Mlengo wa Kati
JF-Expert Member
- Feb 16, 2011
- 2,730
- 492
Nimekua nikufuatilia kwa makini tangu wiki iliyo pita baada ya kile kilicho elezwa nkuwa ni kujivua gamba kwa CCM ssa ni dhahili kila mtanzania ameanza kuimba wimbo wao wa kujivua gamba iwe ni kwa kusifia au kupinga hatua hiyo ya kujivua gamba! Ukiangalia hap JF thread nyingi zinazunguka na CCM! Magazeti mengi na vyombo vya habari Radio,Tv na hata tovuti navyo vinajadili habari ya CCM kujivua gamba! Suala la kujivua gamba kwa CCM limefanya hata Dr Slaa asahua na ile habari yake ya kuipa Serikali siku 21 kule Arusha juu ya Meya alie ingia madarakani kiujanjaujanja! Watalaamu wa Siasa wanasema hata habari ya Dr Slaa kule tabora kuongeza orodha mpya ya Mafisadi nayo ni taharuki ya CCM kujivua gamba! Wengine wanasema orodha mpya ya Dr Slaa ambayo imemhusiha na Dr Magufuli haijapokelewa kwa umakini na Watanzania kwani wingu liliopo ni habari ya kujivua gamba! Nape Nnauye amekua kinara kwa kuogelea juu ya agenda ya kujivua gamba! Leo Katibu wa Uenezi Chadema bila kujijua nae ameingia kwenye hoja hii ya kujivua gamba! Leo gazeti la Mwananchi ukurasi wa mbele imeandikwa kuwa Dr Slaa amempa Kikwete siku 90 ajivue gamba ikumbukwe tayari Dr Slaa anakipolo chake cha siku 21 kule Arusha alicho ipa serikali! pia Dr Slaa amekaririwa akisema kitendo cha kutakuwafukuza Lowasa,Rostam na Chenge ndio anguko la CCM vipande vipande!,lakini amesahau kuwa Lowasa,Rostam na Chenge hakuna chama chochote hapa Tanzania kinacho weza kuwapokea kwa sasa wananuka na wamekosa mvuto wa kisiasa kabisa,kuondoka kwao CCM ni sawa na kutupa mzoga na nzi wasikufuate tena! Hivyo imekua gamba gamba gamba kila kona.......!
My take: Siasa mara nyingi inahitaji uwe focused na mambo unayo yasimamia,lakini kuna utalaam wa kupindisha hoja ya mwenzako kwa kuibua jambo fulani kwa jamii!
Chadema ni mhimu kupima suala hili lasivyo itajipotezea muda wake kwa kurukia agenda wasiyo ijua!
My take: Siasa mara nyingi inahitaji uwe focused na mambo unayo yasimamia,lakini kuna utalaam wa kupindisha hoja ya mwenzako kwa kuibua jambo fulani kwa jamii!
Chadema ni mhimu kupima suala hili lasivyo itajipotezea muda wake kwa kurukia agenda wasiyo ijua!