Nape Nnauye: Jamani kuna watu wanataka kunitoa roho...

Jaribuni kuweka chuki pembeni mmuelewe Nape anasema nini. Mapambano ya wazi dhidi ya mafisadi toka ndani ya CCM amebaki yeye tu. Ninyi wengine mnaendesha mapambano haya toka nje na humu JF kwa majina bandia. Tumuelewe Nape. Tumsaidie. Tumlinde ikibidi. Nape ana mapungufu yake kama sisi wengine tulivyo. Lakini vita hii ya ufisadi ni ngumu sana hasa unapopigana ukiwa ndani ya CCM au serikali yake.
 
Kila siku nawapa ushauri wa bure acheni kbisa kuleta habari za huyu kilaza hapa ,yeye kule Michuzi kunamfaa lakini hamsiki haya umizeni vichwa sasa .Mwisho atasema Mchemba kampigie mkewe ngojea tu .
 
...katibu mwenezi wa ccm nape nnauye ameibuka na madai mazito akiwa kwenye mikutano ya chama chake kanda ya ziwa kwa kusema kuwa kuna watu wanataka kumuua kwasababu ya msimamo wake aliouita thabiti wa kupambana na ufisadi ndani ya chama uliopewa jina la kujivua gamba.

Nape aliendelea kusema anawafahamu hao watu na akasema hawezi kurudi nyuma kamwe...aliendelea kusema kuna watu wanamtafuta kwa hali na mali ili kummaliza kabisa na kumtoa katika dunia kwa kutumia pesa zao,na akasema ana hakika mungu yupo pamoja nae na ataendelea na mapambano maana hata yesu alipoingia yerusalem kwa mara ya kwanza alikuta watu wakifanya biashara kwenye hekalu na akachukua hatua ya kusafisha hekalu kwa nguvu.......

muono wangu:

ni kutafuta umaarufu wa kijinga...

Hizi siasa za ccm zisizo na mantiki zimetuchosha,magamba na mafisadi yamo ndani ya ccm na serikali na wanafahamika.vyombo vya dola,mahakama,usalama wa raia na madaraka yote yako chini ya ccm.swali langu kwako wewe nape nini kinawazuia kuchua hatua dhidi ya watu hao??????!!!!badala ya kuchua hatua mnapanda majukwaani kutupulizia vuvuzela za vita ya ufisadi na rushwa unafiki wote mafisadi.Mungu ibariki Tanzania.
 
KAMA ANA USHAHIDI si awape Polisi kama alivyofanya Dr. Mwakyembe
Umaarufu hauji kihivyo apige mzigo mafisadi wang'oke au vita imemshinda anatafuta visingizio
 
Mbona wanachelewa hao kuitoa hiyo roho, itakuwa faraja kubwa kama ingefanyika hivyo leo hii. Baada ya hapo tutasema umeacha pengo kubwa lisiloweza kuzibwa.
 
wewe ni katibu mwenezi na mwenyekiti wako ndio mkuu wa nchi kwanini umwambii akulinde au nae akupendi sasa baada ya kukutumia?
 
aaaha....... si muondoke tu salama kama nyie wenyewe mnataka kuuwana ,nape unapata nini au faida gani kwenye kuzurura kwako tz hii zaidi ya posho?
 
James Ole Milya naye kashasema kuna watu wanataka kumtoa roho! Naye huyu Nape kashasema kuna watu wanataka kumtoa roho! Duh ngoja tuone nani atakuwa wa kwanza kutangulia.
 
Nepi mlango uliotumia kutokea umekosea kabisa..yaani laiti ungejua kuwa fisi mlafi anaweza dakwa kwa kokoto zenye damu usingetokea mlango huu ulioliwa na mchwa na karibia kuanguka..Fikiria mara 2 2 maana ushalegea mlango wenyewe( ccm) simama imara usizuie waliojenga kuingia ndani ya mjengo wao...
 
Nani Anaweza kupoteza Muda Kuua Mavuvuzela!! Mavuvuzela kama Nyie Ndani ya Chama cha Magamba Mko wengi Dogo, Usije Ukawa Unaogopa Kivuli Chako Mwenyewe!! Au Ile Damu Mliyomwaga Igunga Inakuandama? Pia kwenye Chama Chenu cha Magamba sishangai Kwani Najua Apolo Mtakwenda Wengi!! Ila kwa wewe Vuvuzela Usiogope Sana!!!!!
 
Kifo kwake ni wajibu, inabidi atubu kwanza kwa kitendo chake cha kuwatukana wakazi wa Jiji la Mwanza kuwa atawashikisha ukuta! Sina uhakika kama atatubu kweli na kwa imani ipi?
 
Back
Top Bottom