Nape: Nchi hii ina wenyewe na wenyewe ni CCM!

kaka umeniwahi kupost mada hii. Mimi mwenyewe nimemsikia Nape kupitia habari ya ITV. Nimeguswa sana ukizingatia mimi sio mwanachama wa ccm na wala sitegemei kuwa mwanachama wa chama hicho. Kwa kauli hiyo ya Nape anamaanisha wale wote wasio wana ccm nchi hii si yao na hivyo wanapaswa kutafuta mahali pengine pa kuishi. Nape amechoka mapema sana wakati umri wake bado mdogo. Nape atwambie tusio wanachama wa ccm twende wapi kama nchi hii ni ya ccm!!!!!! Vinginevyo ajitokeze hadharani nakufuta kauli yake na akiri kwamba ulimi ulitereza.

Mkuu anza sasa maandalizi ya kuirudisha nchi mikononi mwako.

Mwaka 2015 tunatakiwa kupiga kura ya restoration of our beloved country. Muda wa maandalizi ni sasa, andaa na vijana wenzako.
 
Kuna kitu inaitwa arrogance if power. CCM and its zealots are suffering from that.
 
Nimekuwa mfatiliaji wa siasa za Tanzania tangu mfumo wa vyama vingi,na ninachokifahamu utawala bora ni ule unaowajali watanzania wote bila kujali itikadi zao za kisiasa wala kidini.

Watanzania tunaweza kutofautiana kifkira lakini utu wa Mtanzania hauwezi kudharauliwa kamwe. Kwa takribani wiki moja nimekuwa nkifatilia kauli za Nape Nnauye-Katibu uenezi na Itikadi CCM kauli ambazo hazipaswi kutolewa na kiongozi makini na mwenye kuivusha Tanzania kutoka mahali tulipo. Mojawapo ya kauli iliyonikera ni kwamba nchi hii ya Tanzania ina wenyewe na wenyewe ni CCM. Je watu wasiofungamana katika chama chochote hawana haki ya kuitwa Watanzania? Vp walio vyama vya Upinzani nao wapelekwe nchi gan?

Ushauri wangu kwa Nape:
Kama kijana ambaye unapenda kukua kisiasa chunga kauli zako kwani kauli moja tu inaweza kukuharibia ndoto zako na kumbuka kuwa vijana wengi ndo watakuwa na maamuz katika uchaguzi wa 2015, pia lengo la mfumo wa vyama vingi ni kuharakisha maendeleo katika nchi husika na siyo kutugawa na kuudhalilisha utu wa Mtanzania.
 
Nimepita na kuona mada hii hewani lakini cha kuelewa ni kwamba huyo NAPE ni mtu wa propaganda na ukilitazama neno lenyewe utagundua kuwa yeye ni mtu wa kubadili uongo kuwa ukweli ndo maana kaamua kusema kuwa nchi hii ni ya wana CCM.

Na kama ni hivyo kwa nini kuna vyama vingi au ndo geresha la danganya toto kwa pipi isiyoonekana? Huyu mtoto kachoka mapema na sasa hivi mwisho wake unakaribia!
 
Nadhani anajaribu kuwajibu wale wanaharakati waliosema juzi kwenye mdahalo kuhusu malipo ya dowans kwamba 'wananchi wako juu ya katiba'......yeye ametoka na 'nchi ina wenyewe na wenyewe ni CCM'...! Choice ya location ya kumkaribisha Kafumu Dar pia inaacha maswali mengi ya kujiuliza...! Manzese??
 
Kwa imani kama hizo, kujifanya wao ndo wenye nchi, ndo maana wanafanya lolote wawezalo hata kuvunja sheria, hata kuwachonganisha watu kwa imani zao, hata kuleta vita ili mradi tu wabakie madarakani.
Tumekwisha gundua janja yao, hii nchi ni ya kwetu, watanzania! kama walishauza walionunua wametapeliwa kwani 2015 everything will come back to Tanzanians.
Pole Nape na magamba yako!

Hii dharau anayoiendeleza nape dhidi ya watanzania ni lazima tuikomeshe,tusikubali kurudia kosa mwaka 2015 ni lazima tuirudishe nchi mikononi mwa watanzania wenyewe.

Ndio maana hawaoni aibu kujichukulia mali ya umma kwakuwa tumeiacha nchi mikononi mwa manyang'au wachache.
 
Nimekuwa nikifuatilia matamko ya huyu kijana anayeitwa Nape, ukweli ukiyasoma between the lines, utagendua huwa yamejaa hisia za kichochezi chochezi hivi. Lakini cha kushangaza zaidi, sijui kama yeye mwenyewe anafanya hayo akiyajua au bila kujua au anafanya makusudi kutaka nchi isitawalike.

Mimi napenda kumshauri kitu kimoja tu, asifikiri pinde watanzania watakapoamua kuipigania nchi yao, atakuwa salama, hembu aangalie huko Misri na Libya, jinsi familia za utawala wa kimla zinavyokabiliana na nguvu ya umma kwa sasa. Hayo matamshi yake, yatamcost muda si mrefu.

Kwa majumuisho, ni wazi inaonekana jinsi watu walio ndani ya chama cha ccm wanavyoishiwa Busara na hata kupoteza muelekeo wa kisiasa. Pole zao. Akumbuke pia hao watu wa mazense ndiyo watakao kuja kumnyongelea mbali muda si mrefu.
 
Taarifa ITV muda huu namwona Nape anadai nchi hii ina wenyewe na wenyewe ni chama cha mapinduzi! Hivi huyu mtu ana akili kweli? Ina maana wote wasio katika CCM hawana haki na hii nchi?

Great thinkers nakubaliana na Nape kwa upande mmoja maana ni kweli na ni wazi kuwa CCM iliyoko madarakani ndo inasimamia wageni wananyonya rasimali za watanzania kwa mrija, imewezesha mafisadi kupora fedha na rasimali za watanzania na kujiwekezea ughaibuni, wamefanikisha kujenga matabaka ya matajiri na maskini kwa kauli yao nzuri ya maisha bora kwa kila mtz, imehalalisha giza nchi nzima huku viwanda vikfungwa na vijana kukosa ajira, imeshusha hadhi ya Rais na amiri jeshi wa nchi kwa kumruhusu kurusha matangazo ya TRA ktk TV na kumfanya ku2piwa lawama na kuwa wimbo wa kila mtu kila dakika.
 
Nape bwana kama nchi ni ya ccm matokeo iginga isingekuwa toafauti hiyo ya hamsini na kwa arobaini na, mgeshinda kwa asilimia 100%. Bado hujashtuka kuwa watanzania wameishtukia ccm?
 
Mie nimeshangaa sana sana .Hata la kusema sina kumbe CCM ina vilaza namna hii ? Kweli Nape anaimaliza CCM.
 
Ya kujivua gamba yamepotea na hawajui wanafanyaje sasa anajidai kusaka hoja mpya, pole sana Nape, hivi wale CUF mliofunga nao ndoa kule Zanzibar hao sio wenye nchi kama nyie? au ndo yale ukiolewa basi na wewe unakuwa unatumia jina la mume.... kazi ipo! Nape think Rationally of what you talk and its impact to our society....acha kuwa vuvuzela.... wewe ni kijana msomi, soma alama za nyakati
 
Great thinkers nakubaliana na Nape kwa upande mmoja maana ni kweli na ni wazi kuwa CCM iliyoko madarakani ndo inasimamia wageni wananyonya rasimali za watanzania kwa mrija, imewezesha mafisadi kupora fedha na rasimali za watanzania na kujiwekezea ughaibuni, wamefanikisha kujenga matabaka ya matajiri na maskini kwa kauli yao nzuri ya maisha bora kwa kila mtz, imehalalisha giza nchi nzima huku viwanda vikfungwa na vijana kukosa ajira, imeshusha hadhi ya Rais na amiri jeshi wa nchi kwa kumruhusu kurusha matangazo ya TRA ktk TV na kumfanya ku2piwa lawama na kuwa wimbo wa kila mtu kila dakika.

Hata mimi hilo la TRA kumtumia JK kwenye tangazo lao la kodi limenishangaza, najiuliza kwamba huo ndio uwezo wa TRA wa kubuni matangazo?

Maajabu ya mwaka ni kwamba hao mawakala wao wa kuuza machine za EFD nao hawatoi risiti za EFD, hapo ndio patamu.
 
Nape ni zaidi ya Yusuph Makamba!
Tulifikiri Makamba ni uzee na elimu,sasa Nape cjui tatizo nini?maana ni kijana na ana shule,lakini anachoongea hata mtoto wa nursery school,HAWEZI KULOPOKA UPUUZI KAMA HUO.
 
Nilimuona huyu jamaa amefura kama kitimoto yaani hujui mdomo ni upi pua ni ipi, tumbo linashindana na masaburi yake! Duh! kaazi kweli kweli
 
WanaJF furahini kwa maneno ya Nape.

Kuna watu wanakesha usiku na mchana wakifanya maombi juu ya nchi hii na watu wake. Nadhani Mungu anajibu maombi kwani kwa matamshi aliyotoa Nape ni wazi amevuliwa nguo na kubaki uchi wa mnyama.Amesababisha chuki kuu kutoka kwa wasio wana CCM.

Na hii chuki ya umma itaonyeshwa kwenye sanduku la kura. Niseme wazi ndani ya CCM wapo vijana 2 tu angalao wenye busara nao ni January Makamba na Hussein Bashe. Kwa hakika Nape hatofautiani na Tambwe Hiza
 
Aibu iliyoje kwa CCM kuwa na watu kama Nape. Tanzania ilikuwepo kabla ya ccm, TANU, TAA n.k, na itaendelea kuwepo baada ya chama cha magamba kuondoka.

Kama ambavyo Nyerere alipokufa Tanzania imeendelea kuwepo, basi ccm na Nape wafahamu ya kuwa chama cha magamba sio Tanzania. Hata siku moja hutasikia Republicans au Democrats wanaropoka hadharani ya kuwa USA ni ya Democratic party au ya Republicans, au UK viongozi wanatamka kuwa hii ni nchi ya Labour Party, au Tories. Hivi hawa watu ccm imewaibua wapi? Viongozi wa ccm mmechemsha!!!

Kuna watu waliopigania na kufa kwa ajili ya nchi yetu kabla ya CCM. Ina maana hao hawakuwa watanzania? Wakina Chief Mkwawa na wengi waliokufa enzi za vita vya Maji Maji wakiongozwa na Kinjeketile, hii nchi haikuwa yao? Huyu mtu arudi akasome chekechea, maana hata darasa la kwanza upeo wake haujafikia.

Wahenga wetu walikufa hata kabla jina la Tanzania halijakuwepo, lakini waliifia hii nchi. Leo eti Tanzania ni ya CCM, kichefuchefu...
 
Nimemfananisha Nape na mtoto wa gadhaffi juu ya kauli zake kwa wa libya,lakini sasa anaishi mafichoni na cockroach wako tripol.
Jaji Warioba alisema haioni serikali ya Tanzania iliyopo ni serikali ya CCM.

Nape naye ni kama huyo
 
Back
Top Bottom