Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 41,722
- 55,080
Hizi kamati za bunge ambazo zimekuwa zikiita na kuhoji watu kama CAG Assad, Pascal Mayalla , Mpina na wengine wengi ni vyema sasa zikawa zinarusha live mahojiano hayo kama ambavyo inafanyika kwenye vikao vya bunge.
Demokrasia halisi duniani ndivyo ambavyo zinafanya kazi zake kwa sasa, huko kamati za bunge zinapohoji watu binafsi au viongozi wa serikali huo mjadala unakuwa live na pia baadhi ya raia wanaruhusiwa kuhudhuria mijadala ya hivyo vikao.
Zaidi sana wanaoitwa kuhojiwa huruhusiwa kuingia na wanasheria wao kuwasaidia kutafsiri baadhi ya mambo ya kisheria na kuwapa miongozo mengine muhimu.
Hii ndio njia sahihi ya kuwatendea haki wahojiwa na raia wenye maslahi katika hilo jambo badala ya kufanyia mambo gizani na kuja kusomea watu taarifa bila wananchi kujua nini kilichoendelea nyuma ya pazia. Sio sahihi kukaa kamati nzima ya lundo la watu kumohoji mtu mmoja mafichoni na kufikia maamuzi.
Tunataka public hearing.
Pia soma:Spika Tulia amburuza Luhanga Mpina Kamati ya maadili