Nape: Ni lipi unaloweza kujivunia?

Amiliki

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,085
1,004
Ulipoteuliwa tu katika nafasi uliyonayo, ulianza kwa mkwara mzito, ukijidai eti unataka kukirudishia "mvuto" chama uliopotea miongoni mwa jamii (sijui ni nani aliyekwambia kama CCM wamapoteza mvuto!). Kutekeleza mpango wako, ukawa unapita kila mahali na kelele za kujivua gamba huku ukirusha makombora ya kashfa kwa Edward Lowasa (bila hata kuheshimu mchango wake kwa chama ukiachilia mbali umri wake na kuulinganisha na wako). Ukatupa matumaini makubwa kwamba wale uliowaita mapacha watatu ambao ni Lowasa, Chenge na Rostam, ndio ulikuwa mwisho wao kwenye ulingo wa siasa. Ukiacha Rostam aliyeamua kuondoka mwenyewe kwa kuondokana na Siasa za majitaka, waliobakia wanaendelea kuwepo tena kama haitoshi wameendelea kupata nyadhifa mbalimbali kupitia kwa wanachama wengine wa CCM. Je Nape kule kujivua gamba kumeishia wapi? Au umekuwa Staaring wa kihindi ambaye umekufa kabla ya movie kwisha!
 
Hawezi kujitokeza kukujibu. Hata pro magambaz hawawezi kujibu hili. Weka thread ya kuiponda CDM uone wanavyomwagika
 
Maana toka ametuambia anakirudishia mvuto chama, tunachoshuhudia ni kitu tofauti. Katika chaguzi ndogo, magambaz wamekuwa kama mlevi anayeangukia tumbo, na kuacha masaburi juu, ili wanaoyahitaji wayashughulikie. Anabisha!
 
Atajivunia kuleta mabadiliko makubwa nchini. Wanaiua ccm na kuweka mazingira ya kukijenga cdm. Hii itaishia kwa cdm kuchukua nchi na ccm kuwa chama cha upinzani. Ni jambo litakalomfanya akumbukwe kwa muda mrefu sana na kumpatia heshima kubwa kama kaburu Fredrick de Clack wa SA!
 
Atajivunia ujasiri wa kujitokeza kutetea chama kilichochafka kwa muda mrefu bila kupopolewa au kuzomewa
 
Ulipoteuliwa tu katika nafasi uliyonayo, ulianza kwa mkwara mzito, ukijidai eti unataka kukirudishia "mvuto" chama uliopotea miongoni mwa jamii (sijui ni nani aliyekwambia kama CCM wamapoteza mvuto!). Kutekeleza mpango wako, ukawa unapita kila mahali na kelele za kujivua gamba huku ukirusha makombora ya kashfa kwa Edward Lowasa (bila hata kuheshimu mchango wake kwa chama ukiachilia mbali umri wake ni kuulinganisha na wako). Ukatupa matumaini makubwa kwamba wale uliowaita mapacha watatu ambao ni Lowasa, Chenge na Rostam, ndio ulikuwa mwisho wao kwenye ulingo wa siasa. Ukiacha Rostam aliyeamua kuondoka mwenyewe kwa kuondokana na Siasa za majitaka, waliobakia wanaendelea kuwepo tena kama haitoshi wameendelea kupata nyadhifa mbalimbali kuputia kwa wanachama wengine wa CCM. Je Nape kule kujivua gamba kumeishia wapi? Au umekuwa Staaring wa kihindi ambaye umekufa kabla ya movie kwisha!

Inaonekana wewe current affairs zinakupita mbali Dr. Nape ana mengi ya kujivunia na karibu atatoa kitabu (His Diary on Inner Circles of CCM) na kule Korogwe chuo cha CCM tushampa PhD ya heshima, unataka nini tena kaja Songea mmemtandikia kitenge apite kama mfalme huyaoni hayo, uko kwenye njozi njoo sisiem uzaliwe upya.
 
Hujajibu hoja, swali ni kwamba ishu ya kuvua gamba imeishia wapi?
 
Kuvua gamba ni falsafa kama ilivyokuwa Azimio la Arusha au Ujamaa na Kujitegemea unataka nini zaidi ya hapo, la msingi tuko juu sisiem
 
Kweli povu lako limefikia pabaya. Je Nape kasema kujivua gamba ni falsafa au ni maelezo yako binafsi?? Kwa namna nyingine unaeleza Kuvua Gamba kuwa ni falsafa zilizoshindwa kama vile Azimio la Arusha. You shot yourself in the foot, buddy!!
 
Ulipoteuliwa tu katika nafasi uliyonayo, ulianza kwa mkwara mzito, ukijidai eti unataka kukirudishia "mvuto" chama uliopotea miongoni mwa jamii (sijui ni nani aliyekwambia kama CCM wamapoteza mvuto!). Kutekeleza mpango wako, ukawa unapita kila mahali na kelele za kujivua gamba huku ukirusha makombora ya kashfa kwa Edward Lowasa (bila hata kuheshimu mchango wake kwa chama ukiachilia mbali umri wake ni kuulinganisha na wako). Ukatupa matumaini makubwa kwamba wale uliowaita mapacha watatu ambao ni Lowasa, Chenge na Rostam, ndio ulikuwa mwisho wao kwenye ulingo wa siasa. Ukiacha Rostam aliyeamua kuondoka mwenyewe kwa kuondokana na Siasa za majitaka, waliobakia wanaendelea kuwepo tena kama haitoshi wameendelea kupata nyadhifa mbalimbali kuputia kwa wanachama wengine wa CCM. Je Nape kule kujivua gamba kumeishia wapi? Au umekuwa Staaring wa kihindi ambaye umekufa kabla ya movie kwisha!

Mkuu ukisikia neno kukurupuka ndo hayo mambo alofanya nape!
 
Kuhakikisha chama cha zamani(ccm)kinapoteza uaminifu hata baada kufanya mabadiliko na yeye kupewa mic.
 
Atajivunia kuleta mabadiliko makubwa nchini. Wanaiua ccm na kuweka mazingira ya kukijenga cdm. Hii itaishia kwa cdm kuchukua nchi na ccm kuwa chama cha upinzani. Ni jambo litakalomfanya akumbukwe kwa muda mrefu sana na kumpatia heshima kubwa kama kaburu Fredrick de Clack wa SA!

Mkuu pindi ccm itakapoondoka madarakani kamwe usijekutegemea chama hicho kuendelea kuwepo tena, lazima kitakufa 7bu viongozi wake ni walafi wa madaraka watahamia chama kitakachokuwa madarakani na kukwepa kutofunguliwa mashtaka kwa ufisadi walioufanya na wanaoendelea kuufanya sasa!
 
Kwa kweli nape na lusinde hawana tofauti kabisa nilisikiliza mahojiano yake na mtangazaji wa redio wapo kuhusu muhisani alietoa hela kwa cdm juma hili kwa kweli nape ana maneno wachafu akafikia kumwambia mtangazaji ana pepo. kwa kweli nape ni sifuri.
 
Inaonekana wewe current affairs zinakupita mbali Dr. Nape ana mengi ya kujivunia na karibu atatoa kitabu (His Diary on Inner Circles of CCM) na kule Korogwe chuo cha CCM tushampa PhD ya heshima, unataka nini tena kaja Songea mmemtandikia kitenge apite kama mfalme huyaoni hayo, uko kwenye njozi njoo sisiem uzaliwe upya.

Mh! Wenzake wana PHD ya kukaa darasani yeye anayo ya kupewa tena 7bu ya hicho chuo kinajipendekeza kwake yeye aliyeko madarakani. Pia kutandikiwa vitenge ndo jambo gani hilo la maana aloitendea rip ccm?
 
Hujajibu hoja, swali ni kwamba ishu ya kuvua gamba imeishia wapi?

Labda kwakumsaidia kujibu ni kwamba endapo mapacha watatu wakijivua gamba ujue hilo gamba litaondoka na wengi kuanzia m/kiti wao na wengineo wengi kwenye chama chao
 
Kweli povu lako limefikia pabaya. Je Nape kasema kujivua gamba ni falsafa au ni maelezo yako binafsi?? Kwa namna nyingine unaeleza Kuvua Gamba kuwa ni falsafa zilizoshindwa kama vile Azimio la Arusha. You shot yourself in the foot, buddy!!

nani kasema falsafa ya Azimio la Arusha imeshindwa? kwa ushahidi upi, Nape ni mwanchama kama mwanachama mwengine si lazima yeye asemse katika Sisiem tunafuata mwongozo wa Chama sio kauli ya nape na kujivua gamba ni falsafa kama nyengine meaning haina mwisho katika uetelezaji inaweza kuchukua hata miaka 100 kukamilika la msingi hatuja abandon kujivua gamba
 
Nape na dhaifu jk wanajivunia kuingia kwenye historia ya kuua ccm na kuipa cdm chance ya kuwin
 
Nape si uje ujibu hoja siku hizi jf unaiona ya moto na tangu ulivyoambiwa ulete kadi yako ya ccm ndo ulipotimua mbio
 
amejitahidi ku attain sifa ya uvuvuzela...kupiga kelele za kujivua gamba nchi nzima halafu mwisho na rais mwenyewe anafahamika kuwa ni gamba
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom