Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,703
- 4,697
Ni takribani mwaka mmoja Nape uliamini uko sahihi kutangaza na kulinda kwa nguvu uamuzi wako wa kuzuia Bunge live. Uliamini uko sahihi kwa kuwa uamuzi huo haukugusa marafiki zako, wasanii na wamiliki wa vyombo vya habari. Huo ndo ulikuwa wakati mzuri wa kuonyesaha uelewa wako na ungeweza kujiuzuru. Uliamini ni sahihi bila kujali wingi wa vilio vya wananchi.
Sasa yamekufika ya kufanya utetezi usio na mipaka. Ukaunda kamati ya uchunguzi iliyosheheni marafiki zako, waandishi wa habari, kumchunguza mtu ambaye huna madaraka juu yake! Ulilewa pongezi.
Nashauri: Ukiwa madarakani, usiwe kama mcheza mpira. Unaposhangiliwa usipoteze muelekeo na kuanza kujirusha kuliko uwezo wa mwili, utaumia. Sasa hivi tulia ujiulize nini hujajifunza ktk maisha yako. Usipojielewa ukazidisha manjonjo, tutaanza na kuangalia vyeti vyako tukienda juu.