Mtazamo wangu: CCM ipi ni safi kati ya hizi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtazamo wangu: CCM ipi ni safi kati ya hizi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, Oct 15, 2011.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Siasa za Makundi zilizonogeshwa na Kile kilichoitwa "Kujivua Gamba Ili Kukinusuru Chama" sasa zimepelekea kutokea Makundi Makubwa ndani ya CCM yanayohatarisha Ustawi wa Chama hicho ( Tuendelee kuomba Mungu Kife Kabisa). Kwa Mtu anayefuatilia kwa Karibu Kabisa Mienendo na Minyukano ndani ya Chama Kicho Chenye Fikra zinazofanana Uzee wake ataona kwamba CCM sasa imegwanyika katika Makundi yafuatayo

  1. CCM -Sitta: Hili ni lile kundi ambalo baada ya Kushindwa kanzisha CCJ sasa linaonekana kwamba linataka kuanzisha Chama ndani ya Chama. Hili ni kundi ambalo linajitahidi sana kutaka kuaminika kwa Watanzania kwamba ni Watakatifu ndani ya CCM. Nyuma ya kundi hili wamo akina Nape, Ole Sendeka, Kilango, Mwakyembe. Kundi hili linapambana kuhakikisha kwamba mwaka 2015 linafanikiwa kumpenyeza Mgombea wao wa Urais. Ni kundi ambalo limejaa wanafiki tukianzia na Samwel Sitta ambaye leo anaiita Kampuni ya Dowans aliyozima Mjadala wake Bungeni kuwa ni ya Kihuni. Huyu Babu ni Mnafiki anayeongozwa na Visasi vya Kuukosa Uwaziri Mkuu 2010. Ni kundi ambalo linaonekana kutumia Kujivua Gamba kama turufu ya kuwamaliza wabaya wao wa Kisiasa.

  2. CCM-Lowasa: Hili ni lile kundi linaloamini kwamba Lowasa hakuwa na kosa katika kashfa ya Ricmond na kwamba Lowasa aliamua Kujitoa Sadaka ili kukiokoa Chama. Kundi hili linaona kwamba yule aliyejitoa Sadaka ili kukiokoa Chama dhidi ya Hasira ya wananchi sasa amekuwa Kafara. Ni kundi lenye Nguvu sana na Nguvu ya hili kundi ilidhihirika pale Lilipowazuia wale "Mitume" katika kundi la kwanza kukanyaga Igunga katika kipindi cha Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Igunga. Ni Kundi ambalo linaamini kwamba Katika CCM hakuna aliye Msafi wa Kumyooshea Kidole Mwezake kwamba ni Fisadi. Ikumbukwe kwamba Lowasa anashutumiwa kwa Ishu ya Richmond pekee. Wachambuzi wa Mambo wanauliza kwamba Iweje IPTL iwe haramu lakini Richmond iwe Nongwa? Wanauliza vipi Kagoda, Deep Green , Meremeta, Tangold mbona Haziguswi? Kundi hili limeapa kufa na CCM

  3. CCM-Membe. Hii ni CCM ambayo inategemea kudra na Huruma za Mwenyekiti, Wachambuzi wa Mambo wanasema kwamba Kundi hili liko kwenye Kundi la Kukosa maana kwa Sasa Mwenyekiti hana nguvu za kuamua nani awe Mgombea Uraisi. Ni Kundi ambalo linajaribu kujipendekeza zaidi katika Kundi la CCM-Sitta kama Fisi likingoja Mfupa Uanguke.

  Wachambuzi wa Mambo wanasema kwamba Kwa Hali ilivyofikia ndani ya CCM ni Kudra za Mwenyezi Mungu zitakiwezesha chama hicho kikongwe kabisa Kupita salama katika Uchaguzi wa 2015

  4-CCM-JF. Katika mtandao wa hapa jamii forums pia Makada wa CCM wametofautiana Kimtizamo na Kitu pekee kinachowaweka pamoja ni pale inapokuwa CCM against CDM.

  4.1-CCM-Rostama: Hii ni CCM ambayo haitaki kusikia kwamba Rostam ni Gamba ni CCM ambayo kwao Rostam ni Role Model. Ni CCM inayoongozwa na Mwanamama FaizaFoxy na Malaria Sugu. Ni CCM ambayo imeapa kufa na Rostam
   
 2. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Unapotaja CCM umetaja uchafu,huwezi kukusanya makundi ya uchafu alafu ukauliza uchafu upi msafi.
  Hizo CCM ulizozitaja zote zitupie kwenye dustbin zitajuana zenyewe.
   
 3. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu Ndani ya CCM kuna Mitume 12 unatambua hilo?
   
 4. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  CCM ni CCM tu!hakuna cha 6 wala lowasa wala nape wala ff au ms!wote wanafiki na walaghai!wote ni wezi,zaidi wanazidiana katika uwizi ndo maana wamegawanyika!Damn ccm
   
 5. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #5
  Oct 15, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Kinacho ingia kwenye uchafu, ni kichafu. Japo ccm ni chafu lakini pia unaweza kuiweka kwenye makundi 5 tofauti na hayo 4 hapo juu.
  1. Ccm asilia- hawa ni kina mzee Butiku, salim ahmedi salimu, madaraka nyerere, maria nyerere na aina ya watu wa Renatus Mkinga.
  2. Ccm mamboleo- hawa ni mafisadi waliojiita wanamtandao wakati wanamuingiza mwenzao madarakani. Hapa wapo wengi sana na ndio zao la tunacho kiona leo. Mfano. EL, Ra, Ac, jk, kutaja tu wachache.
  3. Ccm chumia tumbo- hawa nao wako wengi sana mpaka vijana wanaingia humu mfano T.hiza, makambale, kibonde, ze comedy, tot nk.
  4. Ccm ***** mtozeni aka ccm jamii hapa wako kina nepi, mwaky, 6, na wengine
  5. Ccm fuata upepo- kilango, sendeka, kigwa, nk
  ongeza wengine...
   
 6. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 490
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  kuna kundi jingine linalopigiwa chapuo na joseph warioba, joseph butiku, H kitime na baadhi ya wazee wengine wa chama ambao wanaona chama kimepoteza muelekeo katika kusimamia mambo ya msingi na matokeo yake kimejikita katika majungu na tamaa za kutaka madaraka. hawa wanakosa nguvu ndani ya chama mana wao wanataka kukirudisha chama kwenye mstari wakati wenzao wanataka kuwajenga watu ndani ya chama kwa maslahi yao. maneno ya mwalimu kuwa upinzani wenye nguvu utategemea kuyumba kwa ccm unaanza kutimia!
   
 7. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Je unafikiri kwamba 2015 Hizi CCM zinaweza kufunika Kombe Mwanaharamu apite?
   
 8. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kazi ipo! Kama analysis hizi ni sahihi basi mparaganyiko ni dhahiri. Ni bora kila mtanzania kuomba huu mparaganyiko utokee kwa maslahi ya nchi, na kama kuna mtanzania anaweza kuchochea hili litokee upesi afanye hivyo na nchi itamuenzi kwa njia moja ama nyingine.
   
 9. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Heko sana Albedo, inventive piece of analysis.
   
 10. A

  Ame JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  CCM born again by the spirit of uzalendo and called CDM kama Mbowe, Slaa, Ndesa pesa, Mtei, Makani, Ame etc nao wakazaa watoto wengi sana na wakakulia katika kujisimamia bila kubebwa kama Zitto, Mnyika, Mdee, Owenye and the like and the rest of wakulima na wafanyakazi rural and urban...Hawa wanapigana kufa na kupona kurudisha uhuru uliotekwa na wakoloni weusi CCM-FISADI
   
 11. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hili suala la UVCCM kufungua Matawi Arusha limewatisha CCM-Sitta yaani hawa jamaa ndio wanajiona wao katika CCM ndio wanastahili kufungua Matawi. Very soon watasema kwamba hawayatambui hayo Matawi
   
 12. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mkuu Albedo,

  Bila shaka wewe ni shabiki wa CCM - LOWASA ila unajipambanua upo kwenye kivuli cha Mwanamageuzi.

  Analysis yako inaonesha haiko balanced na kwa LOWASA umepaint kama anaonewa na katolewa kafara,
  na kuwa kuna ufisadi mwingine haujashikiwa bango kama RICHMOND, hapa ndio ulipoharibu hoja yako
  yote, na wakati makundi mengine umeyaponda outright.

  Si dhambi kujitokeza na kusema openly unamsupport LOWASA, kuliko kujitia Mwanamageuzi huku akili
  zote zinafuatilia makundi ya CCM. Maana kwa wana CCM-LOWASA ni bora chama kife kuliko the BOSS
  wenu aukose urais.

  Go back to the drawing board halafu urudi na more balanced analysis.
   
 13. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,322
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  The all groups sound nothing to me, no one is better than the other!!!!!!!!
   
 14. A

  Ame JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Katibu mwenezi na Itikadi teh!
   
 15. M

  Makupa JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mbona hamsema makundi yaliyopo cdm ambayo ni kamabifuatavyo,zito na kundi lake,mboe na kundi lake,na shibuda na kundi lake
   
 16. kamatembo

  kamatembo JF-Expert Member

  #16
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 180
  this is why i spend much time reading comments on jf some dudes are quite smarts

   
 17. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #17
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu Alwatan kwanza Nashukuru kwa Kutambua kwamba Ndani ya chama chenu kuna vyama vingi na kwa kuniweka katika kundi la CCM-Lowasa umethibitisha hilo.

  Kwamba Mimi ni CCM-Lowasa au la Nakushauri fuatilia historia yangu hapa Jamvini utajua Msimamo wangu katika Siasa za Nji hii kwa hiyo hamna haja ya kuhisi msimamo wangu juu ya siasa za Tanzania

  Nimesema ndani ya CCM kuna Vyama vingi na nikajaribu kutaja hivyo vyama na nini kila kimoja kinasimamia ili kiweze kufika 2015 kikiwa na nguvu za Kusimamisha Mgombea, nikaenda Mbali zaidi na kutaja Baadhi ya Wafuasi wa Vyama hivyo sasa kama wewe unaona Uchambuzi wangu hauko sasa ni vyema ukaupinga kwa Hoja.
   
 18. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #18
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Anzisha thread yake tutakuja kuchangia
   
 19. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #19
  Oct 16, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Yeah tunatambua wapo mitume 12 wa uchafu, ni ngumu sana tena next to impossible kwa mtu msafi kubaki active member ndani ya CCM hadi leo hii ambapo ni dhahiri kabisa chama hiki kimegeuka pango la wanyang'anyi. Hao unaowaona wanang'ang'ana kuwa na makundi, wanafanya hivyo ili wakishika nchi watuibie kama watangulizi wao, usidhani kuwa wanapigania kwenda Ikulu ili kuwaendeleza wananchi, kama wana nia ya kuwaendeleza wananchi si wafanye hivyo kwa nafasi walizo nazo sasa hivi???kwani ni lazma hadi ufike Ikulu ndo uendeleze nchi???

  Nionavyo mimi CCM kinapaswa KUJIVUA MWILI MZIMA, NA SIO GAMBA TU ili kiiache roho ikapumzike nacho kianze upya, kila mwanaccm nimwonaye najua either njaa inamsumbua, hivyo anatumikia kafiri (CCM) ili apate rizki (kina Nape, Malisa, etc) au ni Jizi (Kingunge,Rostam, EL,Masaburi, Simba,Ben, linaloneemeka na rasilimali za taifa kupitia ufisadi etc. I really have this party, wamesababisha hata nguo za kijani zipoteze sifa ya kuvaliwa na vijana makini.

  Ukiona mwana CCM anasema rasilimali za nchi hazitumiki kwa usawa, jua waliomo madarakani kwa wakati huo hawajazifaidi rasilimali hizo za Taifa, nenda kacheki mgawanyo wa Hunting Blocks pamoja na Hotel Sites in Game Reserves na National Parks ndo utajua nini namaanisha. Wananchi wazalendo tuipinge CCM kwa hali yoyote ile maana hawana nia njema na nchi yetu, msihadaike na haya makundi kujifanya yanawapenda sana wananchi wakati miaka 50 sasa wamo madarakani na mauchafu yote yanatokea wakiwemo madarakani. Chukulia makundi yote hayo ni ya wahuni, wezi na watu wenye uchu na kuingia Ikulu ili wapitishe mikataba kama ya Kina Chief Mangungo. Mtu asiye na sifa nlizozitaja hawezi kuwa CCM hadi leo.
   
 20. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #20
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Dah Ongezea na Mabanda ya Sabasaba Mengi ni miradi ya Wake zao
   
Loading...