Nape, Simamia Tanganyika na Vijana Wenzako

Nape, Simamia Tanganyika na Vijana Wenzako

Mkuu wangu Mchambuzi huyu kada wa CCM Nape Nnauye kazi aliyopewa Secretary for Ideology & Publicity ni kubwa sana.Nafasi hii ilihitaji mwanaCCM anayekijua chama chake nje ndani,mwanaCCM mwenye ujuzi na uwezo wa kuchambua siasa,uchumi na masuala ya kijamii kwa ujumla.

Ni bahati mbaya CCM ya Kikwete imeidharau nafasi hii muhimu na nyeti sana katika duru za siasa za sasa ambazo zimejikita katika ushindani wa hoja badala yake tunashuhudia chama kikijikita zaidi katika kuomba usaidizi wa vyombo vya dola.

Kazi ya Nape inakuwa ngumu zaidi kwasababu pia CCM imejiondoa rasmi kama chama cha wakulima na wafanyakazi.Chama kimekosa dira kimebaki kuwa chama cha wafanyabiashara na waporaji wa rasilimali za taifa (gesi,dhahabu....)Nape akikisema chama ni lazima awasemee kundi hilo kundi lazima ataonekana kichekesho.
 
Safi sana. Tatizo ni uliye mwandikia kama ataelewa. Tatizo la Nape ni kutaka kupingana na upepo.
 
Mkuu wangu Mchambuzi huyu kada wa CCM Nape Nnauye kazi aliyopewa Secretary for Ideology & Publicity ni kubwa sana.Nafasi hii ilihitaji mwanaCCM anayekijua chama chake nje ndani,mwanaCCM mwenye ujuzi na uwezo wa kuchambua siasa,uchumi na masuala ya kijamii kwa ujumla.

Ni bahati mbaya CCM ya Kikwete imeidharau nafasi hii muhimu na nyeti sana katika duru za siasa za sasa ambazo zimejikita katika ushindani wa hoja badala yake tunashuhudia chama kikijikita zaidi katika kuomba usaidizi wa vyombo vya dola.

Kazi ya Nape inakuwa ngumu zaidi kwasababu pia CCM imejiondoa rasmi kama chama cha wakulima na wafanyakazi.Chama kimekosa dira kimebaki kuwa chama cha wafanyabiashara na waporaji wa rasilimali za taifa (gesi,dhahabu....)Nape akikisema chama ni lazima awasemee kundi hilo kundi lazima ataonekana kichekesho.

Well spoken MKuu. Huyu kijana(huenda sio kijana) hiyo nafasi inampwaya sana. Hana hoja za kukitetea chama na inaonesha hajui sera wala ilani ya chama chake ndio maana amekuwa kama katibu mwenezi wa CHADEMA. Anachojua kutamka mdomoni mwake ni CHADEMA, Slaa, udini, ukabila na ukanda. Basi! Tathmini yangu ni kuwa uwezo wa Nape ndio unareflect uwezo wa mwenyekiti vinginevyo Nape na Mwigulu wasingeachwa kuififisha CCM. Huyo nafasi ambayo ingemfaa ni kuwa tarishi hapo Lumumba au dereva wa katibu mwenezi wa chama!
 
Ni kweli kama Kikwete alitaka kuwanyanyua vijana bila kuangalia uwezo basi Nape & Mwigulu ni level ya wilaya ujinga wao hauwezi kukiumiza chama kama inavyoonekana sasa.

Well spoken MKuu. Huyu kijana(huenda sio kijana) hiyo nafasi inampwaya sana. Hana hoja za kukitetea chama na inaonesha hajui sera wala ilani ya chama chake ndio maana amekuwa kama katibu mwenezi wa CHADEMA. Anachojua kutamka mdomoni mwake ni CHADEMA, Slaa, udini, ukabila na ukanda. Basi! Tathmini yangu ni kuwa uwezo wa Nape ndio unareflect uwezo wa mwenyekiti vinginevyo Nape na Mwigulu wasingeachwa kuififisha CCM. Huyo nafasi ambayo ingemfaa ni kuwa tarishi hapo Lumumba au dereva wa katibu mwenezi wa chama!
 
Kwenye Bandiko Namba 42 hapo juu, nimewasilisha taarifa kutoka Gazeti la RAIA MWEMA toleo la (Agosti 31, 2013), lenye kichwa cha habari katika kurasa yake ya mbele kwamba:

"Takwimu za TRA Zaipinga CCM Kuhusu Serikali Tatu."

Pamoja na mjadala huo ambao unadhihirisha jinsi gani Nape Nnauye anavyopotosha umma kuhusiana na mfumo wa serikali tatu na gharama kwa walipa kodi, Nape hajarudi humu kupangua hoja. Nape hana ulazima wa kuja katika uzi huu, lakini kwa vile ni jadi yake kuanzisha nyuzi mbalimbali kila mara anapotaka kutoa ufafanuzi juu ya nukuu juu yake kwenye magazeti mbalimbali, Nape alikuwa na fursa ya kufanya hivyo katika suala hili la RAIA MWEMA kwani gazeti hili limemtaja kwa jina na cheo chake kwamba ‘analalamikia mapendekezo ya mfumo wa shirikisho la serikali tatu kwamba utaongeza gharama za uendeshaji wa serikali ya JMT'; Nape Nnauye, upo wapi kuthibitisha au kukanusha taarifa hizi?

Nukuu kamili juu ya Nape kwenye gazeti la RAIA MWEMA, la Agosti, 13, 2013, ukurusa wa mbele, ni kama ifuatavyo:

"Katibu wa CCM wa itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amenukuliwa na vyombo vya habari mwishoni mwa wiki akilalamika urasimu na ongezeko la gharama utakaosababishwa na muundao wa serikali tatu"[/quote]

Hoja kuhusu GHARAMA chini ya muundo wa Seritaki Tatu tumejeshalijadili kwenye bandiko #42 , na tunasubiri majibu kutoka Nape Nnauye; Ningependa kuadili hoja nyingine ya Nape Nnauye kuhusiana na muundo wa Serikali Tatu na URASIMU;

Swali muhimu kwa Nape ni kwamba, je:

· Baina ya Muungano wa Serikali Moja, Serikali mbili au Mfumo wa Shirikisho la Serikali Tatu, mfumo upi offers/promotes more/better social, economic and political outcomes kwa watanzania?

Kwa nafasi yake, hili ndio ilitakiwa iwe hoja yake ya msingi katika kushawishi umma badala ya kufanya kazi za copy and paste nukuu za Mwalimu bila ya kuzichambua;

Muungano wa mwaka 1964 ulidhamiria uwepo wa a federal constitutional arrangement na hili suala tumeshalijadili kwa kirefu; Badala yake, baada tu ya muungano kusainiwa, TANU ikaiteka agenda ya federation per articles of the union (1964) na kuigeuza into a unitary agenda; Kwa wale ambao hawaelewi sana tofauti baina ya unitary na federation systems of governance:

Kwa mujibu wa wikipedia:

"A Unitary government is a state governed as one single unit in which the central government is supreme and any administrative divisions exercise only powers that their central government chooses to delegate";

Kwa upande mwingine:

"A political entity characterized by a union of partially self-governing states or regions united by a central (federal) government. In a federation, the self – governing status of the component states, as well as the division of power between them and the central government, are typically constitutionally entrenched and may not be altered by a unilateral decision by the states";

Sidhani kama kuna haja sana ya kuchambua tofauti hizi kwani zipo wazi; Ukizisoma kwa umakini, ni rahisi kubaini kwamba mfumo wa muungano wetu ni mfumo usiotufaa kwani kwa mfano, ni Zanzibar peke yake ndio yenye haki to partially self govern its self wakati Tanganyika haijapewa haki hii; Vinginevyo, a unitary system of governance is common katika mataifa mengi ambayo hayajaingia katika mikataba wa ushirikiano au muungano wa aina yoyote with other sovereign states; Lakini pale one sovereign state inapoingia katika mkataba wa muungano with another sovereign state, a federation has always been the ordr of the day kwani hivyo ndivyo ufanisi kwa pande zote hujitokeza – kisiasa, kiuchumi na kijamii; Ndio maana Mkataba wa Muungano (1964)ulilenga mfumo wa namna hii, na baada ya miaka 50 ya uchakachuaji wa Mkataba wa Muungano (1964), ndio maana Tume ya Warioba inapendekeza mfumo wa shirikisho, huku Nape akinukuliwa kusema kwamba CCM itaulinda mfumo wa kikandamizaji mpaka ‘mwisho wa dunia';

Kwanza, ni muhimu Nape aelewe kwamba hakuna mahali popote duniani ambapo kuna democracy iliyoingia katika muungano na taifa lingine na kufanikiwa to move from Constitutional status of a federation to a status of a Unitary; Badala yake, ukweli umekuwa kinyume chake i.e. transition from a unitary to a federation constitutional status; Nape Nnauye - Kwanini CCM is trying to reinvent the wheel? At what costs? For whose benefits? How are the benefits justified?

Pili, Nape aelewe kwamba Demokrasia zote kubwa duniani (akiamua azitazame kwa ukubwa wa by population or ukubwa wa land size), kwa sasa zote ni FEDEDARAL (Constitutionally);

Tatu, Nape atambue kwamba karibia robo tatu ya raia wanaoishi katika demokrasia ya uliberali yenye vyama vingi (duniani kwa ujumla ) wanaishi under Federal Polities;

Hizi ni political facts ambazo tulitegemea Nape kwa nafasi yake angekuwa anakuja kuzijadili kwa hoja pale msimamo wa CCM unapokuwa challenge, badala yaku ‘copy and paste' nukuu za Mwalimu Nyerere, kisha kukimbia mijadala;

Nape, kama ulikuwa hauna ufahamu, dunia nzima inapigania decentralization and democracy, hand in hand, kwani hivi haviachani hata siku moja katika karne hii ya ishirini na moja; Vile vile, utambue kwamba Decentralization and Good Governance hand in glove; Inastaajabisha jinsi gani CCM imekuwa imekuwa ikijivunia kutekeleza dhana ya Utawala Bora (good governance) huku ikiacha kuheshimu demokrasia na decentralization as a ‘pair'; CCM haiwezi kuwa na moral authority to state kwamba chama kinatekeleza dhana ya utawala bora ikiwa chama hicho hicho kitatoa matamshi kupitia Nape kwamba itapigania mpaka mwisho wa dunia a unitary constitutional arrangement ambayo inapingana moja kwa moja na dhana nzima ya decentralization and good governance katika mazingira ya muungano; Moral authority hiyo ingekuja iwapo tu CCM ingekuwa inaunga mkono a federation constitutional arrangement; not a unitary constitutional arrangement;

Nape, tukirudi nyuma kidogo katika historia ya dunia, tunaona kwamba kufikia miaka ya sitini (1960s), kulikuwa na three models of development that were dominant across the third world ya wakati ule (Tanganyika, South Korea, n.k):

1) Socialism
2) Export oriented industrialization
3) Import Substitution

What was common in all the three models was that – they featured a leading role of the state (serikali) katika uchumi; Miradi mikubwa ya kiuchumi ilianzishwa chini ya central direction (of the state), na miradi yote ya namna hii paved way for economic and social development in third world countries, including Tanzania (kwa mfano ujenzi wa ujamaa na kujitegemea); Tukichukulia taifa kama la South Korea, hili ni taifa linalofuata a unitary system of governance, na waliweza utilize unitary system of governance to promote better economic, social and political outcomes kwa vile hawakupitia mazingira to combine efforts za two sovereign and independent states kama ilivyokuwa kwa Tanganyika na Zanzibar, 1964, ambapo ndani ya miaka mitatu ya uhuru wa dola hizi mbili (uhuru wa miezi mitatu kwa Zanzibar na uhuru wa miaka kama miwili na nusu kwa Tanganyika), dola hizi huru ziliungana na kuzalisha JMT (1964); Lakini badala ya kufuata makubaliano ya muungano (shirikisho la serikali tatu), JMT ikaingizwa katika unitary system; Vinginevyo kuna kila ushahidi kwamba iwapo TANU/CCM ingeamua kufuata Mkataba wa muungano (mfumo wa serikali tatu), leo hii Tanganyika ingekuwa mbali sana kiuchumi ( and I believe Zanzibar pia);

Kinachotugharimu watanganyika ni mfumo kiini macho kama nilivyojadili kwenye bandiko namba moja ambapo matrilino ya walipa kodi yanapotea kila mwaka, huku CCM ikiendelea kutojali kurekebisha kasoro hii, licha ya mapendekezo ya tume ya Warioba; Mwalimu Nyerere alituonya sana kutotumia usisi na uwao linapokuja suala la Tanganyika na Zanzibar kwani tutamalizana; Pamoja na ukweli huu, ukweli mkubwa zaidi unabakia wazi kwamba umimi na uwao ni muhimu sana katika kujenga self determination and democracy ndani ya pande husika, kwani hivyo ndivyo muungano (iwapo umma wa pande mbili utaridhia uendelee), ndio utakuwa na manufaa zaidi kwa pande zote mbili; Lakini tatizo lililopo ni kwamba viongozi wengi wa CCM (upande wa Tanganyika) badala ya kujenga vizuri hoja juu ya usisi na uwao katika muktadha wa self determination and democracy (rejea umuhimu wa federation), wengi ya viongozi hawa wanapotosha kwamba a call for self determination and democracy ni ubaguzi wa kidini na kikabila;

Nikirejea katika suala la Unitary System under TANU/CCM kwa miaka karibia 50, mtu anaweza kujenga hoja kwamba serikali mbili chini ya CCM ya mwalimu ilifanikiwa katika maeneo kadhaa; Ni kweli, kwani viwanda vilijengwa, vijiji vya ujamaa vilianzishwa vikiwa na huduma mbalimbali za kijamii, literacy rates, primary enrollment rates, life expectancy rates zilipanda, and so forth and so forth; Lakini swali linalofuatia ni je, did all these sustain? The obvious answer is NO!; Na moja ya sababu kubwa kwanini sustainability haikutokea kwa mfano katika sekta ya viwanda, vyama vya ushirika n,k, ni URASIMU uliojitokeza; Leo Nape anathubutu kuja na hoja kwamba Serikali tatu itatuletea mzigo wa URASIMU wakati urasimu chini ya serikali mbili ndio imekuwa ni sumu kwa uchumi wa taifa letu, hasa at the micro level kwani on the macro level, mafanikio yapo (economic growth etc), lakini mafanikio haya kimsingi yananufaisha tu wawekezaji and less than 5% ya watanzania;

Nape pia aelewe kwamba mageuzi ya kiuchumi yaliyokuja katika dunia ya tatu (sio Tanzania tu) yalilenga kuondoa urasimu ili kuongeza efficiency katika uchumi, na moja ya maeneo yaliyokuwa tackled kwanza ikawa ni kuiondoa Serikali from the commanding heights of the economy; Kwa bahati mbaya, the period 1985 – 1995 was a lost decade for Tanzania kwani we ended up being the among the worse reformers na kupelekea nchi kuwa ya tatu toka mwisho kwa umaskini in 1993-94 period; Urasimu ulitokana na sera ya CCM ya serikali mbili ulichangia sana katika hili; Leo yapo mafanikio, lakini the macro success doesn't trickle down to the common man (micro level, hasa vijijini) kwa sababu CCM haina mikakati ya maana to tackle the crisis on the micro level; It remains to manage the macro level kwa ushirikiano na donor community, under the Washington consensus, and increasingly, the Beijing consensus;

Mwisho, ni msisitizo kwa Nape kwamba focus ya dunia ya leo (21[SUP]st[/SUP] century) ni decentralization katika ngazi zote – iwe ni serikali, kampuni n.k, kwani ufanisi ndio hupatikana kwa njia hiyo; Utafikti mdogo tu unaonyeshwa kwamba that has been the order of the day kufuatia economic reforms in early 1980s as the has shifted to local level – initiatives, microenterprises, NGOs, together with fostering of democratic institutions; It has been proven all over the world over and over again kwamba DECENTRALIZATION is key to good governance and Fiscal Discipline, na huko ndio Warioba na Tume yake ya Katiba inataka kutupeleka watanzania kwa kwa kuelewa kwamba - mfumo wa shirikisho wa serikali tatu is synyonymous to DECENTRALIZATION na kwamba Federalism and Decentralization will offer and promote better social, economic and political outcomes kwa watanzania ndani ya Muungano, kuliko approach ya mfumo wa serikai mbili under CCM, mfumo ambae Nape amenukuliwa kwamba CCM itaupigania mpaka mwisho wa Dunia; Given facts tulizojadili, kauli hii ya Nape inaweza tafsiriwa kwamba chini ya CCM, watanzania wasitarajie kuona maisha yao yakiboreshwa in any meaningful way– kisiasa, kiuchumi na kijamii;
 
Last edited by a moderator:
Tume ya Warioba imekuja na mahesabu haya:
Swali: Gharama za uendeshaji wa Serikali hizi utakuwaje, huoni kama Rais wa Muungano atategemea zaidi fedha na msaada kutoka Tanganyika na Zanzibar?


Warioba: Katika Katiba ya sasa mapato ya Muungano yanatokana na vyanzo vitatu, Kodi ya Mapato (income tax), Ushuru wa Forodha (custom duty) pamoja na ushuru wa bidhaa (excise duty).


Kodi ya mapato ndiyo inatoa fedha nyingi sana na inafuatiwa na kodi ya ushuru wa bidhaa na ushuru wa forodha. Kutokana na hesabu tulizopiga, tumeona matumizi katika Serikali ya Muungano yapo katika sehemu mbili, moja ni yale ya Muungano na ya pili ni yale ya Tanganyika ambayo yanachukua fedha nyingi.


Mwaka 2010/2011 mapato ya kodi ya mapato yalikuwa Sh2 trilioni na mapato ya ushuru wa bidhaa yalikuwa Sh1trilioni na mapato ya ushuru wa forodha yalikuwa Sh600 bilioni.


Ni kwamba matumizi ya mambo ya Muungano yalikuwa chini ya Sh1trilioni, ndiyo maana tumechagua ushuru wa bidhaa, kwani tukipata fedha zile zitaweza kumaliza matumizi yote ya Serikali ya Muungano.


Hivyo basi kama tukiendelea na utaratibu huu wa Serikali tatu, ni wazi kwamba Serikali ya Muungano haitakuwa na haja ya kukopa fedha kwa kuwa itakuwa nazo za kutosha,......

Chanzo Warioba: Serikali ya Muungano haitakopa fedha - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Kwa mahesabu haya, Serikali ya Muungano itatumia chini ya Trilioni 1....Tusisahau pia mambo ya muungano pia yanaingiza fedha .(Mapato na matumizi). Wengi tunajikita katika matumizi tu bila kuangalia mapato/fedha ambazo mambo ya muungano yanaingiza.
 
Ni muhimu kwa ccm kujipanga vizuri badala ya kukurupuka katika suala zima la serikali tatu; Ifike wakati sasa kwa kamati kuu ya ccm waelewe kwamba, nchi ilipofikia, itakuwa ni rahisi kwa wananchi kustahimili kifo cha ccm kuliko kustahimili kifo cha Tanganyika;

Cc Nape Nnauye

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Nape Nnauye,

Hivi kweli imefikia mahali hadi wazee wetu kina Samuel Sitta ndio watusaidie vijana kuizindua Tanganyika yetu badala ya nyinyi vijana mliopo kwenye nafasi zenye ushawishi ndani ya chama (Kamati Kuu, NEC) na wenzako huko UVCCM, je tutawaamini vipi katika ujenzi wa Tanganyika Yetu Mpya?


Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Hivi karibuni, Katibu Wa Itikadi na Uenezi wa CCM (Taifa), Nape Nnauye, ambae pia ni mdau mwenzetu humu Jamiiforums alikuja na bandiko lenye nukuu ya mwalimu kama ifuatavyo:

Mkuu mchambuzi naomba ubadili msimamo wako badala yake Nape na Chama chake wasimimie kitu Kikubwa zaidi yaani uundwaji wa;

SERIKALI MOJA YA TANZANIA KAMA KWELI WAKO NA NIA NA DHAMIRA YA KUJIENZI WAO NA NYERERE.

Hii inamaanisha Serikali ya Mapinduzi Zanzibar nayo Ife ilituweze kusonga mbele salama salimi.

Dawa lakini ngumu kumesa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom