Nape waombe radhi serikali ya mapinduzi Zanzibar, adai Seif alikubali muafaka sababu ya njaa zake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape waombe radhi serikali ya mapinduzi Zanzibar, adai Seif alikubali muafaka sababu ya njaa zake!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Duble Chris, Jul 17, 2011.

 1. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Naombeni radhi JF kuchelewa kuileta hii habari mapema hii ni sababu ya Ngeleja na miradi yake
  mkutano ulikuwa na watu wengi kutoka wilya zote za Mbeya ila ni 1/4 ya Ile ya CDM palepale uwanja wa Dr Slaa kama wengi sasa wanavyouita

  Alianza katibu CCM mkoa alimuomba mgeni rasmi - NAPE badaye akabidhi kadi 497 za wanachama wapya akiwemo diwani wa CDM wa Kata ya NZOVWE aliyejiuzuru na wanachuo cha TEKU 300.Zikafuta salamu;

  alianza Dr H. MWAKYEMBE aliongea mambo mawili

  1.Alisema Mbeya tunaipenda na hatuwezi kuiacha ila kwa sasa hatujakaribishwa sababu mbunge wenu yuko busy mno anazunguka majimbo ya CCM na kuwaahidi wananchi kuwa atawatafutia mtu wa kuwang'oa

  2. Alisema maamuzi magumu yanafanywa na yeyote hata kibaka anapo amua kumuibia mtu ni uamuzi mugumu ila CCM inafanya uamuzi makini na sahihi kama kujenga chuo cha Dodoma nk

  Alifuata C. O. SENDEKA
  Pamoja na kuimba mashairi mawili jukwani (MOJA LA TOTI) alimuunga mkono Dr. MWAKYEMBE kwa mambo yote mawili na kuongelea zadi suala la ufisadi kuwa CCM sasa imeamka chini ya Jemadari JK

  Alifuata ASHA JUMA yeye alijisifu na kumsifia JK kuwa ni rais wa kwanza kuingia WHITE HOUSE na yeye ndiye aliye msindikiza hivyo wananchi waachane kabisa na hivyo vyama vya DEMA na NGALAWA

  Alifuata NW wa Viwanda na biashara yeye alitoa matumaini chanya makubwa kwa WTZ zaidi juu ya huu mwaka wa 50 toka uhuru kuwa huu mwaka ni mwisho udharimu wote eg watu walio pora mashamba ya watu, wafanyabishara wa kigeni wanao fanya zile zinazofanya na wazawa nchi hii, waliua viwanda kama viwanda cha nyama nk

  Wabunge wa Mbeya waliomba umoja ushirikiano na mshikamano na kuwa upinzani hawana upendo wa dhati kwa wanambeya

  S.Sitta aliongea mengi kama
  ...Wananchi wasikubalikutekwa na vyama vyama msimu
  ...Tatizo la umeme si maji pekee bali pia kutotekelezwa kwa umakini kwa mipango iliyo wekwa ambayo imeuawa na mafisadi pindi CCM ilipo lala
  ...Yeye hatetei posho kama ilivyo sema bungeni na anavyo nuniwa na wabunge wa upinzani bungeni kutokana kauli yake kuwa kama kweli wapo seriuos na posho basi warejeshe zote walizo kula awali
  ....Wenye pesa walitaka kumng'oa Uanachama CCM lakini alishinda ndiyo maana anaitwa chuma cha pua hii ndiyo sababu vyama vingine vilimuomba agombee urais kama CCJ
  .... Serikali ina mpango wa kuzalisha umeme wa kutosha hata wa kuuza nje kama SOUTH SUDAN and SOUTH AFRICA

  NAPE M ,N ndiye aliye kuwa mgeni rasmi aliongea mengi ya SS
  ...CCM ina sumu iliyoongezeka mara mbili
  ...Mfano wa nyoka ni mzuri angalia wana- Israel walipo umwa na nyoka jangwani waliambiwa wamtazame nyoka wa shaba ndiye CCM

  ...CCM ya sasa ipo makini baada ya kujivua gamba na hatuahii itaedelea hadi ngazi ya kitongoji kuwawajibisha wauza duka wote waunao uza kwa bei tofauti na waliyo pangiwa yaani wanao tekeleza ilani ya tumbo badala ya CCM
  ...Aliwasema CUF kuwa Sharif Hamadi alipo ona njaa inauma aliomba pesa alipwe kama WK msitaafu alipewa mashart akatekeleza, akapewa ilipo uma tena akakubaliana kuunda muafaka sasa ana gonga wisky ikulu hivyo wana nchi msiwakubalie kila wanalosema wapinzani kwani wao wanapalilia ulaji kama walivyo fanya ARUSHA, MARA
  ( KIMSINGI ALIONGEA MENGI MENGINE NI JOKES NITAYAPELEKA JUKWAA LA JOKES)

  Aliyekuwa mgombea ubunge kupitia CUF alimponda live Dr Slaa jukwani kuwa alianzaje kuchukua mke wa mtu na kusema ni wake NA kuondolewa jukwani na NAPE.

  kati ya waliopewa kadi DIWANI wa CHADEMA hakuwepo kama walivyo sema ila taarifa za chini zinasema DIWANI huyu haelewani na katibu wa CDM hata hivyo MADIWANI wenzake walimuomba aachane na uamuzi wake wa kuhama chama jambo ambalo amekuliana nalo wanamsubiri MEYA yupo safirini ARUSHA kwa sasa.

   
 2. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nape na dharau zake yatamtokea puani.

  Amemkashifu sana Maalim seif... Na anaifananisha chadema na CuF ya seif, ngoja ataona moto wake.
   
 3. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Pamoja na mimi kutomkubali Seif, lakini kiuhalisia Nape ni Junior mara milioni moja ya Seif. Kumkebehi kwa staili hiyo ni kudharau wazanzibari, ni kuwaambia kuwa kiongozi wao mkuu amefuata wisky tu na sio kuwatumikia. Ni kudharau damu za wazanzibari zilizomwagika Jan 21 kwa lengo la kutaka Seif awaongoze. Ni kudharau akili za wazanzibari walioridhia kwa amani mabadiliko ya katiba yaliyompa seif nafasi hii aliyonayo sasa. Nape hana sifa za kuongoza, he is completely not dplomatic
   
 4. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Masikini Maalim Seif anadharirishwa kiasi hicho?kwamba ni njaa zake ndio zimesababisha aolewe?
  Ni bora kufa kiume kuliko kuishi kwa masimango kama hayo.
   
 5. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Ati nini?? Aiyetamka hayo ajiandae kushushwa BUSHA
   
 6. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,093
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280
  OMG! NAPE hapa heshima ya kawaida hauna? Unamsimanga maalim seif kiasi hicho? Umewasha moto sijui kama utaweza kuuota.
   
 7. WILLY GAMBA

  WILLY GAMBA JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 210
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hili la Nape kumsingizia Maalim Seif ana kunywa whisky ni direct attack kwa wana wa zuoni wote..TAKBIIIIIIIR!!!!!TAKBIIIIIIIIIR!!!! C.C.M الانتهاء
   
 8. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo umenena mkuu!
   
 9. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Alitumia neno 'anagonga whisky' Ikulu 'Siku hizi anang'ara'
   
 10. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,053
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Huyu Nauye atulie tu naamini Mtatiro anamvutia kasi na ataisoma chakula yake,huyu diwani anatakiwa afukuzwe chamani make tayari anaonekana is not committed na anaweza kutuchuuza pia huko baadae,he is so cheap material!!
   
 11. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Huyu Nnape kwa mara nyingine tena amedhihirisha uropokaji wake usiokuwas na breki. Mimi nasema CCM wamwangalia sana huyu jamaa atasambaratisha CCM yote. RA juzi ameondoka akimlalamikia yeye Nape na Chiligati!

  Haya maneno aliyozungumza hapa hayakupashwa yatamkwa na Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM! Ati kwamba Sharrif Hamad wa CUF alipoona njaa ndiyo ilyomfanya akubaliane na mwafaka na sasa ana gonga whisky Ikulu!!!Pambaf kabisa. Nnape hapa ameropoka bila kupima maneno yake. Nnape anatakiwa ajue haya yafuatayo kuhusiana na SHARRIF HAMAD WA CUF NA MWAFAKA WA VISIWANI.
  1. Kwanza ajue kwamba Sharrif Hamad si size yake hata kidogo.
  2. Mwafaka huu kati ya CCM na CUF ulipata baraka zote za pande mbili huku Rais Kiwete mwenyekiti wake Nnape akilivalia junga swala hili.
  3. Lakini pia anatakiwa ajue kuwa Hamad ndiye ALIYESHINDA URAIS WA VISIWANI na si DK.SHEIN WA CCM kama ambavyo Nnape anataka kuwadanganya Wa-tz.
  4. Kwa hiyo Nnape anapojaribu kum-beza Sharrif Hamad wa CUF ina maana anabeza mafanikio ya Mwafaka ambayo yameleta serikali ya Umoja wa Kitaifa Visiwani na kuondoa msuguano ambao umekuwepo kwa takribani miaka 19!!!
  Nnape hakika ni BOMU kwa Chama Cha Magamba. Very soon it shall explode and kill the already crippled CCM.
   
 12. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #12
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Honestly,Nape is a waste of a space.Hivi anajua terms and conditions za muafaka? He needs a healing therapy and diplomatic Eloquence! Si kila kitu kinastahili propaganda.hii ni weakness kubwa.Tutakapochukua dola 2015,huyu jama ni lazima tumpe award kama njia ya kisataarabu ya kutambua mchango wake katika kuia CCM na kuimarisha kambi ya Upinzani.Go Nape,unafanya kazi nzuri so far!


  I am extremely shocked at the fact that he is trying to convince us how educated and above average he and his party linage
  he is, but i can assure him, he sound very deprived of common sense and certainly very short on any formal or informal education. His thought pattern shows a deep poverty of facts and an unusual confusion. His flow of eloquence are sewage rated, and i need not to tell him how wasteful they are.

  Muafaaka wa Zanzibar unastahili kuwa adressed in a very respective way.....Nape aache siasa za u-Simba na U-yanga.Zimepitwa na wakati.


   
 13. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,073
  Likes Received: 4,001
  Trophy Points: 280
  17th July 11
  Nape ambeza Seif Shariff

  Thobias Mwanakatwe
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Nape Nnauye amembeza Makamu wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad kuwa njaa yake ndiyo iliyomfanya aitambue Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na hatimaye kukubali kuingia kwenye Serikali ya mseto.
  Nnauye aliyasema hayo jana wakati akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wenye lengo la kuelezea maana ya CCM kujivua gamba uliofanyika Jijini Mbeya.
  Alisema baada ya Hamad kubanwa na njaa kali aliamua kurudi kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kudai alipwe mafao yake kama katibu kiongozi wa Serikali hiyo, wakati akiwa haitambui.
  "Tulimuuliza anataka alipwe mafao yake na Serikali ipi, maana wakati huo yeye (Sharif Hamad) na chama chake walikuwa hawaitambui Serikali, ndipo alipokubali kuitambua serikali ya Karume (Rais Mstaafu wa Zanzibar Aman Abeid Karume)," alisema Nnauye.
  Akizungumzia suala la kujivua gamba, Nnauye alisema hatua hiyo imejichukulia chama ili kiwe na uwezo mzuri wa kusimamia serikali kwa kuhakikisha kuwa watendaji wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili na siyo kwa manufaa ya matumbo yao. Alisema tatizo lililokuwa limejitokeza ndani ya chama ni kwamba maadili kwa viongozi ndani ya chama na serikali yalikuwa yameporomoka ambapo baadhi walitumia madaraka yao kujinufaisha wenyewe.
  "Tatizo lililojitokeza ni kwamba baadhi ya viongozi ndani ya chama na serikali waliacha kutekeleza ilani ya chama, badala yake wakaanza kutekeleza ilani ya matumbo yao ndiyo sababu tumeamua kujivua gamba," alisema Nnauye.
  Nnauye alisema hivi sasa viongozi waliopo serikalini wasipotekeleza ilani ya chama, chama kitawashughulikia kabla wananchi hawajakishughulikia.
  Alisema lengo la chama ni kutaka kurejesha misingi sahihi ya chama kama ilivyoasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
  "CCM imekusudia kujirekebisha na kurejesha maadili ndani ya chama kama yalivyokuwa wakati wa chama kilipoanzishwa chini ya uongozi wa Baba wa Taifa," alisema Nnaye.

  NIPASHE JUMAPILI
  Nape ambeza Seif Shariff

  MY TAKE:
  Hapa CHADEMA inabidi wajifunze waone jinsi CCM wanavyokuchana siku ukiridhia matakwa yao! wamemshikisha hela ustaadh kilichobaki ni kumvua nguo! hahah lahaula...naona ndoa ya CUF na CCM inaelekea ukingoni!
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Nape Nnauye amembeza Makamu wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad kuwa njaa yake ndiyo iliyomfanya aitambue Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na hatimaye kukubali kuingia kwenye Serikali ya mseto. Nnauye aliyasema hayo jana wakati akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wenye lengo la kuelezea maana ya CCM kujivua gamba uliofanyika Jijini Mbeya. Alisema baada ya Hamad kubanwa na njaa kali aliamua kurudi kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kudai alipwe mafao yake kama katibu kiongozi wa Serikali hiyo, wakati akiwa haitambui.

  “Tulimuuliza anataka alipwe mafao yake na Serikali ipi, maana wakati huo yeye (Sharif Hamad) na chama chake walikuwa hawaitambui Serikali, ndipo alipokubali kuitambua serikali ya Karume (Rais Mstaafu wa Zanzibar Aman Abeid Karume),” alisema Nnauye. Akizungumzia suala la kujivua gamba, Nnauye alisema hatua hiyo imejichukulia chama ili kiwe na uwezo mzuri wa kusimamia serikali kwa kuhakikisha kuwa watendaji wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili na siyo kwa manufaa ya matumbo yao. Alisema tatizo lililokuwa limejitokeza ndani ya chama ni kwamba maadili kwa viongozi ndani ya chama na serikali yalikuwa yameporomoka ambapo baadhi walitumia madaraka yao kujinufaisha wenyewe.
  “Tatizo lililojitokeza ni kwamba baadhi ya viongozi ndani ya chama na serikali waliacha kutekeleza ilani ya chama, badala yake wakaanza kutekeleza ilani ya matumbo yao ndiyo sababu tumeamua kujivua gamba,” alisema Nnauye.

  Nnauye alisema hivi sasa viongozi waliopo serikalini wasipotekeleza ilani ya chama, chama kitawashughulikia kabla wananchi hawajakishughulikia. Alisema lengo la chama ni kutaka kurejesha misingi sahihi ya chama kama ilivyoasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. “CCM imekusudia kujirekebisha na kurejesha maadili ndani ya chama kama yalivyokuwa wakati wa chama kilipoanzishwa chini ya uongozi wa Baba wa Taifa,” alisema Nnaye.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hoja ya Nape kumshambuilia Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar hadharani kuja hoja ya msingi?Kwa mtazamo wangu amemshambulia mtu binafsi na si hoja ya msingi ya kisiasa. Huyu kijana ni mchafu mno
   
 16. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #16
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  [h=2]SIKUAMINI MASIKIO NA MACHO YANGU,kama hali ndiyo hiyo basi maamuzi yote ya CCM ni usanii soma kauli ya Nape huko Mbeya Source:NIPASHE
  huyu dogo Nape inabidi avalishwe pampes ya mdomo kwa sababu kauli zake zimelenga kujipatia sifa binafsi kuliko kukinusuru chama cha mafisadi.Sasa hapa tujiulize huo muafaka uliofikiwa ulishirikisha pande mbili CCM na CUF ulikua ni usanii wa CCM?Kama Seif alifanya hivyo kama anavyodai Dogo kwa sababu ya njaa basi CCM ilikua na njaa mara dufu ya Seif ndio maana ikakubali serikali hiyo ya mseto kwa shinikizo la Seif Hamad kwa kua CCM mfu wa kuatatua matatizo na kero nyingi ikiwemo swala la muungano ilikubaliana na shinikizo la Sharif au serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa sababu iligundua ni serikali au chama kisicho na nguvu ya kutatua tatizo lolote ispokua familia na matumbo yao.Na hapa naona nia ya CCM ilikua uchaguzi upite kwa amani kwa mwamvuli wa serikali ya mseto"NAPE WAOMBE RADHI SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR"


  Nape ambeza Seif Sharif


  NA THOBIAS MWANAKATWE


  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Nape Nnauye amembeza Makamu wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad kuwa njaa yake ndiyo iliyomfanya aitambue Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na hatimaye kukubali kuingia kwenye Serikali ya mseto.
  Nnauye aliyasema hayo jana wakati akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wenye lengo la kuelezea maana ya CCM kujivua gamba uliofanyika Jijini Mbeya.
  Alisema baada ya Hamad kubanwa na njaa kali aliamua kurudi kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kudai alipwe mafao yake kama katibu kiongozi wa Serikali hiyo, wakati akiwa haitambui.
  "Tulimuuliza anataka alipwe mafao yake na Serikali ipi, maana wakati huo yeye (Sharif Hamad) na chama chake walikuwa hawaitambui Serikali, ndipo alipokubali kuitambua serikali ya Karume (Rais Mstaafu wa Zanzibar Aman Abeid Karume)," alisema Nnauye.
  Akizungumzia suala la kujivua gamba, Nnauye alisema hatua hiyo imejichukulia chama ili kiwe na uwezo mzuri wa kusimamia serikali kwa kuhakikisha kuwa watendaji wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili na siyo kwa manufaa ya matumbo yao. Alisema tatizo lililokuwa limejitokeza ndani ya chama ni kwamba maadili kwa viongozi ndani ya chama na serikali yalikuwa yameporomoka ambapo baadhi walitumia madaraka yao kujinufaisha wenyewe.
  "Tatizo lililojitokeza ni kwamba baadhi ya viongozi ndani ya chama na serikali waliacha kutekeleza ilani ya chama, badala yake wakaanza kutekeleza ilani ya matumbo yao ndiyo sababu tumeamua kujivua gamba," alisema Nnauye.
  Nnauye alisema hivi sasa viongozi waliopo serikalini wasipotekeleza ilani ya chama, chama kitawashughulikia kabla wananchi hawajakishughulikia.
  Alisema lengo la chama ni kutaka kurejesha misingi sahihi ya chama kama ilivyoasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
  "CCM imekusudia kujirekebisha na kurejesha maadili ndani ya chama kama yalivyokuwa wakati wa chama kilipoanzishwa chini ya uongozi wa Baba wa Taifa," alisema Nnaye.
  huyu dogo Nape inabidi avalishwe pampes ya mdomo kwa sababu kauli zake zimelenga kujipatia sifa binafsi kuliko kukinusuru chama cha mafisadi.Sasa hapa tujiulize huo muafaka uliofikiwa ulishirikisha pande mbili CCM na CUF ulikua ni usanii wa CCM?Kama Seif alifanya hivyo kama anavyodai Dogo kwa sababu ya njaa basi CCM ilikua na njaa mara dufu ya Seif ndio maana ikakubali serikali hiyo ya mseto kwa shinikizo la Seif Hamad kwa kua CCM mfu wa kuatatua matatizo na kero nyingi ikiwemo swala la muungano ilikubaliana na shinikizo la Sharif au serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa sababu iligundua ni serikali au chama kisicho na nguvu ya kutatua tatizo lolote ispokua familia na matumbo yao.Na hapa naona nia ya CCM ilikua uchaguzi upite kwa amani kwa mwamvuli wa serikali ya mseto"NAPE WAOMBE RADHI SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR"
   
 17. Mbassa

  Mbassa JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 247
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Maskini Seif!, ona sasa wanavyomdhalilisha!
   
 18. MCHONGANISHI

  MCHONGANISHI JF-Expert Member

  #18
  Jul 17, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 363
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  sasa huyu Nape na CDM nani anidhalilisha serikali ya umoja wa kitaifa?
   
 19. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwangu mimi nakubali aliyoyasema Nape,tena this time kaonyesha ukomavu wa kumchomoa MwanaCUF aliyekosa BREAK,ambayo kama WANACDM wangetaka kulusha tuhuma wangemwagia huyo aliyeanza story zilizokosa support toka siku hizo za kumtukana Mwanaharakati Kiongozi wa CDM Mzee Slaa.Lakini tofauti na hayo kamsifia kiongozi wa CUF kuwa anakula BATA IKULU,Watu wamekasirika na kumrushia matusi kuwa kamtukana Mzee SHARRIF HAMAD.

  You guys,hivi lini chma cha UPINZANI kikajiunga na Serikali kisha mtegemee,yale chama kilichoyaanzisha na kuyasimamia kikayetekeleza kwa kushirikiana na chama kilicho kwenye MFUMO.Sijaona zaidi ni mmoja kumzidi KETE MWENZIE.

  Mlitegemea aseme yuko ikulu anapata SHIDA,au tunajua MCHUMIA JUANI ANALIA KIVULINI,jamani hiyo mbona iko wazi tu hata kwa misemo yetu ya KISWAHILI na Wahenga wetu wanasema kuwa UKIONA SHIDA ZINAZIDI NEEMA IMEKALIBIA.Kwa chama cha CUF kukubaliana na CCM hayo ndio waliyoyayataka,vinginevyo wasingeyata wasinge ungana na CCM.Tatizo nini MWAFAKA uliletwa Mezani wakakubali ukawa ndio MWISHO wa CUF.

  Ni sawa LEO CDM wameingia MKENGE wa kukubali MWAFAKA ARUSHA kesho MADIWANI WAO WAANZE KULA BATA,kisha muwalaumu.Utakuwa ni upumbavu kusikia kesho kuna mgogolo wa ndani ya mwafaka.Ningeunga mkono kama wangekuwa nje ya muafaka wakaendeleza mapambano ya kuazimia na kutaka kupewa nafasi na umma ili kuyatekeleza yale yaliyowafanya WAWE CHAMA CHA CDM YAANI CHAMA CHA UPINZANI AU CHAMA CHA SERIKALI TALAJIWA.

  CHAMA CHA UPINZANI HAKIWI CHAMA KINACHOUNDA SERIKALI KISHA KIJIITE CHAMA CHA UPINZANI.Mbio za na maazimio ya chama cha CUF zilikua ndio hizo zilizowafikisha hapo ITS OVER!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.

  Kabla Tanzania aijapata uhuru,ndio zama hizo Mwalimu JK anaanza mikakati ya kuutafuta uhuru na Wanadar es salaam.Mwalimu alikuwa anapita mitaa ya JIJI la Dar es Salaamu akiwa na rafiki yake mwenye asili ya kiasia,basi mitaan huko wakakumbana na muasia mwingine ambae alimtusi Mwalimu,Muasia rafiki wa Mwalimu akamshawishi Mwalimu wamfungulie Muasia mwenzie kesi kwa kosa la kumtukana na Mwalimu.Kumbuka wakati huo Mwalimu si chochote ni msomi anaeangaikia mbinu za kujikomboa. Jibu la Mwalimu kwa Muasia rafiki yake lilikuwa "HUYO ACHANA NAE DAWA YAKE HIPO JIKONI YAAJA"Pata picha Mwalimu alikua anafikilia nini ndani akiri yake.Mwalimu anasema jamii ya hao waliomtukana yeye ni wengi tu ndani ya Tanganyika wakati huo,hivyo kuangaika na huyo mmoja mahakamani sio suruhu au tiba dhidi ya wazalimu wa aina hiyo.

  Hivyo chama chochote cha upinzani lazima kisimamie kusudio lake la kuwa chama cha UPINZANI.Na kinapofikia hapo CUF walipofika pa kumpeleka mtukanaji wa Mwalimu Mahakamani basi hapo ndio kusudio au lengo la CUF lilifika mwisho kimaono.Au vinginevyo kingesimamia pale ambapo Mwalimu alipopaona ambako aikujalisha muda bali ni kufika huko kwa kuakikisha kuwa watukanaji wote [Waasia na Wazungu watawala wa kikoloni ] waliokuwa ndani ya mfumo wa kikoloni wamefungasha na kuondoka [Kwa lugha ya sasa ni Kusepa].

  Uwa nakubaliana na UKOMAVU WA CCM,japo nachukia wanavyotuendeshea Nchi yetu, wakiamini wao ndio wao.Ndio wanauzoefu wa kuendesha dola lakini wamelewa Madaraka na kutumia nafasi yao ya uzoefu wa kuongoza katika kuliangamiza Taifa ,kwa matendo ya baadhi ya viongozi wao.Na uwa naumia kwa jinsi Wanaojiita vyama vya UPINZANI kujisahau, kujifunza ni namna gani wanaweza kujinasua na mbinu na maarifa ya CCM,ili waweze kufika kwenye dhamila yao ya KUSTAWAISHA TAIFA kwa mbinu nyingine tofauti na zile za CCM.

  Big up CCM,CUF wako IKULU wanakunywa WHISKY.Naamini uenda kuna siku kiongozi wa CDM,ambae kimawazo na fikra walipaswa kufikilia ni jinsi gani wako IKULU wakisikiliza na kutatua shida za Wananchi.Lakini wakiwazia kualikwa IKULU na kukubali kushea IKULU tukawaambia wanakunywa WHISKY wasichukie kwa kuwa ndilo waliloweza kulifikilia japo,tunajua WHISKY ni mvinyo unaonyweka wakati watu wamepumzika baada ya kufanya maamuzi ama shughuli yenye faida na mchangao mkubwa kwa mhuhusika.

  BADO NAPE YUKO SAHIHI SIONI NI KWANINI ASHUTUMIWE KWA HOJA YAKE SAHIHI,YAANI KWA LUGHA NYINGINE WALIOKUWA WANATEGEMEA NDONDI ZA CUF NA CCM BAADA YA KUUNGANA ILI WAENDELEZE UJINGA WAO IMEKULA KWAO.

  TUNACHOKIJUA SASA HIVI AMBACHO JAMII INAKIUNGA MKONO KUWA NI CHAMA CHA UPINZANI,NI CHAMA CHA MAENDELEO [CHADEMA].NA AMBACHO NACHO KINAELEKEA KULE KULE AMBAKO CUF NA MBIO ZAKE ZIMEMFIKISHA KUWA MSHIRIKA WA CCM.

  MIMI SINA CHAMA CHA SIASA ,KWANGU MIMI TANZANIA MBELE.HUWA NAONA AIBU NA KUCHEKA SANA WATU WAZIMA VIONGOZI WA UPINZANI,KUTEGEMEA CCM ITAWASTAWISHA ILI WASIMAME KUINGIA MADALAKANI "PLEASE SHAME ON YOU", KAMA KUNA VIONGOZI WA KWELI WA UPINZANI WANALITEGEMEA HILO NI TISHIO KUWA NA UPINZANI WENYE FIKRA MFU.

  KIONGOZI WA UPINZANI SIO MBAYA UKIALIKWA IKULU NENDA UKANYWE WHSKY [MAONGEZI] KISHA UTAMBAE,NAWE UKITOKA UKO UWE NA KIU YA KUINGIA HUKO NA KUALIKA VIONGOZI WA VYAMA VYA UPINZANI WAJE WANYWE WHISKY.
   
 20. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Ulikuwa hujui kuwa huyu kijana ni hatari hachagui maneno hana huyu ni mkubwa na anastahili heshima fulani hata ile ya kumshambulia Kikwete kuwa naye ni gamba lakini hawawezi kumvua kwa vile yeye ni m/kiti ni true story, i tell you this guy is a wasted spade atakigawa chama mapande mapande wait&see.
   
Loading...