NAPE: Tutashinda Arumeru, Chadema wameishiwa

kakakuona40

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
300
52
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema chama chake kinajiandaa kusherehekea ushindi Arumeru kutokana na nusu ya maofisa wa Chadema kuanza kuingia mitini kutokana na ukosefu wa fedha za kufanyia kampeni, anaripoti Sifa Lubasi kutoka Dodoma.

Nnauye alisema hayo Mjini Dodoma wakati akimnadi mgombea wa kiti cha Udiwani katika Kata ya Chang’ombe, Manispaa ya Dodoma na kutaka wananchi wasifanye kosa kuchagua chama kingine badala ya kuichagua CCM.

Alisema kuwa, katika ushindi wa Ubunge huko Arumeru CCM itaibuka na ushindi kutokana na kuwa Kata 17 za Arumeru Mashariki madiwani wake wote ni wa CCM.

“Tumeanza kuandaa sherehe za ushindi, walikwenda Igunga na Uzini na kufanya kampeni za mbwembwe, sasa wameishiwa hivi ninavyoongea nusu ya maofisa wa Chadema kutokana na ukosefu wa fedha za kampeni hata wafadhili wao sasa wamekunja mikono, tumewapiga chaguzi mbili wafadhili wao wamewabania,” alisema.

Aidha, alisema kuwa yuko tayari kupokea wanachama wa Chadema watakaorudi CCM kutokana na hali halisi ilivyo hivi sasa.

“Nasikia Zitto Kabwe ilikuwa aje huku kuzindua kampeni lakini alipodokezwa kuwa mimi ndiyo nakuja huku akaingia mitini, wapeni adhabu wapinzani kwa kuwanyima kura,” alisema Nnauye ambaye amewataka wakazi wa Kata ya Chang’ombe kumchagua Bakari Fundikira wa CCM.

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Anne Kilango-Malecela ambaye pia ni Mbunge wa Same Mashariki, aliwataka Wana- Chang’ombe kumchagua mgombea wa CCM ili waweze kutafuta amani ya kudumu.

“Kinamama wa Kata hii mzunguke nyumba kwa nyumba kutafuta kura za CCM ili mtafute amani ya kudumu kwani amani ikipotea waathirika huwa kina mama kama ilivyokuwa kwenye mgomo wa madaktari walioathirika zaidi ni kinamama,” alisema katika uzinduzi huo uliohudhuriwa karibu na viongozi wa CCM wa ngazi zote kutoka mkoani Dodoma.


Source: HabariLeo | Nnauye-Tutashinda Arumeru, Chadema wameishiwa
 
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema chama chake kinajiandaa kusherehekea ushindi Arumeru kutokana na nusu ya maofisa wa Chadema kuanza kuingia mitini kutokana na ukosefu wa fedha za kufanyia kampeni, anaripoti Sifa Lubasi kutoka Dodoma.

Nnauye alisema hayo Mjini Dodoma wakati akimnadi mgombea wa kiti cha Udiwani katika Kata ya Chang'ombe, Manispaa ya Dodoma na kutaka wananchi wasifanye kosa kuchagua chama kingine badala ya kuichagua CCM.

Alisema kuwa, katika ushindi wa Ubunge huko Arumeru CCM itaibuka na ushindi kutokana na kuwa Kata 17 za Arumeru Mashariki madiwani wake wote ni wa CCM.

"Tumeanza kuandaa sherehe za ushindi, walikwenda Igunga na Uzini na kufanya kampeni za mbwembwe, sasa wameishiwa hivi ninavyoongea nusu ya maofisa wa Chadema kutokana na ukosefu wa fedha za kampeni hata wafadhili wao sasa wamekunja mikono, tumewapiga chaguzi mbili wafadhili wao wamewabania," alisema.

Aidha, alisema kuwa yuko tayari kupokea wanachama wa Chadema watakaorudi CCM kutokana na hali halisi ilivyo hivi sasa.

"Nasikia Zitto Kabwe ilikuwa aje huku kuzindua kampeni lakini alipodokezwa kuwa mimi ndiyo nakuja huku akaingia mitini, wapeni adhabu wapinzani kwa kuwanyima kura," alisema Nnauye ambaye amewataka wakazi wa Kata ya Chang'ombe kumchagua Bakari Fundikira wa CCM.

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Anne Kilango-Malecela ambaye pia ni Mbunge wa Same Mashariki, aliwataka Wana- Chang'ombe kumchagua mgombea wa CCM ili waweze kutafuta amani ya kudumu.

"Kinamama wa Kata hii mzunguke nyumba kwa nyumba kutafuta kura za CCM ili mtafute amani ya kudumu kwani amani ikipotea waathirika huwa kina mama kama ilivyokuwa kwenye mgomo wa madaktari walioathirika zaidi ni kinamama," alisema katika uzinduzi huo uliohudhuriwa karibu na viongozi wa CCM wa ngazi zote kutoka mkoani Dodoma.


Source: HabariLeo | Nnauye-Tutashinda Arumeru, Chadema wameishiwa


  1. Source: Habari Leo
  2. Arumeru iko Dodoma?
  3. HabariLeo | Gwiji la Habari Tanzania Nnauye-Tutashinda Arumeru, Chadema wameishiwa
  4. Dk Slaa atua Arumeru kwa kishindo
 
Haya ndiyo maendeleo ya ccm tokea miaka 50 iliyopita
WANAFUNZI.JPG
 
nape anachekesha.Hivi zitto anaweza kumkimbia nape? unaweza linganisha nazi (nape) na jiwe(zitto).?
 
Sometime napata tabu kujua nani ni nafuu kati ya Nape na Wassira, who is the best kwa miropoko?
 
hoja ya Nape haina mashiko, chadema ni chama kinacho o focus hawawezi kufanya kama walivyofanya Igunga na ndio unaona hata makampeni meneja ni wengine na style wanayotumia ni nyingine wanafanya kampeni kuendana na jiografia ilivyo. Tatizo sio pesa kinachotafutwa ni ushindi kwa taarifa yake huyo Nape ajue kuwa pesa wanazogawa ccm ni mtaji wa cdm.
 
Nilitegemea kusikia CDM wameishiwa sera kumbe wameshiwa pesa akili matope kabisa. Yeye yuko Dodoma halafu anasema wameshashinda Arumeru Mashariki na wanajiandaa kufanya sherehe, badala ya kukazania diwani wa Chang'ombe ashinde yeye anawaza jimbo ambalo hajui hata vumbi lake likoje.
 
Nilitegemea kusikia CDM wameishiwa sera kumbe wameshiwa pesa akili matope kabisa. Yeye yuko Dodoma halafu anasema wameshashinda Arumeru Mashariki na wanajiandaa kufanya sherehe, badala ya kukazania diwani wa Chang'ombe ashinde yeye anawaza jimbo ambalo hajui hata vumbi lake likoje.

Kama mtu anakwenda kuzindua kampeni Dodoma lakini anazungumzia matumaini ya ushindi Arumeru ni dalili ya wazi kwamba hawana matumaini ya kushinda arumeru mashariki kwahiyo wamebaki kuweweseka.
Makada wao wote walioko arumeru wamekwenda kuhubiri matusi wakati makamanda wa chadema wanamwaga sera tu.
Hii ya kwamba chadema wameishiwa fedha ni kiwewe cha kuona wananchi wanavyomchangia mgombea wa chadema kila anakopita kufanya mikutano ya kampeni.
 
Nape Nnauye,Mwigulu Nchemba,Benjamini Mkapa na Livingstone Lusinde ni kama mapacha..yaani wana akili za kitoto kweli kweli...kazi yao ni kuropoka bila kutafakari.
 
Nape Nnauye,Mwigulu Nchemba,Benjamini Mkapa na Livingstone Lusinde ni kama mapacha..yaani wana akili za kitoto kweli kweli...kazi yao ni kuropoka bila kutafakari.

Hao wote wameishiwa sera hawana la kuwaambia watu.
 
Kumkomoa huyu Nepi inabidi tuzidishe michango yetu ya hali na mali kwa CDM. Wao wanachota fedha zetu hazina na kupokea fedha chafu toka kwa wahindi wakwepa kodi wanajiona wameshinda kwa hela. Wana Arumeru wana msimamo wao wa KULA ccm KURA CDM na fedha nyingine toka ccm wanamchangia Nassary
 
makamanda wapo arumeru wanajenga mazingira ya ukombozi....nape uliona kazi ya mh zitto wakati akizindua kampeni za udiwani mwanza?kama unaweza moto wa makamanda kalibu arumeru"
 
Nape bwana kweli vuvuzela yani hao mabwana sasa badala ya kunadi sera zao wameanza kuingelea cdm. Alafu huyu nape huwa anapenda kuropoka wakati wa uchaguzi igunga alibandika matokeo kwenye page yake wakati yalukuwa bado hayajatangazwa rasmi sasa ameanza na Arumeru kuandaa sherehe za ushindi wakati hata uchakuzi bado nimeanini Magamba ni majizi
 
Kampeni Dodoma, analeta habari za Arumeru. Kama anatamani si aende akapambane na kina Nyerere kama anataka.
 
Inabidi Nape ahojiwe!Atatangazaje kuanza maandalizi ya kusherekea ushindi wakati ndo kwanza kampeni zimeanza.Inaelekea ana uhakika wa njama za kuhujumu matokeo Arumeru.
 
Kimwili yupo Dodoma, kimawazo yupo Arumeru, poor Nape. Anateseka na kuweweseka.
 
Kilango anazungumzia amani, hahaha, ipi hiyo? ya polisi kuua watu. Hivi kwa nini yasitengenezwe mabango makubwa na vipeperushi vyenye picha za akinamama wamelala chini mahospitalinini, wanafunzi wansoma chni ya mti, n.k ambayo yanaonesha ukatili wa CCM, yatumike kwenye kampeni?


Mi nafikiri zitakuwa na impact kubwa kwa jamii pale watakapoziona.
 
Back
Top Bottom