Nape Nnauye, kujiuzulu ni uungwana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape Nnauye, kujiuzulu ni uungwana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Sep 14, 2011.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Ukiwa kijana uliyeonyesha uwezo wa kuwa mwanasiasa. Ulikubali kujitoa mhanga kutetea jengo la umoja wa vijana lisiuzwe kwa ulaghai kwa nguvu ya mafisadi. Hapo ndipo ulipoanza kuonyesha kuwa unaweza kupambana na nguvu kubwa ndani ya chama chako. Umeridhi siasa kutoka kwa mzazi mwadilifu, mnyenyekevu na mwenye maadili, alichukia rushwa na kuonea watu, alichukia kugandamiza masikini na kuwatenga. namkumbuka mzee Moses Mnauye kijijini kwetu alicheza na watoto na aliwaacha wachezee kinananda chake ishara ya upendo.

  Kijana Nape najua unamatumaini makubwa sana ya kisiasa na kukwea ngazi kufikia ubunge, waziri hata juu zaidi. Ila kaka yangu ulipofikia sasa inabidi utumie busara na hekima kuamua.

  Ukiwa tu umeteuliwa katibu mwenezi wa CCM ulikuja na kauli mbiu ya kuvua watu magamba na uliwataja kwa majina Rostam Azizi, Chenge na E lowasa. ulienda mbali zaidi na kusema wana siku tisini lazima wajivue gamba au chama kitawavua magamba. Mheshimiwa siku tisini zilikwisha na hakuna kinachojulika ziadi. kauli hizi zilipingwa na Mukama mbele ya vyombo vya habari kuwa hakuna swala la siku tisini. Wakati anaachia ubunge wa igunga Rostom azizi alisema anaachana na siasa uchwara ambazo kwa tafsiri yangu wewe ndiye unaziendesha.

  Kikao cha kamti kilichokaa juzi juzi inasemakana kilikupiga marufuku usihudhurie kampeni za Igunga kitu ambacho kwa tafsiri yangu nina amini kwani mpaka sasa hujahudhuria kampeni yeyote Igunga hata ile ya ufunguzi ikizingatiwe hapo ndio pangekuwa mahala pako. Hilo haliajinishtua katu.

  Mshtuko wango ni pale ninapoona ulikazwa usiende Igunga ili gamba mlilokuwa mnalipigia kelele liweze kuchukua nafasi yenu nyite kuwasaidia kushinda uchaguzi mliosema mnafukuza mafisadi wanaoharibu taswira ya chama mbele ya jamii. Je ni jamii ipi tena wakati hao hao ndio mnawahitaji mnapoona hamyawezi?????

  Ndugu Nape ulisema chama ni zaidi ya mtu na mtu hawezi kuwa maarafu kuliko chama. je bado unaona vita vya kutoa magamba vipo? Je si kweli kwamba kamati kuu ilimwomba Rostam Aziz kusaidia kampeni za Igunga? na kama ni kweli nini yeye atapata ? ameahidiwa nini kutoka kamati kuu au Rostam alijipeleka mwenyewe Igunga??? Nape huoni wenzako wamekusaliti kwa kiwango kikubwa sana, huoni umeachwa kama yatima nyikani, huoni utu wako umedhalilishwa kwa kutetea wasiyoamini wala labda kututma kutoka mioyoni mwao, huoni unatumiwa kama dodoki na mwisho utatupwa jalalani???

  Nape Nnauye kama mimi ningekuwa wewe ningejiuzulu wadhifa wangu huo kwani ni kazi ya kinafiki na isiyotekelezeka, kupewa maagizo ya kinafiki na majukumu ya uongo ni unafiki mkubwa sana.

  Kama kweli wewe ni mwana mapinduzi pima yote yanayotokea, kama hayo ndiyo yanatoa picha ya Nape Nnauye endelea ila kama una utu na unasimamia unayoongea ni muda wa kujiuzulu.

  najua siasa ni kazi na mshahara na marupu rupu ndio yanayoangamiza dhamiri zetu za ndani, wamekukamata pazuri. wamejua huna jinsi ya kupata mkate wamekutumia kama dodoki sasa wanakucheka ujinga. Leo wanamhitaji Rostam kuliko wewe kesho watamhitaji Chenge Mwanza kuliko wewe kesho watamhitaji E lowasa Arusha kuliko wewe kesho kutwa watamhitaji Manji kuliko wewe, wewe utangojea kutumwa tu pale wasipotaka kuharibu urafiki wao. Hapo ndipo elimu na uelewa binafsi unapohitajika unapigania nini??

  Mambo kama haya ndio chanzo cha vijana wengi makini kuamua kuachana na CCM na kujiunga na vyama vya upinzani. Ni heri kufa masikini na kulinda utu na uelewa wangu kuliko kudhalilisha utu wangu kwa kibaba cha mchele.

  Kwa kumpandisha Gamba ambalo mnalia nalo na kukushusha wewe huhitaji miujiza mingine zaidi ya kujua unatumika kama kifuu.

  Akili ni nyele kila mtu ana zake. Ukistaabu ya musa utaona ya firauni. Muungwana ni vitendo.

  Viongozi makini hutoa maamuzi makini
   
 2. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #2
  Sep 14, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  mhhhhhhhhhhh,ndugu yangu uliyoyanena yote huenda yanaukweli ndani yake kwani hata nasi tulikuwa tukiyasoma ktk vyombo vya habari,lakini yasemekana Nape alikuwepo Igunga kwa kile kifo kilichotokea baada ya kijana mmoja kugongwa na gari

  sasa hatujui kama alikwenda kwa nauri yake ama alikwenda kichama

  yetu ni macho

  ila namkubali sana Nape kwa misimamo yake,kinachoniuzi ni kufanya Siasa za kukomoana hicho ndicho sikipendi toka kwake
   
 3. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nape it is high time now kufikiria kuachana na magamba kwani huu mpango wa kampeni Igunga ni wanakudhalilisha na upiganaji wako unakuwa hauna maana think twice na uachane na magamba bora ukaendeleze chama choko cha CCK
   
 4. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye Blue umenena mkuu. Ila nawasiwasi wa hilo Gamba linalomfunga nape asiwe na macho ya kuona na masikio ya kusikia na ufahamu wa kuelewa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 5. T

  Tata JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Chief Mkwawa kimsingi unajenga hoja kuwa Nape amekuwa gamba linalotakiwa kujing'oa lenyewe toka CCM. Nadhani kosa lake kubwa ni kutokujua dhamira hasa ya wakubwa wake wa chama waliomtuma kuongelea suala la Mapacha Watatu. Wakubwa walimtumia Nape kuongea aliyoyaongea kama mkakati wa kupima reaction ya jamii kwenye suala husika na kupooza hasira za kundi la waliokuwa wakitaka mapacha waondoke. Lakini kamwe hawakumaanisha kile walichokuwa wakiongea kupitia kwa Nape.
   
 6. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #6
  Sep 14, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nape kijana mwenzangu, hachana na magamba hao kwanza hata huendani nao, njoo uku upande wa pili tuendeleze mapinduzi ya ukweli.
  Kwa mfano, sasa hivi utapata wapi ujasiri wa kusema mafisadi waliosalia wajivue gamba wakati Rostam mliempigia kelele nyingi ajivue gamba (alisababisha mkakosa ushindi wa kishindo 2010) leo mnamtaka aende igunga akawanadi, hivi c.c.m mnafikiri kwa kutumia nini?
  Nape vaa Magwanda hachana na Magamba hao.
   
 7. only83

  only83 JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ........Nimewai kusema na nitaendelea kusema hapa JF,ukiwa mwanachama wa CCM akili zinapoteza uwezo wa kufikiria na kufanya mambo..uwezo wa Nape kufikiri na kutenda ndio umeishia pale,hawezi fanya lolote hata kwa fimbo.
   
 8. F

  FUSO JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,339
  Trophy Points: 280
  "Leo wanamhitaji Rostam kuliko wewe kesho watamhitaji Chenge Mwanza kuliko wewe kesho watamhitaji E lowasa Arusha kuliko wewe kesho kutwa watamhitaji Manji kuliko wewe, wewe utangojea kutumwa tu pale wasipotaka kuharibu urafiki wao. Hapo ndipo elimu na uelewa binafsi unapohitajika unapigania nini??"

  Hakika mwenye maskio na asikie -- Ujumbe Mzito huu.
   
 9. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Nape dear boy, see how you're loved - whom you're repeatedly letting down. Getting free advice.
  Chief Mkwawa has recited a very strong wisdom in his post above! Come on out Nape and free your conscience, there is life (better one) outside magamba' party.
  Go back and follow your right path of creating an oppostion party, be assured of big support.
  You'll never win the war of fighting mafisadis while eating from their filthy plates.
   
 10. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Well said Chief Mkwawa ila kwa nchi yetu hii sidhani kama ana guts za kufanya hivyo
  Uchambuzi wako nimeukubali mkuu umeenda shule na kama ana masikio ya kusikia ni bora auchukue na kuufanyia kazi
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Sep 14, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Chief umeuliza maswali magumu sana, Nape hawezi kuyajibu, elimu yake ya Kihindi.
   
 12. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  sikio la kufa halisikii dawa.
  huwezi kufanya kazi na wachawi kama wewe si mchawi,nape ni gamba kama magamba mengine ndani ya ccm,tena kawazidi wenzake kwani yeye ni gamba vuvuzela.
  rstam gamba mbeleko,
  chenge gamba kauzu kama dagaa
  ,lowasa gamba makini,
  kikwete gamba kuu,pinda gambakimyakimya,
  sita gambanafiki,
  mkapa gamba dikteta,
  ngeleja gamba uso wa mbuzi,
  mwigulu gamba kichwakichwa,
  kafumu gamba jipya,
  magufuli gamba machale,

  mengine watamalizia wengine
  nawakilisha.
   
 13. i

  ipod Member

  #13
  Sep 14, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nape hujui JK kigeugeu
   
 14. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  aaa wpi hawezi kutoka kwan naye ni njaa njaa tu. kwa jinsi alivyopigwa mizengwe uteuzi wa ubunge ubungo ckudhani hata kama angekubali nafasi ya ukuu wa wilaya na hatimaye ukatibu mwenezi. dhamira ya kweli hana ila njaa inamsumbua anaonekana yu tayari kudhalilika kuliko utu wake njaa..njaa.,...njaa
   
 15. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  hamuwajui mgamba kwa uongo nyie...gamba nnauye atakuja na story ya kutunga kwamba kashindwa kwenda igunga sababu anaumwa,...au wakishaona wameharibu sana kwa kumkataza kwenda igunga watamtuma siku za mwisho mwisho...kufanya kazi chini ya jk ukubali kudhalilika kama pinda na magufuli...njaa haivumiliki kwa baadhi ya watu,..ni kwa wanamapinduzi wa kweli ndio wanaweza kujiuuzulu lakini sio hao...
   
 16. o

  ommy15 Senior Member

  #16
  Sep 14, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Nape kunamaisha nje ya ccm,ingawa umeshachafuka tena zaidi ya Rostam,Chenge na Lowassa nashauri ujiengue mapema kabla hawaja kuvua ww. ujue hawakukutana barabarani,gamba ni wewe.
   
 17. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nape mkubwa wetu huku mtaani tunakuona unatembea uchi bila kujijua, wamekuchafua ccm unanuka harafu ya ufisadi..njoo uoge huku upinzani uwe safi kwa maslahi ya Taifa
   
 18. kiroba

  kiroba JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2011
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nape my dear brother. We trust on your brother, but umetuangusha kijana mwenzetu. Hivi kinachokufanya usichukue hatua kwa msimamo wako ni kipi? Hapa umesalitiwa na wenzako wote. Yu wapi Samwel Sitta, Olesendeka, na wenzake wengi wanaojiita wapinga ufisadi. Hapa mngeungana pamoja mngelishinda hii vita.

  Hii vita mlikuwa hamjui adui zenu ni akina nani. Hapa mlikuwa mmezungukwa na maadui wengi sana lakini hukupata hekima ya kuwajua. Sasa umewatambua maadui unaopaswa kupambana nao. Sasa uamuzi upo kwako wewe kama kusuka au kunyoa.
   
 19. M

  Manyema JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  ukiangalia hapo kwenye nyekundu..ni kitu kinawasumbua vijana wengi sana kwenye chama cha magamba. Mwenyekiti wa chama ni mnafiki mkubwa siyo mtu wa kumfuata. ona sasa unavyo dahlilika kijana.
   
 20. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye nyekundu umesema kweli
  Jibu ndilo hilo nape alichukuwe nami nilipo kuwa CCM nilikuwa na gombana sana na viongozi wa juu kuachana na mtido wa kuwatumia vijana wenzangu kumbe vijana nao walikuwa hawajui wana danganywa na vijisenti me nikawaambia kwa hali hii kweli chukeni vyeo vyenu kwahelini bakini na chama chenu hamuoni hata alama za nyakati kila kukicha ni nyie wazeee kuwa tumiaa vijana mbona hamtokia hapo vijana nao wawaonyeshe uzoefu wao hamtaki.

  My Take;

  Vijana wa UVCCM me nawakalibisheni sana CDM hatuangalii wazamani wala wa juzi kwetu Vijana ni aseti kubwa na muhimu sana ndio Majembe yetu hayo. Nendeni huko mijini muwaulize vijana gani wana support CCM na wako CCM uone kama wataweza nyanua midomo none zero kabisa
   
Loading...