NAPE,ARUMERU MASHARIKI si IGUNGA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NAPE,ARUMERU MASHARIKI si IGUNGA

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by KIROJO, Feb 23, 2012.

 1. K

  KIROJO Senior Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  LEO naomba niandike makala hii katika ‘capacity’ yangu kama Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Arusha.
  Nakuandikia Nape Nnauye pamoja na viongozi wenzako wa CCM baada ya kusikia matamko yako kadhaa kwenye vyombo vya habari kuhusiana na uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha.
  Kwanza nilikusikia ukitamba kwamba jimbo lile ni lenu mna uhakika wa kulirejesha kwa kupata ushindi wa kishindo. Baadaye nikakusikia ukidai kwamba eti nyinyi katika chama chenu mnakesha na kuomba kwamba CHADEMA impitishe Dk. Willbrod Slaa kugombea ubunge katika jimbo hilo ili ashindwe, hivyo mmalize kisiasa asifae kugombea urais mwaka 2015.
  Nape, kabla ya yote naomba nikueleze kwamba hauna akili nyingi sana za kuweza kuwadanganya CHADEMA wote. Wana CHADEMA wote wanatambua kwamba hizo ni kelele za mfa maji.
  Wanaelewa kwamba CCM itashindwa vibaya Arumeru Mashariki kwa mgombea yeyote atakayesimamishwa. Lakini CCM itagaragazwa kama mbwa mwizi kama CHADEMA itamsimamisha Dk. Slaa katika kinyang’anyiro hicho.
  Ndiyo maana sasa Nape unajidai kuvujisha siri ili CHADEMA wauchukue ushauri wako wasimsimamishe Dk, Slaa. CHADEMA haijawahi kufanya siasa kwa kuongozwa na CCM. Tungefanya siasa kwa kuongozwa na CCM chama kingeshakufa miaka mingi.
  Nachukua fursa hii kukueleza Nape na viongozi wenzako wa CCM kwamba chama hakitamsimamisha Dk. Slaa. Slaa anatokea katika Mkoa wa Arusha ambako amekuwa mbunge tangu mwaka 1995 mpaka 2010 alipoombwa na Kamati Kuu kugombea urais.
  Baada ya hapo aliletwa mpaka Karatu wakaulizwa kwanza wananchi wa jimbo lake kama wanaridhia akagombee urais, wakakubali.
  Baadaye aliletwa kwenye uwanja wa NMC mjini Arusha mahali ambapo walikusanyika wana CHADEMA na wananchi wa kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha nao wakaulizwa na wakaridhia kumwachia Dk. Slaa kugombea urais.
  Wana Arusha tulishamtoa Dk. Slaa kwa ngazi ya kitaifa na hatuna mpango wa kumrudisha kwa sasa katika ngazi ya jimbo wala mkoa.
  Kama anawatesa sana huko kwa kufanya kazi za katibu mkuu wa chama kwa ufanisi zaidi na kukijenga chama kwa kasi bila kutingwa na majukumu ya kibunge, option mliyonayo ni moja tu: Kujiandaa kung’oka madarakani badala ya kutafuta mbinu zisizo na mafanikio.
  Kwetu sisi wana CHADEMA wa Arusha tunaona kama kumleta Dk. Slaa kugombea ubunge Arumeru Mashariki ni sawa na kutumia tofali kuua mbu. Ni matumizi mabaya ya rasilimali watu.
  Nape naomba sasa niingie katika uchaguzi wenyewe wa Arumeru Mashariki. Narejea kauli mbiu yenu ya siku hizi kwamba ‘ushindi ni lazima.’
  Naomba niwatahadharishe kwamba Arumeru Mashariki si Igunga wala haiko katika Mkoa wa Tabora, iko katika Mkoa wa Arusha. Nakumbuka wakati Rostam Aziz anatangaza kujiuzulu ubunge wa Igunga na ujumbe wa NEC ya CCM alitamka kwamba wamefanya kazi kubwa sana katika Mkoa wa Tabora kiasi kwamba pamoja na nguvu kubwa ya upinzani iliyopo nchini kwa sasa, Tabora ni mkoa mmojawapo ambao hakuchaguliwa mbunge yeyote kutoka upinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
  Ni kweli maneno yake kwamba mbinu chafu za chama chenu kujumlisha hali ya kisiasa na uelewa wa wananchi wa Tabora, baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hapakuwa na mbunge yeyote wa upinzani aliyeshinda jimbo lolote la mkoa wa Tabora.
  Katika Jimbo la Igunga kwa mfano CHADEMA haikuwa na mgombea ubunge katika uchaguzi mkuu uliopita. Lakini nikukumbushe Nape na wenzako mtiti mliokumbana nao kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo hilo. Kwa Arumeru Mashariki ni tofauti kabisa.
  Arusha ni mkoa wa CHADEMA na hata nyinyi mnalifahamu hilo. Kama hamna uhakika waulizeni viongozi wenu wa mkoa huku Arusha watawaeleza vizuri.
  Wanaelewa mazingira maalumu yaliyowawezesha kutangazwa washindi kwenye Jimbo la Arumeru Mashariki, mazingira ambayo hayapo kwenye uchaguzi mdogo. Muulizeni Dk. Burian atawaeleza vizuri CHADEMA Arusha ikoje.
  Muulizeni Ole Medeye ambaye naye alitangazwa mshindi katika mazingira maalumu katika Jimbo la Arumeru magharibi. Hawa watakuwa mashahidi wenu wazuri. Najua mwaka 2008 ulikuwa hujawa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama chako.
  Na hivyo naelewa kwamba uchaguzi wa Tarime ulikupita pembeni. Kamuulize Yusuph Makamba akueleze hali ilikuwaje kule kwenye uchaguzi mdogo wa mwaka 2008, halafu kile atakachokueleza zidisha mara moja na nusu ndipo ujue Arusha itakuwaje!
  Nakushauri kama kiongozi kijana. Achana na siasa za kikongwe za kina Ngombare- Mwiru na kina Malecela za kutaka kuhakikisha wanatangazwa washindi hata pale pasipowezekana!
  Jifunze kukubaliana na hali. Angalia vijana wenzako kina Mtatiro na Jussa, wale ambao mlishirikiana sana kule Igunga na Uzini kuipiga propaganda CHADEMA. Wamepima kina cha maji, wameingia mitini.
  Najua Arumeru Mashariki mnakwenda kumtumia mzee wa Kiraracha. Nawahakikishia kwamba athari yake kwa kura za CHADEMA ni 0.0001%, kimahesabu ni sawa na 0.00%.
  Nape, jaribu kukaa na wenzako mezani ili mfanye hesabu upya. Arusha mbinu zenu hazina nafasi. Matumizi ya Green guards huku hayakubaliki na hayatafanikiwa. Mkijaribu kutumia Green guards kuleta fujo, kunyanyasa wananchi, kufanya vurugu na kutisha watu, kupiga wana timu ya kampeni ya chama chetu, naomba niwahakikishie kwamba tukiamua kutumia Red brigade tuna uwezo kuwa na red watano kwa kila green mmoja mtakayemleta Arumeru.
  Nawashauri kwa usalama wenu na mustakabali mwema wa nchi hii msijaribu kufanya mchezo huo.
  Tambueni kwamba vijana hao mnaowadanganya kwa shilingi elfu tano kwa siku na kuwaleta kukata watu mapanga, kupiga na kuumiza watu kwa mbinu zozote zile, ni vijana wa Kitanzania mliowanyanyasa kwa kuwanyima elimu na ajira.
  Sasa wanasota mitaani bila kazi, wakijaribu umachinga mnawafukuza, wamekata tamaa! Nanyi sasa mmebuni njia nyingine ya kuwatumia.
  Mnawakusanya na kuwavutisha bangi halafu mnawatawanya kufanya fujo. Ole wenu madhira yoyote yatakayowapata vijana hao katika mapambano na wananchi yatawarudia nyinyi.
  Propaganda za udini na ukabila huku hazina nafasi. Labda nikueleze kwamba si kweli kwamba wananchi wote huku Arusha na Kilimanjaro wana kadi za uanachama wa CHADEMA.
  Bali wameamua kuweka itikadi pembeni na kuangalia mustakabali wao kama jamii moja. Huku CHADEMA ni CHADEMA na CCM ni CHADEMA.
  Hii maana yake ni kwamba katika kanda hii wananchi wameamua kusahau uanachama wao kwenye vyama na kuangalia chama kimoja chenye uwezo wa kuwakomboa kiuchumi na kuwaletea maendeleo.
  Ndiyo maana kwa mfano katika Halmashauri ya Hai, madiwani wa CCM walimpigia kura mwenyekiti wa halmashauri kupitia CHADEMA na akashinda. Tumepita Meru yote, wanawasubiri kwa hamu. Wametahadharisha kwamba wao ni waelewa wa mambo ya kisiasa, ni wastaarabu na ni wacha Mungu.
  Hawapendi vurugu na ni wapenda haki. Kwa Meru suala si chama bali masilahi yao kwanza. Wakisha-establish maslahi yao wanachokiangalia ni chama kipi kina uwezo wa kuwatimizia mahitaji yao. Na hapo haitajalisha kama chama hicho ni tawala ama cha upinzani.
  Kwanza sasa Wameru wanakiona CHADEMA kama kimbilio pekee la kuwatoa kwenye lindi la umaskini unaotisha wakati wakiwa wamezungukwa na rasilimali za kutosha.
  Ardhi nzuri yenye rutuba, maji safi yanayotumiwa mpaka Arusha mjini yanatoka Mlima Meru ambao uko ndani ya jimbo lao. Hifadhi ya Taifa ya Arusha (ANAPA) iko ndani ya jimbo lao lakini hawana wanachofaidika isipokuwa manyanyaso.
  Itakumbukwa kwamba miaka michache iliyopita hifadhi hii imejitanua na kuongeza eneo la hifadhi kwa mabavu na kuwahamisha wananchi kwa nguvu ya dola kutoka katika maeneo waliyokuwa wanaishi na kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji bila fidia yoyote.
  Malalamiko yao hayakusikilizwa, si tu na serikali bali hata mbunge aliyekuwepo. Hayo ni katika kata zinazoizunguka hifadhi ya taifa ya Arusha.
  Badala ya hifadhi kutumia sehemu ya pato lake kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wanaoizunguka, wanatumia pato hilo kugharamia magari na polisi wa kwenda kuwahamisha wananchi hao kwa nguvu.
  Katika Kata ya Kikwe, tajiri mwenye nguvu ya pesa kapora eneo. Anawatumia polisi kuwanyanyasa wananchi waliokataa kuhama na kumpisha.
  Wanawake wenye umri mkubwa wamefikia mahali pa kukamatwa na polisi na kudhalilishwa. Muda si mrefu uliopita polisi wamevamia wananchi usiku wakiwa wamelala na kuwakamata wakiwa uchi wanaume kwa wanawake. Manyanyaso ya namna gani haya!
  Polisi! Walinzi wa usalama wa raia na mali zao leo wanageuka wanyanyasaji wa raia kiasi hiki? Halafu serikali ya CCM iko kimya! Leo wanarudi kwa Wameru eti wawape kura katika uchaguzi mdogo!
  Katika Meru hakutakuwa na itikadi, sote wana CHADEMA, wana CCM na wasio na vyama tutapiga kura kumchagua mbunge makini kupitia CHADEMA akaungane na kina Lissu, Mnyika, Zitto, Lema, Msigwa, Halima, na wengineo kuwapigania wananchi.
  Viongozi wa CCM na mkoa na wilaya wanalitambua hili. Waulizeni watawaambia kwamba kwa Arusha CHADEMA haikamatiki. Kama ni intelijensia hapa ndipo mahali pake.
  Timu ya mgombea wenu wa ubunge Arusha mjini mwaka 2010 walikuwa wakipanga mikakati miovu saa tisa usiku, saa nne asubuhi sisi tunaongea na vyombo vya habari na kuanika mipango yao.
  Walipojaribu kuwatumia baadhi ya viongozi wetu wa wilaya kutuvuruga wanajua ni nini kilitokea. Walipojaribu hivi karibuni kuwatumia madiwani wa chama chetu kukivuruga chama, hata wewe Nnauye utajua kilichotokea.
  Na nina uhakika kwamba nguvu ya CHADEMA katika Mkoa wa Arusha siyo jambo lisilofahamika kwako. Ndiyo maana ulipoteuliwa kuwa katibu wa itikadi na uenezi wewe na wenzako mlipita mikoa yote kujitambulisha na kuwadanganya wananchi na kiini macho cha kujivua gamba lakini Arusha hukugusa.
  Ulipofika Moshi kile ulichokishuhudia tena kutoka kwa vijana wa CCM ambao walikubebea mabango na kukutaka uondoke na magamba yako, hukuthubutu tena kuendelea na safari ya Arusha. Ulirudia hapo hapo.
  Nape Igunga mwaka 2010 CCM ilikuwa na kura 35,674 na 73% wakati CHADEMA ilikuwa na kura 0 sawa na 0.00% lakini kwenye uchaguzi mdogo wa mwaka Oktoba mwaka jana (chini kidogo ya mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu) CCM ilipata kura 26,266 na CHADEMA kura 22,443.
  Sijui kama unaiona hiyo tofauti. Sasa leo Meru 2010 matokeo yalikuwa ni CCM kura 34,661 sawa na 62.23% wakati CHADEMA ilipata kura 19,123 sawa na 34.33%. unategemeaje kushinda?
  Narudia kuwaonya kwamba Arumeru Mashariki si Igunga na CHADEMA Arumeru si sawa na CHADEMA Meru. Mkija na kaulimbiu ya ‘Ushindi lazima’, mtajibu mashitaka ICC! Karibuni ulingoni!
  Source: Kalama ya Mwigamba-Tanzania Daima
   
 2. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mwache kutamba humu mwende arumeru mkasaidie kampeni,tuone mshindi nani,sina hakika kama kuna watakaopiga kura arumeru wapo hapa jamvini,kati ya watanzania zaidi ya mil 40 ,member humu ni zaidi ya elfu 64,wengi wao wakiwa na mult ID
   
 3. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Kweli siasa ni mchezo mchafu, Nape anaenda kumpigia kampeni MKWE WA LOWASSA...
   
 4. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  atajifanya hajaisoma hii
   
 5. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,791
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Huyo tapeli hana ujanja.
  Tulishamswaga kanda ya ziwa itakuwa Arumeru Mashariki.
  Yani CCM tunawapa kichapo Home and Away!!
   
 6. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Hivi nimeishia wapi kuusoma huu waraka naona kama narudia rudia,au ndo nimekuwa kama Wassira aliyemuuliza Kinana kuwa suala la unec limeishia wapi ,wakati naye yupo hapo hapo
   
 7. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,541
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Hata wana ccm arumeru wenyewe hawataki kumsikia nepi.
   
 8. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Huku kuna watu wanalipwa na huyo mtu,fasta watamwambia na ataingia!!!! Sina cha kuongeza Kamanda Kirojo Umemaliza kila kitu.
   
 9. E

  ESAM JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hii iko gazetini ndugu kwa hiyo hata walengwa wengi watasoma tu sio hapa JF peke yake
   
 10. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hapo ndipo ntachoka kumsikiliza nepi sijui atasemaje nahisi hatagusa hilo
   
 11. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Safi sana, nimeipenda sana hii 'rap'

  Namwomba Nape a - respond!
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkiambiwa Miafrica haisomagi utabisha?
   
 13. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 910
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Hii makala kweli kiboko! Imebeba ujumbe mzito, nahisi atapandishwa huyu mwandishi atamandishwa tena kizimbani!
   
 14. i

  igoji Member

  #14
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siku hazigandi. tusubiri tuone mpambano
   
 15. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Alikuwa amesinzia wakti wanatoa uamuzi
   
 16. mamaWILLE

  mamaWILLE Senior Member

  #16
  Feb 23, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tathimin yako imegusa ukweli kwa 80% ni kweli mtupu wa hoja zako. Ukweli mwingine igunga pesa ilishindwa na hoja za chadema. Kilicho saidia ni dola kwa kutumia vitisho na mabom
   
 17. M

  Mayuka Member

  #17
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwisha habari yenu CCM nyie ni majambazi wakubwa na adui wa watanzania.
   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Feb 23, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Ataijibu hii muda si mrefu, "namuaminia" Nape
   
 19. mpiganiahaki

  mpiganiahaki Senior Member

  #19
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  chadema kamwe haifanyi siasa kwa kuongozwa/kushauriwa ccm!
   
 20. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mwenzenu ameshaokoka kwa gwajima,dhambi za kiba kura,kudhamini wahalifu kaacha siku hizi ukimpiga shavu la kulia anakugeuzia kushoto.

  tegemeeni uchaguzi wenye uenezi wenye upako.

  akikiliuka ungamo nitawasiliana na gwajima.
   
Loading...