe wakweli tumhoji Mbunge huyu na Katibu wa Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi, Mwigulu, je, waliuawa kwa sababu gani? Waliuawa ili watu wasiridhiane? Pamoja na kwamba ninajitahidi hapa kumtetea mzee wetu, Maalim Seif Sharif Hamad kuwa ametukanwa, ila kwa upande mwingine mambo haya CUF mmejitakia.

Nasema wamejitakia kwa sababu iliungana na CCM kwa lengo la kuleta umoja lakini wenzao hawakufanya hivyo kwa roho safi, ndiyo maana hivi sasa wameanza kejeli na udhalilishaji ambao kimsingi haupaswi kuachwa uendelee kuota mizizi.

Fedheha uliyofedheheshwa Maalim Seif inatosha!

Mgogoro uliozaa wakimbizi Watanzania kwa mara ya kwanza, mgogoro uliosababisha Watanzania kuuawa, mgogoro uliosababisha Wazanzibari kutopanda chombo kimoja cha usafiri, mgogoro uliosababisha watu kutengana kwenye shughuli za mazishi, mgogoro uliovutia mpaka kelele za mataifa ya nje, unapoisha ndipo Nape anaona si jambo jema, anazungumzia njaa ya Maalim Seif, Mwigulu, anazungumzia ndevu za Maalim Seif! Haya ni matusi ya nguoni,
yanayostahili kuombewa radhi kwa Watanzania wote. Ikiwezekana wasemaji wa kauli hizi watafakari au kupima upya uwezo wao wa kuongoza siasa za Tanzania. Dalili zote za nje zinaonyesha ni wachochezi na wasiofaa.
 
View attachment maalimu.bmpView attachment maalimu.bmpeEEe
Habari kwa hisani ya Nova Tzdream -
Zanzibar,

Kufuatia matamshi ya kejeli yaliyotolewa na katibu wa Itikadi na uenezi Bw Nape Nauye pamoja na Mwigulu Ncemba dhidi katibu mkuu wa CUF na Makamu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Seif Sharif Hamad hali ya mambo imezidi kuharibika nchini.
Uchunguzi uliofanywa na jopo la waandishi wa tovuti hii unaonyesha kuwa baadhi ya wazee wanaoheshimika ndani ya CCM na serikali wamemtaka Nape Nauye na Mwigulu Nchemba kuokuomba radhi kwa Maalim Seif . Nape na Mwigulu wamekaririwa wakitoa lugha ya dhihaka kwa Seif kuwa ni kiongozi mbinafsi na pia tangu aingizwe kwenye serikali ya umoja wa kitaifa ameanza kunyoa ndevu.
Pia lile kundi maarufu la wanasiasa wanaokwenda kwa jina la Conservatives huko Zanzibar wametishia kuandaa maandamano kupinga dharau za Nape na Nchemba dhidi ya Seif waliyemwita ni kiongozi wa kitaifa anayestahili heshima.
Dar es salaam,
Duru za kisiasa kutoka ndani ya CCM ofisi ndogo eneo la Lumumba jijini Dar es salaam zinadai kuwa kumekuwa na vuta nikuvute ndani ya chama hiko huku baadhi ya watetezi wa Nape na Nchemba wakisema kuwa hizo zilikuwa ni kauli za kisiasa hivyo hakuna sababu ya kukuza mambo hayo.
Bukoba,
Nako huko Bukoba Naibu waziri wa mambo ya ndani na mbunge wa Bukoba mjini amekaririwa akiponda mkakati wa kujivua gamba jinsi unavyopotoshwa na watendaji wa CCM .
Balozi Hamis Kagasheki amekaririwa akiwataka wananchi kutosikiliza majungu na propaganda za kujivua gamba na badala yake wawahoji juu ya maendeleo yao kama umeme, maji na elimu.
Makao makuu CUF,
Wakati huohuo uongozi wa CUF unajiandaa kutoa tamko rasmi kupinga kauli hizo za Nape na Nchemba ambazo zinadaiwa kuwadhalilisha wao kama chama na Maalim Seif kama mlengwa mkuu wa matamshi hayo ya dhihaka.
 
View attachment 34433View attachment 34433eEEe
Habari kwa hisani ya Nova Tzdream -
Zanzibar,

Kufuatia matamshi ya kejeli yaliyotolewa na katibu wa Itikadi na uenezi Bw Nape Nauye pamoja na Mwigulu Ncemba dhidi katibu mkuu wa CUF na Makamu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Seif Sharif Hamad hali ya mambo imezidi kuharibika nchini.
Uchunguzi uliofanywa na jopo la waandishi wa tovuti hii unaonyesha kuwa baadhi ya wazee wanaoheshimika ndani ya CCM na serikali wamemtaka Nape Nauye na Mwigulu Nchemba kuokuomba radhi kwa Maalim Seif . Nape na Mwigulu wamekaririwa wakitoa lugha ya dhihaka kwa Seif kuwa ni kiongozi mbinafsi na pia tangu aingizwe kwenye serikali ya umoja wa kitaifa ameanza kunyoa ndevu.
Pia lile kundi maarufu la wanasiasa wanaokwenda kwa jina la Conservatives huko Zanzibar wametishia kuandaa maandamano kupinga dharau za Nape na Nchemba dhidi ya Seif waliyemwita ni kiongozi wa kitaifa anayestahili heshima.
Dar es salaam,
Duru za kisiasa kutoka ndani ya CCM ofisi ndogo eneo la Lumumba jijini Dar es salaam zinadai kuwa kumekuwa na vuta nikuvute ndani ya chama hiko huku baadhi ya watetezi wa Nape na Nchemba wakisema kuwa hizo zilikuwa ni kauli za kisiasa hivyo hakuna sababu ya kukuza mambo hayo.
Bukoba,
Nako huko Bukoba Naibu waziri wa mambo ya ndani na mbunge wa Bukoba mjini amekaririwa akiponda mkakati wa kujivua gamba jinsi unavyopotoshwa na watendaji wa CCM .
Balozi Hamis Kagasheki amekaririwa akiwataka wananchi kutosikiliza majungu na propaganda za kujivua gamba na badala yake wawahoji juu ya maendeleo yao kama umeme, maji na elimu.
Makao makuu CUF,
Wakati huohuo uongozi wa CUF unajiandaa kutoa tamko rasmi kupinga kauli hizo za Nape na Nchemba ambazo zinadaiwa kuwadhalilisha wao kama chama na Maalim Seif kama mlengwa mkuu wa matamshi hayo ya dhihaka.

Mkuu kwani Huoni Maalim Siku Hizi ananyoa Ndevu ha ha ha Na Anang'ara kama ana miaka 18 Unachecha na Mvinyo wa Ikulu nini Mkuu
 
Naye Maalim Seif kwani nini anamkawiza huyu dogo si angemsomea dua mbaya tu aokote makopo na kula majalalani?
 
Nape anafanya kazi nzuri sana kwa sasa ila Upinzani watamuelewa siku si nyingi.

Nafikiri Slaa kashamuelewa au niseme wameshapatana kwenye mawimbi wanayoongelea.

Lengo lao ni moja ila kila mtu ana njia tofauti. TUTAFIKA TU bandugu.............
 
Nape anafanya kazi nzuri sana kwa sasa ila Upinzani watamuelewa siku si nyingi.Nafikiri Slaa kashamuelewa au niseme wameshapatana kwenye mawimbi wanayoongelea.Lengo lao ni moja ila kila mtu ana njia tofauti. TUTAFIKA TU bandugu.............
Nape ni mpuuzi tu!hawezi kufanya dharau kiasi hicho!tunajua katumwa na jk a.k.a brazamen
 
Back
Top Bottom