kakakuona40
JF-Expert Member
- Oct 3, 2011
- 300
- 52
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema chama chake kinajiandaa kusherehekea ushindi Arumeru kutokana na nusu ya maofisa wa Chadema kuanza kuingia mitini kutokana na ukosefu wa fedha za kufanyia kampeni, anaripoti Sifa Lubasi kutoka Dodoma.
Nnauye alisema hayo Mjini Dodoma wakati akimnadi mgombea wa kiti cha Udiwani katika Kata ya Changombe, Manispaa ya Dodoma na kutaka wananchi wasifanye kosa kuchagua chama kingine badala ya kuichagua CCM.
Alisema kuwa, katika ushindi wa Ubunge huko Arumeru CCM itaibuka na ushindi kutokana na kuwa Kata 17 za Arumeru Mashariki madiwani wake wote ni wa CCM.
Tumeanza kuandaa sherehe za ushindi, walikwenda Igunga na Uzini na kufanya kampeni za mbwembwe, sasa wameishiwa hivi ninavyoongea nusu ya maofisa wa Chadema kutokana na ukosefu wa fedha za kampeni hata wafadhili wao sasa wamekunja mikono, tumewapiga chaguzi mbili wafadhili wao wamewabania, alisema.
Aidha, alisema kuwa yuko tayari kupokea wanachama wa Chadema watakaorudi CCM kutokana na hali halisi ilivyo hivi sasa.
Nasikia Zitto Kabwe ilikuwa aje huku kuzindua kampeni lakini alipodokezwa kuwa mimi ndiyo nakuja huku akaingia mitini, wapeni adhabu wapinzani kwa kuwanyima kura, alisema Nnauye ambaye amewataka wakazi wa Kata ya Changombe kumchagua Bakari Fundikira wa CCM.
Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Anne Kilango-Malecela ambaye pia ni Mbunge wa Same Mashariki, aliwataka Wana- Changombe kumchagua mgombea wa CCM ili waweze kutafuta amani ya kudumu.
Kinamama wa Kata hii mzunguke nyumba kwa nyumba kutafuta kura za CCM ili mtafute amani ya kudumu kwani amani ikipotea waathirika huwa kina mama kama ilivyokuwa kwenye mgomo wa madaktari walioathirika zaidi ni kinamama, alisema katika uzinduzi huo uliohudhuriwa karibu na viongozi wa CCM wa ngazi zote kutoka mkoani Dodoma.
Source: HabariLeo | Nnauye-Tutashinda Arumeru, Chadema wameishiwa