Nape, Simamia Tanganyika na Vijana Wenzako

Nape, Simamia Tanganyika na Vijana Wenzako

Acheni kuzunguka mbuyu mtanzania bara wa Manyoni ananufaika nini muungano huu? mimi sijawahi hata siku moja kuona hata chembe ya manufaa ya muungano huu kama hoja ni usalama wa taifa tutafuta njia mbadala za kukabiliana na hujuma zozote dhidi ya taifa hili; nyie kama mnataka aamueni muachane na muungano huu; uhuru wenu unatuumiza sisi nyie mzigo kwetu na sisi tunawavumilia kwasababu tumekuwa kama ndugu; nyie watu mna roho mbaya na ubinafsi siku mlipopata fununu ya mafuta kwenye pwani ya Zanzibar mlichokimbilia kusema mafuta hayamo kwenye muungano mkasahau kabisa kuwa Zanzibar baada ya karafuu kuanguka bei ililishwa sana na almasi na dhahabu; pamba na mkonge za Tanzania bara; muungano huu utakuwa na heri kama mtaacha ubinafsi wenu; Tanzania bara ina rasilimali nyingi sana za kuweza kujimudu kiuchumi!

Ndugu yangu unapozungumzia mbadala wa kitu lakini tayari unakitumia haiondowi ukweli kuwa unakitumia. Mimi sijakueleza habari ya ulinzi lakini wewe mwenyewe unajishuku baada ya kubaini kuwa mliwatumia ndugu zetu kule Msumbiji, Malawi, Uganda na sasa Congo na Sudan. Hilo ni lako mwenyewe. Ninachokusudia kukwambia ni kuwa iwapo miji mikuu ya Bara imejengwa na mnaowaita Wapemba hata iwe kwa pesa zenu basi mmepata faida kwani hao mkiamuwa kuwaondowa mtabaki navyo wenyewe.

Mimi kwa upande wako kama unavyoona wewe kuwa muungano haujakusaidia chochote kwa vile unaweza kufanya mbadala wa hayo manufaa, na mimi nahisi hivyohivyo, kwani tuliungana tangu 1964 na Zanzibar haikuwahi kutegemea chochote kutoka Bara kwa vile ilikuwa huru. Baada ya kuingia CCM wenzetu mkafunga njia zote za sisi kuwa huru ili mtutawale na kwa bahati mbaya nyinyi wenyewe hamuwezi kujitegemea (kiasi watu wanakufa kwa njaa) mtawezaje nyinyi muwe mnatuhudumia sisi na kusema tunakutegemeeni?
Hebu niambie kipi hasa ambacho mnakitowa bure kutupa? Na iwapo mnakitowa basi mnakitowa ili kiwe chambo cha kututawala. Tatizo liko wapiiwapo mnaumia na sisi tunaamuwa kutoka kwenye ubeleko wenu? Bila shaka mlikuwa mkijipendekeza ili kutegemea kitu fulani, pengine hayo mafuta unayosema.
Unaposema sisi ni wabinafsi, ubinafsi wetu umekuja kwa hayo mafuta? Na lile la nyie kuzuwia kila hatuwa za maendeleo tunazotaka kuzipiga unaiita kitu gani? Hili la mtu kumiliki chake si jambo geni hapa Tanzania kwani kiasi gani cha pato la almasi, tanzanite, dhahabu na wanyama linakwenda kule Zanzibar kutujengea mahospitali, mabarabara, viwanja vya ndege, bandari na mashule?
 
Busara ninazo nyingi na ndio maana hatuna haja ya kulazamisha kama kulikuwa na sababu za kuwepo muungano huu na nyie wazanzibar mmeziona hazipo na ufe tena kifo cha mende! tumechoka na hizi kelele zenu nyie ndio mmekuwa wanufaika wakubwa wa muungano lakini hamuishi kulialia labda ni kuulize bara tunanufaika na kitu gani kutoka Zanzibar? Leo hii hujui maana ya manufaa? unataka nalo nikufundishe?

Utanifundisha kwa nyenzo gani uliyonayo kunizidi? Umri, maarifa au elimu? Nimeshakupima na nina hakika vyangu viko juu.
Nimeona nini unaita manufaa posti yako ya chini na kubaini kuwa huna unaloweza kunifundisha juu ya manufaa kwani wewe mwenyewe hujuwi maana ya hilo neno, sikwambii sasa kuorodhesha.
Kwa ufupi hoja tulionayo hapa ni kwa CCM na vijana wake wakubali ukweli kama kweli wanakusudia muungano na kwa bahati nzuri Wazanzibari walio wengi hawataki unafiki kuwa Muungano katika muundo wa sasa una manufaa kwa wote (kama anavyodai Nape) tofauti na unavyofikiria kuwa huo muungano unawanufaisha Wazanzibari!
 
Haki yako unaidai vipi? wewe kama unaona haki yako imechukuliwa unachotakiwa kuifanya ni kuichukua tu iwe kwa nguvu au amani; watanzania bara tulishakuwa huru siku nyingi ulishawahi kumsikia mbara akidai uhuru? na uhuru huo tuudai kutoka kwa nani?

Ahsante Bwana Chama umesema mengi kwa maneno machache! Lakini;
1.Ushauri wako wa kudai chetu tunaamuwa kwa njia ya amani.
2.Kama mlivyopata uhuru nyie basi na iwe zamu yenu kutuachia huru sisi
3. Kama muingereza alikupeni uhuru na hamkuuchukuwa wenyewe basi na sisi tunadai na mtupe kwa amani vile vile.
4. Naomba kukuuliza hiyo nchi yako huru inaitwaje na nini mipaka yake?
 
Nape anaenda mbali sana kudanganya umma kwamba muungano wa serikali mbili ndio uliodhamiriwa katika mkataba wa muungano, 1964; Ana bahati anakimbia mijadala ambayo tungemwomba ushahidi; Na anajifunga sana kuja na hoja kwamba sera ya serikali mbili ni sera ya ccm ambayo ccm itaipigania mpaka mwisho wa dunia;kwani ccm (au hata TANU) ilitajwa sehemu yoyote ya mkataba wa muungano? TANU ilikuja baadae sana katika makabrasha ya muungano huku yale original yakipotezwa, ambapo kupitia sheria namba 24 ya mwaka 1967, jina Tanganyika likazikwa rasmi na kubatizwa Tanzania Bara; Kwa vile hili lilikuwa ni kosa, haikuwezekana kwa TANU kuja na katiba mpya ya JMT ndio maana mwaka 1965, badala ya marais wa pande zote mbili kuja na baraza la katiba kwa ajili ya serikali ya JMT ndani ya miezi kumi na mbili kama mkataba wa muungano ulivyoelekeza, nchi ikaingizwa katika katiba ya muda kuanzia 1965 hadi 1977 solution ilipobainika kwamba ni kwa kushawishi ASP wajiunge na TANU ili kuzaa CCM na kuipa CCM (dodoma) mamlaka juu ya masuala ya muungano na yasiyo ya muungano (ya Tanganyika na Zanzibar); Hapo ndipo chama kikashika hatamu rasmi, huku zanzibar chini ya katiba ya JMY (1977) sambamba na malengo ya katiba ya ccm (1977),zanzibar ikabadilishwa jina kuwa Tanzania zanzibar ili kiini macho cha serikali mbili kifanikiwe;kiini macho hiki kikashtukiwa na zanzibar ambapo baada ya miaka miwili (1979) wakaunda katiba yao ya kwanza since mapinduzi (1964), na mwaka 1984 wakafanikiwa kurudisha utambulisho wao za zanzibar badala ya "Tanzania Zanzibar" kwa mujibu wa katiba ya JMT (1977); Watanganyika wakaendelea kunywa kilevi cha kiini macho hivyo kutoona madhara ya kuitwa Tanzania bara badala ya Tanganyika;leo watanganyika ndio wanaamka, lakini badala ya kuelewa kwamba adui yao ni katiba ya JMT 1977, eti adui ni zanzibar wakati hawa wanafuata mkataba wa muungano,1964, ambao nape anathubutu kuupotosha kwenye magazeti;

Jamani, muungano wetu haukuwa muungano wa vyama vya siasa (Tanu na Asp), bali wa wananchi, ndio maana mkataba wa muungano ulikidhi vifungu vya mikataba ya mahusiano ya kimataifa, na ndio maana ukitazama mkataba wa muungano kurasa ya kwanza hadi ya mwisho, hakuna sehemu inataja chama au vyama vya siasa, au tanu na asp;

Nape anaposema muungano ni sera ya ccm, yupo sahihi, lakini aje kujibu hapa kwamba tangu lini sera ya chama cha siasa ikawa sheria? hata chadema ni muhimu wawe waangalifu, wasiseme kwamba muungano wa serikali tatu ni sera ya chadema kwani watatupeleka kule kule kwenye madudu ya ccm pale TANU ilipoteka muungano 1965 kupitia katiba ya muda; Chama cha siasa kuja na sera ya muungano ni hatari kwani kikija chama nje ya ccm na cdm na kusema sera yao ni serikali kumi, tutafika wapi? Cha lufanya ni kurudisha mamlaka kwa wananchi kupitia kura ya maoni juu ya muungano; Chadema, ccm, wote waje na msimamo kwamba sera yao ni muungano utokanao na wananchi walio wengi kupitia kura ya maoni; vinginevyo kauli za Nape kwamba ccm itaulinda muungano wa serikali mbili maana yake ni mbili:kwanza, anajua kwamba muungano wa serikali mbili maana yake ni TANU + ASP = CCM; Hakika, serikali tatu itavunja ccm katika vipande sio chini ya vitatu - wana asp die hards ambao hawakushirikishwa 1964, wana asp walioshirikishwa,, wana ccm wa 1977, na wana tanu wanaotafuta tanghanyika yao, na hivyo kupelekea ccm kupoteza legitimacy, hasa zanzibar;Pili, Nape anatoa ishara kwamba tofauti na mwalimu kusema kwamba watakaokataa muungano hatowapiga mabomu, kwa kauli ya nape kwamba ccm itaupigania mfumo wa sasa hadi mwisho wa dunia, basi tukijiandaa kuandamana kupinga hilo, tutarajie MABOMU; hata tukiuwawa au kuzuiwa kufanikiwa kimaisha, hakuna kilicho na faraja kama ukifa ukijua unasimamia haki na kitu unachokiamini na sio tumbo;

Kesi iliyofunguliwa zanzibar kuhusiana na nyaraka za mkataba wa muungano, 1964 will be interesting to watch, na tuombee uzima kuona how the entire saga unfolds; Vinginevyo tatizo la muungano ni ccm, tukiri hilo ili tuanza upya kama kweli chama kina nia ya kuendelea kuwa na uhalali wa kutawala;

cc: Jasusi, JokaKuu, Nguruvi3

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Nina uhakika 100% Nape hawezi kusoma chote kilichoandikwa na hata akifanikiwa kusoma bado asingeweza kuelewa na hata akielewa hawezi kujibu chochote na kama akijibu kitu basi ni mashudu matupu.

Habari ndio hiyo.
labda mleta mada angeileta kwa njia ya PICHA/MZIKI hii mada.
 
Tanganyika ni haki yetu Watanganyika.
CCM hawaitaki Tanganyika kwa vile wanakumbatia na kuwapa uongozi maghaibhu kama vile sisi wamatumbi hatupo
 
Watanganyika msipo badilika wakati utakubadilisheni kwa lazima.
 
Watanganyika msipo badilika wakati utakubadilisheni kwa lazima.

Tatizo ni kwamba wengi wanadhania kwamba hata suala la kubadilika ni la kisera zaidi i.e. top - down approach, wakati mabadiliko ni wao wenyewe i.e. bottom - up approach;
 
Tanganyika ni haki yetu Watanganyika.
CCM hawaitaki Tanganyika kwa vile wanakumbatia na kuwapa uongozi maghaibhu kama vile sisi wamatumbi hatupo

Muungano wa Tanganyika na zanzibar ulikuja mwaka 1964,na wakati huo CCM haikuwepo bali TANU; na hata TANU yenyewe, ilikuwa bado inaendelea kutafuta uhalali wa kisiasa Tanganyika nzima, huku kwa upande wa Zanzibar, napo ASP ikiwa inaendelea kutafuta uhalali wa kisiasa Zanzibar nzima; Pamoja na hayo, Mkataba wa Muungano hautaji chama chochote cha siasa, sio TANU wala ASP vinatajwa kwenye Mkataba wa Mungano. TANU ilikuja ingia kwenye suala la muungano (kisheria) baada ya mkataba kusainiwa;

Unaposema hapo juu kwamba:

CCM hawaitaki Tanganyika


Tujiulize, je ni lini CCM ilihusishwa na Tanganyika? iliyohusishwa na Tanganyika ilikuwa ni TANU, sio CCM (yani TANU + ASP), kwahiyo sio kitu cha ajabu kwa ccm kutoitaka Tanganyika kwani haina uchungu nae kwani CCM sio mzazi wa Tanganyika bali TANU; implications za ccm kuikubali Tanganyika maana yake ni CCM minus (sio Plus) ASP yani (CCM - ASP which equals to TANU);Kumbuka pia kwamba, mfumo wa serikali mbili ambayo ni sera ya CCM , maana yake ni muungano wa Vyama Viwili vya TANU (tanganyika) na ASP (zanzibar); Lakini pia tufahamu kwamba sera ya chama cha siasa haiwezi kuwa sheria, hilo liliwezekana chini ya katiba ya JMT (1977) ambayo literally ni TANU + ASP, ambayo iliipa CCM (dodoma), hatamu na kuwa juu ya kila kitu - bunge, mahakama, serikali na hata katiba ya nchi (1977) katika masuala ya muungano, masuala yasiyo ya muungani zanzibar na masuala yasiyo ya muungano tanganyika; Katika zama hizi za vyama vingi, hilo haliwezekani tena - yani kuifanya sera ya chama cha siasa kuwa sheria ya nchi; CCM wataendelea kupambana na hili lakini mwisho wake itaanguka tu; Ni muhimu ianze kuzuia anguka lake katika hili mapema sana kama kweli nia ni kuendeleza uhalali wa CCM kuongoza nchi;
 
Tatizo la Nape Nnauye si mtu wa mijadala ya hoja,anaanzisha mjadala alafu analala mbele.Kimsingi aliibua hoja nzuri tatizo hakujipanga kuisimamia.

Hoja za muungano zimeibuka miaka mingi zikapuuzwa lakini sasa naona mabadiliko makubwa ya lazima yanakuja.

CC Tundu Lissu
 
Last edited by a moderator:
Hoja za muungano zimeibuka miaka mingi zikapuuzwa lakini sasa naona mabadiliko makubwa ya lazima yanakuja.

CC Tundu Lissu

Ni kweli lakini sidhani itatokea kabla ya kina mchambuzi na wengine wanaodai haki yao ya wazi na ya msingi kabisa, kushughulikiwa; Tunazidi kusali kwa mwenyezi mungu isitokee hivyo;


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli lakini sio kabla ya kina mchambuzi na wengine kushughulikiwa;


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mkuu hili swala sasa ni mjadala wa kitaifa hivyo ili iwe kama wanavyotaka ni kuzima mjadala kuhusu muungano kibabe (hii itawapa nafasi ya kupumua for sometimes) lakini kwavile ni swala la katiba mpya halikwepeki mbele ya UMMA!!

Kelele za katiba mpya ilikuwa ni kutoa fursa kama hizi hivyo wakati ndio huu na Umma unahoji sasa.
 
Mkuu hili swala sasa ni mjadala wa kitaifa hivyo ili iwe kama wanavyotaka ni kuzima mjadala kuhusu muungano kibabe (hii itawapa nafasi ya kupumua for sometimes) lakini kwavile ni swala la katiba mpya halikwepeki mbele ya UMMA!!

Kelele za katiba mpya ilikuwa ni kutoa fursa kama hizi hivyo wakati ndio huu na Umma unahoji sasa.

Kuna maswali kadhaa nilimuuliza mdau mwenzetu nguruvi3 katika mjadala tofauti na huu, na moja ya maswali hayo lilikuwa hili lifuatalo:

Je, unadhani ccm itafanya maamuzi gani kuhusiana na mfuno wa muungano ndani ya katika mpya na nini kitatokea as a result? Jaribu to time travel kidogo assuming unaweza predict move ya ccm;


Majibu ya nguruvi3 yalikuwa kama ifuatavyo:

Kuhusu swali la Pili, kwasasa hivi CCM inataka serikali 2 kwa faida zake kisiasa .
Kinachofuata baada ya kufundisha mabaraza ya kata ni kuweka shinikizo kwa viongozi wa tume ya Warioba.
Hadi sasa tayari wameanza kuwatisha kuwa nchi inaingia katika matatizo kwasababu yao.

Halafu watatumia bunge la katiba kupitisha kwa nguvu rasimu ambayo wao wanaitaka.
Wanachotaka ni ku buy time kuwa rasimu ya mwisho iwe na option mbili ya serikali mbili na tatu.

Wakivuka kikwazo hicho basi watatumia bunge la katiba ambalo kwa namna lilivyokubaliwa litakuwa na wajumbe wengi wa CCM. Hoja itapitishwa kwa nguvu kuwa wananchi wanataka serikali 2.

Bunge la katiba litakuwa na CCM wengi ambao matamanio yao ni 2015. Wengi hawataweza kufanya maamuzi ambayo ni independent kwa faida ya nchi. Nguvu ya wapinzani itazimwa kwasababu bunge hilo litakuwa na spika wa CCM atakayerekebisha mambo. Kura itatumika sana kuzima hoja za upinzani.
Mkuu mtazamo, nini maoni yako katika hili.

cc Nguruvi3
 
Kuna maswali kadhaa nilimuuliza mdau mwenzetu nguruvi3 katika mjadala tofauti na huu, na moja ya maswali hayo lilikuwa hili lifuatalo:


[/SIZE][/FONT]
Majibu ya nguruvi3 yalikuwa kama ifuatavyo:

Mkuu mtazamo, nini maoni yako katika hili.

cc Nguruvi3

Mkuu wangu,

Mzee wetu Nguruvi3 amejibu vizuri sana lakini mpango huo wa CCM unachangamoto ngumu kama ifuatavyo;-

1) Msimamo wa Wazanzibar kuhusu muungano hawana ubavu wa kuubadilisha kupitia bunge la katiba (labda wakubaliane nao kukubali mapendekezo yao yote ya msingi lakini chini ya serikali mbili ambacho ni kituko).

2) Wapinzani hasa Chadema kuunga mkono mapendekezo ya tume huku wakionekana kukubalika na UMMA hivyo kuwapa nguvu tume kufanya maamuzi yatayoweza kuwashangaza (najua tume ipo makini kila hatua ili usitokee mkaragano wa ghafla utaopelekea nguvu ya katiba ya sasa kutumika ipasavyo (nadhani umenielewa)).

3) Yote juu ya yote katiba mpya itaamuliwa kukubaliwa au kataliwa na Watanzania wenyewe hivyo nguvu ya UMMA ipo pale pale.Lazima CCM wakitaka kushinda ni kwa ushawishi tu wa hoja na si ujanja ujanja.Ndio maana Upinzani unavyoweka mtaji wake ktk UMMA hasa kuwaelimisha naona anguko la kila hila juu ya katiba mpya.
 
Last edited by a moderator:
Mkiwa na nchi ambayo mtu kama nape ndio mshauri wa mambo ya msingi basi hiyo nchi ipo mahutihuti!!!! Tanzania is a Union of TANGANYIKA and Zanzibar if they think they love Muungano. Wauwe Zanzibar nchi iwe moja Tanzania Otherwise the best OPTION is three Governments............We need out Tanganyika to be Recognised!
 
Mkiwa na nchi ambayo mtu kama nape ndio mshauri wa mambo ya msingi basi hiyo nchi ipo mahutihuti!!!! Tanzania is a Union of TANGANYIKA and Zanzibar if they think they love Muungano. Wauwe Zanzibar nchi iwe moja Tanzania Otherwise the best OPTION is three Governments............We need out Tanganyika to be Recognised!

Zanzibr msitarajie kufa labda ife tanzania murudi kuwa watanganyika.
 
Mkuu wangu,

Mzee wetu Nguruvi3 amejibu vizuri sana lakini mpango huo wa CCM unachangamoto ngumu kama ifuatavyo;-

1) Msimamo wa Wazanzibar kuhusu muungano hawana ubavu wa kuubadilisha kupitia bunge la katiba (labda wakubaliane nao kukubali mapendekezo yao yote ya msingi lakini chini ya serikali mbili ambacho ni kituko).

2) Wapinzani hasa Chadema kuunga mkono mapendekezo ya tume huku wakionekana kukubalika na UMMA hivyo kuwapa nguvu tume kufanya maamuzi yatayoweza kuwashangaza (najua tume ipo makini kila hatua ili usitokee mkaragano wa ghafla utaopelekea nguvu ya katiba ya sasa kutumika ipasavyo (nadhani umenielewa)).

3) Yote juu ya yote katiba mpya itaamuliwa kukubaliwa au kataliwa na Watanzania wenyewe hivyo nguvu ya UMMA ipo pale pale.Lazima CCM wakitaka kushinda ni kwa ushawishi tu wa hoja na si ujanja ujanja.Ndio maana Upinzani unavyoweka mtaji wake ktk UMMA hasa kuwaelimisha naona anguko la kila hila juu ya katiba mpya.
MTAZAMO hapa umegusia jambo moja muhimu sana ambalo ni ujanja ujanja wa CCM.

Kuna makosa makubwa sana yanayofanywa na CCM hasa kwa kuwatumia vijana kama akina Nape.
Hoja ya katiba mpya ilitekwa kiujanja ujanja, mswada ukapitishwa kiujanja ujanja na hata tume ikaundwa kiujanja ujanja.

Ulikuwa ni upotofu wa kudhani kuwa tunaweza kuandika katiba bila kukaa pamoja kama taifa na kujiuliza tunaandika katiba kwa sababu zipi na ikidhi haja zipi ambazo zimejitokeza kutokana na nyakati na kizazi.
Hoja ya nyakati na kizazi inaweza kutolewa mfano mzuri kwa suala la muungano.

Ni kuanzia hapo tulipaswa kujiuliza kama sababu za muungano bado zipo na endapo sababu hizo zina manufaa kwa pande zote mbili za muungano. Jibu lingepatikana kwa kupitia mijadala ya kitaifa na kisha kura ya maoni.
Tungekuwa na majibu hadi sasa kama tunahitaji muungano na ni wa aina gani au wakati umepita na hatuhitaji kabisa.

Ujanja wa CCM ni huu wa kupitia mabaraza ya katiba na kulitegemea bunge la katiba kwa kuzingatia wingi wao.
CCM na akina Nape wanasahau kuwa hatuandiki katiba ya vyama bali ya nchi na mustakabali wa nchi na kizazi kijacho.

CCM imeshau kuwa Jaji Warioba akiwa mwanasheria mkuu wa serikali alikataa kabisa kuliongelea suala la katiba akisema iliyopo inatosha na hakuna sababu za kuandika mpya. Lilikuwa ni suala la wakati na Jaji Warioba huyo huyo amekubali ulazima wa kuandika katiba. Maana yake ni kuwa nyakati na kizazi havikuweza kuzuilika kwa kutumia ujanja ujanja.

Sasa hivi wanatumia ujanja ujanja kuvuta subira ili kushinikiza uwepo wa serikali 2 au tatu katika rasimu ya mwisho il kura zipigwe na kwa kutumia ujanja ujanja wanaweza kushinda kwa majority.

Huu ujanja ujanja ni wa kitoto na usio na chembe ya fikra. Nape anapaswa ajiulize nguvu kama za kutaka Tanganyika irudi zinatoka wapi? Nguvu za kudai katiba mpya zinatoka wapi? Na kwamba, je, ujanja huo unaweza kutupa muafaka wa kitaifa?

Tatizo linalomkabili Nape ni kuamani kuwa nchi ni CCM na kwamba masilahi ya CCM ni bora zaidi kuliko masilahi ya umma. Nape ameamua kuupiga mabomu muungano kwa kutoujadili kwa haja na mantiki bali nukuu mbili zisizowakilisha dhana ya Mwalimu Nyerere.

Nyerere alitamka kuwa hawezi kuwapiga mabomu wznz kama hawataki muungano. Sijui nape anasemaje kuhusu mwalimu kama Watanganyika hawatautaka muungano.

Watu kama akina Nape ndio wanaoua muungano kama haja ya uwepo wake ipo. Kwa kutumia vikao wamekuwa wanalaghai kuhusu tume na vikao vya kero za muungano na hivyo kuudhoofisha kiasi cha kufikia mahali haupo tena kimantiki bali kinadharia.

Muhimu sana kwa akina Nape ni kuelewa kuwa nguvu ya umma inaweza kuzimwa kwa siku moja kwa mabomu na ujanja lakini haitoi jibu la kudumu hata siku moja.

Shah wa Iran alipoakumbuna na nguvu ya vijana alitumia kila silaha iliyokuwepo katika ghala .
Mwisho akawa mkimbizi na kufia ughaibuni. Ndivyo ilivyokuwa kwa Fernando Marcos, Tianmen, n.k.

Nguvu ya kizazi cha vijana wa leo ni kuona Tanganyika inarudi, inalinda utaifa wake na watu wake, inasimamia rasilimali zake na inajiendeleza kwa faida ya watu wake.

Tanganyika ni second to none, na kama ipo haja ya muungano basi iangaliwe kama inakidhi na ina masilahi kwa Tanganyika.

Nguvu hii ya vijana ndio Nape anayojaribu kupambana nayo na ujanja ujanja, lakini lazima ajiulize kama Mwalimu alishaiona na kusema hatapiga mabomu nchi kwasababu ya muungano, wapi ushujaa wa Nape wa kupambana na nguvu inayotaka kujitambua kama taifa?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nguruvi3,

Hoja zako katika bandiko #38 zinasisimua sana, hasa kuhusiana na mtazamo wako kuhusiana na jinsi gani unadhani CCM itajihusisha na mchakato wa katiba mpya, hasa suala zima la uamuzi juu ya mfumo “sahihi” wa muungano;

Nadhani ni muhimu tukajikita pia katika kujadili Mwalimu’s fears kuhusiana na ujio wa serikali ya Tanganyika ili tupime uzito wa hoja za Nape, hasa hoja yake kwamba msimamo wa CCM ni kulinda mfumo uliopo (serikali mbili) hadi ‘Mwisho wa Dunia’. Bear in mind, to everything, there is an opposite, hivyo kauli ya Nape implies, serikali tatu ndio mwisho wa CCM;

Kama unakumbuka vizuri, uongozi wa CCM katika awamu ya pili (uongozi ambao leo bado upo chini ya chama kile kile cha CCM), uliruhusu hoja ya Tanganyika iende bungeni; Ningependa kusikia maoni yako, hasa kuhusiana na uamuzi wa wakati ule chini ya Rais wa pili wa JMT (Ali Hassan Mwinyi), Waziri Mkuu wa JMT (John Malecela), Katibu Mkuu wa CCM Taifa (Marehemu Kolimba), Spika wa Bunge (Pius Msekwa) na wengineo; Kwa maoni yako, Je:

· Kitendo Cha kuruhusu hoja husika iende bungeni, kilikuwa ni cha Kishujaa au ilikuwa ni Udhaifu kwa upande wa uongozi wa nchi katika awamu ya pili?

Pia, sote tunaelewa jinsi gani agenda ya Tanganyika hatimaye ilipanguliwa kwa hoja (kupitia Mwalimu Nyerere), hasa kwa hoja kwamba ujio wa Tanganyika ungepelekea kuvunjika kwa muungano uliopo; Katika hili, ningependa kusikia maoni yako, Je:

· Kitendo cha viongozi wa CCM wa wakati ule to make decisions contrary to Nyerere’s wishes (kuruhusu hoja ya Tanganyika iende bungeni), were they acting for the “unity of the party (CCM)” or for the “unity of the country (Tanzania)”?

· Na vipi kuhusiana na Mwalimu Nyerere, je intervention yake ililenga kipi zaidi in your view – partisanship (ccm) or country’s interest?

· Kufuatia hoja mbalimbali za Nape kuhusiana na msimamo wa CCM juu ya Serikali mbili, je kwa mtazamo wako, Nape is acting for what interest - for the unity of the party through unity of the country or for the Unity of the country through unity of the party?

Suala lingine ambalo ningependa kujadili ni kwamba, katika muktadha wa katiba mpya na changamoto za muungano, wapo wanaoweza kujenga hoja kwamba linapokuja suala la Tanzania (sio Zanzibar pekee au Bara pekee), so far hakuna chama cha siasa ambacho kina provide a viable alternative to “Tanzanians” in terms of vision, leadership, organization, na progammes za kulipeleka taifa la Tanzania mbele; Kwa mfano, kwa upande mmoja, leo CUF inaweza jadilika as an alternative to CCM kwa wazanzibari wengi, huku chama hicho (CUF) kikiwa hakina much influence kwa upande wa “Bara”; Kwa upande mwingine, Chadema inaweza jadilika as an alternative to CCM “Bara”, huku chama hicho kikiwa hakina much influence kwa upande wa Zanzibar;

Kutokana na mapungufu haya ya vyama vikubwa nchini nje ya chama tawala (CCM) - CUF na Chadema, watu wanaweza kujenga hoja kwamba its by default that CCM emerges as the only political party that can unite both sides of the Union kwa mafanikio zaidi; Tukumbuke pia kwamba CCM is nothing more than Chama cha Siasa chenye sura ya Umoja wa Kitaifa (TANU na ASP), na kama tunakubaliana katika hili, basi ni rahisi pia kukubaliana kwamba Umoja huu wa Kitaifa ambao ndio umezaa muungano kupitia katiba za JMT (1977) na CCM (1977), utaingia dhoruba kali sana iwapo Serikali ya Tanganyika itafanikiwa kurudi kwani muungano wa TANU na ASP kwa mujibu wa Katiba ya CCM (1977) utapoteza legitimacy, hasa upande wa Zanzibar ambao bado una ASP die hards waliopo katika sehemu mbalimbali; Ningependa kusikia maoni yako kwamba je:

· Ni sahihi kusema kwamba the unity of CCM in this period is a factor of stability in the country (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)?

· What should be CCM’s stabilizing role katika nyakati hizi za mabadiliko? Katika muktadha huo, What should CCM prepare to loose, and what will it gain, if any?


Nitarudi kujadili Mwalimu's fears kuhusiana na serikali ya Tanganyika;
 
Gazeti la leo la RAIA MWEMA(Agosti 31, 2013), lina taarifa ukurasa wa mbele yenye kichwa cha habari kisemacho:

"Takwimu za TRA Zaipinga CCM Kuhusu Serikali Tatu."

Kwa mujibu wa taarifa hizo, shirikisho ndani ya muundo wa serikali tatu si gharama kwa wananchi kwani takwimu za TRA zinapingana na hoja za Nape Nnauye na wenzake ndani ya CCM; Nape na baadhi ya viongozi wa ccm wamekuwa wakijenga hoja kwamba, muundo wa serikali tatu utazidisha gharama kwa wananchi na utaongeza urasimu, lakini kwa mujibu wa uchunguzi wa raia mwema, hoja ya Nape na wenzake haina mashiko kwasababu Tume ya warioba imelenga kupunguza gharama hizo kupitia mapendekezo ya tume ya kupunguza masuala ya muungano kutokea 22 hadi saba tu; hoja hii imekuja ikijadiliwa na Nguruvi3 mara kwa mara, lakini pia binafsi, nimekuwa nikijadili jinsi gani gharama za kuendesha muungano zinavyokuwa kubwa kutokana na kuhudumia kiini macho badala ya uhalali wa muungano kwa mujibu wa Mkataba wa muungano, 1964;

Kwa mujibu wa gazeti la raia mwema ambalo linadai lina vyanzo vya uhakika kutoka serikalini, muundo wa sasa wa muungano kupitia sera ya ccm ya serikali mbili, muundo ambao Nape ameshasema ccm itaupigania hadi mwisho wa dunia, muundo huo ambao una masuala 22 ya muungano gharama zake ni shillingi trilioni 1.2 kwa mwaka (one point two trillion shillings per year); sasa kwa vile tume ya warioba inapendekeza masuala 22 ya muungano yapungue kubakia masuala saba tu chini ya katiba mpya, maana yake ni kwamba gharama ya 1.2 trillion shillings lazima itashuka;

Chanzo cha uhakika kutoka serikali kilichonukuliwa na raiamwema kinasema kwamba - kwa sasa, mapato yanayokusanywa na serikali ya JMT ni karibia shillingi trillioni 5.5, ambapo kodi ya mapato (excise duty) zinakusanywa sh trilioni nne na ushuru wa bidhaa shilingi bilioni 500 na ushuru wa bidhaa shilingi trilioni 1.1, ambazo hutumika kugharamia shughuli za muungano (masuala 22) na shughuli za Tanzania bara (Tanganyika);

Rasimu ya katiba inapendekeza vyanzo vya mapato ya serikali ya shirikisho la JMT (serikali tatu) liwe ni ushuru wa bidhaa na maduhuli yatokanayo na vyanzo nje ya kodi kama vile Jeshi la wananchi, polisi, uhamiaji na wizara ya mambo ya nje, taasisi na vyomba ambavyo hukusanya mapato kutokana na huduma mbalimbali za vyombo hivi kwa umma; Kwa mujibu wa chanzo cha serikali kwa raia mwema, mapato ya maduhuli yanayokusanywa na taasisi za muungano yanafikia shillingi bilioni 79;

Kwa maana hii, Nape Nnauye hana hoja kwani anapingana na rasimu ya katiba yenye lengo la kupunguza gharama za muungano, na takwimu husika zipo hadharani;nadhani Nape na wengine ndani ya ccm wenye mtazamo kama wake sasa watakuwa waangalifu na kuacha kudanganya umma kwa malengo ya siasa binafsi; waelewe kwamba, muda sio mrefu, umma utaelimika kwamba ujio wa serikali ya Tanganyika itakuwa nafuu kwao na vizazi vyao kwani itapunguza gharama za kuendesha muungano, hasa ikizingatiwa kwamba masuala ya muungano yatapungua kutoka 22 hadi saba, na pia kwamba fedha zitokanazo na excise duty na maduhuli zitatosha kabisa kuendesha muungano;

Vinginevyo, Nape Nnauye, kwa vile ulikuja humu kurekebisha taarifa zilizochapishwa juu yako na gazeti la mtanzania, leo tena, gazeti la raiamwema pia limekujadili (pia meya ma------)katika habari hiyo hapo juu kwamba unapinga serikali tatu kwa hoja kwamba itakuwa ni ongezeko kwa gharama za kuendesha muungano; tungefarijika sana iwapo ungejitokeza kujadili taarifa za raiamwema la leo kwa hoja ili tufahamu iwapo raiamwema wamepotosha ukweli wenyewe au huo ndio msimamo wako;

Cc Nguruvi3, JokaKuu, Jasusi, MTAZAMO, Kobello, Ngongo, AshaDii, Mzee Mwanakijiji@zomba, Ritz, ZeMarcopolo, Zakumi;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom