Nape Nnauye: Jamani kuna watu wanataka kunitoa roho...

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Katibu mwenezi wa CCM Nape Nnauye ameibuka na madai mazito akiwa kwenye mikutano ya chama chake kanda ya ziwa kwa kusema kuwa kuna watu wanataka kumuua kwasababu ya msimamo wake aliouita thabiti wa kupambana na ufisadi ndani ya chama uliopewa jina la kujivua gamba.

Nape aliendelea kusema anawafahamu hao watu na akasema hawezi kurudi nyuma kamwe, aliendelea kusema kuna watu wanamtafuta kwa hali na mali ili kummaliza kabisa na kumtoa katika dunia kwa kutumia pesa zao,na akasema ana hakika Mungu yupo pamoja nae na ataendelea na mapambano maana hata YESU alipoingia Yerusalem kwa mara ya kwanza alikuta watu wakifanya biashara kwenye hekalu na akachukua hatua ya kusafisha hekalu kwa nguvu.

Muono wangu:
Ni kutafuta umaarufu wa kijinga...
 
Nape anaogopa kivuli chake mwenyewe!utakufa kwa pressure dogo!kiatu ulichokivaa ni kikubwa sana kwako!waachie wenyewe!
 
ni nani hao?au ni green guard ya ccm?
peleka malalamiko polisi uunganishe masudi na wale kina mama wawili wa igunga ili hilo kundi harramu(janjaweed)lidhibitiwe.
mafunzo ya misigiri yanakutisha na wewe?
 
Sifa za kijinga
wamtoe fasta
si ni kibaraka wao????

Rest in peaces broda
umeyataka mwenyewe
 
R.I.P mkuu
ahahahahaaaaaaaaaaa!..binadamu wanavyoogopa kifo!...sidhani kama kuna haja sana ya kuogopa kitu ambacho for certain kitatokea,..suala ni ku take care tu,...anyway_Nape jua mara zote Mungu yuko upande wenye haki mkuu,....so dont be afraid
 
Endeleza mapambano hakuna kulala hadi chama kiwe safi. ...........hiyo ndio kaži uliopewa dogo....inayokuweka mjini......ila masikio na macho yako yawe wazi....hawaminiki hao
 
Huenda ndio ulieropoka mafisadi wamerejesha pesa walizokwapua bila kuwataja,yaani we "mweupe" kweli,acha uvivu wa kufikiria
 
mwongo! Unawajua si uwaambie polisi?


Mkuu,
Hata wakubwa wana wakubwa wao! Hata akienda polisi hakuna kitakachofanyika maana wameshawekwa sawa na wakubwa! Ndio maana anabaki kulia majukwaani. Juzi tumemwona kaimu kamanda wa polisi Arusha akiwatangazia waandishi wa habari kwamba James Millya anatafutwa na polisi kwa kuwatuhumu kutumika" huku wakiwa wanafahamu sio tu kazini na home, bali hata bar anayokunywa! Angekuwa ni Lema!? Hukusikia kuna mbunge huko mby amechukuliwa kijijini kwake hadi mjini na kikosi cha polisi! Lakini Millya amewaita waandishi akatangaza kuwa ataenda mwenyewe na akafanya hivyo kesho yake akiwa na kikundi cha wapambe na alipotoka wakampokea na kumsindikiza kwa mbwembwe bila bughudha yoyote wakati wanachama wa cdm walipigwa mabomu walipomsindikiza Lema kutoka mahakamani!? Ndio maana dogo analia jukwaani maana ukubwa wake na mkubwa wake si wakubwa tena na wana wakubwa zaidi yao!
 
Awafafanulie ule msemo alioutumia kuelezea kazi zake CCM; yaani si vyema mwenye mbwa akabweka wakati mbwa wake yupo. Wakielewa kuwa yeye ni mbwa tu hawatamsumbua badala yake watashughulika na mwenye mbwa.
 
Back
Top Bottom