Nape, Simamia Tanganyika na Vijana Wenzako

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,436
Hivi karibuni, Katibu Wa Itikadi na Uenezi wa CCM (Taifa), Nape Nnauye, ambae pia ni mdau mwenzetu humu Jamiiforums alikuja na bandiko lenye nukuu ya mwalimu kama ifuatavyo:

Re: JK NYERERE: "Serikali tatu ni sumu kwa Muungano"
By Nape Nnauye

Haya ni maneno ya Mwl kwenye kamati kuu ya CCM mwaka 1993:
"Huwezi kumpima mgonjwa, ukajua ugonjwa wake halafu dawa ikawa sumu! Nakubali yapo matatizo katika Muungano wetu, tutafute dawa ya matatizo hayo na dawa haiwezi kuwa serikali tatu, serikali tatu ni sawa na kumpa sumu mgonjwa atakufa tu"!

Nape Moses Nnauye
The CCM Secretary for Ideology & Publicity

Pamoja na umuhimu wa bandiko lako hili, kwa bahati mbaya, haukurudi kusimamia hoja uliyoanzisha. Inawezekana ulibanwa na majukumu ya Chama, lakini mbaya zaidi, haikuchukua muda mrefu kabla ya bandiko husika kuhamishwa na moderators wa Jamiiforums na kupelekwa kwingine, na hivyo fursa yetu vijana kujadiliana hoja hii muhimu kwa maslahi ya taifa, kuyeyuka. Hili ni tatizo kwani mwenendo mzima wa mjadala ulitoa ishara kwamba pengine Nape alikuwa anawasilisha msimamo rasmi wa CCM kuhusiana na mfumo wa muungano chini ya Katiba Mpya. Kama nipo sahihi, basi uamuzi wa CCM wa kutumia nukuu hii ya Mwalimu bila ya kuifanyia upembuzi yakinifu, hasa kwa kutotilia maanani mahitaji na mazingira ya sasa ya nchi, it will be a grave mistake that CCM will live to regret.

Nape, una career ndefu bado ahead of you kwani bado ni kijana, hivyo ni muhimu ukaanza kuchambua mambo kwa mtazamo wa kitaifa zaidi, hasa kwa kulenga mahitaji ya vijana nchini badala ya kuendelea kung'ang'ania mawazo na mitazamo mingine ambayo aidha imepitwa na wakati au haitatui tatizo ina ahirisha na kulea tatizo. Iwapo una amini katika Tanganyika, hata ikitokea kwamba utapewa adhabu na chama kwa msimamo huo, fahamu tu kwamba bado utaheshimika kwa kuchagua the correct side of our country's history. Usidanganywe otherwise.

Nianze moja kwa moja na nukuu yako kutoka kwa Mwalimu Nyerere kwamba:

"Nakubali yapo matatizo katika Muungano wetu."

Ni muhimu ukaelewa kwamba, kabla ya kingine chochote, Mwalimu (miaka 23 iliyopita) anakiri kwamba Muungano una matatizo. Vijana wengi tulitarajia kwamba ungeonyesha uwezo na weledi wako kwa kumuunga mkono Baba wa Taifa kuhusiana na hoja kwamba "muungano wetu unakabiliwa na matatizo". Kitendo chako kumuunga mkono Mwalimu Nyerere, hasa kutokana na nafasi yako ndani ya CCM, would have sent a very positive vibe kwa Vijana wenzako ndani na nje ya CCM ambao kila kukicha, wanazidi kuelewa juu ya umuhimu wa serikali ya Tanganyika. Ni bahati mbaya sana kwamba umepoteza fursa hiyo. Vinginevyo, vijana wengi nje na ndani ya CCM wanazidi kuelewa kwamba Mwalimu alikuwa na NIA nzuri kwa Muungano wetu, tatizo likawa ni UTEKELEZAJI wa NIA husika, hasa kwa kusimamia sera ya CCM ya mfumo wa serikali mbili, ambayo practically, haiwezekani kulinda muungano wetu. Dawa sahihi ya kutibu tatizo ndani ya muungano wetu ni kwa kuirudisha serikali ya Tanganyika, serikali ambayo ilifutwa kwa mujibu wa sheria namba 24, mwaka 1967.

Kuirejesha Tanganyika itakuwa ni dawa kwani hivyo ndivyo hali ya Haki na Usawa miongoni mwa washiriki wa muungano itarejea, la sivyo hali ilivyo itapelekea Tanganyika kujitoa kabisa katika muungano. Vinginevyo, sababu ya msingi kwanini watanganyika wengi (ukipenda waite watanzania bara) wanaendelee kuona kwamba Zanzibar ni mzigo mkubwa kwa Tanganyika ni kwamba. Kwanza, watanzania wengi hawajui kwamba wazanzibari wanajaribu kufuata kilichokubaliwa chini ya Mkataba wa Muungano (1964). Pili, Katiba ya JMT (1977) inamfanya Rais wa Muungano pia kuwa Rais wa Tanganyika, ingawa Urais wa Tanganyika unafichwa na kiini macho kilichopo ndani ya mfumo wa serikali mbili ambapo Katiba ya JMT (1977) ndio hiyo hiyo inatumika kama Katiba ya Tanganyika, kuendesha mambo ya Tanganyika (Tanzania bara) yasiyo ya muungano. Ndio maana gharama za kuendesha muungano zimekuwa ni KUBWA kwani Watanganyika (Tanzania bara) wanagharamia kiini macho badala ya reality per articles of the union, 1964.

Nape, tukiendelea kuisoma zaidi nukuu yako ya mwalimu hapo juu, tunaona Mwalimu Nyerere anaendelea kujadili kwamba:

"Tutafute dawa ya matatizo hayo na dawa haiwezi kuwa serikali tatu, serikali tatu ni sawa na kumpa sumu mgonjwa atakufa tu."

Nape, hapa tunagundua kwamba Mwalimu Nyerere anakiri kwamba Muungano unakabiliwa na matatizo, lakini Mwalimu falls short of mentioning Tanganyika, badala yake anaijadili "Serikali ya tatu" ambayo sote tunajua kwamba it is synonymous to ‘Tanganyika'. Nadhani unafahamu kwamba kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano (1964), serikali zilizohusishwa zilikuwa ni za Tanganyika na Zanzibar, lakini kufuatia Katiba ya JMT (1977), mwaka ambao CCM pia ilishika hatamu baada ya kuungana kwa vyama vya TANU (kutoka Tanganyika) na ASP (kutoka Zanzibar) na kuzaa rasmi CCM February 1977, sera rasmi ya CCM juu ya Muungano imekuwa ni Serikali mbili:

Kwanza ni Serikali ya Zanzibar inayoshughulikia masuala ya Zanzibar yasiyokuwa ya muungano (uvuvi, afya, n.k); Pili ni Serikali ya Muungano inayoshughulikia masuala ya Muungano tu (Ulinzi, Mambo ya Ndani, Mambo ya Nje n.k). Je, masuala ya Tanganyika (au bara) ambayo siyo ya muungano (e.g. Elimu, Afya, Kilimo), haya yanashughulikiwa na Serikali ipi? Jibu ni Serikali ya Muungano, mifano ipo mingi lakini mifano rahisi ni pamoja na kwamba – kwa miaka karibia 50 sasa, it has become common practice kwa Rais wa muungano kuunda idara, taasisi, na wizara mbalimbali ambazo hazina uhusiano na masuala ya muungano, huku Rais huyo huyo pia akiunda idara, taasisi na wizara mbalimbali za kusimamia na kuratibu masuala ya muungano, huku Rais wa Zanzibar yeye akifanya hayo kwa masuala ya zanzibar ambayo yapo nje ya muungano. Kwa maana hii, kwa miaka karibia 50, the practice has been three governments, huku sera rasmi ya CCM (in theoretical and rhetoric terms) ikiendelea kuwa serikali mbili – Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano. Huu ndio mzizi wa tatizo ambalo Nyerere anakiri kwamba limekuwepo huku DAWA ikionekana kuwa ni SUMU.

Swali langu kwako Nape ni Je:

  • Je, hakuna uwezekano wa SUMU kufanya kazi kama DAWA?

Nape, hapa ndipo weledi na umakini wako kama Kiongozi ndio ulihitajika kuwakilisha maoni, matakwa na matarajio ya kizazi cha vijana wenzako kujadili sehemu iliyobakia ya hoja ya Mwalimu Nyerere uliyotuwekea hapo juu kwamba:
"tutafute dawa ya matatizo hayo na dawa haiwezi kuwa serikali tatu, serikali tatu ni sawa na kumpa sumu mgonjwa atakufa tu."

Tulikutarajia uonyeshe weledi na leadership yako kwa niaba yetu sisi vijana wenzako, hasa kutokanana nafasi yako hadimu ndani ya chama tawala (CCM) kwa kushawishi na kushauri mamlaka husika kwamba katika nyakazi hizi, vijana wengi hawana Shaka kabisa juu ya NIA ya Mwalimu kuhusiana na Muungano; Shaka yao ipo zaidi katika UTEKELEZAJI wa NIA husika – kwamba Sera serikali mbili kwa mujibu wa CCM ni sera mfu katika nyakati hizi kwani tayari Mwalimu ameshatusaidia kuonyesha wazi kwamba mfumo uliopo una matatizo, kwahiyo haina haja ya kufanya utafiti wa kina kugundua kwamba jinsi tunavyozidi kuelekea kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya muungano mwakani (Apirli 26, 2014), migogoro ya Muungano have overshadowed mafanikio ya Muungano.

Nape, hivi unasahau kwamba wakati wa uhai wake, Mwalimu aliapa kukilinda na kukitetea CCM kwa nguvu na uwezo wake wote, only to change his position baadae ambapo miaka ya mwisho mwisho ya uhai wake alitamka wazi kwamba "CCM sio mama yake, anaweza kuachana nayo"? Nape, sio Nyerere huyu huyu ambae mwaka 1995 alichukizwa sana na Siasa Za CCM kiasi cha kumfanya aamue kumpigia kampeni waziwazi mgombea wa upizani (NCCR) Kanda ya Ziwa? Hoja yangu ya msingi hapa ni kwamba Mwalimu alikuwa ni mtu mwelewa sana, na alianza kubadilisha mtazamo wake kutokana na siasa uchwara za CCM (pamoja na ufisadi), lakini pia alikuwa ni kiongozi aliye heshimu sana nguvu za wanyonge (umma). Ndio maana kwa nyakati mbalimbali, Mwalimu alikuwa anatoa matamshi makali sana kutetea umma kwa kukosoa waziwazi uongozi wa nchi, maneno ambayo kama ingekuwa sio Mwalimu bali mtu mwingine wa kawaida, mtu huyo angeweza kamatwa na kushitakiwa kama mchochezi.

Nape, Mwalimu alikuwa ni kiongozi msikivu sana tofauti na hoja kwamba alikuwa ‘aambiliki'. Mwalimu alikuwa aambiliki pale tu hoja zilizopelekwa kwake zilipokuwa hazina maslahi kwa taifa, hasa wanyonge. Nje ya hapo, wanaomuita mwalimu aambiliki ilikuwa ni wale waliokuwa wanazibiwa miraji ya kufisadi. Iwapo Mwalimu angekuwa aambiliki na hajali matakwa ya umma, asingeweza kutamka haya kwa Mwandishi wa Gazeti la The Observer, la Uingereza, toleo la Aprili 20, 1968:

"Iwapo Umma wa Zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa Muungano una hasara kwa uhai wao, sitowapiga mabomu kuwalazimisha. Muungano utakuwa hauna maana tena sababu ya kuendelea iwapo washiriki wake wataamua kuukana"

Pengine nikuulize:

  • Iwapo wengi wetu vijana, bila ya ushawishi kutoka nje na kwa sababu zetu wenyewe tunaona mfumo wa muuungano wa sasa una hasara kwa uhai wetu, je CCM mtatupiga mabomu kutulazimisha tuukubali?
  • Je, muungano wa kulazimisha utaendelea kuwa na sababu za maana kuendelea hata kama mshiriki mmoja wapo (Tanganyika) tutaamua kuukana kwa sababu hatupewi utambulisho wake?

Nape, vijana wengi tulitarajia utumie busara zaidi katika mjadala kuhusiana na Muungano badala ya kumnukuu Mwalimu kichwa kichwa. Tulitarajia ungekuwa na weledi wa kuelewa kwamba mara nyingine, poison is utilized to fight poison. Hata Mwalimu angekuwa hai leo (mungu amlaze mahali pema peponi), sisi vijana tungetafuta platform ya kumfikia na kumweleza hilo – kwamba POISON can also serve as a CURE; Tungemfafanulia kwa mifano mingi, kwa mfano SUMU inaweza kutumika kama anti-toxin na kwamba this has been a common practice in modern medicine kwa zaidi ya karne moja sasa.

Kwa vile Mwalimu alikuwa ni msikivu sana (tofauti na wengi wasiomjua wanavyo hadithiwa), sisi kama vijana, kwanza, tunaelewa na kukubali kanuni ya Mwongozo wa CCM (1982) kwamba "Kukosoa na Kukosolewa Ndio Silaha Ya Mapinduzi", hivyo viongozi wanapokosolewa, hawatakiwi kuwa na hamaki au kuanza kutafuta visasi. Pili, tungemshukuru Mwalimu - kwamba elimu tuliyopata wakati wa mfumo wa Azimio la Arusha, ndio imetujenga kufikia hatua hii ya kuwa na mapinduzi ya kifikra ambapo sasa tunaweza kuchambua pumba na mchele bila ya uwoga wa status quo. Ni katika mlolongo huu wa elimu dunia, tungemweleza Mwalimu kwamba uwezo wetu vijana wa leo ni matokeo/matunda ya juhudi zake za kutukomboa kifikra, na kwamba elimu hii imetufundisha kwamba – ‘wakati mwingine, mgonjwa anaweza kupimwa, ugonjwa wake ukajulikana, na dawa ya kutumiwa kuokoa maisha ikalazimika iwe ni SUMU'.

Tunajua Mwalimu angefurahi sana na kutusikiliza kwa tabasamu pana – tungeendelea kwa kumpa mifano mingi kama vile jinsi gani biophysicists hutumia Protein from Venom to combat deaths from heart attacks, pia hutumia kutibu aina Fulani za cancer (saratani) n.k. Mwalimu angemaliza kikao nasi vijana kwa kuelewa kwamba in the 21[SUP]st[/SUP] Century, doctors have methods za kupigana na Venom in humans by employing the same Venom as an anti-dote to fight poison. Hakika tunamkosa sana Mwalimu kwani katika suala la muungano, hakika angekaa upande wa walio wengi kwani katika miaka ya mwisho ya uhai wake, alikuwa anakwepa sana kung'ang'ania madhaifu yaliyojitokeza chini ya utawala wake.
Nape, unapoteza fursa ya kukaa on the correct side of our country's history.

Suala la pili na la Mwisho ambalo ningependa kujadili ni kurudia historia ili kuelewa malengo hasa ya Mwalimu yalikuwa ni nini kuhusiana na muungano wetu pamoja na changamoto za wakati ule wa vita baridi vya dunia/Cold War. Historia inatuonyesha kwamba, lengo la Mwalimu kuhusiana na muungano wetu lilikuwa ni muungano wa shirikisho, huku kila taifa likiwa na Serikali yake. Miezi mitatu baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (1964), Mwalimu Nyerere kupitia OAU, alithibitisha haya kwa maneno yake mwenyewe akiwa na hamasa kubwa juu ya federation in Africa kwamba mfumo wa serikali moja au mfumo wa tangamano la majimbo usingefaa katika mazingira ya Kiafrika; Mwalimu Nyerere alitoa waraka mrefu ambao pia ulipatiwa fursa ya kuchapishwa kwenye African Forum, ambapo alisema yafuatayo [Source: Julius K. Nyerere: The nature and requirements of African Unity" Katika African Forum Vol 1, Na. 1 (1965), ukusara 46. Kwa makala yote, soma kurasa 38 – 52]:

"Bara lenye ukubwa wake kamili, moja na lisilogawika, ndilo nataka liwepo; Hii haina maana huku ni kuwa na serikali moja kwa bara lote, katika hali ya kuwa na serikali kuu yenye mamlaka yote; Kinachotakiwa ni kuwa na serikali moja inayounganisha nyingi na kuwa na mamlaka katika maeneo Fulani Fulani; Zaidi ya hapo kunaweza kuwepo na serikali nyenginezo, hizi zikiwa na mamlaka yaliyo hafifu kidogo, na mamlaka hayo yakiwa yanatokana zaidi na katiba za ndani sio kutoka serikali kuu; Hii ni sawa na kusema kuwa afrika mpya inaweza kuwa ni dola ya shirikisho, ambayo nguvu zake zinagawiwa baina ya serikali kuu na serikali za mataifa washiriki kwa mujibu wa matakwa ya waanzilishi na vizazi vijavyo."

Swali linalofuata ni, je kwanini Mwalimu alibadili mtazamo wake juu ya Muungano wetu hasa kupitia Katiba ya JMT (1977)?

Sidhani kama nina majibu yote kwa hili, lakini nina maoni yangu kama ifuatavyo. Mfumo wa Federation (shirikisho), kwa kawaida huwa unahitaji adjustments and adaptations mbalimbali kutokana na competing objectives, lakini muhimu zaidi, kulingana na conflicting objectives; Katika kipindi cha Cold War, Mwalimu alikabiliwa na many competing, but importantly conflicting objectives. Lakini kutokana na umakini wake, nchi haikuingia katika machafuko, na pia he did not profit from politics.

Kwa kawaida, mfumo wa shirikisho una sura mbili kuu: Sura ya kwanza, federalism is an instrument of unity within states, na hili huwa ndio chimbuko la intra-state politics ; Tukiingia kwenye sura ya pili, ni kwamba, federalism is a means by which established states zinajaribu to forge closer relationships between states, na hivyo ndivyo inter-state politics arise. Iwapo tupo pamoja hadi hapa, then sio vigumu kubaini kwanini Mwalimu alikuja geuka kimtazamo baada ya Muungano (1964), hasa ikizingatia kwamba muungano ulikuja katika kipindi ambacho the world offered two alternatives paths to development: Ujamaa/Ukomunisti & Ubepari; Nadhani unaelewa kwamba Muungano wetu ulizaliwa in the womb of cold war politics.

Nimalizie tu kwa kusema kwamba, mabadiliko ya kweli kwa manufaa ya watoto, wajukuu na vitukuu vyetu, yatatokana na kazi ya kizazi cha vijana wa sasa, sio wazee kwani ubunifu wao ndio umegotea hapa tulipo, na huu ni ukweli katika familia, vyama vya siasa na jamii kwa ujumla. Nape, kwa vile wewe tayari upo katika nafasi muhimu na hadimu to influence maamuzi mbalimbali juu ya mustakabali wa taifa letu, huu ni wakati wako sasa wa kuendeleza mazuri ya Mwalimu Nyerere huku na sisi vijana wenzako tukifanya hivyo kupitia njia zetu mbalimbali, kwani ujenzi wa taifa lako sio lazima ufanyike kupitia nafasi ya uongozi. Kama wananchi hawajakupa dhamana ya kuwaongoza, zipo njia mbalimbali za kufanikisha ujenzi wa taifa, na hivyo ndivyo sisi vijana wenzake tunavyofanya sasa kupitia fursa mbalimbali tunazopata ndani ya jamii ya nchi yetu.

Tuungane katika kuendeleza mazuri ya Mwalimu Nyerere huku pia tukiwa wadadisi wa mitazamo na misimamo yake kadhaa, hasa kwa kufahamu kwamba his views were always dynamic, not static kama jinsi unavyotaka tuelewe bandiko juu ya nukuu ya Mwalimu hapo juu kuhusiana na Muungano wetu. Ni dhahiri Mwalimu alikuwa na mapungufu kadhaa kama ilivyo kwa binadamu wengine na alikiri katika hilo. Pia, kupitia njia mbalimbali, tumeona jinsi gani baba wa mataifa mengi duniani (India, Marekani, Afrika ya Kusini n.k), walifanya mengi ya maana na mengi ya kipuuzi kwa mataifa yao, lakini vizazi vilivyokuja baadae vikaja kuendeleza ya maana na kuachana na ya kipuuzi, vinginevyo mataifa hayo yasingekuwa na mafanikio makubwa kama ilivyo sasa. Isitoshe, linapokuja suala la Mwalimu, huwa ni kawaida yangu kusema kwamba njia bora ya kupima achievements za Mwalimu Nyerere ni kwa kuelewa kwamba, achievements zake hazikutokana sana na the Success of his strategies (kwa mfano Muungano na Azimio la Arusha), bali uwezo wake to persuade the donor community na pia population (watanzania) kwamba his objectives were sincere; And indeed, they were very sincere. Kwahiyo, kupitia nafasi zetu mbalimbali ndani ya jamii na kwa kutumia elimu zetu zilizotokanana fedha za walipa kodi, exposure na uzoefu mbalimbali, let us also be sincere with our objectives, hasa kuhusiana na mwananchi wa kijijini ambae ndiye aliyetufikisha sisi wachache hapa tulipo.

Nape, simamia Tanganyika, kwani hata ushujaa wa Mwalimu Nyerere ulianza na Tanganyika, kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuwa on the correct side of our country's history. Natumaini wapambe ndani ya CCM hawataweza kukushawishi otherwise.

Cc Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Jasusi, EMT, AshaDii, JokaKuu, Kobello, Kimbunga, FaizaFoxy, Ritz, zomba, chama, TIMING, JingalaFalsafa ZeMarcopolo, THE BIG SHOW,Barubaru, Zakumi SOBY, Mimibaba, Candid Scope, Mag3, Pasco, Bongolander, [URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=11987"]Ngongo[/URL] et al.
 
CCM kwa kutafuta pakutokea hawajambo! JK Nyerere huyohuyo hakutaka kabisa ubinafshaji wa investments kama benki ya NBC na migodi lakini alipuuzwa! Lakini leo hili la serikali tatu nyerere alisema... ... Mbona mengi tu aliyosema mnakiuka?
 
Hivi karibuni, Katibu Wa Itikadi na Uenezi wa CCM (Taifa), Nape Nnauye, ambae pia ni mdau mwenzetu humu Jamiiforums alikuja na bandiko lenye nukuu ya mwalimu kama ifuatavyo:

Nape, simamia Tanganyika, kwani hata ushujaa wa Mwalimu Nyerere ulianza na Tanganyika, kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuwa on the correct side of our country’s history. Natumaini wapambe ndani ya CCM hawataweza kukushawishi otherwise.

Mkuu mchambuzi naomba ubadili msimamo wako badala yake Nape na Chama chake wasimimie kitu Kikubwa zaidi yaani uundwaji wa;

SERIKALI MOJA YA TANZANIA KAMA KWELI WAKO NA NIA NA DHAMIRA YA KUJIENZI WAO NA NYERERE.

Hii inamaanisha Serikali ya Mapinduzi Zanzibar nayo Ife ilituweze kusonga mbele salama salimi.
 
Nina uhakika 100% Nape hawezi kusoma chote kilichoandikwa na hata akifanikiwa kusoma bado asingeweza kuelewa na hata akielewa hawezi kujibu chochote na kama akijibu kitu basi ni mashudu matupu.

Wasimsingizie Nyerere, kwani Ufisadi, rushwa, udini na utekaji wa watu, Amri za WAPIGWE TU, Wizi wa fedha za EPA, DEEP GREEN, Kuanzisha Mitandao nako waliambiwa na Nyerere? Kuua Azimio la ARUSHA TENA BADO ALIWA HAI, Kuuza mashirika ya UMMA, Kuanzisha Biashara Ikulu, nako Nyerere aliwaambia?
 
Mkuu Mchambuzi
Muungano sio kitu cha kulazimishana hata Mwalimu hakuulazimisha yalikuwepo maongezi ya kiungwana wakakubaliana na Mzee Karume; sasa kama hawa ndugu zetu hawautaki hatuna sababu hata moja ya kulazimishana na kujeangana chuki ambazo hazina maana yoyote; binadamu akitaka lake atapindisha maneno na kusema kile ambacho anakitaka; mimi binafsi kama mtanzania bara sijwahi kunufaika na muungano huu; ila nina waunguja na wapemba wengi wananufaika kimaisha na kielimu kutokana na muungano huu inachukua muda mrefu sana kwa akili zakitumwa kufutika ndani ya ubongo.
 
Last edited by a moderator:
Mabaki ya jikoni yana thamani kuu kwa nguruwe kushinda lulu na vito vya thamani! Mkuu, naona umeamua kutapanya lulu hadi kwenye "mabanda ya nguruwe"; bahati mbaya sana wala hawatakuelewa zaidi ya kugeuka na kuendelea kula vinyesi vyao kwani lulu si mali kitu kwao!

Nakuhakikishia hii thesis uliyoiweka hapa ni wachache mno ndani ya hilo "banda" wenye uthubutu wa kuitolea majibu sembuse huyo uliyemchagua; size yao hao ni mabaki ya jikoni tu - siasa za maji taka na fitna ndicho wanachoweza bahati mbaya sana kwa maangamizi ya taifa.
 
Mkuu Mchambuzi
Muungano sio kitu cha kulazimishana hata Mwalimu hakuulazimisha yalikuwepo maongezi ya kiungwana wakakubaliana na Mzee Karume; sasa kama hawa ndugu zetu hawautaki hatuna sababu hata moja ya kulazimishana na kujeangana chuki ambazo hazina maana yoyote; binadamu akitaka lake atapindisha maneno na kusema kile ambacho anakitaka; mimi binafsi kama mtanzania bara sijwahi kunufaika na muungano huu; ila nina waunguja na wapemba wengi wananufaika kimaisha na kielimu kutokana na muungano huu inachukua muda mrefu sana kwa akili zakitumwa kufutika ndani ya ubongo.
Umesoma msimamo wa chama chako kuhusu serikali tatu na sababu za kitoto walizotoa baada ya kikao cha kamati kuu Dodoma?
Unajua kuwa waliweka hoja kuwa serikali tatu ni mzigo wa gharama , ila walishindwa kuonyesha hizo gharama ni kiasi gani na wanachama wa CCM waliomezeshwa hilo kwenye mabaraza ya katiba wamejikuta wakishindwa kujibu maswali ya kuwataka wafafanue kuhusu hizo gharama na badala yake wanaishia kupandwa na jazba kwa kudhalilika mbele ya wajumbe wengine ambao wanamuono mpana?
Mchambuzi hoja yako ni ya msingi sana, nitaweka andishi moja baadae kuhusiana na umuhimu wa serikali tatu ili kuwez
 
Ule ni msimamo wa viongozi; mimi kama mtanzania sioni haja ya kulazimisha muungano; kama hoja ni kuenzi yaliyoasisiwa na mwalimu yapo mengi sana; kuna kupiga vita umasikini na mradhi; rushwa; kuendeleza siasa ni kilimo sasa sielewi hiki kinachong'ang'niwa kwenye huu muumngano kama wazinzabari wanautaka na uendelee kama hawautaki na ufe kama hoja ya kutembea visiwani tutakwenda Mafia!
 
Hivi karibuni, Katibu Wa Itikadi na Uenezi wa CCM (Taifa), Nape Nnauye, ambae pia ni mdau mwenzetu humu Jamiiforums alikuja na bandiko lenye nukuu ya mwalimu kama ifuatavyo:

Pamoja na umuhimu wa bandiko lako hili, kwa bahati mbaya, haukurudi kusimamia hoja uliyoanzisha. Inawezekana ulibanwa na majukumu ya Chama, lakini mbaya zaidi, haikuchukua muda mrefu kabla ya bandiko husika kuhamishwa na moderators wa Jamiiforums na kupelekwa kwingine, na hivyo fursa yetu vijana kujadiliana hoja hii muhimu kwa maslahi ya taifa, kuyeyuka. Hili ni tatizo kwani mwenendo mzima wa mjadala ulitoa ishara kwamba pengine Nape alikuwa anawasilisha msimamo rasmi wa CCM kuhusiana na mfumo wa muungano chini ya Katiba Mpya. Kama nipo sahihi, basi uamuzi wa CCM wa kutumia nukuu hii ya Mwalimu bila ya kuifanyia upembuzi yakinifu, hasa kwa kutotilia maanani mahitaji na mazingira ya sasa ya nchi, it will be a grave mistake that CCM will live to regret.

Nape, una career ndefu bado ahead of you kwani bado ni kijana, hivyo ni muhimu ukaanza kuchambua mambo kwa mtazamo wa kitaifa zaidi, hasa kwa kulenga mahitaji ya vijana nchini badala ya kuendelea kung'ang'ania mawazo na mitazamo mingine ambayo aidha imepitwa na wakati au haitatui tatizo ina ahirisha na kulea tatizo. Iwapo una amini katika Tanganyika, hata ikitokea kwamba utapewa adhabu na chama kwa msimamo huo, fahamu tu kwamba bado utaheshimika kwa kuchagua the correct side of our country's history. Usidanganywe otherwise.

Nianze moja kwa moja na nukuu yako kutoka kwa Mwalimu Nyerere kwamba:

Ni muhimu ukaelewa kwamba, kabla ya kingine chochote, Mwalimu (miaka 23 iliyopita) anakiri kwamba Muungano una matatizo. Vijana wengi tulitarajia kwamba ungeonyesha uwezo na weledi wako kwa kumuunga mkono Baba wa Taifa kuhusiana na hoja kwamba "muungano wetu unakabiliwa na matatizo". Kitendo chako kumuunga mkono Mwalimu Nyerere, hasa kutokana na nafasi yako ndani ya CCM, would have sent a very positive vibe kwa Vijana wenzako ndani na nje ya CCM ambao kila kukicha, wanazidi kuelewa juu ya umuhimu wa serikali ya Tanganyika. Ni bahati mbaya sana kwamba umepoteza fursa hiyo. Vinginevyo, vijana wengi nje na ndani ya CCM wanazidi kuelewa kwamba Mwalimu alikuwa na NIA nzuri kwa Muungano wetu, tatizo likawa ni UTEKELEZAJI wa NIA husika, hasa kwa kusimamia sera ya CCM ya mfumo wa serikali mbili, ambayo practically, haiwezekani kulinda muungano wetu. Dawa sahihi ya kutibu tatizo ndani ya muungano wetu ni kwa kuirudisha serikali ya Tanganyika, serikali ambayo ilifutwa kwa mujibu wa sheria namba 24, mwaka 1967.

Kuirejesha Tanganyika itakuwa ni dawa kwani hivyo ndivyo hali ya Haki na Usawa miongoni mwa washiriki wa muungano itarejea na kupelekea Tanganyika kutishia kujitoa. Vinginevyo, sababu ya msingi kwanini watanganyika wengi (ukipenda waite watanzania bara) wanaendelee kuona kwamba Zanzibar ni mzigo mkubwa kwa Tanganyika ni kwamba. Kwanza, watanzania wengi hawajui kwamba wazanzibari wanajaribu kufuata kilichokubaliwa chini ya Mkataba wa Muungano (1964). Pili, Katiba ya JMT (1977) inamfanya Rais wa Muungano pia kuwa Rais wa Tanganyika, ingawa Urais wa Tanganyika unafichwa na kiini macho kilichopo ndani ya mfumo wa serikali mbili ambapo Katiba ya JMT (1977) ndio hiyo hiyo inatumika kama Katiba ya Tanganyika, kuendesha mambo ya Tanganyika (Tanzania bara) yasiyo ya muungano. Ndio maana gharama za kuendesha muungano zimekuwa ni kwani Watanganyika (Tanzania bara) wanagharamia kiini macho badala ya reality per articles of the union, 1964.

Nape, tukiendelea kuisoma zaidi nukuu yako ya mwalimu hapo juu, tunaona Mwalimu Nyerere anaendelea kujadili kwamba:

Nape, hapa tunagundua kwamba Mwalimu Nyerere anakiri kwamba Muungano unakabiliwa na matatizo, lakini Mwalimu falls short of mentioning Tanganyika, badala yake anaijadili "Serikali ya tatu" ambayo sote tunajua kwamba it is synonymous to ‘Tanganyika'. Nadhani unafahamu kwamba kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano (1964), serikali zilizohusishwa zilikuwa ni za Tanganyika na Zanzibar, lakini kufuatia Katiba ya JMT (1977), mwaka ambao CCM pia ilishika hatamu baada ya kuungana kwa vyama vya TANU (kutoka Tanganyika) na ASP (kutoka Zanzibar) na kuzaa rasmi CCM February 1977, sera rasmi ya CCM juu ya Muungano imekuwa ni Serikali mbili:

Kwanza ni Serikali ya Zanzibar inayoshughulikia masuala ya Zanzibar yasiyokuwa ya muungano (uvuvi, afya, n.k); Pili ni Serikali ya Muungano inayoshughulikia masuala ya Muungano tu (Ulinzi, Mambo ya Ndani, Mambo ya Nje n.k). Je, masuala ya Tanganyika (au bara) ambayo siyo ya muungano (e.g. Elimu, Afya, Kilimo), haya yanashughulikiwa na Serikali ipi? Jibu ni Serikali ya Muungano, mifano ipo mingi lakini mifano rahisi ni pamoja na kwamba – kwa miaka karibia 50 sasa, it has become common practice kwa Rais wa muungano kuunda idara, taasisi, na wizara mbalimbali ambazo hazina uhusiano na masuala ya muungano, huku Rais huyo huyo pia akiunda idara, taasisi na wizara mbalimbali za kusimamia na kuratibu masuala ya muungano, huku Rais wa Zanzibar yeye akifanya hayo kwa masuala ya zanzibar ambayo yapo nje ya muungano. Kwa maana hii, kwa miaka karibia 50, the practice has been three governments, huku sera rasmi ya CCM (in theoretical and rhetoric terms) ikiendelea kuwa serikali mbili – Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano. Huu ndio mzizi wa tatizo ambalo Nyerere anakiri kwamba limekuwepo huku DAWA ikionekana kuwa ni SUMU.

Swali langu kwako Nape ni Je:

  • Je, hakuna uwezekano wa SUMU kufanya kazi kama DAWA?

Nape, hapa ndipo weledi na umakini wako kama Kiongozi ndio ulihitajika kuwakilisha maoni, matakwa na matarajio ya kizazi cha vijana wenzako kujadili sehemu iliyobakia ya hoja ya Mwalimu Nyerere uliyotuwekea hapo juu kwamba:
"tutafute dawa ya matatizo hayo na dawa haiwezi kuwa serikali tatu, serikali tatu ni sawa na kumpa sumu mgonjwa atakufa tu."

Tulikutarajia uonyeshe weledi na leadership yako kwa niaba yetu sisi vijana wenzako, hasa kutokanana nafasi yako hadimu ndani ya chama tawala (CCM) kwa kushawishi na kushauri mamlaka husika kwamba katika nyakazi hizi, vijana wengi hawana Shaka kabisa juu ya NIA ya Mwalimu kuhusiana na Muungano; Shaka yao ipo zaidi katika UTEKELEZAJI wa NIA husika – kwamba Sera serikali mbili kwa mujibu wa CCM ni sera mfu katika nyakati hizi kwani tayari Mwalimu ameshatusaidia kuonyesha wazi kwamba mfumo uliopo una matatizo, kwahiyo haina haja ya kufanya utafiti wa kina kugundua kwamba jinsi tunavyozidi kuelekea kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya muungano mwakani (Apirli 26, 2014), migogoro ya Muungano have overshadowed mafanikio ya Muungano.

Nape, hivi unasahau kwamba wakati wa uhai wake, Mwalimu aliapa kukilinda na kukitetea CCM kwa nguvu na uwezo wake wote, only to change his position baadae ambapo miaka ya mwisho mwisho ya uhai wake alitamka wazi kwamba "CCM sio mama yake, anaweza kuachana nayo"? Nape, sio Nyerere huyu huyu ambae mwaka 1995 alichukizwa sana na Siasa Za CCM kiasi cha kumfanya aamue kumpigia kampeni waziwazi mgombea wa upizani (NCCR) Kanda ya Ziwa? Hoja yangu ya msingi hapa ni kwamba Mwalimu alikuwa ni mtu mwelewa sana, na alianza kubadilisha mtazamo wake kutokana na siasa uchwara za CCM (pamoja na ufisadi), lakini pia alikuwa ni kiongozi aliye heshimu sana nguvu za wanyonge (umma). Ndio maana kwa nyakati mbalimbali, Mwalimu alikuwa anatoa matamshi makali sana kutetea umma kwa kukosoa waziwazi uongozi wa nchi, maneno ambayo kama ingekuwa sio Mwalimu bali mtu mwingine wa kawaida, mtu huyo angeweza kamatwa na kushitakiwa kama mchochezi.

Nape, Mwalimu alikuwa ni kiongozi msikivu sana tofauti na hoja kwamba alikuwa ‘aambiliki'. Mwalimu alikuwa aambiliki pale tu hoja zilizopelekwa kwake zilipokuwa hazina maslahi kwa taifa, hasa wanyonge. Nje ya hapo, wanaomuita mwalimu aambiliki ilikuwa ni wale waliokuwa wanazibiwa miraji ya kufisadi. Iwapo Mwalimu angekuwa aambiliki na hajali matakwa ya umma, asingeweza kutamka haya kwa Mwandishi wa Gazeti la The Observer, la Uingereza, toleo la Aprili 20, 1968:

"Iwapo Umma wa Zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa Muungano una hasara kwa uhai wao, sitowapiga mabomu kuwalazimisha. Muungano utakuwa hauna maana tena sababu ya kuendelea iwapo washiriki wake wataamua kuukana"

Pengine nikuulize:

  • Iwapo wengi wetu vijana, bila ya ushawishi kutoka nje na kwa sababu zetu wenyewe tunaona mfumo wa muuungano wa sasa una hasara kwa uhai wetu, je CCM mtatupiga mabomu kutulazimisha tuukubali?
  • Je, muungano wa kulazimisha utaendelea kuwa na sababu za maana kuendelea hata kama mshiriki mmoja wapo (Tanganyika) tutaamua kuukana kwa sababu hatupewi utambulisho wake?

Nape, vijana wengi tulitarajia utumie busara zaidi katika mjadala kuhusiana na Muungano badala ya kumnukuu Mwalimu kichwa kichwa. Tulitarajia ungekuwa na weledi wa kuelewa kwamba mara nyingine, poison is utilized to fight poison. Hata Mwalimu angekuwa hai leo (mungu amlaze mahali pema peponi), sisi vijana tungetafuta platform ya kumfikia na kumweleza hilo – kwamba POISON can also serve as a CURE; Tungemfafanulia kwa mifano mingi, kwa mfano SUMU inaweza kutumika kama anti-toxin na kwamba this has been a common practice in modern medicine kwa zaidi ya karne moja sasa.

Kwa vile Mwalimu alikuwa ni msikivu sana (tofauti na wengi wasiomjua wanavyo hadithiwa), sisi kama vijana, kwanza, tunaelewa na kukubali kanuni ya Mwongozo wa CCM (1982) kwamba "Kukosoa na Kukosolewa Ndio Silaha Ya Mapinduzi", hivyo viongozi wanapokosolewa, hawatakiwa kuwa na hamaki au kuanza kutafuta visasi. Pili, tungemshukuru Mwalimu - kwamba elimu tuliyopata wakati wa mfumo wa Azimio la Arusha, ndio imetujenga kufikia hatua hii y akuwa na mapinduzi ya kifikra ambapo tunaweza kuchambua pumba na mchele bila ya uwoga wa status quo. Ni katika mlolongo huu wa elimu dunia, tungemweleza Mwalimu tumejifunza ni matokeo/matunda ya juhudi zake za kutokomboa kifikra, na kwamba elimu hii imetufundisha kwamba – ‘wakati mwingine, mgonjwa anaweza kupimwa, ugonjwa wake ukajulikana, na dawa ya kutumiwa kuokoa maisha ikalazimika iwe ni SUMU'.

Tunajua Mwalimu angefurahi sana na kutusikiliza kwa tabasamu pana – tungeendelea kwa kumpa mifano mingi kama vile jinsi gani biophysicists hutumia Protein from Venom to combat deaths from heart attacks, pia hutumia kutibu aina Fulani za cancer (saratani) n.k. Mwalimu angemaliza kikasi nasi kwa kuelewa kwamba in the 21[SUP]st[/SUP] Century, doctors have methods za kupigana na Venom in humans by employing the same Venom as an anti-dote using to fight poison. Hakika tunamkosa sana Mwalimu kwani katika suala la muungano, hakika angekaa upande wa walio wengi kwani katika miaka ya mwisho ya uhai wake, alikuwa anakwepa sana kung'ang'ania madhaifu yaliyojitokeza chini ya utawala wake.
Nape, unapoteza fursa ya kukaa on the correct side of our country's history.

Suala la pili na la Mwisho ambalo ningependa kujadili ni kurudia historia ili kuelewa malengo hasa ya Mwalimu yalikuwa ni nini kuhusiana na muungano wetu pamoja na changamoto za wakati ule wa vita baridi vya dunia/Cold War. Historia inatuonyesha kwamba, lengo la Mwalimu kuhusiana na muungano wetu lilikuwa ni muungano wa shirikisho, huku kila taifa likiwa na Serikali yake. Miezi mitatu baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (1964), Mwalimu Nyerere kupitia OAU, alithibitisha haya kwa maneno yake mwenyewe akiwa na hamasa kubwa juu ya federation in Africa kwamba mfumo wa serikali moja au mfumo wa tangamano la majimbo usingefaa katika mazingira ya Kiafrika; Mwalimu Nyerere alitoa waraka mrefu ambao pia ulipatiwa fursa ya kuchapishwa kwenye African Forum, ambapo alisema yafuatayo [Source: Julius K. Nyerere: The nature and requirements of African Unity" Katika African Forum Vol 1, Na. 1 (1965), ukusara 46. Kwa makala yote, soma kurasa 38 – 52]:

"Bara lenye ukubwa wake kamili, moja na lisilogawika, ndilo nataka liwepo; Hii haina maana huku ni kuwa na serikali moja kwa bara lote, katika hali ya kuwa na serikali kuu yenye mamlaka yote; Kinachotakiwa ni kuwa na serikali moja inayounganisha nyingi na kuwa na mamlaka katika maeneo Fulani Fulani; Zaidi ya hapo kunaweza kuwepo na serikali nyenginezo, hizi zikiwa na mamlaka yaliyo hafifu kidogo, na mamlaka hayo yakiwa yanatokana zaidi na katiba za ndani sio kutoka serikali kuu; Hii ni sawa na kusema kuwa afrika mpya inaweza kuwa ni dola ya shirikisho, ambayo nguvu zake zinagawiwa baina ya serikali kuu na serikali za mataifa washiriki kwa mujibu wa matakwa ya waanzilishi na vizazi vijavyo."

Swali linalofuata ni, je kwanini Mwalimu alibadili mtazamo wake juu ya Muungano wetu hasa kupitia Katiba ya JMT (1977)?

Sidhani kama nina majibu yote kwa hili, lakini nina maoni yangu kama ifuatavyo. Mfumo wa Federation (shirikisho), kwa kawaida huwa unahitaji adjustments and adaptations mbalimbali kutokana na competing objectives, lakini muhimu zaidi, kulingana na conflicting objectives; Katika kipindi cha Cold War, Mwalimu alikabiliwa na many competing, but importantly conflicting objectives. Lakini kutokana na umakini wake, nchi haikuingia katika machafuko, na pia he did not profit from politics.

Kwa kawaida, mfumo wa shirikisho una sura mbili kuu: Sura ya kwanza, federalism is an instrument of unity within states, na hili huwa ndio chimbuko la intra-state politics ; Tukiingia kwenye sura ya pili, ni kwamba, federalism is a means by which established states zinajaribu to forge closer relationships between states, na hivyo ndivyo inter-state politics arise. Iwapo tupo pamoja hadi hapa, then sio vigumu kubaini kwanini Mwalimu alikuja geuka kimtazamo baada ya Muungano (1964), hasa ikizingatia kwamba muungano ulikuja katika kipindi ambacho the world offered two alternatives paths to development: Ujamaa/Ukomunisti & Ubepari; Nadhani unaelewa kwamba Muungano wetu ulizaliwa in the womb of cold war politics.

Nimalizie tu kwa kusema kwamba, mabadiliko ya kweli kwa manufaa ya watoto, wajukuu na vitukuu vyetu, yatatokana na kazi ya kizazi cha vijana wa sasa, sio wazee kwani ubunifu wao ndio umegotea hapa tulipo, na huu ni ukweli katika familia, vyama vya siasa na jamii kwa ujumla. Nape, kwa vile wewe tayari upo katika nafasi muhimu na hadimu to influence maamuzi mbalimbali juu ya mustakabali wa taifa letu, huu ni wakati wako sasa wa kuendeleza mazuri ya Mwalimu Nyerere huku na sisi vijana wenzako tukifanya hivyo kupitia njia zetu mbalimbali, kwani ujenzi wa taifa lako sio lazima ufanyike kupitia nafasi ya uongozi. Kama wananchi hawajakupa dhamana ya kuwaongoza, zipo njia mbalimbali za kufanikisha ujenzi wa taifa, na hivyo ndivyo sisi vijana wenzake tunavyofanya sasa kupitia fursa mbalimbali tunazopata ndani ya jamii ya nchi yetu.

Tuungane katika kuendeleza mazuri ya Mwalimu Nyerere huku pia tukiwa wadadisi wa mitazamo na misimamo yake kadhaa, hasa kwa kufahamu kwamba his views were always dynamic, not static kama jinsi unavyotaka tuelewe bandiko juu ya nukuu ya Mwalimu hapo juu kuhusiana na Muungano wetu. Ni dhahiri Mwalimu alikuwa na mapungufu kadhaa kama ilivyo kwa binadamu wengine na alikiri katika hilo. Pia, kupitia njia mbalimbali, tumeona jinsi gani baba wa mataifa mengi duniani (India, Marekani, Afrika ya Kusini n.k), walifanya mengi ya maana na mengi ya kipuuzi kwa mataifa yao, lakini vizazi vilivyokuja baadae vikaja kuendeleza ya maana na kuachana na ya kipuuzi, vinginevyo mataifa hayo yasingekuwa na mafanikio makubwa kama ilivyo sasa. Isitoshe, linapokuja suala la Mwalimu, huwa ni kawaida yangu kusema kwamba njia bora ya kupima achievements za Mwalimu Nyerere ni kwa kuelewa kwamba, achievements zake hazikutokana sana na the Success of his strategies (kwa mfano Muungano na Azimio la Arusha), bali uwezo wake to persuade the donor community na pia population (watanzania) kwamba his objectives were sincere; And indeed, they were very sincere. Kwahiyo, kupitia nafasi zetu mbalimbali ndani ya jamii na kwa kutumia elimu zetu zilizotokanana fedha za walipa kodi, exposure na uzoefu mbalimbali, let us also be sincere too with our objectives, hasa kuhusiana na mwananchi wa kijijini ambae ndiye aliyetufikisha sisi wachache hapa tulipo.

Nape, simamia Tanganyika, kwani hata ushujaa wa Mwalimu Nyerere ulianza na Tanganyika, kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuwa on the correct side of our country's history. Natumaini wapambe ndani ya CCM hawataweza kukushawishi otherwise.

Cc Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Jasusi, EMT, AshaDii, JokaKuu, Kobello, Kimbunga, FaizaFoxy, Ritz, zomba, chama, TIMING, JingalaFalsafa ZeMarcopolo, THE BIG SHOW,Barubaru, Zakumi SOBY, Mimibaba, Candid Scope, Mag3, Pasco, [URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=13571"]Bongo[/URL]lader, [B][URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=11987"]Ngongo[/URL] et al.[/B]

Huyu jamaa (Mnauye) anafikiri kukifold kitu katika himaya yako ndio maendeleo na ndio maana anapigania kujitowa muhanga kwa Tanganyika ili Zanzibar iwe kwenye mamlaka ya Tanganyika. Ni leo tu eti anauliza Watanganyika wanakosa nini kwa kutokuwepo kwenye Muungano. Ni fikira za kitoto sana hizi kwani kama Muungano una nia ya kuleta maendeleo si itakuwa jambo la maana kuwa kila nchi (Zanzibar na Tanganyika) zijitegemee ili kuleta maendeleo yatakayoleta uimara wa serikali ya Muungano?
 
CCM kwa kutafuta pakutokea hawajambo! JK Nyerere huyohuyo hakutaka kabisa ubinafshaji wa investments kama benki ya NBC na migodi lakini alipuuzwa! Lakini leo hili la serikali tatu nyerere alisema... ... Mbona mengi tu aliyosema mnakiuka?

Mzee wa watu walimuuwa kihoro kwa kumvunjia Azimoi la Arusha, leo wanajidai!
 
Mkuu Mchambuzi
Muungano sio kitu cha kulazimishana hata Mwalimu hakuulazimisha yalikuwepo maongezi ya kiungwana wakakubaliana na Mzee Karume; sasa kama hawa ndugu zetu hawautaki hatuna sababu hata moja ya kulazimishana na kujeangana chuki ambazo hazina maana yoyote; binadamu akitaka lake atapindisha maneno na kusema kile ambacho anakitaka; mimi binafsi kama mtanzania bara sijwahi kunufaika na muungano huu; ila nina waunguja na wapemba wengi wananufaika kimaisha na kielimu kutokana na muungano huu inachukua muda mrefu sana kwa akili zakitumwa kufutika ndani ya ubongo.
Sijui kwako manufaa ni kitu cha namna gani lakini kwa namna moja au nyengine wewe Mtanzania Bara na mimi Mzanzibari tuko sawa katika suwala la kunufaika au la!
Hivyo kwa fikira zako yule mfungwa gerezani anaepewa chakula na magereza utasema anafaidika eti kwa kuwa anapewa bure? Pengine analazimishwa tu kukubali aina ya chakula na pengine angekuwa kwake angepata chakula bora kwa kutumia jasho lake. Fikira mfano huo na Wazanzibari wanavyolazimika kuvumilia kwa kukosa uhuru wa kujiamilia mambo yao.
Njoo upande wa pili na ufikiri pale unapompa makazi mgeni na mgeni huyo akawa mbunifu wa kuendeleza hiyo sehemu uliyompa pengine alijenga njia ambayo unapitisha gari yako kwenda nyumbani kwako, huhisi kuwa unanufaika kuwepo kwake yule alieijenga barabara?

Narejea tena kuwa manufaa ya muungano hayataonekana mpaka kila mmoja atakaporidhika kuwa anatowa nguvu zake kwa hiari yake kuuendeleza huo muungano na sio hali ya sasa isiyoeleweka!
 
Ule ni msimamo wa viongozi; mimi kama mtanzania sioni haja ya kulazimisha muungano; kama hoja ni kuenzi yaliyoasisiwa na mwalimu yapo mengi sana; kuna kupiga vita umasikini na mradhi; rushwa; kuendeleza siasa ni kilimo sasa sielewi hiki kinachong'ang'niwa kwenye huu muumngano kama wazinzabari wanautaka na uendelee kama hawautaki na ufe kama hoja ya kutembea visiwani tutakwenda Mafia!
Chama, mbona unakosa kuwa na busara kiasi cha kutufanya tuhisi kuwa wewe ni sawa na hao viongozi wako? Unakubali kuwa muungano ni hiyari lakini unafutuka na kutowa laana kwa Wazanzibari ambao wana hiari? Tufahamu kuwa wewe utautaka huo muungano iwapo wazanzibari watautaka? Naam wazanzibari wanautaka lakini uwe kwa makubaliano isiwe kama hapo mwanzo kuwa ni wa kiholeleholela, sasa nini msimamo wako? Nape anasema muundo uwe huuhuu hivyo usipokubaliana nae usiwalaani Wazanzibari bure!
 
Mp Kalix2 said:
Mkuu mchambuzi naomba ubadili msimamo wako badala yake Nape na Chama chake wasimimie kitu Kikubwa zaidi yaani uundwaji wa;

SERIKALI MOJA YA TANZANIA KAMA KWELI WAKO NA NIA NA DHAMIRA YA KUJIENZI WAO NA NYERERE.

Hii inamaanisha Serikali ya Mapinduzi Zanzibar nayo Ife ilituweze kusonga mbele salama salimi .
Njelu Kasaka: Tanganyika lazima

Mwanasiasa aliyewika katika hoja ya ‘kuzaliwa Tanganyika, Njelu Kasaka, amesema Uchaguzi Mkuu wa 2015 haupaswi kuchochea kukamilika kwa Katiba mpya ya Tanzania, huku akisisitiza umuhimu wa kuwapo serikali ya Tanganyika.

Alisema Watanzania wanahitaji muda wa kutosha kwa maandalizi ya Katiba Mpya ya Tanzania na zile za Tanganyika na Zanzibar zinazokidhi matakwa ya Muungano, ikiwa mfumo wa serikali tatu utapitishwa.

ASISITIZA HITAJI LA SERIKALI YA TANGANYIKA

Kasaka alisema kwa hali ilivyo, anaamini hakuna kinachoweza kupinga kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika na kuwapo Katiba yake chini ya serikali na Katiba ya ya Shirikisho.

"Hitaji la muundo wa serikali tatu lipo pale pale kwa vile utaratibu wa sasa wa serikali mbili haukubaliki," alisema.

Kwa mujibu wa Kasaka, hivi sasa ni muda muafaka wa kujadili na kuandaa Katiba Mpya kwa ajili ya kubainisha na kuainisha majukumu ya serikali za Zanzibar, Tanganyika na Shirikisho.

Zaidi bofya hapa Home
 
Sijui kwako manufaa ni kitu cha namna gani lakini kwa namna moja au nyengine wewe Mtanzania Bara na mimi Mzanzibari tuko sawa katika suwala la kunufaika au la!
Hivyo kwa fikira zako yule mfungwa gerezani anaepewa chakula na magereza utasema anafaidika eti kwa kuwa anapewa bure? Pengine analazimishwa tu kukubali aina ya chakula na pengine angekuwa kwake angepata chakula bora kwa kutumia jasho lake. Fikira mfano huo na Wazanzibari wanavyolazimika kuvumilia kwa kukosa uhuru wa kujiamilia mambo yao.
Njoo upande wa pili na ufikiri pale unapompa makazi mgeni na mgeni huyo akawa mbunifu wa kuendeleza hiyo sehemu uliyompa pengine alijenga njia ambayo unapitisha gari yako kwenda nyumbani kwako, huhisi kuwa unanufaika kuwepo kwake yule alieijenga barabara?

Narejea tena kuwa manufaa ya muungano hayataonekana mpaka kila mmoja atakaporidhika kuwa anatowa nguvu zake kwa hiari yake kuuendeleza huo muungano na sio hali ya sasa isiyoeleweka!

Acheni kuzunguka mbuyu mtanzania bara wa Manyoni ananufaika nini muungano huu? mimi sijawahi hata siku moja kuona hata chembe ya manufaa ya muungano huu kama hoja ni usalama wa taifa tutafuta njia mbadala za kukabiliana na hujuma zozote dhidi ya taifa hili; nyie kama mnataka aamueni muachane na muungano huu; uhuru wenu unatuumiza sisi nyie mzigo kwetu na sisi tunawavumilia kwasababu tumekuwa kama ndugu; nyie watu mna roho mbaya na ubinafsi siku mlipopata fununu ya mafuta kwenye pwani ya Zanzibar mlichokimbilia kusema mafuta hayamo kwenye muungano mkasahau kabisa kuwa Zanzibar baada ya karafuu kuanguka bei ililishwa sana na almasi na dhahabu; pamba na mkonge za Tanzania bara; muungano huu utakuwa na heri kama mtaacha ubinafsi wenu; Tanzania bara ina rasilimali nyingi sana za kuweza kujimudu kiuchumi!
 
Chama, mbona unakosa kuwa na busara kiasi cha kutufanya tuhisi kuwa wewe ni sawa na hao viongozi wako? Unakubali kuwa muungano ni hiyari lakini unafutuka na kutowa laana kwa Wazanzibari ambao wana hiari? Tufahamu kuwa wewe utautaka huo muungano iwapo wazanzibari watautaka? Naam wazanzibari wanautaka lakini uwe kwa makubaliano isiwe kama hapo mwanzo kuwa ni wa kiholeleholela, sasa nini msimamo wako? Nape anasema muundo uwe huuhuu hivyo usipokubaliana nae usiwalaani Wazanzibari bure!

Busara ninazo nyingi na ndio maana hatuna haja ya kulazamisha kama kulikuwa na sababu za kuwepo muungano huu na nyie wazanzibar mmeziona hazipo na ufe tena kifo cha mende! tumechoka na hizi kelele zenu nyie ndio mmekuwa wanufaika wakubwa wa muungano lakini hamuishi kulialia labda ni kuulize bara tunanufaika na kitu gani kutoka Zanzibar? Leo hii hujui maana ya manufaa? unataka nalo nikufundishe?
 
Acheni kuzunguka mbuyu mtanzania bara wa Manyoni ananufaika nini muungano huu? mimi sijawahi hata siku moja kuona hata chembe ya manufaa ya muungano huu kama hoja ni usalama wa taifa tutafuta njia mbadala za kukabiliana na hujuma zozote dhidi ya taifa hili; nyie kama mnataka aamueni muachane na muungano huu; uhuru wenu unatuumiza sisi nyie mzigo kwetu na sisi tunawavumilia kwasababu tumekuwa kama ndugu; nyie watu mna roho mbaya na ubinafsi siku mlipopata fununu ya mafuta kwenye pwani ya Zanzibar mlichokimbilia kusema mafuta hayamo kwenye muungano mkasahau kabisa kuwa Zanzibar baada ya karafuu kuanguka bei ililishwa sana na almasi na dhahabu; pamba na mkonge za Tanzania bara; muungano huu utakuwa na heri kama mtaacha ubinafsi wenu; Tanzania bara ina rasilimali nyingi sana za kuweza kujimudu kiuchumi!

Sasa kama mna rasilimali nyingi mbona ombaomba?hii si karne ya maguvu mkuu na wala usitokwe na mapovu kwa wazbr kudai haki yao,tumia nguvu zako kuurejesha uhuru wa mtanganyika.
 
Haki yako unaidai vipi? wewe kama unaona haki yako imechukuliwa unachotakiwa kuifanya ni kuichukua tu iwe kwa nguvu au amani; watanzania bara tulishakuwa huru siku nyingi ulishawahi kumsikia mbara akidai uhuru? na uhuru huo tuudai kutoka kwa nani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom